Spika Dkt. Tulia ajuzwe Wabunge 19 hawajawahi kuteuliwa na CHADEMA. Wameingia kwa kufoji nyaraka

Tatizo letu kubwa ni impunity...

"Exemption from punishment or freedom from the injurious consequences of an action."

Nchi nzima inajua wale sio wabunge halali, lakini wanaendelea kulindwa kwa sababu wanajua hatuna kitu tutafanya.

Taasisi yenye viongozi wanaojiheshimu; walipaswa ku-take a step back na kuipa nafasi hiyo doubt. Hivi kweli mtu una mke, then unaambiwa na mama wa mke wako, hao watoto sio wa kwako; hutaki hata kustuka!
 
Tatizo letu kubwa ni impunity... "Exemption from punishment or freedom from the injurious consequences of an action."

Nchi nzima inajua wale sio wabunge halali, lakini wanaendelea kulindwa kwa sababu wanajua hatuna kitu tutafanya.

Taasisi yenye viongozi wanaojiheshimu; walipaswa ku-take a step back na kuipa nafasi hiyo doubt. Hivi kweli mtu una mke, then unaambiwa na mama wa mke wako, hao watoto sio wa kwako; hutaki hata kustuka!
Viongozi wa nchi yetu hawajawahi kukumbana na nguvu ya umma.

Wanafanya haya kwa kujua hakuna la kuwafanya. Wanajua kwamba wanadanganya, na wanajua umma unajua lakini pia wanajua umma hauna lolote dhidi yao

Spika Tulia ni Mwanasheria na Mhadhiri kisheria. Alikuwa naibu Spika mkasa ukitokea
Anajua A-Z za kila kitu. Juzi katika interview utadhani ndio anaingia Bungeni kwa mara ya kwanza

Bunge ni taasisi inayopaswa kujiheshimu ili iheshimiwe. Majukumu ya Bunge kama'' kikao cha wananchi wa Tanzania'' ni pamoja na kutunga sheria. Bunge hilo hilo linafanya mambo ya ajabu sana.

Spika Tulia hawezi kuwaondoa Wale 19 (sio wabunge) .
Hao 19 wameshiriki kumpigia kura. Hata kama wasingekuwepo angekuwa Spika, hofu yake ni kuwa ikibanika ni Watu wa nje na walimpigia kura mchakato wa kumpata yeye unaingia doa.
Hivyo atawalinda kwa gharama na heshima ya Bunge na nchi ili aendelee kuwa Spika

Tukae chini na kuandika utaratibu mwingine, huu wa katiba ya leo hautufai
 
Nimemsikiliza juzi Spika Tulia nikasikitika sana. Sijui kwanini aliamua kujibu maswali yale
Amedhalilika sana ukizingatia ni mwanasheria tena mhadhiri. Ilikuwa aibu

Tulia anasema suala waulizwe Tume ya uchaguzi. Sophia alipotimuliwa JYN alitangaza kupokea barua ya CCM. Sheria za nchi zinasema mtu akifukuzwa chama anapoteza Ubunge. Hivi hili nalo mhadhiri wa sheria halijui

Pili, anasema, Chadema wafuate taratibu! pathetic.
Taratibu za chama zinasimamiwa na chama si Spika wa Bunge.

Ikiwa alishajivua nafasi kwa kutupa mzigo kwa tume, ni taratibu gani za Bunge zinazoelekeza ''utaratibu ufuatwe'? Hapa watu wasifikirie utumbo wa Ndugai alioutengeneza kulinda COVID-19 kwa sababu zake

Chadema wametoa tuhuma nzito za kufoji nyaraka kutoka Tume ya uchaguzi. Ni wajibu wa vyombo husika kufuatilia. Wote wamekaa kimya kana kwamba hakuna kilichotokea

Kisheria Tulia amechaguliwa na baadhi ya watu wasiowabunge kinyume cha sheria.

Tulia ni Spika, mwanasheria na Mhadhiri wa chuo kikuu! nadhani sisi kama nchi tujiulize
Hapa Luna neno,Spika sio halali ikitokea wabunge wasiokuwa na sifa kuondolewa?
Je aliyesimamia uchaguzi wa Spika na Naibu watakuwa wahujumu uchumi au kesi ya jinai kuruhusu wapiga kura wasio halali?
 
Mkuu P. Hapa kuna hoja nyingi sana zitokanazo. Kwanza, DCI anapokea taarifa lakini pia ana mamlaka ya kuchunguza kwa kushirikiana na vyombo vingine. Ikiwa kuna tuhuma vyombo hapo juu vinaweza kufanya kazi pamoja.

Hapana, waandishi wa kichunguzi wanatafuta habari kwa source zao hawasubiri kuletewa mezani

Yes to some extent kuna ukweli, kulikuwa a hint za jambo hilo. Kwasababu zisizojulikana Chadema hawakuweza ku pre-empty situation na handling yake baada ya pale ilikuwa poor! kuna ukwel
Mkuu Nguruvi3, kwenye hili la forgery ya wabunge wa Chadema, let's not beat around the bush, forgery imefanyika ndani ya Chadema, NEC wamepokea barua ya uteuzi kutoka Chadema, ikijua ni barua bonafide genuine, hivyo ikawateua wabunge 19 ikawakabidhi Bungeni. Spika akawapokea akawaapisha chap chap fasta fasta.

Ndipo Chadema waibuka na kudai kumefanyika forgery na kukurupuka kuitisha CC kwa mtindo wa a kangaroo court na kuwatimua.

Kwa vile anayejua Luna forgery ni mtu mmoja as an entity, then, huyo anajua kuna forgery anapaswa akaripoti police ili ndipo DCI aanzishe uchaguzi.

Kwa upande wa sisi waandishi, the primary source ya IJ hii ni hiyo barua ya uteuzi ya Chadema kwenda NEC kuwateua hao wabunge 19. Kwa hapa jambo hili lilipofikia, no Tanzanian journalist or media can do anything without a police report kwasababu hiyo barua ndio the bone of contention inalindwa as number 1, top Classified document, the only way to get hold of that document ni kwa Chadema kuripoti polisi kuwa wao kama chama hawajaandika barua yoyote ya uteuzi wa wabunge wake wa viti maalum kwenda NEC, hivyo barua iliyopelekwa NEC imefojiwa. Jeshi la polisi Tanzania ndio mamlaka pekee yenye uwezo wa kulazimisha NEC kuitoa copy ya hiyo barua ya uteuzi na IJ ndio can start there.

Mfano mzuri na hai ni issue ya Barua ya Job Ndugai kujiuzulu uspika, was wrongly addressed to CCM instead of Bunge, watu tukapiga kelele lakini hazikusaidia kitu, lakini mara baada ya James Mbatia ku institute mashitaka, barua batili ile ilikuwa withdrawn, ile press release ya JYN ikaondolewa kwenye Website ya Bunge as if haikuwahi kuwepo, ikaandikwa a proper letter bacdated and correctly addressed, ikawasilishwa mahakamani na kuufunga mjadala.

Jinai haina limitation of time, hivyo Chadema wakiamua to do the right thing, kama tulivyo shauri hapa
CHADEMA kubalini matokeo na m-survive, or shupazeni shingo. You go to hell 6ft under Hao Makamanda 19 ni mashujaa, kuendelea Ubunge wao,
watafanya na kulimaliza hili, wakiamua kuendelea kushupaza shingo na kuendelea na hizi dilly dallying, they can.
P
 
Spika Tulia hawezi kuwaondoa Wale 19 (sio wabunge) .
Hao 19 wameshiriki kumpigia kura. Hata kama wasingekuwepo angekuwa Spika, hofu yake ni kuwa ikibanika ni Watu wa nje na walimpigia kura mchakato wa kumpata yeye unaingia doa.
Hivyo atawalinda kwa gharama na heshima ya Bunge na nchi ili aendelee kuwa Spika
As far as their status is concerned, mpaka tunapoandika hapa, wale wabunge 19 ni wabunge halali, waliteuliwa kihalali na barua ya uteuzi halali kutoka Chadema, hivyo NEC ikawapa barua za uteuzi viti maalum na kumpelekea Spika. Wakaapishwa, hivyo mpaka sasa bado ni wabunge halali hadi pale Chadema itakapo fanya the right thing, ama ithibitishe forgery, ama kikao cha Baraza Kuu kithibishe yale maamuzi ya ile kangaroo court, ndipo watenguliwe, inayotengua ubunge wao ni mamlaka yao ya uteuzi ambayo ni NEC na sio Bunge!. Na hata wakitenguliwa, kura zao kumchagua Tulia ni kura halali, kwasababu wakati wanapiga kura walikuwa wabunge halali!.
P
 
Hata kama Spika atawachukulia kuwa NI wanachama halali wa Chadema. Chadema imeshatoa ufafanuzi nyaraka zilizotumika kuwaingizwa bungeni zimefojiwa.

Na wanaoandaa nyaraka hizo wameshatoa taarifa za sahihi zao na majina yao kufojiwa. Sijui wanataka Nani aje asibitishe Hilo. Wakati wewe unasema huyu ndio aliyeandaa Orodha ya Wabunge. Kamati kuu inakaa kikao inakupa barua kuwa hatukuandaa sisi. Na wanakujulisha Spika kuwa hao NI waalifu wamefoji nyaraka.

CHADEMA haina haja ya kutoa taarifa za uhai au kutokuwa mwanachama ili kuonesha uhalali wa akina mdee. Sababu hawatakiwi kuwepo bungeni sababu wameingia kwa njia haramu.

Basi Spika ajikite kuonesha uhalali wa nyaraka zilizotumika na majina na sahihi na katibu aliyepeleka majina kwa spika. Na vikao vilivyopitisha majina hayo.

Kushindwa kufanya hivyo kutaendelea kuoneshaa dunia kuwa Sheria ya Kinga dhidi ya kushitakiwa kwa spika ililetwa ili kumfanya Spika kutoa maamuzi ya kuangamiza upinzani. Na kuwe akuna mwanya wa kuipata haki kokote atakapoweza kuitafunga au kuipokonya kwa nguvu.

Kwa Sheria hiyo Spika Sasa ameweza kuvunja katiba bila hofu ya kushitakiwa, kupingwa Wala maamuzi yake kukatiwa rufaa.
MBOGA MBOGA FC wametoa tumbili wameingiza kingedele😂😂
 
Tatizo letu kubwa ni impunity...

"Exemption from punishment or freedom from the injurious consequences of an action."

Nchi nzima inajua wale sio wabunge halali, lakini wanaendelea kulindwa kwa sababu wanajua hatuna kitu tutafanya.

Taasisi yenye viongozi wanaojiheshimu; walipaswa ku-take a step back na kuipa nafasi hiyo doubt. Hivi kweli mtu una mke, then unaambiwa na mama wa mke wako, hao watoto sio wa kwako; hutaki hata kustuka!
Ninachokiona kwenye hilo sakata taasisi zote hakuna inayojitegemea katka ufanyaji kazi wake, mkuu wa nchi akishasema hakuna taasisi inayoweza kusema hapana.
 
As far as their status is concerned, mpaka tunapoandika hapa, wale wabunge 19 ni wabunge halali, waliteuliwa kihalali na barua ya uteuzi halali kutoka Chadema, hivyo NEC ikawapa barua za uteuzi viti maalum na kumpelekea Spika. Wakaapishwa, hivyo mpaka sasa bado ni wabunge halali hadi pale Chadema itakapo fanya the right thing, ama ithibitishe forgery, ama kikao cha Baraza Kuu kithibishe yale maamuzi ya ile kangaroo court, ndipo watenguliwe, inayotengua ubunge wao ni mamlaka yao ya uteuzi ambayo ni NEC na sio Bunge!. Na hata wakitenguliwa, kura zao kumchagua Tulia ni kura halali, kwasababu wakati wanapiga kura walikuwa wabunge halali!.
P
Kama covid 19 walofoji wakajipeleka bungeni, mbona chadema hawajatoa orodha ya wabunge ambayo si ya kufoji Hadi leo?
Chadema toeni orodha ya wabunge halali acheni kulialia.
 
Hili sakata la kina Mdee,Spika,Chadema na Bunge linanipeleka kwenye kile kisa cha mbuzi,swala,kijiji na tembo ambacho kiko hivi...Kijijini kulitokea msako wa mbuzi na wakawa wanakamatwa na kuwekwa jela.Swala alivyo ona hivyo akaamua kutoroka hicho kijiji na kukimbia speed ya ajabu ili asikamatwe.

Njiani Tembo akamsimamisha na kumuuliza mbiyo zoote hizo za nini.?Swala akamjibu huko kijijini mbuzi woote wanakamatwa hivyo nakimbia nisikamatwe,Tembo akamwambia lakini weye ni Swala,jibu la Swala likawa wakinikamata itawachukuwa miaka kumi kuthibitisha mimi siyo mbuzi.

Nadhani tupo pamoja.
 
Ninachokiona kwenye hilo sakata taasisi zote hakuna inayojitegemea katka ufanyaji kazi wake, mkuu wa nchi akishasema hakuna taasisi inayoweza kusema hapana.
Mkuu wa nchi anapaswa kusimamia sheria, na kama akishindwa anapasww kuwajibishwa. Hakuna uwajibikaji nchini hapa. Ndio maana watu wanafanya watakalo na hamna kitu tunafanya
 
Viongozi wa nchi yetu hawajawahi kukumbana na nguvu ya umma.

Wanafanya haya kwa kujua hakuna la kuwafanya. Wanajua kwamba wanadanganya, na wanajua umma unajua lakini pia wanajua umma hauna lolote dhidi yao

Spika Tulia ni Mwanasheria na Mhadhiri kisheria. Alikuwa naibu Spika mkasa ukitokea
Anajua A-Z za kila kitu. Juzi katika interview utadhani ndio anaingia Bungeni kwa mara ya kwanza

Bunge ni taasisi inayopaswa kujiheshimu ili iheshimiwe. Majukumu ya Bunge kama'' kikao cha wananchi wa Tanzania'' ni pamoja na kutunga sheria. Bunge hilo hilo linafanya mambo ya ajabu sana.

Spika Tulia hawezi kuwaondoa Wale 19 (sio wabunge) .
Hao 19 wameshiriki kumpigia kura. Hata kama wasingekuwepo angekuwa Spika, hofu yake ni kuwa ikibanika ni Watu wa nje na walimpigia kura mchakato wa kumpata yeye unaingia doa.
Hivyo atawalinda kwa gharama na heshima ya Bunge na nchi ili aendelee kuwa Spika

Tukae chini na kuandika utaratibu mwingine, huu wa katiba ya leo hautufai
Tunahitaji mwanzo mpya... Hizi tabia za forgery kwenye mambo ya serikali zimekuwa nyingi sana. Boniface Jacob aliondolewa kwenye umeya kwa forgery, tukawa kimya, baadae tumepata wabunge wa forgery. Leo inawezekana tuna Spika ambaye ni matokeo ya forgery; lile barua la CAPITAL LETTER sijui kama ni la kweli
 
Kwa upande wa sisi waandishi, the primary source ya IJ hii ni hiyo barua ya uteuzi ya Chadema kwenda NEC kuwateua hao wabunge 19. Kwa hapa jambo hili lilipofikia, no Tanzanian journalist or media can do anything without a police report kwasababu hiyo barua ndio the bone of contention inalindwa as number 1, top Classified document, the only way to get hold of that document ni kwa Chadema kuripoti polisi kuwa wao kama chama hawajaandika barua yoyote ya uteuzi wa wabunge wake wa viti maalum kwenda NEC, hivyo barua iliyopelekwa NEC imefojiwa. Jeshi la polisi Tanzania ndio mamlaka pekee yenye uwezo wa kulazimisha NEC kuitoa copy ya hiyo barua ya uteuzi na IJ ndio can start there.
Mkuu moja kati ya sifa za IJ ni kutafuta habari , kuzifanyia utafiti na kuzitoa hadharani.
Mwandishi wa habari John Miller wa ABC alimhoji Osama Bin Laden kabla ya shambulio la Dar es Salaam na Nairobi. Kwenda kuonana na OBL si mchezo, ni kuweka roho rehani, aliweka.

Tazama akina Nima Albagir na habari za Horn of Afrika au Arwa Damon na akina C.Amapour kwa uchache. Hawa hutafuta habari ambazo si rahisi kuzipata katika media bila utafiti n.k.

Kwa Tanzania issue hii ndipo IJ walitakiwa wafanye kazi. Kuwa IJ si reporter wa kusubiri mtu aje kuhubiri, ni kazi ya kuchimba , kudodosa hadi ukweli ujitokeze.

Mfano, habari ingekuwa endelevu wangejitokeza tu ima kukanusha au kukubali.
Juzi Spika katupa zigo NEC, hii maana yake kuna weak point na hapo ndipo IJ anapoingia. Kudodosa si kuuliza tu bali kumlazimisha mtu atoe habari bila kupenda, ni kukera ni kuchokoza .

Jeshi la Polisi lina mamlaka kwa mujibu wa sheria na maandishi. Kwa matendo na ''competence'' si hivyo na ni kuwabebesha mzigo tu! Hivi hawa si ndio wanaofanya kazi na DCI kama alivyosema JokaKuu

Jeshi la Polisi halisubiri kuletewa habari. Hivi kukiwa na habari za hatari kwa usalama wa nchi jeshi litasubiri mtu au watu waende kulalamika.

As far as their status is concerned, mpaka tunapoandika hapa, wale wabunge 19 ni wabunge halali, waliteuliwa kihalali na barua ya uteuzi halali kutoka Chadema, hivyo NEC ikawapa barua za uteuzi viti maalum na kumpelekea Spika. Wakaapishwa, hivyo mpaka sasa bado ni wabunge halali hadi pale Chadema itakapo fanya the right thing, ama ithibitishe forgery, ama kikao cha Baraza Kuu kithibishe yale maamuzi ya ile kangaroo court, ndipo watenguliwe, inayotengua ubunge wao ni mamlaka yao ya uteuzi ambayo ni NEC na sio Bunge!. Na hata wakitenguliwa, kura zao kumchagua Tulia ni kura halali, kwasababu wakati wanapiga kura walikuwa wabunge halali!.
P
Mbona muzee unachanganya mwenyewe unakiri Mbatia alichukua hatuwa mahakama ikaficha bunge likazunguka kuitoa kwenye Website huoni Chadema hawana cha kufanya ila wao bunge wafanye kama walivyo fanya kwenye Website?
 
Tunahitaji mwanzo mpya... Hizi tabia za forgery kwenye mambo ya serikali zimekuwa nyingi sana. Boniface Jacob aliondolewa kwenye umeya kwa forgery, tukawa kimya, baadae tumepata wabunge wa forgery. Leo inawezekana tuna Spika ambaye ni matokeo ya forgery; lile barua la CAPITAL LETTER sijui kama ni la kweli
Mkuu Mtama mchungu, tofautisha forgery, kughushi, na void or voidable, batili na batilifu.
Ile taarifa ya capital letters sio forgery, ile ni bonafide genuine, ila ni batili kutokana na ubatilifu, na akina sisi tuliisha muombea msamaha Msameheni bure Job Ndugai, amechanganyikiwa baada ya kuomba msamaha batilifu uliokataliwa! Barua yake ya Kujiuzulu nayo pia ni batilifu!

Ingekuwa forgery kama ingeandikwa na mtu mwingine na kusainiwa na mwingine kwa kujifanya ni JYN. Ile taarifa imeandikwa na JYN mwenyewe na kusainiwa na yeye mwenyewe ila ni batili kwasababu imekuwa addressed to a wrong person, badala ya kupekwa Bunge, ikapelekwa CCM!

Tofauti kati ya batili na batilifu ni batili hairekebishiki, hivyo inakuwa void ab Initial, lakini batilifu, voidable inarekebishika na kuuondoa ubatili kama nilivyoeleza hapa Je, wajua haramu isipoharimishwa inageuka halali? Na batili isipobatilishwa inageuka halali. Je, tuhalalishe ubatili huu kwa mhimili wetu wa Bunge?

Hatimaye ubatili huo uliondolewa, ile taarifa ya capital letters ikaondolewa, ikaandikwa barua nyingine ya kujiuzulu, properly addressed kwa kuwa backdated na kuwa submitted to the proper authority, hivyo ubatili ule kuondolewa na tukapongeza

Sasa mambo haya ni safi, yamenyooka yako kwenye mstari.
Hili la wabunge viti maalum Chadema ambao Chadema wenyewe wanadai ni forgery, bado halijakaa vizuri, forgery ni jinai, hatua ya kwanza ni kwa Chadema kuripoti polisi. Hili halichafanyika, hivyo mpaka hivi ninapoandika hapa, barua ile ya uteuzi wao inahesabika ni barua halali, na wabunge hao ni wabunge halali mpaka pale Chadema watakapo fanya the right thing.
P
 
Basi Spika ajikite kuonesha uhalali wa nyaraka zilizotumika na majina na sahihi na katibu aliyepeleka majina kwa spika. Na vikao vilivyopitisha majina hayo.
Kwani msiende mahakamani kuonyesha bunge na hao 19 wamefoji documents ili sheria ichukue mkondo wake?
Kwa hiyo mnalea watu wa kufoji documents kisha mnataka madaraka makubwa nchini?
Haiwezekani kabisa.
 
Mkuu moja kati ya sifa za IJ ni kutafuta habari , kuzifanyia utafiti na kuzitoa hadharani.
Mwandishi wa habari John Miller wa ABC alimhoji Osama Bin Laden kabla ya shambulio la Dar es Salaam na Nairobi. Kwenda kuonana na OBL si mchezo, ni kuweka roho rehani, aliweka.

Tazama akina Nima Albagir na habari za Horn of Afrika au Arwa Damon na akina C.Amapour kwa uchache. Hawa hutafuta habari ambazo si rahisi kuzipata katika media bila utafiti n.k.

Kwa Tanzania issue hii ndipo IJ walitakiwa wafanye kazi. Kuwa IJ si reporter wa kusubiri mtu aje kuhubiri, ni kazi ya kuchimba , kudodosa hadi ukweli ujitokeze.

Mfano, habari ingekuwa endelevu wangejitokeza tu ima kukanusha au kukubali.
Juzi Spika katupa zigo NEC, hii maana yake kuna weak point na hapo ndipo IJ anapoingia. Kudodosa si kuuliza tu bali kumlazimisha mtu atoe habari bila kupenda, ni kukera ni kuchokoza .

Jeshi la Polisi lina mamlaka kwa mujibu wa sheria na maandishi. Kwa matendo na ''competence'' si hivyo na ni kuwabebesha mzigo tu! Hivi hawa si ndio wanaofanya kazi na DCI kama alivyosema JokaKuu

Jeshi la Polisi halisubiri kuletewa habari. Hivi kukiwa na habari za hatari kwa usalama wa nchi jeshi litasubiri mtu au watu waende kulalamika.
Mkuu Nguruvi3, kwenye hili la IJ, nakubaliana na wewe, it's a weakness on our part!.

P
 
Ata Kama Spika atawachukulia kuwa NI wanachama halali wa chadema. Chadema imeshatoa ufafanuzi nyaraka zilizotumika kuwaingizwa bungeni zimefojiwa.

Na wanaoandaa nyaraka hizo wameshatoa taarifa za sahihi zao na majina yao kufojiwa. Sijui wanataka Nani aje asibitishe Hilo. Wakati wewe unasema huyu ndio aliyeandaa Orodha ya Wabunge. Kamati kuu inakaa kikao inakupa barua kuwa hatukuandaa sisi. Na wanakujulisha Spika kuwa hao NI waalifu wamefoji nyaraka.

Chadema haina haja ya kutoa taarifa za uhai au kutokuwa mwanachama ili kuonesha uhalali wa akina mdee. Sababu hawatakiwi kuwepo bungeni sababu wameingia kwa njia haramu.

Basi Spika ajikite kuonesha uhalali wa nyaraka zilizotumika na majina na sahihi na katibu aliyepeleka majina kwa spika. Na vikao vilivyopitisha majina hayo.

Kushindwa kufanya hivyo kutaendelea kuoneshaa dunia kuwa Sheria ya Kinga dhidi ya kushitakiwa kwa spika ililetwa ili kumfanya Spika kutoa maamuzi ya kuangamiza upinzani. Na kuwe akuna mwanya wa kuipata haki kokote atakapoweza kuitafunga au kuipokonya kwa nguvu. Kwa Sheria hiyo Spika Sasa ameweza kuvunja katiba bila hofu ya kushitakiwa, kupingwa Wala maamuzi yake kukatiwa rufaa.
Bunge halipokei nyaraka toka Chadema.
Bunge linapokea nyaraka toka Tume ya Uchaguzi.
Watanzania tufahamu kuwa 'Nyaraka' zilizopo kwa Spika Tulia, (na Spika Ndugai kabla yake), ni NYARAKA HALALI maana zimetoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
Tuwaulize Tume ya Taifa ya Uchaguzi: Hayo majina waliyapeleka Bungeni kwa kigezo kipi wakati Chadema hawajawahi kuteua majina ya Viti Maalum?
Tume ya Uchaguzi inaendeleza uchafuzi katika uchaguzi.
Tume ya Uchaguzi wametenda kosa la jinai. Tume ni watuhumiwa.
 
Mkuu Nguruvi3, kwenye hili la IJ, nakubaliana na wewe, it's a weakness on our part!.

P
Paskali, ukiona wakati mwingine wanaJF wanakusema kwa lugha hasi, fahamu kwamba hawakuchukii wewe mwenyewe binafsi, bali wanaonyesha hasira zao kwa Waandishi wa Habari kupitia kwako kwa sababu mbele ya macho yetu, wewe ni Mwandishi Jasiri.
Tunapoona ujasiri umeyeyuka miongoni mwa Waandishi wa Habari, we have been channeling our disappointments and frustrations through you.
And I believe you know this.
Paskali, you are a flag bearer.
Na umeendelea kulithibitisha hili pale ulipokaribishwa Star TV ukaupiga mwingi kwa kutema madini yasiyo ya kawaida.
Nina ombi maalum kwako, ambalo litajibu tatizo la hawa Wabunge 19.
Ninakuomba ufanye mahojiano mahsusi na Mwenyekiti au Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, ili kupitia majibu utakayopewa, Watanzania tujue ni kwa namna gani Tume ilipeleka Majina ya akina Halima Mdee kwa Spika wa Bunge.
Watanzania wanamtuhumu Spika badala ya kutuhumu Tume ya Uchaguzi.
Tunajua Tume ya Uchaguzi ikiingia kwenye 18 za 'Paskali', Watanzania tutajua pia 'logic behind' ukataji wa majina ya Wagombea wa Upinzani tu, kwa kukosea kujaza Fomu za kuomba kugombea, wakati kwa Wagombea wa CCM, HAKUNA HATA MMOJA ALIYEKOSEA KUJAZA FOMU.
Yaani, asilimia zaidi ya 95 ya Wapinzani walikosea kujaza Fomu, wakati Wagombea wa CCM walipatia kwa ASILIMIA 100.
Paskali, tusaidie tafadhali.
Please, fahamu kuwa, hapa JF, Paskali, au P. ni 'brand'
 
Paskali, ukiona wakati mwingine wanaJF wanakusema kwa lugha hasi, fahamu kwamba hawakuchukii wewe mwenyewe binafsi, bali wanaonyesha hasira zao kwa Waandishi wa Habari kupitia kwako kwa sababu mbele ya macho yetu, wewe ni Mwandishi Jasiri.
Na kwa hili tunampongeza Paskali, tuna channel ulichosema ''hasira' zetu si kwakwe bali kwa kutambua ni yeye aliyejitokeza na tunayemjua tena akikabiliana na hoja hata zisizopendeza.
Hili kwa kweli tumsifu
Tunapoona ujasiri umeyeyuka miongoni mwa Waandishi wa Habari, we have been channeling our disappointments and frustrations through you.
And I believe you know this.
Paskali, you are a flag bearer.
Kwakweli ujasiri na IJ hakuna hapa nchini. Hili lisingefika hapa kama lingekuta wenye weledi.
Nakumbuka kisa cha BW Mkapa na yule bw nadhani Kitime. Nakumbuka BWM na Idd Simba.
Akina Jenerali walifanya homework na kila kashfa ikawa ''mantra'

Nchi za wenzetu viongozi wakiamka asubuhi kitu cha kwanza ni kusoma habari! Tanzania kitu cha kwanza ni supu . Hawana wasi wasi nani atawawajibisha?

Hili tu lilipaswa liwe kashfa kwa jeshi la Polisi, PCCB, Ofisi ya DCI n.k. maana Tume ya uchaguzi kutuhumiwa kwa forgery na bado haina majibu na Watanzania hawana majibu, inasikitisha
 
Back
Top Bottom