Watanzania ni mabingwa katika kumalizia hasira zao kwenye keyboard and keypad, kwa njia hii kila aina ya maneno machafu wanayajua. Inapokuja kwenye physical confrontation na ukichukulia hata kanuni za bunge wengi hawazijui, thubutu, huwezi kuwaona.
Mama Spika wala usiwe na wasiwasi, haya ni maneno ya debe tupu. hakuna mtu atakaye kudhuru kwa sababu ya kanuni ambazo wachache sana wanazijua. kilichofanyika ni mob mentality kuchagizwa na waheshimiwa ambayo imewasukuma watu kutenda deindividuation.
Huu ni upepo tu na utapita.
Utasubiri sana.Bado wanazidi kutumia kodi zetu vibaya,upuuzi huu unaweza kufanyika Tanzania tu.
Lakini mda si mrefu Haki itashinda.
Insha yako sijaweza kuisoma,nitaipitia baadae.Another example of physical thinking rather than brain thinking.
Kwanza, nani ana uhakika kuwa spika na naibu wake wametukanwa?[
Ni matusi gani aliyotukanwa?
Watu wanabwabwaja huku hawajui kama ni kweli spika ametukanwa au hajatukanwa. Hata Mnyika alipotamka kuwa, 'Chanzo cha matatizo mengi ya nchi hii ni kuwa na Serikali na Rais dhaifu', wapo wengi waliosema kuwa ametukana. Lakini je, maneno haya ni tusi? Kama tungeelezwa hizo message zimesema nini, huenda wengi wetu tungeshangaa kwa vile kinachotajwa kuwa ni matusi inaweza kuwa ni kuambiwa ukweli jinsi spika na Naibu wake wanavyofanya kazi. Kama ni matusi kweli, wapeleke mahakamani, wanangoja nini? Namna nyingine hizi ni hadithi za alinacha.
Nilipokuwa pale chuo kikuu wakati wa utawala wa Mwinyi, chuo kilifungwa kwa maelezo kuwa sisi wanachuo tumemtusi Rais matusi ya nguoni (kwa mara ya kwanza ndiyo hilo neno 'matusi ya nguoni' lilisikika kwenye msamiati wa kiswahili) lakini ukweli ni kuwa hakuna mahali iwe kwa maandishi au kauli tuliona au kusikia hayo yaliyotajwa kuwa ni matusi ya nguoni. Nakumbuka maandishi pekee ambayo yalichukuliwa kuwa ni matusi kwa Rais ni bango liliandikwa kuwa: Jangala anataka kuendesha mambo yake kwa mila na desturi (wakati ule kulikuwa na mchezo wa Kibuku uliokuwa na mwigizaji maarufu Jangala akimlazimisha mtoto wake aitwaye Kidole kuwa ni lazima amwoe binti mmoja hapo kijijini kwa sababu ni mila na desturi mtoto kutafutiwa mchumba na wazazi wake), Mwinyi anaendesha mambo yake kwa mila na desturi (Rais Mwinyi alidai kuwa aliwashauri wanachuo kuingia darasanai lakini wao wakasema kuwa ushauri siyo lazima ukubaliwe, wanachuo walisahau kuwa kwa mila na desturi za kiafrika ushauri kutoka kwa mkubwa kwenda kwa mdogo ni amri, na kutoka kwa mdogo kwenda kwa mkubwa ni ombi), hivyo JANGALA = MWINYI. Maneno haya yalitafsiriwa kuwa ni matusi ya nguoni kwa Rais, chuo kikafungwa. Ikaundwa tume ya jaji kuchunguza utovu wa nidhamu uliofanywa na wanachuo kwa Rais. Taarifa ya tume ikasema kuwa serikali ilifanya makosa na wanachuo hawakuwa na hatia, chuo kikafunguliwa, hakuna hata mtu mmoja aliyeshtakiwa kwa kumtusi Rais maana hakukuwa na tusi.
Sasa kwa Makinda, huenda ikawa ni namna hiyo hiyo. Subirini mwone kama kweli kuna kesi yoyote ya matusi kwa spika itafunguliwa, nasema hakuna kesi ya matusi kwa Spika itakayofunguliwa mahakamani zaidi ya hizi porojo za mitaani.
Inasikitisha kukutana na watu wa aina yako,inavyoonekana hujui unatoka wapi unakwenda wapi katika ulimwengu wa siasa.Wewe ni bure kabisa.Acheni uzushi CDM imefanya lini mkutano Mwembe Yanga? mwandishi kanjanja.............. na mhariri kanjanja......!!!!!!
Piga 911 halafu operator atakuunganisha na spika lakini usisahau kumwambia dhamira yako.Mimi nilikosa kuhudhuria huo mkutano wa Temeke.
Msaada kwa mwenye namba hizo nipate kuwasalimia na kuwapa pole.
Mkuu wewe ni GT big up"
nakuongezea hapo Kinana analitia hasara taifa akiwa anajua kabisa madhara ya kutumia dola badala
ya Tzs kwenye malipo yetu ya ndani,kupitia kampuni yake ya shipping line na yard ya magari ya TALL
wanacharge malipo yote kwa kutumia dollar badala ya Tshs"
Nenda ikulu getini ukamalize hasira zako.Mkuu naomba ya Kikwete nina hasira nae sana...
Mwanakijiji acha unazi,chanzo cha matusi kwa spika ni mkutano wa Mwembe yanga tena mtoa namba alisisita hadhara imtumie ujumbe spika.Na hizi ndio athari za jazba za siasa za kutaka sifa za kijinga majukwaani.
Insha yako sijaweza kuisoma,nitaipitia baadae.
Piga 911 halafu operator atakuunganisha na spika lakini usisahau kumwambia dhamira yako.
Watumie hata chopa kwenda kijijini kwao!! Iliyobaki wahame NCHI. mambo yamechacha!!![]()
Hivi karibuni gazeti hili liliripoti kuwa Spika Makinda amepokea ujumbe mfupi wa simu zaidi ya 400 na kupigiwa simu zinazofikia 200 za kumkashifu na vitisho.
SPIKA wa Bunge, Anne Makinda ameongezewa ulinzi pamoja na kubadilishiwa namba za gari analotumia kutokana na vitisho anavyovipata kutoka kwa wananchi ambao wamekuwa wakimtumia ujumbe wa simu.
Taarifa ambazo Mwananchi imezipata zinaeleza kuwa hatua hiyo imekuja baada ya viongozi wa Chadema kutoa namba za Spika na kuzigawa kwa wafuasi wake waliofika kwenye mkutano uliofanyika kwenye Viwanja vya Mwembe Yanga, jijini Dar es Salaam hivi karibuni ili wamtumie ujumbe mfupi wa simu.
Hivi karibuni gazeti hili liliripoti kuwa Spika Makinda amepokea ujumbe mfupi wa simu zaidi ya 400 na kupigiwa simu zinazofikia 200 za kumkashifu na vitisho.
Taarifa zilizopatikana jana zinaeleza kuwa Spika Makinda amekuwa akitumiwa ujumbe mfupi wa vitisho ambavyo inaonyesha kuwa wananchi wana hasira naye na ndiyo maana ameongezewa ulinzi.
Vyanzo vyetu vya habari vimeeleza kuwa gari la Spika Makinda limebadilishwa namba kwa kuondolewa herufi S ambayo humaanisha Spika na kuwekwa namba nyingine ambazo bado hazijajulikana.
"Watu wanaomtumia ‘meseji' wana hasira, wanaweza kumdhuru na ndiyo maana ameongezewa ulinzi. Hata magari yake aliyokuwa akitumia yamebadilishwa na kupewa mengine tofauti," kilieleza chanzo chetu cha habari.
Spika Makinda mwenyewe alipopigiwa simu ili kueleza kuhusu suala hilo la kuongezewa walinzi simu yake ilikuwa ikiita tu bila kupokelewa.
Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililah naye simu yake ilikuwa ikiita tu bila kupokelewa.Tangu Chadema wagawe namba hiyo baada ya kumtuhumu Spika pamoja na msaidizi wake, Job Ndugai kuwa amekuwa akipindisha kanuni wakati wa kuliongoza Bunge.
Taarifa zilieleza kuwa wamekuwa wakisumbuliwa na kutumiwa ujumbe za vitisho.Wakati hayo yakitokea, tayari Ofisi ya Bunge imesema itawachukulia hatua kali wale wote waliotumia lugha chafu kwa ujumbe mfupi ama kupiga moja kwa moja kwa Spika na Naibu wake.
Katibu Mkuu wa Bunge, Dk Kashililah juzi alisema kuwa kutoa namba si tatizo, bali kuzitumia namba hizo kinyume na taratibu ndiyo haitakiwi, jambo ambalo linaweza kusababisha baadhi yao kuchukuliwa hatua za kisheria.
"Wote waliotoa lugha za matusi kwa Spika Makinda na Naibu Ndugai watachukuliwa hatua za kisheria. Tutawatafuta kwa njia zote, hii itasaidia kuwa fundisho kwa watu wenye tabia kama hizo ambao wanapewa namba kwa manufaa ya wananchi, lakini wanazitumia kinyume chake," alionya Kashililah.
"Tutawasaka kwa kila hali, tutawabaini tu kwa kushirikiliana na idara mbalimbali ikiwemo Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na Polisi ili wachukuliwe hatua kali."
Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa Chadema, John Mnyika alipoulizwa jana kuhusu msimamo wa chama chake baada ya kutoa namba hizo kwa wananchi alisema; "Bunge halijatuuliza ila wakituuliza tutajibu."
Hawa watu wapuuzi sasa; kwani namba za Spika zilikuwa hazijulikani? MBona ni public information? Namba za Rais zinajulikana, namba za Waziri Mkuu zinajulikana; imekuwa namba za Spika? Chadema hawakutoa namba za Spika hadharani; namba hizo alizotoa yeye mwenyewe, CDM wao walizirudia tu kwenye mkutano wa hadhara; wangeweza kumwelekeza mtu aende kwenye tovuti ya Bunge au kuzitafuta kwa namna nyingine.
Kosa la wale viongozi waliotaja jamba za Spika na Naibu wake hawakuwa na ujumbe Specific wa kumwambia Spika. They should have a standard message - short, clear and pointed.
Hii number ni ya kumpa pole spika.Ina maana hii ndio namba waliyotoa pale Temeke siku ya mkutano!!!!
MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
Hii number ni ya kumpa pole spika.
Mwanakijiji acha unazi,chanzo cha matusi kwa spika ni mkutano wa Mwembe yanga tena mtoa namba alisisita hadhara imtumie ujumbe spika.Na hizi ndio athari za jazba za siasa za kutaka sifa za kijinga majukwaani.