Jiwe Linaloishi
JF-Expert Member
- May 24, 2008
- 3,736
- 2,139
Pana watu humu wanatutafutia ban kwa nguvu.
hata mi nishaliona hilo najitahidi kupunguza tempa
Pana watu humu wanatutafutia ban kwa nguvu.
wakati ukilaumu wengine kwa vitisho wakati huo huo wewe mwenyewe Dr.kashillah(wa kichina)unatoa vitisho kwa wengine Ebu waache wananchi waendelee kutoa maoni bila kujaribu kuwatisha kwani wanalipia hizo simu waache watoe mawazo yao
"Wote waliotoa lugha za matusi kwa Spika Makinda na Naibu Ndugai watachukuliwa hatua za kisheria. Tutawatafuta kwa njia zote, hii itasaidia kuwa fundisho kwa watu wenye tabia kama hizo ambao wanapewa namba kwa manufaa ya wananchi, lakini wanazitumia kinyume chake," alionya Kashililah.
"Tutawasaka kwa kila hali, tutawabaini tu kwa kushirikiliana na idara mbalimbali ikiwemo Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na Polisi ili wachukuliwe hatua kali."
Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa Chadema, John Mnyika alipoulizwa jana kuhusu msimamo wa chama chake baada ya kutoa namba hizo kwa wananchi alisema; "Bunge halijatuuliza ila wakituuliza tutajibu."
Shule bwana sasa hao wanamtumia vitisho wakati namba zao za simu wamezisajiri wakikamatwa wakabinywa korodani kwa plais wanabaki wanalia lia
Mkuu naomba ya Kikwete nina hasira nae sana...Hawa watu wapuuzi sasa; kwani namba za Spika zilikuwa hazijulikani? MBona ni public information? Namba za Rais zinajulikana, namba za Waziri Mkuu zinajulikana; imekuwa namba za Spika? Chadema hawakutoa namba za Spika hadharani; namba hizo alizotoa yeye mwenyewe, CDM wao walizirudia tu kwenye mkutano wa hadhara; wangeweza kumwelekeza mtu aende kwenye tovuti ya Bunge au kuzitafuta kwa namna nyingine.
Kosa la wale viongozi waliotaja jamba za Spika na Naibu wake hawakuwa na ujumbe Specific wa kumwambia Spika. They should have a standard message - short, clear and pointed.
Yaani kila ninapo ona vitisho hivi ndiyo naongeza kuhamasisha na kutuma sms kwa bi kiroboto...Wakiweza kufanya hilo waje watuambia kilichowashinda kukamata wale jamaa wa DR Ulimboka nini wakati namba zilitolewa na majina yalitolewa, je walikatazwa, walishindwa, au walikuwa ni wenzao??
Na je wakina lusinde wako juu ya sheria? mbona walitukana na hakukamatwa?
abadili na nyumba sasa akaishi dodoma
Shule bwana sasa hao wanamtumia vitisho wakati namba zao za simu wamezisajiri wakikamatwa wakabinywa korodani kwa plais wanabaki wanalia lia
Hawa watu wapuuzi sasa;
Chadema wanalitia gharama taifa!!!
-Wanaolitia gharama taifa ni wale wanaoshabikia elimu ya kipuuzi kwa walalahoi wao wakineemeka, tangu lini hesabu zikawa multiple choice? wewe unaridhika na mwenendo wa elimu ya tanzania kwa watanzania waleo na wale wa kesho?
-Wanaolitia gharama taifa ni wale wanaoruhusu meli zao kubeba shehena za meno ya tembo kwenda ughaibun. KINANA katibu mkuu ccm
-Wanaolitia gharama taifa ni wale wanaotafuta uraisi kwa nguvu ya udini kuwagawa watanzania, wao wakila bata ikulu-ccm na viongozi wake
-Wanaolitia gharama taifa ni wale waloshindwa kuboreha hospitali ya muhimbili na kuigeuza India ya wahindi kuwa muhimbili wanatufedhehesha sana maana walalahoi hawawezi kuenda huko wao kwao DAR muhimbili wewe unalizika na kitendo hicho cha wao kila kukicha India?
-Wanaolitia gharama taifa ni wale wanaoficha fedha za taifa uswis kwa mabilioni sisi tukiteseka na maisha magumu
.
.
.
. EPA, Richimond, twiga ndani ya ndege kuelekea arabun, mikataba ya gesi imefichwa kwa faida ya nani?..........
Tumia akili yako kuwaunganisha watanzania kudai haki zao za msingi.
Mwanakijiji acha unazi,chanzo cha matusi kwa spika ni mkutano wa Mwembe yanga tena mtoa namba alisisita hadhara imtumie ujumbe spika.Na hizi ndio athari za jazba za siasa za kutaka sifa za kijinga majukwaani.