Spika aongezewa ulinzi

Spika aongezewa ulinzi

Physical confrontation kama ipi washike mapanga? kama kuandamana wameandamana, wamehudhuria mikutano na wamechukua hatua za kidemocrasia kuelezea kutokuridhika kwao na matendo ya maspeaker ulitaka wananchi wafanye nini zaidi!

Point yangu ilikuwa ni serikali kuingia gharama za ulinzi zaidi wa Mh. Makinda for nothing kana kwamba inaweza ikatokea physical harm wakati frustration ya Watanzania ilikuwa inaishia kwenye ujumbe mdogo wa simu.
 
acha ushamba wewe! No. Za viongozi zipo kwny anuani za serikali. Na matus yatakuwa yametokana na uzembe wa spika wako na naibu wake. Mbona mrema alitoa no. Alitukanwa? Mbona rais, waziri mkuu namb zao tunazo je uliwah wasikia kuwa wanatukanwa? Hebu jiongeze kidogo
Huwezi kumuhukumu mtu kwa matusi.
 
wangemwamishia ahera kabisa wangekuwa wamesaidia kumuongezea ulinzi na kubadilisha magari bado hawajasaidia labda sana sana wanatumia kodi zetu vibaya tu. Watanzania wanahaki ya kuzungumza juu ya viongozi wao
 
Ule ulinzi wa kufungia watu njia hautoshi maana toka apate uspika amekuwa ana hofu na maisha yake kama anafanya mema amwachie Mungu atamlinda
 
Hawa watu wapuuzi sasa; kwani namba za Spika zilikuwa hazijulikani? MBona ni public information? Namba za Rais zinajulikana, namba za Waziri Mkuu zinajulikana; imekuwa namba za Spika? Chadema hawakutoa namba za Spika hadharani; namba hizo alizotoa yeye mwenyewe, CDM wao walizirudia tu kwenye mkutano wa hadhara; wangeweza kumwelekeza mtu aende kwenye tovuti ya Bunge au kuzitafuta kwa namna nyingine.

Kosa la wale viongozi waliotaja jamba za Spika na Naibu wake hawakuwa na ujumbe Specific wa kumwambia Spika. They should have a standard message - short, clear and pointed.

Huko si kutibu tatizo mkuu;
 
SPIKA wa Bunge, Anne Makinda ameongezewa ulinzi pamoja na kubadilishiwa namba za gari analotumia kutokana na vitisho anavyovipata kutoka kwa wananchi ambao wamekuwa wakimtumia ujumbe wa simu.

Taarifa ambazo Mwananchi imezipata zinaeleza kuwa hatua hiyo imekuja baada ya viongozi wa Chadema kutoa namba za Spika na kuzigawa kwa wafuasi wake waliofika kwenye mkutano uliofanyika kwenye Viwanja vya Mwembe Yanga, jijini Dar es Salaam hivi karibuni ili wamtumie ujumbe mfupi wa simu.


Hivi karibuni gazeti hili liliripoti kuwa Spika Makinda amepokea ujumbe mfupi wa simu zaidi ya 400 na kupigiwa simu zinazofikia 200 za kumkashifu na vitisho.
Taarifa zilizopatikana jana zinaeleza kuwa Spika Makinda amekuwa akitumiwa ujumbe mfupi wa vitisho ambavyo inaonyesha kuwa wananchi wana hasira naye na ndiyo maana ameongezewa ulinzi.


Vyanzo vya habari vimeeleza kuwa gari la Spika Makinda limebadilishwa namba kwa kuondolewa herufi S ambayo humaanisha Spika na kuwekwa namba nyingine ambazo bado hazijajulikana.



“Watu wanaomtumia ‘meseji’ wana hasira, wanaweza kumdhuru na ndiyo maana ameongezewa ulinzi. Hata magari yake aliyokuwa akitumia yamebadilishwa na kupewa mengine tofauti,” kilieleza chanzo chetu cha habari.


Spika Makinda mwenyewe alipopigiwa simu ili kueleza kuhusu suala hilo la kuongezewa walinzi simu yake ilikuwa ikiita tu bila kupokelewa.


Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililah naye simu yake ilikuwa ikiita tu bila kupokelewa.Tangu Chadema wagawe namba hiyo baada ya kumtuhumu Spika pamoja na msaidizi wake, Job Ndugai kuwa amekuwa akipindisha kanuni wakati wa kuliongoza Bunge.


Taarifa zilieleza kuwa wamekuwa wakisumbuliwa na kutumiwa ujumbe za vitisho.Wakati hayo yakitokea, tayari Ofisi ya Bunge imesema itawachukulia hatua kali wale wote waliotumia lugha chafu kwa ujumbe mfupi ama kupiga moja kwa moja kwa Spika na Naibu wake.


Katibu Mkuu wa Bunge, Dk Kashililah juzi alisema kuwa kutoa namba si tatizo, bali kuzitumia namba hizo kinyume na taratibu ndiyo haitakiwi, jambo ambalo linaweza kusababisha baadhi yao kuchukuliwa hatua za kisheria.


“Wote waliotoa lugha za matusi kwa Spika Makinda na Naibu Ndugai watachukuliwa hatua za kisheria. Tutawatafuta kwa njia zote, hii itasaidia kuwa fundisho kwa watu wenye tabia kama hizo ambao wanapewa namba kwa manufaa ya wananchi, lakini wanazitumia kinyume chake,” alionya Kashililah.


“Tutawasaka kwa kila hali, tutawabaini tu kwa kushirikiliana na idara mbalimbali ikiwemo Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na Polisi ili wachukuliwe hatua kali.”
Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa Chadema, John Mnyika alipoulizwa jana kuhusu msimamo wa chama chake baada ya kutoa namba hizo kwa wananchi alisema; “Bunge halijatuuliza ila wakituuliza tutajibu.”
Source: Mwananchi Jumapili 17/02/2013.
 
CHADEMA kutoa namba za Spika si jambo baya, lakini hao wanaotumia vibaya hiyo namba ndio tatizo.
 
Inamaana kwa sasa spika anaishi kwa kujificha kama digidigi?
 
Hiv ni lini serikali zetu zitajifunza kutafuta kiini cha tatizo ktk kutatua migogoro inayozikabili. Matukio kadhaa ya Mh Makinda na msaidizi wake yameonesha kutokiweza kiti kile. Lakini hata kama wangeliweza-post zao ni kisiasa-sms zaidi ya 400 ni ujumbe tosha pande zote mbili serikali na waheshimiwa kutambua hasira ya wananchi zidi yao.

Cha msingi si kuongeza ulinzi kwa makinda, nikuangalia kwa nini hasira hizi-a very simple qn 'are we in the right way'? Kama jibu ni hapa, please fanya masahihisho.

Kwa migogoro kama hii serikali haiwezi kulinda kila kiongozi wa nchi hii kwa wakati wote na kila mahali. Nafasi za kisiasa ni nzuri- na uzuri wake utokana na ualali wa watu wenyewe.
 
Mwanakijiji acha unazi,chanzo cha matusi kwa spika ni mkutano wa Mwembe yanga tena mtoa namba alisisita hadhara imtumie ujumbe spika.Na hizi ndio athari za jazba za siasa za kutaka sifa za kijinga majukwaani.

Mkuu ungemalizia hapo kwenye wekundu.
Ni ujumbe gani mtoa namba za simu alisisitiza atumiwe mhe. Spika?
 
Mkuu ungemalizia hapo kwenye wekundu.
Ni ujumbe gani mtoa namba za simu alisisitiza atumiwe mhe. Spika?
Ninatoa maoni kwa wale wenye uelewa na kujua kilichotoke mwembe yanga,kama hukuwepo au haujui kilichosemwa wewe baki kuwa mtazamaji au tafuta muda wako kujua.
 
Ninatoa maoni kwa wale wenye uelewa na kujua kilichotoke mwembe yanga,kama hukuwepo au haujui kilichosemwa wewe baki kuwa mtazamaji au tafuta muda wako kujua.

Mkuu, kama huna hoja humu si mahala pako. Weka kila kitu wazi watu wakupime na kukujadili kwa unavyojieleza.
 
kati ya mwanakijij na wewe mingoi nani mnazi???
Mwanakijiji acha unazi,chanzo cha matusi kwa spika ni mkutano wa Mwembe yanga tena mtoa namba alisisita hadhara imtumie ujumbe spika.Na hizi ndio athari za jazba za siasa za kutaka sifa za kijinga majukwaani.
 
Watumishi wa Mungu wametishiwa maisha na ambao walituzunga huu utawala ni wa kutoka juu, hawawekewi ulinzi.
 
Wamlinde kwa chopa kama wataona inafaa!sasa kama wananchi unaojidai uwawakilisha wanakuwinda mpaka inafikia kujificha kiasi hicho kuna maana gani?Mwakilishi wa Wananchi mlinzi pekee ni wananchi wenyewe.
 
Back
Top Bottom