Special Thread: Ya kale ni dhahabu

Hance Mtanashati

JF-Expert Member
Sep 7, 2016
17,463
21,180
Huu ni uzi maalumu unaojumuisha maisha yote ya kale tuliyoyaisha ,mashujaa wetu wa enzi hizo visa vyao na burudani kwa ujumla.


Karibuni .


1694607575585.jpg
 
MZEE MORRIS NYUNYUSA WA NGOMA ZILE ZA Redio Tanzania Dar es Salaam (RTD)

Kwa miaka mingi tulikuwa tunasikia midundo ya ngoma kuashiria kuanza kwa taarifa ya habari kwenye redio ya Taifa RTD na baadae TBC.

Ilikuwa ni midundo maarufu sana na yeyote aliyeisikia hata kwa mbali alijua wazi huu ni wakati wa taarifa ya habari, ila kwa majonzi makubwa midundo hii haipo tena huko TBC.

Midundo hii ni ufundi wa Mzee Morris Nyunyusa mlemavu wa macho aliyekuwa na kipaji cha ajabu cha kupiga ngoma 17 kwa wakati mmoja, na midundo hii ilihusisha ngoma zote hizi.

Umahiri wake huu ulimfanya ajulikane ndani na nje ya nchi huku akipata mialiko mingi tu!, ikiwamo ziara mojawapo aliyowahi kuifanya nchini JAPAN ambapo alipewa mualiko nchini humo. Katika ziara hiyo Mzee Morris aligeuka kuwa kivutio kikubwa mno kwa maonyesho hayo, hata kumfanya mwanamziki nguli bwana Mbaraka Mwinshehe kumtungia wimbo mzee huyu juu ya umahiri aliouonyesha katika tamasha hilo.

Hakika mzee huyu likuwa kivutio cha wageni mbalimbali kutoka mabara mbalimbali, pindi walipokuja nchini kwetu walikuwa wakipata shauku ya kutamani kukumbana na huduma yake ya kipekee ya Mzee huyu mwenye upofu wa macho.

Mzee huyu ambaye kwa sasa ameshafariki tayari, alikuwa ni tunu ya Taifa kwenye sanaa. Ni miaka mingi imepita hakumbukwi popote hata pengine kwenye vyuo vyetu vya sanaa.

natamani hili litokee kizazi cha leo wala hakimjui lakini wakati ule picha zake ziliwekwa mpaka kwenye stamp.

1694376388368.jpg
 
MABIBI WA ZAMANI WALIKUWA SIO WACHOYO...WALIKUWA WANATUPENDA KUTOKA MOYONI!! HAPO NI MDA WA KULA UGALI...ILIKUWA KILA MTOTO NA BAKULI LAKE LA MBOGA.


1694687311515.jpg
 
1694687825235.jpg



Kwa faida ya vijana wetu wa kizazi cha amapiano, hiyo Celtel ilibadilishwa jina na kuitwa Zain mwaka 2007 au 2008 kama sikosei haikudumu sana ikabadilishwa tena jina na kuitwa Airtel ambayo jina hilo linatumika mpaka sasa.

Tigo Zamani ilikuwa inaitwa Buzz (Buzz ni bombaaaa) kwa Sasa inaitwa Tigo.

Vodacom ni Vodacom
 
Je uliwahi kuangalia sinema kwenye kumbi hizi?
Kumbi zilizopendwa zaidi ni
EMPIRE Cinema. (Masela na watoto wa mjini)
AVALON na Empress Cinema. ( Washua )
Drive in Cinema. Wote walioamua kuingia na magari yao
CAMEO:- Picha za Kihindi tu...
IMG_1693114685014.jpg
 
Picha hii imepigwa mwaka 1926 ni tukio la kuinuliwa kwa Meli ya MV Liemba baada ya kuzamishwa.

Mandhari kwenye bandari ya Kigoma (1926) - MV LIEMBA (meli ya Ujerumani) iliyozama wakati wa vita yainuliwa kutoka ziwani mwaka 1926

Ilianza kutumika kutoa huduma kama chombo cha usafiri mwaka 1927



1694724286557.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom