Kipanya yupo sahihi.
Ni mangapi yametokea na hakuna record tena? Kila week kuna jipya na tukio moja hufuta jingine.
Hivi Media Houses, New Papers dealers,
Hamuwezi kuanzisha jarida maalum litakalo kuwa linafuatilia kwa karibu kwa kufanya uchunguzi wa kitaaluma na wa kina kwa matukio makubwa yanayotokea nchini?
Natamani kuona gazeti kama hili litakalo kuwa na watu wa taaluma tofauti MAHILI {waandishi wa habari na wahariri, wanasheria, wachumi, wahandisi (fani zote), madaktari wa tabibu, IT, private i
nvestigators (polisi wastaafu na watu binafsi), watalaam wa michezo}....
Chombo hiki kinaweza kujipanga kutoa taarifa kwa umma mara moja kwa mwezi au kila baada ya miezi mitatu kikianisha ni hatua zipi zilizochukuliwa na kutekelezwa kwa kiwango gani.
Manufaa ya kuwepo chombo hiki
1. Kuchunguza kwa kina na kupata ukweli halisi wa tukio husika
2. Kupendekeza njia sahihi kuepuka jambo kama hilo kutokea tena ama kama ni tukio jema basi kupendekeza njia nzuri Zaidi kuboresha ufanisi
3. Kufuatilia wahusika wote na kuhakikisha wametekeleza wajibu wao kwa wakati kulingana na mapendekezo kuepuka utokeaji wa jambo kama hilo kwa siku za baadaye (corrective actions)
4. Kutunza kumbu kumbu ili jambo lisisahaulike
5. Kuwepo kwa chombo hiki kutasaidia intelijensia au makundi yasiyo julikana kuunda matukio yasiyo na tija kwa maslahi ya Taifa. Makundi maalum huanzisha mijadala kufunika mambo mengine ili yasahaulike.
Watalaam mlione hili na mlifanyie kazi, chombo hiki kitasaidia sana nchi.