Nimeshuhudia AFCON nyingi ila hii ni Kali sana, imejaa ufundi mwingi sana. Michuano hii ina top players wengi wanaocheza vilabu vikubwa barani Ulaya na wanaanza kwenye first eleven ya vilabu vyao. Jambo zuri ni kwamba wanacheza kwa kujituma sana tofauti na AFCON 2023 iliyopita haikua na mvuto sana, wachezaji hawakucheza kwa intensity ya juu wakihofia kupata majeraha hata mechi nyingi ziliisha kwa sare ya bao Moja au bila kufungana.
Bingwa wa hii michuano atatoka kwenye mechi ya Nigeria vs Morocco. Hizi ndio timu zenye ufundi wa hali ya juu sana kwenye hii michuano.