Kuelekea uchaguzi wa UWT: Bi Anne Kilango Malecela achafuliwa na wapinzani wake... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuelekea uchaguzi wa UWT: Bi Anne Kilango Malecela achafuliwa na wapinzani wake...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by only83, Aug 6, 2012.

 1. only83

  only83 JF-Expert Member

  #1
  Aug 6, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 444
  Trophy Points: 180
  ....Katika kile kinachoonekana kama ni kuanza kwa mbio za uenyekiti wa UWT kati ya wagombea wakubwa wawili yaani Bi Anne Kilango na Bi Sophia Simba hali imeanza kuwa mbaya kwa Bi Anne Kilango. Taarifa zilizotoka leo zinadai kuwa Bi Anne Kilango amekusanya ameanza rafu kwa kukusanya pesa kiwango kikubwa kwa ajili ya kugawa takrima aka rushwa. Na fununu zinasema kuwa wanaume wengi wako nyuma yake kuliko hata wanawake na lengo ni kuhakikisha kuwa Bi Sophia Simba anang'olewa kwenye kiti kile.

  ....Itakumbukwa kuwa ugomvi na kusuguana kwa hawa wagombea wawili akujaanza leo wala jana, kumeanza tangu ambapo Bi Sophia Simba alipomtaja Bi Anne Kilango kama mchangiaji anayeropoka na anajifanya anatetea maslahi ya umma wakati harusi yake na Mzee Malecela ilichangiwa na mafisadi wakubwa. Hoja hii ilimfanya Mzee Malecela asimame na kuomba kuwa kuna wabunge wanapaswa wapelekwe mirembe akimlenge Bi Sophia Simba.

  Source: Magazeti ya leo.

  Habari zaidi:-

   
 2. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #2
  Aug 6, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  kwani ni uongo? na sasa hivi anatuhumiwa na kuomba rushwa, Anna Kilango ni fisadi hana jipya anyway magamba mtajiju!
   
 3. K

  KANA KA NSUNGU J Member

  #3
  Aug 6, 2012
  Joined: Jul 18, 2012
  Messages: 23
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Naya ! Yangu macho.Nasikiliza mie
   
 4. Ston Merchant

  Ston Merchant JF-Expert Member

  #4
  Aug 6, 2012
  Joined: Aug 1, 2011
  Messages: 395
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  ww mtoa mada unaonekana kbs ni mpambe wa Sophia Simba na umetumwa hpa...........

  wte ni magamba tu.............. simba + kilango = zero
   
 5. M

  MIGNON JF-Expert Member

  #5
  Aug 6, 2012
  Joined: Nov 23, 2009
  Messages: 2,586
  Likes Received: 1,562
  Trophy Points: 280
  Sophia Simba alitumia vibaya nafasi yake alipokuwa waziri anayehusika na mambo ya usalama.Alipitia mafaili na kapata nyepesi nyepesi za Malecela na kama kawaida ya wanawake wa Uswahilini alipoguswa kidogo akaropoka.
   
 6. peri

  peri JF-Expert Member

  #6
  Aug 6, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 2,588
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  ndio siasa ilivyo, full kuchafuana mpaka mambo ya ndani.
   
 7. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #7
  Aug 6, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  ee mungu wa mbinguni tunaomba usambaratishe wanafiki wanaoiharibu nchi hii.
   
 8. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #8
  Aug 6, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  pwagu na pwaguzi
   
 9. Kasimba G

  Kasimba G JF-Expert Member

  #9
  Aug 6, 2012
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,568
  Likes Received: 568
  Trophy Points: 280
  Angel msofe niko pamoja na wewe pwagu na pwaguzi! Woote uozo mtupu, sera yao kubwa inajurikana ni rushwa kwenda mbele!
   
 10. KIJOME

  KIJOME JF-Expert Member

  #10
  Aug 6, 2012
  Joined: Jun 7, 2012
  Messages: 3,079
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Wanajuana hawa wote mafisadi tu hakuna wa kumfunga paka kengele...wezi wakubwa.
   
 11. Ufunuo

  Ufunuo JF-Expert Member

  #11
  Aug 6, 2012
  Joined: Jun 6, 2011
  Messages: 566
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  ya ngoswe mwachie ngoswe.
   
 12. b

  busar JF-Expert Member

  #12
  Aug 6, 2012
  Joined: Dec 22, 2011
  Messages: 501
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
  Kuna rushwa ya Ngono nini huko?
   
 13. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #13
  Aug 6, 2012
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Mmoja ni afadhali na mwingine ni potelea mbali. Watachagua wenyewe magamba yupi afadhali na yupi potelea mbali.
   
 14. S

  SUWI JF-Expert Member

  #14
  Aug 6, 2012
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 548
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Hata kama atakuwa mpambe au la, ukweli ndo huo.. Anne Kilango alikuwa anabwabwaja mwanzoni tukadhani mkombozi kumbe zilikuwa hasira za mumewe kukosa uteuzi wa ubunge nk.... alikuwa anapigania maslahi binafsi... sasa hivi ameshashtukiwa!!! hafai hana uzalendo wowote.. anapigania vya tumbo lake tu!!
   
 15. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #15
  Aug 6, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  si kilango tu,hata yule mzee wa RIPOT YA RICHMOND NA OLE S
   
 16. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #16
  Aug 6, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Swali kwa wafurukutwa wa ccm, hivi huko uwt hakuna mwanamke mwingine mnayeweza kumpatia uenyekiti zaidi ya hawa waganga njaa??
  au ndio aina ya wanawake mlionao ndani ya chama chenu, kwahiyo wote wanafanana tabia na mienendo yao?
   
 17. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #17
  Aug 6, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Mzee wa Rula sidhani kama kuna afadhali hapo, wote ni potelea mbali, tena huenda ikawa ni potelea mbali sana!!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 18. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #18
  Aug 6, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Mzee wa Rula sidhani kama kuna afadhali hapo, wote ni potelea mbali, tena huenda ikawa ni potelea mbali sana!!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 19. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #19
  Aug 6, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  kama Anne kilango na Sophia Simba tunaona hawatoshi kwa nini tusimjadili zaidi yule wa tatu nadhani anaitwa MaryRose aliletwa hapa na PASCO? ndio njia pekee ambayo itatusaidia kuwajua wagombea wote na kisha kuchagua iliye bora.

  hakuna jambo baya kuelekea kwenye uchaguzi kama kutumia muda mwingi kujadili wagombea wasiotosha na kuwasahua wanaotosha.
   
 20. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #20
  Aug 6, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  [h=2][/h]JUMATATU, AGOSTI 06, 2012 05:48 NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM

  WAKATI mbio za kuwania nafasi mbalimbali zikiendelea ndani ya Chama Cha Mapinduzi, hali ya mambo imeanza kubadilika. Kubadilika huko, kumeibuka ndani ya Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), ambapo mmoja wa wagombea wa nafasi ya Mwenyekiti na Mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango baada ya kudaiwa kupewa kitita cha fedha na kampuni moja ya Kichina (jina tunalo).

  Kampuni hiyo, ujenzi wa gati katika Bandari ya Dar es Salaam, inadaiwa kutoa kitita cha fedha, ili kuhakikisha Kilango, ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Miundombinu ya Bunge, anachaguliwa katika kwenye nafasi hiyo.

  Kilango, ambaye hivi sasa amechukua fomu ya kuwania nafasi kwa ajili ya kugombea nafasi ya uenyekiti UWT), anatarajiwa kupambana na mwenyekiti wa sasa, Sophia Simba.

  Kila mmoja wa wabunge ambao, wanasifika kwa kujipambanua kama wabunge wanapinga ufisadi ndani na nje ya Bunge.

  Habari za kuamini zilizoifikia MTANZANIA, zinasema Kilango alianza kazi ya kuwafikia baadhi ya makatibu wa mikoa wa UWT na kuanza kuwashawi, ili wamchague katika nafasi ya Uenyekiti kwa ahadi ya kuondoa ukomo kwa wabunge wa Viti Maalum kupitia CCM.

  Chanzo hicho, kinasema baadhi ya makatibu wa mikoa ambao hakuwafikia alilazimika kuwapigia simu, ili wamuunge mkono, huku wale wote waliogoma kufanya hivyo, alitumia lugha kali.

  Baadhi ya makatibu hao, waliiambia MTANZANIA na walikiri kupokea fedha kutoka kwa mbunge huyo, kama njia ya ushawishi katika harakati za kuwania nafasi hiyo.

  Taarifa hizo, zinasema nguvu ya fedha ilianza kuonekana Machi 13-14 mkoani Dodoma, baada ya kuandaa semina kwa kukusanya wenyeviti wa wilaya na mikoa, waliokuwa wakihudhuria semina elekezi, kuelekea uchaguzi wa ndani na nafasi ya mwanamke katika kuwania uongozi.

  Katika semina hiyo, inadaiwa mbunge huyo, alitumia nafasi hiyo hasa muda wa jioni kufanya ushawishi kwa viongozi wa mikoa na kuwataka kumchagua.

  Viongozi hao, walisema wakati wa semina hiyo, Kilango alitumia nafasi hiyo na kueleza dhamira yake, huku akitoa vitisho hasa kwa watu wanaodaiwa kupewa Sh 30,000, kwa kila mmoja.

  “Nguvu, aliyonayo mama Kilango, hivi sasa naye ni mmoja wa watu waliopata fedha kutoka kwa kampuni ya Kichina na baada ya kupata alianza kufanya ushawishi kwa wanawake wa UWT, hasa makatibu wa mikoa, lakini hivi sasa tutaona mwisho wake nini.

  “Katika kikao cha Dodoma, nakumbuka tulikusanywa usiku na kupelekwa katika Hoteli ya Fity Six, iliyopo jirani na jengo la Bunge, na kuanza kutupatia kitu kidogo… baada ya hapo alituambia hela ya Mpare haiendi bure na kama ukiichukua na ukienda kinyume utakufa, tena akisema atatulisha yamini wote aliotupa fedha.

  “Alisema Sophia Simba, hatakiwi na wabunge wanawake wa CCM, viongozi wa taifa na hata Rais nae hamtaki, hivyo achaguliwe yeye, kwani ana ushawishi ndani ya Kamati Kuu ya CCM (CC), na amekuwa akiungwa mkono na viongozi wote wa taifa,” kilisema chanzo chetu.

  MTANZANI ilipomtafuta Kilango, ili kupata ukweli juu ya tuhuma hizo, alimtaka mwandishi wa habari hizi kuandika chochote anachokijua dhidi yake.

  Mahojiano kati ya MTANZANIA na mbunge Kilango, yalikuwa kama ifuatavyo;

  MTANZANIA: Habari mama Kilango na pole na majukumu.

  Kilango: asante na nani mwenzangu.

  MTANZANI: ninaitwa …. kubwa nilitaka kufahamu ukweli juu ya tuhuma zinazokukabili kuhusu madai ya kupewa hongo na kampuni moja ya Kichina (jina tunalo), je suala hili lina ukweli wowote?

  Kilango: kijana nasema hivi, andika habari zote kama ulivyosikia, ili Watanzania wajue uchafu wangu,” alisema Kilango na kukata simu.


   
Loading...