Soon nakuwa mama wa kambo. Nahitaji maombi yenu na ushauri wa maisha haya mapya

mimi sio mwanamke, tofautisha mwanaume na mwanamke, hatupo sawa na hatutakuja kuwa sawa. watoto wangu nikiamua ataishi nao, wakwake labda kama niliwakuta.
Hehe unaamuaje na ushasema wife hataki umlete?
Ama
Mkuki kwa nguruwe sio lol😅
 
Nampenda sana mama yangu japo si wa kunizaa.
Baba angu aliniiba kwa mama yangu mzazi nikiwa na miezi mi 3 tu duniani akanileta kulelewa kwa huyu mama ambae ndio mkewe wa ndoa.nikawa mtoto wake wa 5.Namkubali sana lich ya mapungufu yake ambayo wengine huwa wanalazimisha niyaone ila hata siyaonagi
Kwanini alikuuiba kwa mama yako ilihali ulikuwa mchanga kabisa
 
Kwani bond yako na baba ake uliipataje? na mlikutana ukubwani?

Au kwa vile ana hela?
 
Kwanini alikuuiba kwa mama yako ilihali ulikuwa mchanga kabisa
My mother alikua mchepuko tu na mzee alikua kaoa tayar na ana watoto wa 4 mpaka wakat huo.So hakukua na namna na yeye hakua tayar kuwa na family 2 apart so akatengeneza zengwe.Ofcz ilikua sio kirahis cz mama alikua mtata na anajimudu kivyote na mzee alikua alwatan kidogo..Ni story ndefu kidogo
 
My mother alikua mchepuko tu na mzee alikua kaoa tayar na ana watoto wa 4 mpaka wakat huo.So hakukua na namna na yeye hakua tayar kuwa na family 2 apart so akatengeneza zengwe.Ofcz ilikua sio kirahis cz mama alikua mtata na anajimudu kivyote na mzee alikua alwatan kidogo..Ni story ndefu kidogo
Thanks
 
Kuletewa mtoto ambaye ulimkuta umleee sidhani kama ni changamoto sababu tayari ulishapewa taarifa kuwa kuna mtoto.

Bond inatengenezwa kwa upendo haijalishi umewahi kuishi nae au laaa. Akija mleee sawa sawa na watoto wako na watoto wako wakiona unawatreat na wao itakuwa rahisi kujifunza upendo.
Kila la kheri kuwa mama mzuri,,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nawasalimu wote.

Kama mada inavyojieleza.

Mume wangu amenitaarifu anamleta rasmi mtoto wake ambae alikuwa haishi na sisi kuja kuishi na sisi. Wakati nasubiri siku ifike lazma nijiandae.i. Sina bond nae wala mazoea nae zaidi ya kumuona hiyo mara chache na sio kwamba alikuja nyumbani.

Awali ya yote sikuwahi kuwaza kuwa mama wa kambo katika maisha yangu. Dakika za mwisho kabla ya kuingia kwenye ndoa nikapewa hizo habari na nilipoambiwa mtoto hakuletwa immediately kuishi na sisi na sikujua kwanini haikuwa hivyo. Pamepita miaka mingi ndiyo analetwa.

Nifanye maandalizi yapi kisaikolojia, kimalezi nk maana nimezoea kuishi na wanangu tu na watu wanajua nina watoto hao tu. Simchukii wala nini hata shopping nimefanya sana tu kwa ajili yake ila hakuwahi kuja nyumbani hata siku moja. Kwa mimi ingekuwa better off angeletwa mapema kabisa kuliko sasa ambapo bond nae sina na wanangu nao hawana bond nae na ni mwaka huu tu wameambiwa ni ndugu yao wa damu wakashangaa mbona hawakuambiwa jambo hilo rasmi japo waliwahi muona mara 2.

Yaani waliambiwa huyu ndugu yenu lakini kivipi hawakuambiwa. Sasa mwenzangu sikujua kwanini ame act that way kutuweka mbali nae. Kwangu huenda angeletwa mapema ingekuwa bora zaidi. Bonding inakuwa easy lakini pia hata malezi angekua kulingana na aina ya malezi ambayo mimi na mwenzangu tunatoa. Babake mwenyewe hata bond nae pia siioni japo matunzo anatoa perhaps hii nayo imechangiwa na kwamba ana doubts zake ambazo amekuwa nazo kwa miaka mingi sana mpaka kusema atampima DNA ila hakuwahi kupima na miaka imeenda now sidhani kama anaona haja ya kumpima tena after all amekuwa akitoa matunzo na kusomesha.

Perhaps na yeye anatakiwa kujiandaa kisaikolojia sijui maana naonaga tu kama hajamu accept fully ila tu afanyeje maana wakati mwingine anasema hafanani nae hata kitu kimoja. Wenye uzoefu dondosheni mawili matatu kwa ajili ya hili jambo.

Natanguliza shukrani!
Tatizo lako LA kwanza ni hapo unapoanza kujiita mama wa kambo,yani hadi hapo umeshaanza kujitenga nae,na kujitofautisha nae,ww ni mama yake,usijiite mama wa kambo utakua unazidi kujiweka mbali nae,bora ujiite mama mlezi lkn sio mama wa kambo.utajisikiaje ukiolewa mahali then mumeo ajiite baba wa kambo kwa mwanao?.....japo kweli ni baba wa kambo kwa kiswahili fasaha lkn neno lenyewe hilo sio tamu masikioni.muite mwanao inatosha,na ujitambulishe kuwa ni mama yake,hata mbele za watu nae akiwepo na akisikia jitambulishe kuwa ww ni mama yake,hio itampa confidence zaidi na kujiamini na usishangae nae atakutambulisha kwa wenzake kuwa ww ni mama yake na hataweza kusema kuwa ww ni mama yake wa kambo,mlee vizuri sana,mpende zaidi ya wanao wa kuwazaa maana mwanao tayari mnaunganishwa na damu ila huyo utajiunganisha nae kwa upendo uliopitiliza,hujui pengine ndio atakua mhimili wako baadae ukizeeka,tumeshaona wazee wengi wakitelekezwa na watoto wao wa damu na kusaidiwa na wengine,kwaiyo usimpuuze kbs kisa na ww umezaa watt wako,wtt wenyewe hawa wa cku hizi wanatukana hadi wazazi.nakusihi mpende sana,MPE malezi bora,usimtenge wala kumnyanyasa,ww ndio uwe mtetezi wake hata pale baba yake mzazi anapomfokea na kumgombeza,..ukifanya hivyo nakuapia mbele za Mungu atakufaa sana cku moja,tena atakufaa kuliko uzao wa tumbo lako.tatizo moja nililoligundua kwako ni kwamba nafsi yako haipo tayari kuishi nae,na hapo unajilazimisha na kujibaraguza hadi kuja kuomba ushauri kwakua tu huna LA kufanya na huwezi kumwambia mumeo kuwa humtaki,laiti ungeweza kuwa na sauti ya kusema humtaki basi ungefanya hivyo ila unakuja kujitia huruma hapa na kujionyesha kuwa hana ubaya nae lkn trust me,...una roho ya kibaguzi na uchoyo km sio roho mbaya kabisa.maisha ya dunia ni haya haya tu
 
nina mtoto wa kambo, wife hataki nimlete. hiyo imeniletea shida sana kwasababu inabidi mara nyingi niwe nawasiliana na mama wa mtoto huyo na kujikuta tumesharudisha majeshi hadi kuogopa kupata mtoto mwingine wa pili. ila angekubali kuishi nami hiyo chain angeshaikata. wanawake kuweni na akili, kuna vitu vingine sio lazima uende shule cha pili, nakushauri usije kumtesa, utafungwa, pia usimbague kwasababu hata ufanyeje watoto wako wanajua hiyo ni damu yao wakiwa wazima utajikuta umelaumiwa, pia watoto wote wa kambo wanaoishi kwa kuteswa na mama wa kambo huwa wanafanikiwa kimaisha kuliko watoto wa ndani ya ndoa. amini usiamini.
Acha Umalaya.
 
Mkeo anakosea sana; ila wewe usitafute justification ya kulala na mzazi mwenzio kisa mawasiliano ya mtoto. Kama bado mnatakana, hata huyo mtoto akija kuishi na mkeo bado mtaendelea kupasha kiporo na huyo baby momma wako. Na kwa nini mliachana kama bado mnatakana? Kwa nini mkeo anamkataa mtoto, subiri agundue mnapasha kiporo, utaenjoy show
Umeona ni umalaya tuu.
 
Back
Top Bottom