SIMULIZI: Safari ya maisha na mikasa mizito ya Msanii Afande Sele

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,118
Sikumfahamu, nilimuona ni mwanamke tu amekaa sebuleni, nilimsalimia na kuendelea na shughuli zangu naye aliniangalia bila kusema chochote, hivyo ndivyo nilivyokutana na mama yangu mzazi kwa mara ya kwanza,” anaanza kusimulia Afande Sele katika mahojiano maalumu na gazeti hili akiwa nyumbani kwake kata ya Mazimbu, mjini Morogoro.

Afande Sele, ambaye jina lake halisi ni Seleman Msindi, kwa hisia kali zenye maumivu anakumbuka namna alivyojilea mtaani, akiwa na umri mdogo akipambana na changamoto za dunia kabla ya mafanikio yake kufunguka kupitia kipaji chake cha muziki hadi kuwa mfalme wa Rhymes 2004.

“Yalikuwa ni maisha mabaya sana kwangu, japo kuna wakati huwa nahisi yalinitokea kwa sababu, labda Mwenyezi Mungu alikuwa na mipango haya yanitokee,” anasema Afande Sele.

Staa huyo wa Bongofleva na baba wa watoto wawili, Tundajema na Asantesanaa, mabinti aliolazimika kuwalea mwenyewe baada ya kifo cha mkewe, Asha (Mama Tunda), kilichotokea miaka tisa iliyopita anasema alipambana ili binti zake hao wasije kuishi maisha kama aliyopitia yeye.

“Tulikuwa na malengo mengi sana na Mama Tunda, nakumbuka Mwenyezi Mungu alipomchukua, Tunda alikuwa kidato cha pili na Asantesanaa alikuwa na mwaka mmoja na miezi kadhaa, sikufahamu nitawalea vipi hawa binti zangu, lakini nilisema sitoruhusu wapitie maisha kama yangu,” anasimulia.

Safari ngumu ya makuzi yake

Anasema baba yake alifariki akiwa na miaka minne, hakuwa akifahamu chochote kuhusu kifo na hakuna ndugu upande wa mama yake mzazi wala mama yake aliyehudhuria mazishi ya baba yake, hawakujua anaishi vipi baada ya kifo cha baba yake.

“Mama na baba walitengana nikiwa mdogo, mama akaenda kuanzisha maisha mengine, sikuwa na kumbukumbu hata na sura ya mama yangu, hata alipofariki baba, mama na ndugu zake hawakuja kwenye msiba.

“Kwa baba yangu nilizaliwa peke yangu, sikuwa na kaka wala dada, kwa kuwa nilikuwa mdogo, nikalazimika kulelewa na mashangazi.

“Nikiwa na umri mdogo, kuna shangazi yangu mmoja ambaye yeye ndiye alijimilikisha mali za familia, aliniambia mama yangu ameshafariki, kwa umri wangu wakati huo sikuwa hata na uwezo wa kusema niende nikatafute kaburi alipozikwa,” anasimulia Afande Sele.

Baada ya kifo cha baba, Afande Sele anasema maisha yalianza kuwa magumu kwake, licha ya kuachwa kwa shangazi yake, lakini hakupata uangalizi wowote wa malezi kama ilivyo kwa watoto wengine.

“Nilijilea mwenyewe, sikuwa na mtu japo hata wa kufuatilia mwenendo wangu shuleni, nikienda sawa, nisipokwenda pia ni sawa, ilikuwa ni juu yangu, hakuna aliyejali nimekula au la, kulala pia ilikuwa ni kwa shida sana,” anasema Afande Sele na kuongeza;

“Nikalazimika katika umri mdogo kuanza kujilea mwenyewe, kuanzia niko darasa la kwanza hadi nafika la sita, sikuwahi kuwa na uangalizi kama watoto wengine, hata kula yangu ilikuwa ni juu yangu mwenyewe.

“Niliishi kupitia shamba ambalo liliachwa na babu na baba yangu kule Kichangani. Mzee alikuwa na eneo kubwa ambalo alipanda miti mingi sana ya matunda, kulikuwa na miembe zaidi ya 40, michungwa, michenza na matunda mengine mengi, mbogamboga na mazao mengine,” anasema.

Anasema shamba lile ndilo lilimlea, kwani alipokuwa akihisi njaa, alikwenda shambani na kukwanyua ndizi na kuzichemsha kwa chumvi na kula, au atachuma mchicha pori na kupika na chumvi kwa kutumia kuni alizookota humohumo shambani kwao, hivyo alianza kujipikia akiwa darasa la kwanza.

“Nikihitaji kitu cha shule, nitaingia shambani, nitaangua matunda yatakayokuwepo kwa wakati huo na kwenda kuuza, shuleni nilikuwa maarufu kwa kuwauzia walimu maembe, machungwa, nazi na mazao mengine.

“Jirani na kwetu kulikuwa na stesheni, hivyo wakati mwingine jioni nakwenda kuuza matunda pale stesheni kwa abiria wanaosafiri na treni na kupata pesa ya kujikimu.

“Nilikuwa na umri mdogo, lakini sikuwa na uangalizi wa mlezi yeyote, niliishi maisha ya mtaani, hakuna aliyejali kuhusu mimi, hata shangazi ambaye ndiye alijimilikisha kunilea hakuwa na muda na mimi,” anasema.

Aambiwa mama alikufa.

Afande Sele anasema kuna siku alimuuliza shangazi yake kuhusu mama yake baada ya kuona kila kitu kinakuwa kigumu kwenye maisha yake.

“Alinijibu, mama yako alikufa siku nyingi, kwa kuwa nilikuwa mdogo na hata sikuwahi kufahamu kuhusu yeye, niliamini ni kweli amefariki dunia na nikaendelea na maisha mengine nikiwa nimekata tamaa, nikiamini wazazi wangu wote wamefariki japo kwa mama sikuwahi kuliona hata kaburi lake,” anasema.

Anakumbuka akiwa ndio ameingia darasa la saba, siku hiyo nyumbani kwao walitembelewa na mgeni, ambaye alizungumza na shangazi yake kisha akaitwa.

“Yule mgeni mbele ya shangazi aliniambia yeye ni mjomba wangu, akitoka kuzaliwa mama yangu anafuata yeye, amehamishiwa kikazi hapa Morogoro. Aliniambia katumwa na mama yangu aje anitafute, pale Kichangani ukoo wetu ulikuwa ni maarufu, hivyo hakupata tabu kufika kwa maelekezo ya dada yake (mama yake Sele) aliyewahi kuishi kule kabla ya kutengana na baba nikiwa mdogo sana.

“Siku hiyo ilikuwa ni mshangao, tena mbele ya shangazi yangu yuleyule aliyeniambia mama amefariki, mjomba akaniambia mama yuko hai na anaishi Moshi, amemtuma afuatilie na kujua ninaendeleaje, japo naye alikuwa na wasiwasi wa namna nitakavyompokea kutokana na ukweli, dada yake aliniacha mdogo, hakuna aliyejali kuhusu mimi hata baada ya baba yangu kufariki.

“Mazingira aliyonikuta nayo pale alilazimika kunichukua na kwenda kuishi nami kwake kambini Mzinga alipokuwa akiishi.”

Anasema aliyafurahia maisha aliyokutana nayo kwa mjomba yake, kwani mwanzo Kichangani alikuwa na maisha ya hovyo, kule kwa mjomba mambo yakabadilika.

“Nimefanya mitihani yangu ya kuhitimu darasa la saba nikiwa kwenye maisha mazuri, nilipohamia kwa mjomba kwa mara ya kwanza hata chai nilianza kunywa, unatoka shule unakuta chakula, jambo ambalo nikiwa mdogo sikuwahi kukutana nalo kabisa,” anakumbuka.

Anaeleza siku alipokutana na mama yake, alikuwa amerejea kutoka shuleni, ilikuwa ni kipindi anakaribia kufanya mitihani yake ya kuhitimu darasa la saba.

“Nilitoka shuleni nikamkuta amekaa sebuleni pale kwa mjomba, nilimuona tu ni mtu, alikuwa anakula, sikumfahamu ni nani, nilimsalimia na kuendelea na mambo yangu, mke wa mjomba akanifuata na kuniambia unamuona yule mwanamke aliyekaa pale, huyo ndiyo mama yako mzazi.

“Wakati huo tayari nilishakuwa na moyo fulani hivi mgumu kutokana na mazingira niliyopitia, moyo wangu ulishakuwa na ganzi, sikuhisi chochote, nilimuangalia tu, nikajisikia huzuni sana,” anasema Afande Sele na kuongeza;

“Wakati huo alikwishatoka kwenye ajira amerudi kijijini kule Moshi, mama yangu ni Mchaga, hivyo alikuwa anahitaji sasa kukaa na watoto wake, hata hivyo sikuwa na namna maana ndiye mama yangu na nimekutanishwa naye japo nilifadhaika sana nilipomuona,” anasema.

Anasema, alipomaliza mitihani yake ya mwisho, kwa mara ya kwanza sasa alikwenda Moshi, ambako alikutana na mjomba wake mwingine akamchukua.

“Ni kama walihitaji kujisafisha kutokana na mazingira waliyoniacha tangu utoto, yule mjomba wangu naye alikuwa vizuri kiuchumi, aliamua kunisomesha.

“Aliniambia siku nyingi sikuwa nao na maisha yangu ya awali tayari walishayajua yalivyokuwa magumu, dada yao aliondoka miaka miwili baadaye baba yangu akafariki, mama yangu wala ndugu yake yeyote hawakuja kwenye msiba wala kujua naishije baada ya kifo cha baba, hivyo ni kama nafsi ziliwasuta, wakawa wanataka kuonyesha walikosea.”

Anasema alipata shule nzuri na kuanza kidato cha kwanza kule Moshi, lakini hakuyafaidi hayo maisha muda mfupi baada ya kumfahamu mama yake.

“Shangazi yangu yule aliyejimilikisha mali za familia na kunichukua mwanzo alileta shida, alitaka nirudi Kichangani, kwenye maisha yangu ya zamani,” anasema kwa sauti ya simanzi kidogo na kuendelea; “Ni kama alitaka tu kuniharibia, vilianza vitisho ikaonekana mimi nikibaki Moshi basi nakaribia kufa, alizungumza vitu vingi akihusisha na mambo ya kishirikina ambayo kule uchagani hayakuwepo kabisa.”

Anasema mama yake, licha ya kuwa mlokole, alikuwa mwoga, alilazimika kumuachia Afande Sele arudi upande wa baba yake baada ya kupewa vitisho.

“Mama alikuwa mcha Mungu, lakini aliamini ushirikina upo, wakati akiwa na baba Kichangani, aliniambia kuna vitu alikuwa akiviona, hivyo baada ya kauli ya shangazi akitaka nirudi akawa na hofu ukizingatia na namna alivyoishi nao awali, alikuwa akiona vitu vingi ajabuajabu, aliwaambia kaka zake waniache nirudi kwetu.

“Iliniumiza sana, lakini mama mwenyewe amelazimika iwe hivyo nafanyaje? Nikarudi kwenye maisha yangu ya awali kule Kichangani,” anasema.

Itaendelea kesho...

SEHEMU YA PILI

Afande Sele alivyokwama kufanya mtihani, atua mtaani kusaka maisha​

Anasema akaendelea na maisha ya mtaani yasiyo na uangalizi baada ya shule. “Baadaye nilikwenda Moshi, nikafanya shughuli kwa mjomba, kisha nikafanya kazi za ulinzi, ujenzi na kuanza kujitegemea na baada ya miaka kadhaa nilipata nafasi ya kujiunga na jeshi, kisha muziki na kuwa kwenye mahusiano yaliyonipa familia yenye upendo, ingawa nilipambana hasa.

“Maisha yale ndio yamenisukuma kuwaongoza wanangu, sio tu wa kuwazaa hadi wengine wanaonisikiliza, huwa napenda kuongeza upungufu na ubora wangu katika kuwafunza wengine, ukiangalia makuzi yangu na niliyowapa wanangu ni tofauti, wao wamepata malezi na ukaribu wangu na ndugu wengine ambao mimi sikuyapata.

“Hiyo imenipa uzoefu na ujasiri mkubwa wa kuwaelimisha, binti zangu nawategulia mitego ambayo kama mimi baba yao nisingeishi hivyo huenda wasingelijua,” anasema.

Anasema, alijikuta ameingia kwenye kuimba akiwa mtaani, Morogoro japo hakuwa maarufu hadi alipokutana na Joseph Mbilinyi (Sugu). “Sugu aliniona naimba, akapenda kipaji changu, nikawa naye hadi nilipoweza kusimama. “Iliniumiza, mzazi mmoja yupo lakini hujawahi kupata mapenzi yake, japo wakati mwingine nasema mitihani niliyopitia ndiyo imefanya niwe hapa nilipo, kabla ya muziki niliwahi kujiunga na jeshi ila kutokana na mambo ya ujana nilifukuzwa.

“Lile jambo pia liliniumiza, sikufahamu kesho yangu itakuwaje, kwani tayari nilishaingia kwenye mfumo na kuanza kulipwa hadi mshahara, lakini katika mazingira ya kidunia nilipoteza ile nafasi, ilikuwa ni bahati mbaya, sio kila kitu ni uzembe au makusudi, hasa sisi ambao tunapitia makuzi ya bila mwongozo wa wazazi.

“Nilikengeuka tu na sikujua hatima yangu baada ya tukio hilo, muziki ulitokea tu, ni karama ilikuja, lakini jeshi ni taaluma ambayo nilikwenda depo kule Zanzibar kujifunza, liliniumiza nilipofukuzwa, najilaumu mwenyewe kwa tukio lile, ilikuwa ni ujana tu na kukengeuka, nilijutia sana japo baadaye nikaja kuwa mwanamuziki.”

Anasema changamoto kubwa kwenye muziki wakati huo jamii haikuwa na uelewa na Bongofleva, wengi walilioshiriki walionekana kama waasi kwenye familia zao. “Kipindi kile ndio muziki tuliofanya ulikuwa unaingia ingia nchini, tena ilikuwa ni ku-rap, sio huu wa kuimba, moja kwa moja ulijumuishwa na uhuni, kipindi hicho miaka ya 1990 kulikuwa na kuuana, ndipo yalifanyika mauaji ya 2PAC na sisi tukaupokea hivyo.”

Anasema ili waeleweke kwenye jamii, walilazimika kuimba nyimbo za kukemea na kutishia, ingawa baadaye wakaingiza meseji zenye mafunzo, japo walionekana kana kwamba ndiyo wameshapotea.

“Tulianza kutunga nyimbo ili watu watuelewe, hata wakitusikiliza pamoja na kwamba tunaonekana wahuni, lakini wajihoji mbona wanaongea vitu vya msingi, haikuwa rahisi eti mtu tu kanywa pombe kalewa anaenda studio, ilikuwa lazima ukae na watu upate historia au ujisomee vitabu ndipo uandike mistari. “Changamoto nyingine ikawa ni studio, zilikuwa MJ Records na Bongo Records tu, hivyo unaweza kwenda siku hiyo kumbe sio zamu yako.

Anasema masilahi kwenye muziki nayo ilikuwa kidogo, japo waliutengenezea njia lakini haukuwalipa, kwani pesa wao walipata kwenye matamasha. “Tulikuwa tunaanda tamasha tunakaa wenyewe mlangoni kukusanya kiingilio, pesa inayopatikana tunagawana, muziki haukuwa na maslahi makubwa.

Ingawa hatukukubali jamii ituone kuwa sisi tuliofanya muziki wakati huo ni kama waasi, tulilazimisha kuandika muziki wenye ujumbe mzito ili jamii ituamini na kutuona hatufanyi uhuni,” anasema na kuongeza; “Wanamuziki wa zamani hatukupata pesa, lakini tulijenga heshima kwenye muziki, nyimbo zetu zilijikita kufikisha ujumbe na kufanya muziki ukubalike, tulitengeneza njia hadi leo ‘watoto’ wanaimba hata matusi wanapata pesa, tunaona mzazi anatoa pesa kumlipia mwanaye ili akarekodi, wakati wetu hayo hayakuwepo,” anasema.

Maisha yake ya sasa

Mwaka 2004, ndipo mwimbaji huyo ambaye sasa ni balozi wa mazingira na mkewe Asha walinunua eneo huko Modeko, Kata ya Mazimbu, mjini Morogoro ambalo walikubaliana kuwa hapo ndipo yatakuwa makazi yao ya kudumu na familia yao.

Katika eneo hilo, Afande Sele ametengeneza kempu tofauti alizozipa majina, kuna Magufuli Site ambayo imewekewa eneo la kupumzika, ina urembo wa chupa mbili za asili, moja ina rangi ya bendera ya taifa na nyingine ina rangi nyekundu, njano na kijani (alama inayotumiwa na marasta).

Kwenye eneo hilo pia kuna picha ya Simba, ambayo anasema Simba ni mnyama shujaa, naye alimuona Magufuli kama mnyama Simba. Eneo jingine ni Samia Site, ambalo amempa heshima Rais Samia Suluhu Hassan ambaye anamtaja kama mwanamke jasiri ambaye aliwatoa Watanzania kwenye simanzi baada ya kifo cha Magufuli.

“Binafsi nilikuwa nawaza itakuwaje baada ya kifo cha Magufuli, lakini tumeona namna Rais Samia alivyoiongoza nchi, kwenye eneo hili ni mahususi kwa ajili ya kufanya usuluhishi wa jambo fulani kama kaka na kioo cha jamii wanaomzunguka wakiwa na ugomvi humfuata na hutumia hilo eneo kuwasuluhisha,” anasema. Pia kuna eneo la Nyerere Site, Karume, Sokoine, Dk Remmy na Asantesanaa Site, yote yakiwa na maana, Nyerere ambaye ni baba wa Taifa, Karume Rais wa kwanza wa Zanzibar na Sokoine, Waziri Mkuu wa zamani ambao wote wametangulia mbele za haki na mwanangu ambaye jina lake lilitokana na shukrani zangu kwenye sanaa,” anasema.

MWANANCHI
 
Nimeangalia chini sijakuta "ITAENDELEA"...ngoja niisome sasa.
 
Jamani tusisahauliane kwenye mwendelezo wa huyu king of rhymes.

Afande Sele nakumbuka lile bifu lake na Oten dah hivi mnawakumbuka watu pori? Ditto(dogo ditto) simsikii tena siku hizi sijui kaacha kuimba
Yupo na aliimba wimbo,moyo sukuma damu si vingine siku hizi anajiita lameck ditto
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom