Somalia yajiunga Uanachama wa Afrika Mashariki (EAC)

Somalia yajiunga Uanachama wa Afrika Mashariki (EAC)

Mkuu naona ni dini na kujistiri nakumbuka nilienda huko miaka ya nyuma nilikuta wanavaa hivyo ila sasa maisha yako tofauti na wanawake pia walikuwa wanavaa kama half naked ila wengi wanajistiri sasa na sio mbaya kuficha mwili kwa mwanamke
Mimi naona kujistiri ni bora kuliko kuachia nyama nje au unasemaje mkuu

Stara ni nzuri ila kanzu ni vazi tu mtu na mtu anaamua kuvaa ila wengi wanavaa suruali kuliko wavaa kanzu
Unajua akina Burhan wa Sudan ni Hadendoa Cushites kama Wasomali lakini Arabization imesababisha wamepoteza hadi lugha yao ya Kikushi na sasa wanaitwa Arabs ninyi msipoangalia mtakuwa kama akina Hamdan Dagalo.
Miaka 70 iliopita Hadendoa Beja Cushites walikuwa wakivaa hivi kimorani lakini leo ni Baraghashia za kiarabu WHY?
0775a084bec73ffdd6f51ca83b8352db--old-photographs-old-photos.jpg
DeoWIS9VAAEhCOW.jpg

Ni saa ngapi hawa Wakushi👆 wamegeuzwa kuwa Waarabu?
Fotoram.io_-2-780x470.jpg
 
Community yenyewe hata sioni umuhimu wake, tumeshapoteza malengo tunajiendea tu, naona wazo zuri kwa sasa na habari ya kuuza gazeti ingekuwa ni kuvunja huo muungano kila nchi ijifie kivyake, kwasasa hakuna lolote la maana zaidi ya kugawana umaskini tu

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
Hili tu la kujiunga nchi za aina hiyo ya Somalia ni kutupeleka kwenye lengo ulilo litaja, la "kuvunja". Kwa maana hiyo naunga mkono kwa Somalia na akina Sudani Kusini kujiunga na umoja huo.
 
Unajua akina Burhan wa Sudan ni Hadendoa Cushites kama Wasomali lakini Arabization imesababisha wamepoteza hadi lugha yao ya Kikushi na sasa wanaitwa Arabs ninyi msipoangalia mtakuwa kama akina Hamdan Dagalo.
Miaka 70 iliopita Hadendoa Beja Cushites walikuwa wakivaa hivi kimorani lakini leo ni Baraghashia za kiarabu WHY?
View attachment 2823823
Mkuu kama hao afadhali wamebadili kuvaa tu kwa sababu ya dini lakini imagine watumwa waliochukuliwa na wazungu na mila zao kuvurugwa mpaka alama zao na hata kutokukumbuka walitoka nchi gani
Yaani wazungu wamewasababishia wasikumbuke hata walikotoka hao ndio wa kuwahurumia zaidi
Yaani anakuambia I'm American not African maana hajui uafirika atauanzia wapi kuelezea

Nilikutana na teacher mmoja London ni black anaetokea st Lucia anaongea kifaransa ndio lugha yao ila nikamuuliza asili yako ni wapi haswa akaniambia sielewi ila hata lugha tunayoongea kuna maneno ambayo sio kifaransa bali tumeyakuta tu na hatujui ni ya nchi gani
Hao nao ni wa kuwahurumia zaidi

Ila mkuu kila binadamu anabadilika kutokana na maisha yanavyokuja
Hata leo kuna watanzania wengi hawajui kuongea kilugha tena wengi sana yaani lugha yake mwenyewe unaweza kumteta na asikuelewe

Acha kila mmoja aamue anavyotaka kuishi mkuu na kuona hiyo ndio inamfaa
Wapo Blacks huko America wao ni jazz tu kwenda mbele
 
Ni aibu sana kuna Mtanzania msomi hajui malengo ya EAC
Kwa hiyo hapa wewe unadhani umeweka mchango muhimu sana katika kumfahamisha hayo malengo?

Haitashangaza hata kidogo endapo wewe mwenyewe hujui hata moja!
 
Wasomali wakiingia Tanzania inabidi watanzania wajiandae kisaikolojia kibiashara na hao jamaa, wasomali ni kama wana asili moja na wachaga ni jamii ya watu wafanyabiashara sana, somalia kama sio vita hiyo nchi, ni nchi ungekuta iko mbali sana
 
Nilikutana na teacher mmoja London ni black anaetokea st Lucia anaongea kifaransa ndio lugha yao ila nikamuuliza asili yako ni wapi haswa akaniambia sielewi ila hata lugha tunayoongea kuna maneno ambayo sio kifaransa bali tumeyakuta tu na hatujui ni ya nchi gani
Somalia na Sudan ziko kwenye Arab League wakati wao sio Waarabu, Waarabu halisi waliohamia Sudan kutoka Syria na Hejaz hawazidi 5% kuhusu hao ndugu zetu waliopelekwa utumwani wanatambua kuwa wao sio Wazungu bali ni Waafrika rejea "African Americans" lakini Wasudani na Wasomali asilimia kubwa wanadai kuwa wao ni Waarabu je unalijua hilo.

Unajua Watumwa wengi walipelekwa Uarabuni kuliko Marekani lakini leo wako wapi wengi walihasiwa ili wasiwanajisi wasichana wa Kiarabu.

Huu ni wakati wa Mwafrika kuamka kutoka usingizini.
 
Wasomali wakiingia Tanzania inabidi watanzania wajiandae kisaikolojia kibiashara na hao jamaa, wasomali ni kama wana asili moja na wachaga ni jamii ya watu wafanyabiashara sana, somalia kama sio vita hiyo nchi, ni nchi ungekuta iko mbali sana
Mbona tunao akina Rage wakulugo.
 
Somalia na Sudan ziko kwenye Arab League wakati wao sio Waarabu Waarabu halisi waliohamia Sudan kutoka Syria na Hejaz hawazidi 5% kuhusu hao ndugu zetu waliopelekwa utumwani wanatambua kuwa wao sio Wazungu bali ni Waafrika rejea "African Americans" lakini Wasudani na Wasomali asilimia kubwa wanadai kuwa wao ni Waarabu je unalijua hilo.

Unajua Watumwa wengi walipelekwa Uarabuni kuliko Marekani lakini leo wako wapi wengi walihasiwa ili wasiwanajisi wasichana wa Kiarabu.

Huu ni wakati wa Mwafrika kuamka kutoka usingizini.
Arab league walikubaliwa kama tulivyokubali wasomali kuingia EA
Ni kama European wapo waliokubali na wapo waliokataa na pia kuna aliejitoa ni kutokana na maamuzi ya nchi husika
Wasudani wamegawanyika pia wenye mafuta na wenye bahari
Na wasomali yao mazito bado wana changamoto zao na hawana msaada mkubwa kutoka kwenye mataifa mengine kwa sababu wao wamekataa kujielewa na kuacha kuuwana kama sisi tulivyogoma kuacha wizi na rushwa
Kuhusu black Americans sawa hao wamepotea mamoja ingawa kuna baadhi wamerudi Africa na kuwekeza

Wale walipelekwa uarabuni sijui idadi zao ila wapo nimefanya kazi na mpalestina mweusi na ana familia mwanamke wa kiarabu
Saudia wapo weusi
Ushahidi ni kuwa nimekaa miaka 10 uarabuni na kufanya kazi na kuzunguka nchi karibu zote kuanzia Saudia, Kuwait, Oman, Bahrain na UAE, nimekaa Iraq wakati wa vita na weusi wapo pia Jordan Amman nimekaa
Kuhusu weusi kuhasiwa labda ila kwa mfano Kuwait kulikuwa na Amir alioa mtumwa na kuzaa nae na mmoja wa watoto wake ambae alitokea kufuata ngozi ya mama black alikuja kuwa mfalme wa Kuwait akiitwa Sheikh Saad bin Abdallah Al Sabah kwa sasa ni marehemu nae alioa cousin yake mweupe
Najua kuna mengi mnasoma na kuhadithiwa ila mimi nilikuwa huko na kujifunza mengi na sasa niko kwa wazungu na maisha yao wote yanatofautiana kabisa ingawa wote ni binadamu
Naona mjadala umekuwa mrefu
Nikutakie mapumziko mema
 
Tusiwe na hofu, tutapata fursa nyingi na watabadilika. Kitendo Cha kuendelea kuwatenga ndicho kinawafanya wawaze vibaya
Hofu kama hiyo iliibuka wakati Rwanda, Burundi na DRC zinajiunga lakini utaona kuwa hakuna shida yoyote

Rwanda, Burundi na DRC Hamna ugaidi kama wa Somalia. Kumbuka Somalia kuna alshabaab
 
Wewe ndo mpumbavu tena sana. Unajua kama Somalia ilikuwa mpatanishi wa mgogoro wa Tanzania na Uganda chini ya Rais Siad Barre? Kabla ya vita ya Kagera nchi ya Somalia ilipambana kupatanisha ili kuepusha vita. Somalia kinachowagharimu ni koo zao kutoelewana.

Mbona wameshindwa kupambana na ugaidi?!
 

Mkutano wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) uliofanyika Jijini Arusha nchini Tanzania, umeridhia Nchi ya Somalia kujiunga na EAC na sasa inakuwa Mwanachama wa nane wa Jumuiya hiyo.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki January Makamba ni miongoni mwa Viongozi waliotoa pongezi za awali kabisa kwa Somalia kuridhiwa kuwa Mwanachama mpya wa EAC ambapo ameitakia kheri Somalia katika kuielewa na kuiishi pamoja na kuitekeleza misingi ya EAC na itifaki zake katika kukuza na kuendeleza Jumuiya hiyo.

Katika hatua nyingine mkutano huo pia umemtangaza Rais wa Sudan, Salva Kiir Mayardit kuwa Mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Itakumbukwa katika mkutano kama huo mwaka jana aliyekuwa Rais wa Kenya na Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo wakati huo, Uhuru Kenyatta alitangaza rasmi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) kujiunga na EAC.
Yaani passport yangu iwe na Somalia?
Loooo!!!
 
Back
Top Bottom