Somalia yajiunga Uanachama wa Afrika Mashariki (EAC)

Somalia yajiunga Uanachama wa Afrika Mashariki (EAC)


Mkutano wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) uliofanyika Jijini Arusha nchini Tanzania, umeridhia Nchi ya Somalia kujiunga na EAC na sasa inakuwa Mwanachama wa nane wa Jumuiya hiyo.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki January Makamba ni miongoni mwa Viongozi waliotoa pongezi za awali kabisa kwa Somalia kuridhiwa kuwa Mwanachama mpya wa EAC ambapo ameitakia kheri Somalia katika kuielewa na kuiishi pamoja na kuitekeleza misingi ya EAC na itifaki zake katika kukuza na kuendeleza Jumuiya hiyo.

Katika hatua nyingine mkutano huo pia umemtangaza Rais wa Sudan, Salva Kiir Mayardit kuwa Mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Itakumbukwa katika mkutano kama huo mwaka jana aliyekuwa Rais wa Kenya na Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo wakati huo, Uhuru Kenyatta alitangaza rasmi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) kujiunga na EAC.
Wanazidi kuyakaribisha magaidi sebuleni!!

Sijui hata vigezo wanavyoangalia ni vipi .....

Migogoro iliyopo tu imeshindwa kutatuliwa... Hata kuwa na soko la pamoja na EA Currency..

Wanaendelea kujaza ma-nchi yenye migogoro isiyoisha!
 
Waliweka kigezo/sharti la ajabu sana, eti nchi yoyote ilipakana na mwanachama wa EAC anaruhusiwa kuomba uanachama. Nionavyo mimi ipo siku hata Ghana utakuta ni mwanachama wa EAC.

Kweli kabisa. Maana hata Sudan ya akina Burhani inataka kuomba uanachama. Ila ndio integration inayopiga kazi.
 
Somalia kama waliweza kuwafukuza Wareno katika Pwani ya Afrika ya Mashariki ni jambo lenye kutia matumaini sana kwetu Waafrika weusi.
 
Ujinga na upumbavu tu kuingiza Somalia EAC
Wewe ndo mpumbavu tena sana. Unajua kama Somalia ilikuwa mpatanishi wa mgogoro wa Tanzania na Uganda chini ya Rais Siad Barre? Kabla ya vita ya Kagera nchi ya Somalia ilipambana kupatanisha ili kuepusha vita. Somalia kinachowagharimu ni koo zao kutoelewana.
 
dc47oec-21121db4-7800-4dbd-8e29-3e34a2b98b91.jpg

Huu ndio wakati muafaka kwa yale makabila yenye watu wafupi haswa Wazaramo na Wadengeleko kwenda South Sudan kuoa Wasichana wa Kidinka ili kuongeza height za ukoo.
 
Hofu yangu ni Majahazi yaliyojaa Wasomali na Bunduki likatie nanga Zanzibar😂 kabla ya Uchaguzi ujao chuki iliyopo Zanzibar inahitaji Spark ndogo tu Kisiwa kinarudi kwa wenyewe🫡
Sidhani mkuu
Wasomali wanauwana Mogadishu tu na hawaingilii siasa za nchi zingine
Ukimuona msomali nchi nyingine ujue ni mtafutaji huyo
Wengi wao ni hustlers
Kisiwa cha Zanzibar hakuna anaekitamani mkuu hata Oman wenyewe labda kuwekeza tena sio wa kuja bali wazawa walioenda Oman na kuishi na kupata watoto huko
Na Oman wako vizuri sana kwa sasa maana hata mafuta ni yao kwa 💯 tangu mkataba ulipoisha na wana Nationalization sasa wao tu ndio wanashika sehemu zote za kazi hawataki ujinga
Kama wewe ni foreigner na ni bank manager ukimaliza mda wako anawekwa M Oman aliesoma

Nafikiri wasomali mpaka uwavuruge kama Kenya walivyovamia Mall majeshi ya kila aina yakashindwa kuwakamata vijana wadogo ila wakaishia kuiba maji ya chupa na kuvunja safe za hela
Yaani aibu ya hivyo mkuu nao ndio walinzi wa nchi je sisi tungekuwa tofauti ?

Kwa usalama wa nchi masikini Mungu tu ndio anajua
 
Tukishakuwa na soko la pamoja na sarafu moja Kwa jumuia za kikanda kama EAC tutakuwa tumefika mahali pazuri,jumuia kama umoja wa ulaya Wana sarafu Yao,inayokubalika nchi zote katika jumuia,ukija hapa kwetu Kila mtu ana sarafu yake,Hali hii inadhoofisha biashara miongoni mwa nchi wanachana.

Sent using Jamii Forums mobile app

Nadhani walikubaliana mwaka 2024 ndio ipatikane sarafu ya pamoja. Ila naona wamesogeza mbele upatikanaji wa hiyo sarafu ya pamoja.
 
Mkuu mbona Wasomali zamani walikuwa wakivaa mavazi ya Kiafrika lakini siku hizi Makanzu kanzu na Mabaibui kama Waarabu ni kwanini au wameshindwa kupambana na Arabization?
View attachment 2823803
Mkuu naona ni dini na kujistiri nakumbuka nilienda huko miaka ya nyuma nilikuta wanavaa hivyo ila sasa maisha yako tofauti na wanawake pia walikuwa wanavaa kama half naked ila wengi wanajistiri sasa na sio mbaya kuficha mwili kwa mwanamke
Mimi naona kujistiri ni bora kuliko kuachia nyama nje au unasemaje mkuu

Stara ni nzuri ila kanzu ni vazi tu mtu na mtu anaamua kuvaa ila wengi wanavaa suruali kuliko wavaa kanzu
 
Kwani malengo ya EAC ni yepi?
Mimi nitakujibu kwa mtizamo wangu, na siyo lazima iwe hivyo:
Jibu - kupata soko kubwa zaidi kwa nchi inayojidhani inavyo viwanda vingi zaidi ya wengine wote.

Ukitaka nieleze, nitaeleza.
 
Back
Top Bottom