Soma kwa makini: Dalili zinaonesha kuwa huenda mkataba wa bandari ukasababisha vifo vya watu

Mr Dudumizi

JF-Expert Member
Sep 9, 2020
6,860
12,293
Habari zenu wana jf wenzangu.

Wakuu baada ya kufuatilia kwa kina kile kinachoendelea katika swala hili la bandari, hususani hapa JF, nimegundua kwamba kuna uwezekano mkubwa wa siku kadhaa zijazo tukashuhudia vifo mbali mbali ndani ya makundi kadhaa nitakayoyaorodhesha hapo chini.

1. Kundi la kwanza, hili ni lile kundi la "wakwepeshaji". Kundi hili lina uwezekano wa kupoteza watu wengi kwa njia ya kujiuwa kwa sumu, kujinyonga, kuanguka ghafla au kulala na kuamka mtu akiwa amekufa kutokana na presha, sonono na stress nyingi walizonazo vichwani kwao sasa hivi.

Kundi hili kazi yake kubwa pale bandarini ilikuwa ni kuongea na wafanyabiashara wa ndani na nje ya nchi, pamoja na wateja wengine waliozoea kutumia bandari yetu kupitisha mizigo yao pale kwamba watawasaidia kuchepusha mizigo yao bila kupitia sehemu husika, alafu watawalipa gharama kidogo tu ya pesa ukilinganisha na ile ambayo anaweza kulipa katika ukaguzi wa kawaida.

2. Kundi la pili ni lile lililokuwa linapitisha mizigo au biashara zao kwa bei chee bila kulipa kodi na ushuru wa bandari.

Kundi la tatu ni la vibaka na vishoka waliokuwa wanaiba vitu mbali mbali pale bandarini na kwenda kuviuza mitaani kwa bei ya kutupa ili vitoke fasta fasta.

Sababu ya vifo vyao itatokana na mambo kadhaa ambayo nayo nitayaandika hapo chini.

1. Kwanza, kuna baadhi ya watu wameshachukua mamilioni ya mikopo kutoka bank na kwa watu binafsi, wengine wanajenga mijengo ya maana huko kwenye miji ya matajiri, wengine wamekopa magari ya kifahari nk wakitegemea kutumia njia zile zile walizo zizowea kupiga hela kiulaini na kulipa madeni yao, kumalizia mijengo yao nk.

Sasa hawa jamaa wa Dubai wakishaingia kazini, inamaana zile hela za dezo walizokuwa wanazipata hawataweza tena kuzipata, hivyo uwezekano wa kunyang'anywa nyumba na bank kwa kushindwa kumaliza deni ni mkubwa, na wale ambao hawana madeni watashindwa kumalizia mijengo yao nk.

2. Pili, kuna watu walipoona hili swala linaanza, na uwezekano wa wao kuendelea kufanya upumbavu wao pale banda hautakuwepo, wakajikusanya na kufanya michango kwa kila mmoja wao kutoa kiasi kadhaa cha pesa ili watafutwe watu wenye ushawishi wapewe chao waanze kuingia kazini kuwatetea wapiga ma deal hao kwa kisingizio cha uzalendo wa bandari. Na kweli tumeona jinsi watu wenye ushawishi na mambo ya siasa, dini nk wakiingia kazini kukamilisha mission.

Watu hao baada ya kumaliza kuwapa deal watu wenye ushawishi niliowataja hapo juu, wakarudi katika mitandao ya kijamii na kukamata baadhi ya wenzetu huku wakihakikisha wale wajanja ambao wana falsafa ya "mkono mtupu haulambwi" familia zao zinaenda msalani kupitia mifuko ya wanaopiganiwa wabaki na bandari, japo kuna wengine wanatumika kwa bure kutokana na akili zao kuwa ndani ya mifuko ya suruali za kina Lisu, Shivji nk.

Kuna jamaa yangu fulan ambae ni mwana JF mkongwe hapa ndani, juzi aliniambia kwamba kama na mimi nataka kuwa natumiwa vocha za bure kupitia PM, basi nibadili upepo na mimi nianze kuponda mkataba kama anavyofanya yeye.

Anasema wale jamaa wa ma deal wakipita na kuona nina thread mbili tatu za kupinga mkataba, basi wataanza na mimi kunitumia vocha ya elfu 5 hadi 10 kulingana na uzito wa thread na muitiko wake katika jamii. Huyo mwana amenitumia meseji mbili za screenshot zinazoonesha vocha mbili tofauti alizotumiwa na wazee wa bandari, ambapo moja ilikuwa ya elf 10 na nyingine ya juzi elf 15. Ila mimi nilikataa katakata kuuza utu wangu na kuyumbisha msimamo wangu sababu ya tamaa yangu.

Kwahiyo kitachowauwa hawa jamaa ni kwasababu wameshatumia mamilioni ya shilingi kutengeneza ushawishi wa kuunga unga, lkn raisi wa nchi haonekani kujali, kusikia wala kuelewa porojo zao.

Ndio kwanza anaendelea na ziara zake mbali mbali za ndani na nje ya nchi.
 
Bora wale hao watanganyika wenzetu pesa itabaki kwenye mzunguko wa ndani kuliko achukue mwarabu akaijenge zaidi Dubai. Mbaya zaidi wakila mafisadi wa Tanzania wataenda kuficha visiwa vya Jersey au Panama kisha wanakopa mabeberu kuja kuwekeza miradi ya kutuibia rasilimali zetu.

BTW, naomba hiyo connection ya vocha ya pinga pinga DP World.
 
Fisadi hana akili.
Anaiba pesa nchini kwake anaenda kujenga vitega uchumi nchi za nje ili awapelekee maendeleo huko nje badala ya kuwekeza ndani awape ajira walipa kodi wakatwe kodi aibe tena.
 
Bora nimsikilize mama Pro. Tibaijuka.

Alipewa mgao wa pesa za mboga za esi-kurowu akaenda kuwapa shule inayo hudumia watoto wa kike wasijazane Uwanja wa Fisi Manzese au Buguruni au kule Temeke kwa wadada wa Kihay*
 
Bora wale hao watanganyika wenzetu pesa itabaki kwenye mzunguko wa ndani kuliko achukue mwarabu akaijenge zaidi Dubai. Mbaya zaidi wakila mafisadi wa Tanzania wataenda kuficha visiwa vya Jersey au Panama kisha wanakopa mabeberu kuja kuwekeza miradi ya kutuibia rasilimali zetu.
BTW, naomba hiyo connection ya vocha ya pinga pinga DP World.
Connection ni wewe kushupaza Shingo kupinga mkataba na kulaghai kwamba bandari yetu inauzwa.

Fasta tu wazee wa bandari watakufuata PM mkuu.
 
Wabinafsishe tuu mbona tulisha zoea toka enzi za Mkapa mm sioni mafanikio yoyote ya hii kampuni iliyopo kwani Paul alisha mwambiaga JK ampe bandari tuu aone kama hajabadilisha nchi, maana yake nikweli kuna urasim mkubwa sana unao endelea bandarini. Wawape hao DP tuu mbona Swissport wako zaidi ya miaka 33 na wanafanya vizuri tuu. Basi watupe hela wote tule ndio na sisi tukishashiba tutawasapport
 
Andiko liko bias na linaonyesha unakubaliana na huo mkataba, eti mtu ajiue kisa alikopa Hela wapi akajenge nyumba?Unafichaficha nini si unyooshe maelezo tu.

Sema tu makundi ya watakaopoteza maisha kisa sakata la Bandari ni Hawa.

1.Wabunge waliohongwa walipokua Dubai.(huko mbele I Kuna kila dalili za visasi)
2.Wanaharakati na wanasiasa wanaopinga mkataba.
3.Makundi hasimu ya waliojimilikisha hatma ya nchi ya nchi hii kuanzia Msoga gang, sukuma Gang na wengine ambao Wana maslahi na bandari.

Acha kuuma maneno wewe mtoa mada
 
Habari zenu wana jf wenzangu.

Wakuu baada ya kufuatilia kwa kina kile kinachoendelea katika swala hili la bandari, hususani hapa JF, nimegundua kwamba kuna uwezekano mkubwa wa siku kadhaa zijazo tukashuhudia vifo mbali mbali ndani ya makundi kadhaa nitakayoyaorodhesha hapo chini.

1. Kundi la kwanza, hili ni lile kundi la "wakwepeshaji". Kundi hili lina uwezekano wa kupoteza watu wengi kwa njia ya kujiuwa kwa sumu, kujinyonga, kuanguka ghafla au kulala na kuamka mtu akiwa amekufa kutokana na presha, sonono na stress nyingi walizonazo vichwani kwao sasa hivi.

Kundi hili kazi yake kubwa pale bandarini ilikuwa ni kuongea na wafanyabiashara wa ndani na nje ya nchi, pamoja na wateja wengine waliozoea kutumia bandari yetu kupitisha mizigo yao pale kwamba watawasaidia kuchepusha mizigo yao bila kupitia sehemu husika, alafu watawalipa gharama kidogo tu ya pesa ukilinganisha na ile ambayo anaweza kulipa katika ukaguzi wa kawaida.

2. Kundi la pili ni lile lililokuwa linapitisha mizigo au biashara zao kwa bei chee bila kulipa kodi na ushuru wa bandari.

Kundi la tatu ni la vibaka na vishoka waliokuwa wanaiba vitu mbali mbali pale bandarini na kwenda kuviuza mitaani kwa bei ya kutupa ili vitoke fasta fasta.

Sababu ya vifo vyao itatokana na mambo kadhaa ambayo nayo nitayaandika hapo chini.

1. Kwanza, kuna baadhi ya watu wameshachukua mamilioni ya mikopo kutoka bank na kwa watu binafsi, wengine wanajenga mijengo ya maana huko kwenye miji ya matajiri, wengine wamekopa magari ya kifahari nk wakitegemea kutumia njia zile zile walizo zizowea kupiga hela kiulaini na kulipa madeni yao, kumalizia mijengo yao nk.

Sasa hawa jamaa wa Dubai wakishaingia kazini, inamaana zile hela za dezo walizokuwa wanazipata hawataweza tena kuzipata, hivyo uwezekano wa kunyang'anywa nyumba na bank kwa kushindwa kumaliza deni ni mkubwa, na wale ambao hawana madeni watashindwa kumalizia mijengo yao nk.

2. Pili, kuna watu walipoona hili swala linaanza, na uwezekano wa wao kuendelea kufanya upumbavu wao pale banda hautakuwepo, wakajikusanya na kufanya michango kwa kila mmoja wao kutoa kiasi kadhaa cha pesa ili watafutwe watu wenye ushawishi wapewe chao waanze kuingia kazini kuwatetea wapiga ma deal hao kwa kisingizio cha uzalendo wa bandari. Na kweli tumeona jinsi watu wenye ushawishi na mambo ya siasa, dini nk wakiingia kazini kukamilisha mission.

Watu hao baada ya kumaliza kuwapa deal watu wenye ushawishi niliowataja hapo juu, wakarudi katika mitandao ya kijamii na kukamata baadhi ya wenzetu huku wakihakikisha wale wajanja ambao wana falsafa ya "mkono mtupu haulambwi" familia zao zinaenda msalani kupitia mifuko ya wanaopiganiwa wabaki na bandari, japo kuna wengine wanatumika kwa bure kutokana na akili zao kuwa ndani ya mifuko ya suruali za kina Lisu, Shivji nk.

Kuna jamaa yangu fulan ambae ni mwana JF mkongwe hapa ndani, juzi aliniambia kwamba kama na mimi nataka kuwa natumiwa vocha za bure kupitia PM, basi nibadili upepo na mimi nianze kuponda mkataba kama anavyofanya yeye.

Anasema wale jamaa wa ma deal wakipita na kuona nina thread mbili tatu za kupinga mkataba, basi wataanza na mimi kunitumia vocha ya elfu 5 hadi 10 kulingana na uzito wa thread na muitiko wake katika jamii. Huyo mwana amenitumia meseji mbili za screenshot zinazoonesha vocha mbili tofauti alizotumiwa na wazee wa bandari, ambapo moja ilikuwa ya elf 10 na nyingine ya juzi elf 15.
Ila mimi nilikataa katakata kuuza utu wangu na kuyumbisha msimamo wangu sababu ya tamaa yangu.

Kwahiyo kitachowauwa hawa jamaa ni kwasababu wameshatumia mamilioni ya shilingi kutengeneza ushawishi wa kuunga unga, lkn raisi wa nchi haonekani kujali, kusikia wala kuelewa porojo zao.

Ndio kwanza anaendelea na ziara zake mbali mbali za ndani na nje ya nchi.
Acheni kuhalalisha baadhi ya "grand assassin's" mlizozipanga .

Jibuni hoja kwa hoja. Acheni kupanga mauaji.
 
Back
Top Bottom