Soma hapa: Ujue kwamba nchi imepigwa bei

Soma hapa: Ujue kwamba nchi imepigwa bei

Heri waje, Wabantu wamelala. Kazi ya mbantu ni kusinzia kila baada ya nusu, hawezi kufanya au kusikiliza kitu kwa nusu saa lazima alale.
 
Heri waje, Wabantu wamelala. Kazi ya mbantu ni kusinzia kila baada ya nusu, hawezi kufanya au kusikiliza kitu kwa nusu saa lazima alale.
 
kwani wewe mpaka sasa umeshaambiwa nini juu ya mikataba ya akia chifu Mangungu, Mkwawa, Carl Peters nk ...ina tofauti yoyote na IPTL/RICHMOND, Meremeta nk!!???
Mkwawa hajawahi ku-sign mkataba mbovu hata siku moja mkuu. Nakiheshimu kichwa hiki. Karl Peters alimdanganya na kumsainisha Chifu Mangungo wa Msovero na wajingawajinga wengine. Rudia history utaona!
 
"Iowa-based Summit Group and Global Agriculture Fund of the Pharos Financial Group, in partnership with AgriSol Energy LLC and the College of Agriculture and Life Sciences at Iowa State University, are developing a large agriculture enterprise in Tanzania.

The site encompasses three abandoned refugee camps Lugufu in Kigoma province (25,000 ha), Katumba (80,317 ha), and Mishamo (219,800 ha), both in Rukwa
province.

The Tanzanian arm of AgriSol Energy: AgriSol Energy Tanzania and Serengeti Advisers Limited, a Tanzanian investment and consulting firm, provide the domestic front for this operation.After the completion of the first feasibility study in early 2011, negotiations are under way with the Tanzanian government involving several issues.

These include: land title (ownership of land title is prohibited for foreigners); award of strategic
investor status to assure availability of incentives (tax holidays, repatriation of dollars out of the country, waiver of duties on diesel, agricultural and industrial equipment and supplies,etc.); and commitment and timetable for construction of a rail link for Mishamo."Mkubwa Kyando hii stori mbona tayari ipo humu JF chini ya kichwa cha habari Land grabbing or Agricultural investment?Habari ndio hiyo jamaa wanakuja kulima Ma GMO na sio kwa ajili ya shibe ya wadanganyika ni mafuta kwao ethanol wakubwa.....na Juu ya ajira tutasikia kwenye bomba hii ndivyo jamaa anasema..............

You know, we havent done thatwhat I appreciate, from a practical standpoint, is how he [The Tanzanian Prime Minister]
understands the country and the capabilities and what well need to bring in.

They quite frankly think well need to [bring in outside farmers], and theyre fine with bringing in South African farm managersthe white South African farm managers, to be able to provide that general expertise
 
[h=6]An article on a big US-based agri-business company which intends to invest heavily in Tanzania has appeared in some US newspapers, and picked by one of the English weeklies.

According to this article, which the local newspaper gave a screaming headline of ‘US investor set to acquire large chunks of land in Tan...zania’, the intention of t...he investor is to bring modern and sustainable agriculture to the country, so that even small holder farmers can learn techniques of the 21st century farming.

The land earmarked for the massive grain and livestock operation is not less than 800,000 hectares.

If things go as planned, the company will secure a 99-year lease of the extensive area “for the purpose of growing crops to be sold in the country, the rest of East Africa and other neighbour countries”.

Some of the experts and international NGOs specializing in Third World development trends are already sounding an alarm about land grabbing in some countries by foreigners, who take advantage of poverty and corruption in targeted regions to effect their mission.

Question here is: who should have powers to give 800,000 hectares to a foreigner under a 99-year lease????
[/h]

Na bado, the worst is still to come.Slavery of the 21st century is here with us.
 
Na bado, the worst is still to come.Slavery of the 21st century is here with us.

Usingependa kufanya kazi ehh?

Kazi ni heshima ya mtu, na wala siyo utumwa. Amka kwenye hiyo mbonji ya ukomunisti. Warusi wenyewe waliotekeleza hii siasa wa kwanza, wameshaachana nayo baada ya kuona ni Utopia.
 
Acha ulalamishi, ardhi ipo kulima hamlimi mnabaki kuzuia tena kwa kutumia mtutu wa bunduki mahindi yasiende nje. Ardhi iko nyingi hamjazuiwa kulima!
 
Mambo yanazidi kuwa mambo habari hii sasa iko magazetini bado tu utekelezaji, Kimsingi sina matatizo na uwekezaji lakini yaliyomo ndani humo ni kama uuzaji wa nchi kwa kweli
 
Mambo yanazidi kuwa mambo habari hii sasa iko magazetini bado tu utekelezaji, Kimsingi sina matatizo na uwekezaji lakini yaliyomo ndani humo ni kama uuzaji wa nchi kwa kweli

Usiogope Moses baada ya miaka hiyo wewe na wanao mtakuwa mnapewa ardhi huko mbinguni, kiufupi hutakuwepo acha watu wafaidi maisha ni mafupi bhana
 
[h=6]An article on a big US-based agri-business company which intends to invest heavily in Tanzania has appeared in some US newspapers, and picked by one of the English weeklies.

According to this article, which the local newspaper gave a screaming headline of US investor set to acquire large chunks of land in Tan...zania, the intention of t...he investor is to bring modern and sustainable agriculture to the country, so that even small holder farmers can learn techniques of the 21st century farming.

The land earmarked for the massive grain and livestock operation is not less than 800,000 hectares.

If things go as planned, the company will secure a
99-year lease of the extensive area for the purpose of growing crops to be sold in the country, the rest of East Africa and other neighbour countries.

Some of the experts and international NGOs specializing in Third World development trends are already sounding an alarm about land grabbing in some countries by foreigners, who take advantage of poverty and corruption in targeted regions to effect their mission.

Question here is: who should have powers to give 800,000 hectares to a foreigner under a
99-year lease????[/h]


wakuu hapa makampuni makubwa yanafanya lease ya sehemu za huduma zake lease ya miaka 99 sio kuuza nchi
mimi naona kama huu ni ukombozi haya dubai tunayotoa mifano kila siku wametumia njia hizi hizi,
cha msingi tuambiwe ni masharti gani yamewekwa kwenye hiyo lease na SCR katika hiyo lease

tunapoliwa WATANZANIA sio kile tunachofanya na makapuni ya nje ile ni kile tunachokubaliana na hayo makampuni nina maana ya uzalando na umakini
 
Ni ule mwekezaji aliyepewa ardhi kwa miaka 99 Kodi ya ardhi sh. 200, Halmashauri kupata sh.500

Diwani wa kata ya Litapunga, Godfrey Lusambo (kulia) akiwa na viongozi wa serikali ya mtaa na wanakijiji cha Kambuzi Halt, Katumba, wilaya ya Mpanda, wakilalamika kwa watafiti wa Shirika la Haki Ardhi na waandishi wa habari.


Wananchi, watendaji wa vijiji na Madiwani wa kata za Litapunga na Mishamo Wilayani Mpanda, Mkoa mpya wa Katavi, wamepinga yaliyokuwa makazi ya wakimbizi ya Mishamo na Katumba, kukodishwa kwa mwekezaji ambaye ni kampuni ya Agriosol ya Marekani, kwa maelezo kwamba uwekezaji huo, hautakuwa na tija kwa taifa.

Makubaliano ya awali (ambayo NIPASHE inayo nakala yake), kati ya mwekezaji huyo na Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda, yanaonyesha kwamba kampuni ya Agrisol itakodisha kwa miaka 99, eneo la Katumba hekta 80,317 na Mishamo hekta 219,800.
Mwekezaji pia atalipa Sh. 200 kama kodi ya ardhi kwa ekari na Halmashauri itapata Sh. 500 kwa ekari, hata hivyo haijulikani malipo hayo yatalipwa kwa muda gani yaani kwa mwezi au kwa mwaka.

Makubaliano hayo yanaonyesha pia kwamba iwapo kutatokea mgogoro, serikali itatumia busara kuutatua lakini ikishindikana, shauri hilo litasikilizwa jijini London, Uingereza na msuluhishi ambaye atakuwa Chemba ya Biashara ya Kimataifa (International Chamber of Commerce).

Kadhalika, inaelezwa kwamba mwekezaji huyo ataajiri mameneja wa mashamba kutoka nje hususan Afrika Kusini na ataendesha kilimo cha mbegu za kimaabara.

Hata hivyo, baadhi ya viongozi wa serikali wakiwemo Mawaziri na wale wa Halmashauri ya Mpanda, wamekuwa 'wakipigia debe' uwekezaji huo, kwa madai kwamba utaongeza uzalishaji wa chakula na kuongeza ajira kwa Watanzania.

WANANCHI
Watendaji wa vijiji na Kata zinazozunguka maeneo hayo, wamepinga uwekezaji huo kwa maelezo kwamba hawajashirikishwa kikamilifu na hati hiyo haina maslahi kwa taifa.

Wakizungumza na waandishi wa habari walioongozana na timu ya watafiti kutoka shirika la HakiArdhi kuhusiana na uwekezaji huo, viongozi hao na wananchi wameitaka serikali ijifunze kwa yaliyotokea kwa kampuni tata ya Dowans kwa kujifunga na mikataba mibovu, ya muda mrefu kwa bei chee.
Mwekezaji pia anaitaka serikali ibadili sheria ili kuruhusu kilimo cha vinasaba (Genetically Modified Crops), ambacho kimsingi kinaua mbegu za asili na kudhoofisha ardhi.

Diwani wa kata ya Litapunga, Godfrey Lusambo, alisema madiwani wa kata zinazozunguka eneo hilo, hawakuwahi hakualikwa kwenye mikutano iliyopitisha makubaliano hayo tata wala kwenda kwenye ziara nchini Marekani.

Viongozi wa wilaya wakiongozwa na Katibu Tawala wa Mkoa, Wenyeviti wa kamati na Madiwani wa kutoka mbali na hapa kama vile Mpimbwe na Ulwila ndio waliokwenda Iowa- Marekani na waliporudi tu sisi tukawa tunaletewa maagizo bila kujua undani wake, alisema.

Msafara wa wajumbe kumi waliokwenda Iowa-Marekani uliongozwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa, Salum Chima, Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Rajabu Rutenge, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mpanda, Philip Kalyalya, Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mpanda Silvester Nswima, Mkurugenzi wa Wilaya Eng. Emmanuel Kalobelo, Mjumbe wa kamati ya fedha Rose Mayaya, na Mjumbe wa Kamati ya maadili Teddy Nyambo.

Wengine ni Mwanasheria wa Halmashauri Patrick Mwakyusa, Afisa Kilimo na Mifugo Fabian Kashindye, na Haruna Mwakitanile (cheo hakikuweza kupatikana mara moja).

Alisema wajumbe hao waliporudi kutoka Marekani, wananchi walishangazwa na kitendo cha Serikali kutenga mipaka kwa ajili ya mwekezaji wakati vijiji hivyo havijawahi kupimwa.

Ofisa Mtendaji wa kata ya Mishamo, Agustino wanga, alisema hawajawahi kuiona kampuni ya AgriSol wala wawakilishi wao ambao ni Agrisol Tanzania Limited, na kwamba wamekuwa wakiwasikia viongozi wakieleza kuwa makazi hayo ya wakimbizi yatakodishwa kwa Wamarekani kwa miaka 99.

Mimi binafsi nina mpango wa kuhama kabisa maana wakiondoka wakimbizi tu, huduma muhimu nazo zitakoma, hatuwezi kuwezana na mwekezaji ambaye hatumjui, alisema.

Kwa upande wake, Katibu wa jumuiya ya wafugaji mkoani Rukwa, Masanja Katambi, alisema inashangaza kuona serikali inaingia mkataba usio na maslahi kwa taifa badala ya kuwapatia wafugaji maeneo hayo ambao wamekuwa wakigombea malisho na wakulima.

Kila siku wafugaji wanagombana na wakulima na mara nyingine kuuana, kwa sababu ardhi haitoshi katika mkoa wetu. Wafugaji hudiriki hata kuwahonga askari wa wanyamapori katika mbuga ya Katavi ili kuingiza mifugo yao kwa malipo maalumu, hili Serikali hailioni? alisema.

Mkuu wa Makazi ya Katumba na Mishamo, Athuman Igwe, alisema anachosubiri ni kutekeleza amri ya serikali pindi taratibu za uwekezaji zitakapokamilika.

Hata hivyo, alisema wakimbizi walipaswa kuwa wameondoka kupisha uwekezaji lakini anashangaa kuona kuwa bado zoezi hilo halijakamilika mpaka hivi sasa.

Hili Zoezi la kuwahamisha wakimbizi linaratibiwa na Tamisemi, sisi tunasubiri utekelezaji tu, alisema mkuu huyo ambae pia ni mratibu wa makazi ya Ulyahulu yaliyopo Kigoma.

Alifafanua kwamba kikwazo ni wakimbizi ambao wanataka walipwe Sh. 19 milioni kila mmoja kama fedha za uhamisho badala ya Sh. 300,000 walizopangiwa.

Mmoja wa wakimbizi, Andrea Helmashi, alisema Sh. 300,000 ni ndogo kwa kuwa wengine wanafamilia ya watu zaidi ya 10 na kupendekeza kwamba wangelipwa Sh. 13 milioni.

SERIKALI INASEMAJE

Mkuu wa Wilaya ya Mpanda, Rajab Rutenge, alitetea uwekezaji huo akieleza kwamba ni wa faida kubwa kwa taifa na wakazi wa maeneo yanayozunguka makazi hayo kwani utaboresha upatikanaji wa chakula nchini.

Mimi ni mtalaamu wa masuala ya chakula na nchi yetu inakabiliwa na janga la njaa, ni lazima tushirikiane na kampuni ya Agrisol kumaliza tatizo hilo, alisema.

Kwa upande wake, Mwanasheria wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda ambaye ni mmoja wa waliotia saini makubaliano hayo, Patrick Mwakuysa, alisema kampuni hiyo ina lengo la kuongeza uzalishaji wa chakula, masoko na kutengeneza ajira kwa Watanzania.

CHANZO: GUARDIAN ON SUNDAY
 
Kikwete hatutakusamehe wewe na kizazi chako, kwa hili.
Sitaki sitaki kusikia ukitetewa kuwa wafasaidizi wako wamekudanganya.
Umeiuza nchi yetu, mchana kweupe.
 
Tupunguze siasa sasa ni wakati wa kuangalia manufaa ya vitu vinavyofanyaka
sio kwa sababu kikwete na serikali yake wamekuwa wachemshashi basi kila kitu ni washemshaji
ili wamepatia labda tu cha kuoji ni huo mkataba unasemaje lakini wawekezaje wameshaweka wazi
wanalima kwa ajili ya TANZANIA na AFRIKA kwa ujmla sasa tunachotaka ni nini kama sio kilimo cha kisasa
ili kupata chakula kwa bei nafuu?

hii ni move nzuri na inafaa pongezi hiyo ardhi ikijaa miti au kilimo cha mkono kwa miaka 99 kuna faida gani?
kwanza hao jamaa kulima na kusababusha chakula kupatikana kwa uhakika sio faraja?

sio kila kitu kina faida ya moja kwa moja wakiti mwingine faida yake ni ile huduma inayokuja kutolewa kwa mfano hapa chakula nafuu na cha ukakika
 
Ni ule mwekezaji aliyepewa ardhi kwa miaka 99
headline_bullet.jpg
Kodi ya ardhi sh. 200, Halmashauri kupata sh.500





MpandaArdhi.jpg

Diwani wa kata ya Litapunga, Godfrey Lusambo (kulia) akiwa na viongozi wa serikali ya mtaa na wanakijiji cha Kambuzi Halt, Katumba, wilaya ya Mpanda, wakilalamika kwa watafiti wa Shirika la Haki Ardhi na waandishi wa habari.


Wananchi, watendaji wa vijiji na Madiwani wa kata za Litapunga na Mishamo Wilayani Mpanda, Mkoa mpya wa Katavi, wamepinga yaliyokuwa makazi ya wakimbizi ya Mishamo na Katumba, kukodishwa kwa mwekezaji ambaye ni kampuni ya Agriosol ya Marekani, kwa maelezo kwamba uwekezaji huo, hautakuwa na tija kwa taifa.
Makubaliano ya awali (ambayo NIPASHE inayo nakala yake), kati ya mwekezaji huyo na Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda, yanaonyesha kwamba kampuni ya Agrisol itakodisha kwa miaka 99, eneo la Katumba hekta 80,317 na Mishamo hekta 219,800.
Mwekezaji pia atalipa Sh. 200 kama kodi ya ardhi kwa ekari na Halmashauri itapata Sh. 500 kwa ekari, hata hivyo haijulikani malipo hayo yatalipwa kwa muda gani yaani kwa mwezi au kwa mwaka.
Makubaliano hayo yanaonyesha pia kwamba iwapo kutatokea mgogoro, serikali itatumia busara kuutatua lakini ikishindikana, shauri hilo litasikilizwa jijini London, Uingereza na msuluhishi ambaye atakuwa Chemba ya Biashara ya Kimataifa (International Chamber of Commerce).
Kadhalika, inaelezwa kwamba mwekezaji huyo ataajiri mameneja wa mashamba kutoka nje hususan Afrika Kusini na ataendesha kilimo cha mbegu za kimaabara.
Hata hivyo, baadhi ya viongozi wa serikali wakiwemo Mawaziri na wale wa Halmashauri ya Mpanda, wamekuwa 'wakipigia debe' uwekezaji huo, kwa madai kwamba utaongeza uzalishaji wa chakula na kuongeza ajira kwa Watanzania.

WANANCHI
Watendaji wa vijiji na Kata zinazozunguka maeneo hayo, wamepinga uwekezaji huo kwa maelezo kwamba hawajashirikishwa kikamilifu na hati hiyo haina maslahi kwa taifa.
Wakizungumza na waandishi wa habari walioongozana na timu ya watafiti kutoka shirika la HakiArdhi kuhusiana na uwekezaji huo, viongozi hao na wananchi wameitaka serikali ijifunze kwa yaliyotokea kwa kampuni tata ya Dowans kwa kujifunga na mikataba mibovu, ya muda mrefu kwa bei chee.
Mwekezaji pia anaitaka serikali ibadili sheria ili kuruhusu kilimo cha vinasaba (Genetically Modified Crops), ambacho kimsingi kinaua mbegu za asili na kudhoofisha ardhi.
Diwani wa kata ya Litapunga, Godfrey Lusambo, alisema madiwani wa kata zinazozunguka eneo hilo, hawakuwahi hakualikwa kwenye mikutano iliyopitisha makubaliano hayo tata wala kwenda kwenye ziara nchini Marekani.
“Viongozi wa wilaya wakiongozwa na Katibu Tawala wa Mkoa, Wenyeviti wa kamati na Madiwani wa kutoka mbali na hapa kama vile Mpimbwe na Ulwila ndio waliokwenda Iowa- Marekani na waliporudi tu sisi tukawa tunaletewa maagizo bila kujua undani wake,” alisema.
Msafara wa wajumbe kumi waliokwenda Iowa-Marekani uliongozwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa, Salum Chima, Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Rajabu Rutenge, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mpanda, Philip Kalyalya, Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mpanda Silvester Nswima, Mkurugenzi wa Wilaya Eng. Emmanuel Kalobelo, Mjumbe wa kamati ya fedha Rose Mayaya, na Mjumbe wa Kamati ya maadili Teddy Nyambo.
Wengine ni Mwanasheria wa Halmashauri Patrick Mwakyusa, Afisa Kilimo na Mifugo Fabian Kashindye, na Haruna Mwakitanile (cheo hakikuweza kupatikana mara moja).
Alisema wajumbe hao waliporudi kutoka Marekani, wananchi walishangazwa na kitendo cha Serikali kutenga mipaka kwa ajili ya mwekezaji wakati vijiji hivyo havijawahi kupimwa.
Ofisa Mtendaji wa kata ya Mishamo, Agustino wanga, alisema hawajawahi kuiona kampuni ya AgriSol wala wawakilishi wao ambao ni Agrisol Tanzania Limited, na kwamba wamekuwa wakiwasikia viongozi wakieleza kuwa makazi hayo ya wakimbizi yatakodishwa kwa Wamarekani kwa miaka 99.
“Mimi binafsi nina mpango wa kuhama kabisa maana wakiondoka wakimbizi tu, huduma muhimu nazo zitakoma, hatuwezi kuwezana na mwekezaji ambaye hatumjui,” alisema.
Kwa upande wake, Katibu wa jumuiya ya wafugaji mkoani Rukwa, Masanja Katambi, alisema inashangaza kuona serikali inaingia mkataba usio na maslahi kwa taifa badala ya kuwapatia wafugaji maeneo hayo ambao wamekuwa wakigombea malisho na wakulima.
“Kila siku wafugaji wanagombana na wakulima na mara nyingine kuuana, kwa sababu ardhi haitoshi katika mkoa wetu. Wafugaji hudiriki hata kuwahonga askari wa wanyamapori katika mbuga ya Katavi ili kuingiza mifugo yao kwa malipo maalumu, hili Serikali hailioni?” alisema.
Mkuu wa Makazi ya Katumba na Mishamo, Athuman Igwe, alisema anachosubiri ni kutekeleza amri ya serikali pindi taratibu za uwekezaji zitakapokamilika.
Hata hivyo, alisema wakimbizi walipaswa kuwa wameondoka kupisha uwekezaji lakini anashangaa kuona kuwa bado zoezi hilo halijakamilika mpaka hivi sasa.
“Hili Zoezi la kuwahamisha wakimbizi linaratibiwa na Tamisemi, sisi tunasubiri utekelezaji tu,” alisema mkuu huyo ambae pia ni mratibu wa makazi ya Ulyahulu yaliyopo Kigoma.
Alifafanua kwamba kikwazo ni wakimbizi ambao wanataka walipwe Sh. 19 milioni kila mmoja kama fedha za uhamisho badala ya Sh. 300,000 walizopangiwa.
Mmoja wa wakimbizi, Andrea Helmashi, alisema Sh. 300,000 ni ndogo kwa kuwa wengine wanafamilia ya watu zaidi ya 10 na kupendekeza kwamba wangelipwa Sh. 13 milioni.
SERIKALI INASEMAJE
Mkuu wa Wilaya ya Mpanda, Rajab Rutenge, alitetea uwekezaji huo akieleza kwamba ni wa faida kubwa kwa taifa na wakazi wa maeneo yanayozunguka makazi hayo kwani utaboresha upatikanaji wa chakula nchini.
“Mimi ni mtalaamu wa masuala ya chakula na nchi yetu inakabiliwa na janga la njaa, ni lazima tushirikiane na kampuni ya Agrisol kumaliza tatizo hilo,” alisema.
Kwa upande wake, Mwanasheria wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda ambaye ni mmoja wa waliotia saini makubaliano hayo, Patrick Mwakuysa, alisema kampuni hiyo ina lengo la kuongeza uzalishaji wa chakula, masoko na kutengeneza ajira kwa Watanzania.



CHANZO: GUARDIAN ON SUNDAY

​

[/QUOTE
Ahsante kwa taarifa hii ya nyongeza, itawasaidia wanaodhani huu ni uwekezaji kama wa Dubai
 
Hii ni nzuri sana!

Modern farming comes to Tanzania at last.

* more food
* employment for rural workers
* opportnity for Tanzanian's to learn how it is done
* real agricultural research, as opposed to pathetic reserach currently done
* industries will spin off to process the output of these farms

Tunahitaji waje wengi zaidi.

Una mawazo kama Ki-Kwe-te


hapana yuko sahihi
TAIFA KWANZA SIASA BAADAYE
 
Utapiamlo utaongezeka kwani watakacholima hakinunuliki na watz wa kawaida. Ukifuatila kilimo huko ulaya na marekani, wakulima hupewa ruzuku na serilkali zao ili kupunguza bei kwa mlaji kwa maana gharama ya kuzalisha kwa kutumia mashine haikwepeki kwani mashine huwezi kuinyonya.
Kama mnakumbuka kuna wakati baba wa taifa aliwaambia wazungu kuwa kama ni kuondoa ruzuku kwenye kilimo wote tuonde halafu tuona nani atashindwa kwenye soko. Wazungu wakaogopa wakijua wakiondoa ruzuku kwenye kilimo bei itapanda sana na hivyo serikali zao zitaangushwa; lakini kwetu walitulazimisha wakisema kama hamuondoi ruzuku hatuwapi misaada.
Hivyo ndugu yangu, kama kampuni itakuja kuzalisha kwa technolojia ya kisasa, na kwa kuwa serikali yetu haitaweza kuweka ruzuku, bei itakuwa kuchaa na watz wa kawaida hawatamudu.

Kwa kuwa kampuni hiyo ni ya nje basi mazao yakipelekwa huko kwao yatapewa ruzuku kama yamezalishwa huko na yataweza kununuliwa.
Ukitaka kujua zaidi ruzuku kwa kilimo just google agricultural subsidy in USA. Hapo utapata yafuatayo:
European Union

In 2010, the EU spent €57 billion on agricultural development, of which €39 billion was spent on direct subsidies.[SUP][1][/SUP] Agricultural and fisheries subsidies form over 40% of the EU budget.[SUP][2][/SUP] Since 1992 (and especially since 2005), the EU's Common Agricultural Policy has undergone significant change as subsidies have mostly been decoupled from production

United States
The United States currently pays around $20 billion per year to farmers in direct subsidies as "farm income stabilization"[SUP][9][10][11][/SUP] via U.S. farm bills. These bills date back to the economic turmoil of the Great Depression with 1922 Grain Futures Act, the 1929 Agricultural Marketing Act and the 1933 Agricultural Adjustment Act creating a tradition of government support. A Canadian report claimed that for every dollar U.S. farmers earn, 62 cents comes from some form of government, with total aid in 2009 from all levels of government adding up to $180.8 billion.[SUP][12][/SUP]

Huko ni marekani na ulaya wana mambo mengi ambayo sisi hatuna kama vile standard ya shamba na tozo kwenye ardhi ndio maana wamepewa kwa bei nafuu

hapa watu wanapina kelele kwamba jamaa wape lease kwa bei kubwa lakini wanasahau kwamba hatakaye lipa hizo ghalama ni mlaji sio mfanyabishara au mkulima maana jamaa lazimi waweke bei itakayowawezesha kufikia BREAK EVEN POINT na faida sasa mnataka lipi?

tufananishe vitu vyenye uwiano sio kuongea tu kilimo cha marekani au ulaya katika ghalama hakizi kulingana na cha tanzania
 
Mi naona lenye Mwanzo na hata lina Mwisho. Lakini Nguvu ya Umma one day itageuka na tutapata ukombozi wa kuwa huru kweli kweli.
 
Afadhali hata hao wakija tutapata chakula na kupunguza utapiamlo, kuliko tuliowapa madini wanakamua peke yao sisi tunaishia kuomba chakula cha msaada. Nchi ishauzwa hii, we fikiria hapo jamaa hadi kuruhusi ardhi yote hiyo kakatiwa bei gani?

Mkuu, hiyo afadhali unayoisema iko wapi? Hivi unajua hizo ekari 800,000 ni sawa na asilimia ngapi ya ardhi inayofaa kwa kilimo hapa TZ? Pili kumbuka watapata lease ya miaka 99!!!! (Karne nzima) takribani vizazi viwili.

Wakatti huo watanzania watakuwa wangapi? ambao kati yao tuseme 70% watataka kulima lakini ardhi yao itakuwa mikononi mwa wazungu. Hicho Mkuu ni KIAMA kwa nchi na vizazi vyake.
 
Back
Top Bottom