DOKEZO Soko la Ilala, Dar es Salaam kwa uchafu huu itakuwa chimbuko la kipindupindu kama cha Msumbiji. Lifungwe

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Rwebo

JF-Expert Member
Oct 17, 2015
980
1,146
Wakuu, kwa wakazi wa jiji la Dar tunatumia SOKO la Ilala kujipatia mahitaji yetu pale, ni aibu na udhalilishaji wa binadamu kuona binadamu anaweza kununua kitu cha kwenda kula toka pale.

SOKO hili lipo kama mita 150 toka ofisi ya mkuu wa mkoa Dar es Salaam na km 5-6 toka Ikulu ya Magogoni. Kwa wale wafugaji wa ng'ombe watanielewa nikisema SOKO hili Sasa hivi ni sawa na zizi la ng'ombe.

Lojo mpaka kwenye ugoko. Viongozi wetu muone aibu kuwa na SOKO kama hili chini yako.

Wewe bwana / bi afya wa mkoa na wilaya hata Waziri wa afya ikitokea kipindupindu kikalipuka toka pale mtabeba 'dhambi' hiyo.

Na Uongozi wa jiji la Ilala kweli mmelala amkeni.
 
Mvua ikinyesha tu watumiaji wa lile soko tunageuka kambale......ni mwendo wa kuswim kwenye tope
 
Back
Top Bottom