DOKEZO Dar: Soko la Ilala ni Chafu, Miundombinu Mibovu, Vyakula Vinauzwa Matopeni

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Nimepita leo kwenye soko la vyakula la Ilala Boma maarufu kama Ilala Sokoni, jamani tunalishwa uchafu hili jiji kwanza nashangaa kwa hali hii kama kweli Dar haina wagonjwa wa Kipindupindu. Wauza Vyakula tena Vibichi wanakaa chini, wanatembea peku wengine, sehemu za kuuzia bidhaa (Vizimba) hakuna.

Cha kusikitisha zaidi Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar yuko mita 50 tu kutoka hapo. Yaani anatengenishwa na Barabara tu. Lakini huko hajawahi kukanyaga kwenda kuangalia Wananchi wake wanafanya biashara katika mazingira gani na walaji wanalishwa nini na kwa style gani.

Badala ya kutumia nguvu kubwa kuelekeza usafi ufanywe kwenye mitaa, Mkuu wa mkoa anapaswa kuagiza usafi kwenye masoko maana huko ndio kuna shida kubwa.

Nimeambatanisha picha chini wakati naenda kununua matunda kwa kweli nimeahirisha na staki tena kula leo.

IMG_20240118_082912.jpg
IMG_20240118_083329.jpg
IMG_20240118_083331.jpg
IMG_20240118_083357.jpg


SOKO HILI LIMEWAHI RIPOTIWA MWEZI APRILI 2023: DOKEZO - Soko la Ilala, Dar es Salaam kwa uchafu huu itakuwa chimbuko la kipindupindu kama cha Msumbiji. Lifungwe
 
Back
Top Bottom