Soda za kampuni ya Coca Cola si salama tena, angalia picha

Soda za kampuni ya Coca Cola si salama tena, angalia picha

Wewe utakuwa mhujumu wa kwanza.Mdudu mkubwa kiasi hicho na soda imefikia robo tatu kweli tupate kuamini unayoyasema kwa tukio hilo.

Pamoja na kuwa kuna uzembe na hili jambo siyo la kushangaza na siyo geni ,lakini kuna walakini kwenye picha unayotaka kutumia kutushawishi.


Coca Cola amkeni tumieni majukwaa kama haya kuboresha product zenu
.

Sass hutaki kuamini au.mbona unabosha vitu vya maana.we endelea kunywa kivyako
 
Ni hali ya kusikitisha sana kwa uzembe unaofanywa na kampuni ya coca cola katika suala zima la usafi na packaging. Jana nimefungua hiyo fanta passion nimekuta mdudu mfano Wa funza ndani, wiki iliyopita rafiki yangu alikunywa tangawizi ndani akakuta kisoda kimekunjwa kiko ndani.

Hali kama hio ni hatari sana kwa afya nafikiri hii kampuni anayeindesha ama anahujumiwa au hayuko makini. Mimi nathubutu kusema hizi sio soda sahihi kunywa.

Tanzania kuna viwanda zaidi ya kimoja vinavyotengeneza soda jamii ya Coca Cola; unaposema soda za coca ni chafu bila kusema zilizotengenezwa na kiwanda kipi unakuwa umewavunjia heshima na kuharibu soko la viwanda vingine vinavyotengeneza soda jamii ya coca cola
 
Pepsi wenyewe Ndo hoi kabisa. In general soda zote sio nzuri
 
Kweli uafisa masoko inataka uwe mbunifu na si kutumia mbinu za Akina changoja na kova kwenye biashara.
 
Any way yawezekana ni kweli anachosema mtoa mada,au si kweli ni fitina tu! za kibiashara,lakini yote kwa yote wahusika wafanyie kazi habari hii,maana Lisemwalo lipo na km halipo basi lipo njiani linakuja.

muwe reasonable jamani awe na fitina kwa manufaa gani?Coca ni Company kubwa hawezi kuwa na hila nayo ingekuw biashara binafsi sawa..cha msingi ni kuchuja tunachoambiwa na kuchukua hatua.
 
weeeee japo inaweza kuwa kweli bt weledi wa hii kampuni unajulikana kimataifa na umakini wao uko juu mara nyingi. Otherws unaweza kuwa umetumwa.

Sound reasonable my friend being big and incognito company doesnt mean hawana mapungufu..we ndio umetumwa.
 
profilepic41512_1.gif
mbna mnamshambulia mtoa mada ilihali ndo mambo yalivyo.Cha msingi tuwe makini tunapoagiza vinywaji, hasa vinavyopakiwa.
 
Mm nauza sodo nishawarudishia sana soda Kama hizo wawe makini sana na afya za watu
 
Vitu hivyo huwa vinatakiwa! Kikubwa ni kujua ni kujua ni hatua gani ya kuchukua ukipatwa na balaa hilo?
 
Ni hali ya kusikitisha sana kwa uzembe unaofanywa na kampuni ya coca cola katika suala zima la usafi na packaging. Jana nimefungua hiyo fanta passion nimekuta mdudu mfano Wa funza ndani, wiki iliyopita rafiki yangu alikunywa tangawizi ndani akakuta kisoda kimekunjwa kiko ndani.

Hali kama hio ni hatari sana kwa afya nafikiri hii kampuni anayeindesha ama anahujumiwa au hayuko makini. Mimi nathubutu kusema hizi sio soda sahihi kunywa.

Kama upo dar,mwanza wapelekee uwaambie wainywe, wakigoma nenda tbs waambie woote ni mburula
 
Back
Top Bottom