Ni hali ya kusikitisha sana kwa uzembe unaofanywa na kampuni ya coca cola katika suala zima la usafi na packaging. Jana nimefungua hiyo fanta passion nimekuta mdudu mfano Wa funza ndani, wiki iliyopita rafiki yangu alikunywa tangawizi ndani akakuta kisoda kimekunjwa kiko ndani.
Hali kama hio ni hatari sana kwa afya nafikiri hii kampuni anayeindesha ama anahujumiwa au hayuko makini. Mimi nathubutu kusema hizi sio soda sahihi kunywa.
Nini faida ya soda mwilini?
Inategemea na Mfumo wa diet yako...
Soda zina tabia ya kuongeza nguvu mwilini kwa virutubisho fulani (mfano Sukari),huku zikipunguza virutubisho vingine vya msingi.
Kama una-diet MBAYA unywaji wa kupitiliza unaweza kukuletea kisukari,matatizo ya figo au unene wa kupitiliza.
muwe reasonable jamani awe na fitina kwa manufaa gani?Coca ni Company kubwa hawezi kuwa na hila nayo ingekuw biashara binafsi sawa..cha msingi ni kuchuja tunachoambiwa na kuchukua hatua.
sure.ila jamaa katumwa kweliHili jambo ni la kawaida kabsa kwenye soda zote iwe za coca ama za pepsi ukiacha hilo la uchafu pia mchanganyiko wake.c mzr so nashauri.watu kutumia maji ama juic za kubrend mwenyewe
sure.ila jamaa katumwa kweli
Sidhani kama,kampuni kubwa kama coca cola ikakubali kushusha hadhi yake kwa uzembe wa staili hii,haiwezekani kufunga soda ktk kiwanda ikiwa na kisoda ndani unless ilifunguliwa kwanza,hawa jamaa wako makini sana, watanzania tupende kufuatilia haya mambo na kua na fact,bora useme wameongeza kiasi cha maji au kemikali fulani sio habari za funza na visoda...I think huko ulikonunua ndio wamefanya hivyo kwa kutokua waaminifu na wateja wao.
Unless umenunua kiwandani hiyo fanta,am not convinced YET.....
Alafu hili suala la kuchukia soda sijui limezuka wapi??? Em tupeni facts jamani,coz hata maji si salama.
Tanzania kuna viwanda zaidi ya kimoja vinavyotengeneza soda jamii ya Coca Cola; unaposema soda za coca ni chafu bila kusema zilizotengenezwa na kiwanda kipi unakuwa umewavunjia heshima na kuharibu soko la viwanda vingine vinavyotengeneza soda jamii ya coca cola
Inapunguza hatari ya kupata ukimwi,bcoz unaua "GEGEDEO SYSTEM!!Nini faida ya soda mwilini?