Sms iliyoniumiza kupita zote

Mwanamke wa kukaa na vitu moyoni sio kabisa. Mi mke wangu nimemfanya kama rafiki, yupo wazi sana nami pia. Japo mikwaruzano ya hapa na pale haikosekani.

You well said kaka. That is it. Keep it up! Ulimbukeni wa mapenzi. Kwa kifupi ni infatuation ambayo ni kupenda kwa kutokujitambua zamani wanasema limbwata. Unakuwa jinga na kila saa na dakika unamuwaza mtu mwingine na hata unajisahau mwenyewe. Mbaya sana. Huu ni utumwa katika mapenzi.
 
Mkuu kama ni kweli mwonyeshe upendo mwenzio, onyesha unamjali kwa vitendo pia
 
Yote Mia...hapo pa barua uchumba mzee...dah sijuii bhana..ila ingekuwa vice versa ungeleta uzi hapa
 
Kupigwa kibuti nilisha wahi pigwa na ninayempenda zaidi kwa kunitumia sms fanya mambo yako, mimi na wewe basi! sikupata kuumia kama hii sms ya mpenzi wangu wa sasa ambayo si ya kunipiga kibuti!
sms yenyewe ni hii:
Sema July! pole kwa uchovu wa jana! mwaka unaisha sasa tunaanza mwaka mpya muda si mrefu kama tukibahatika, ila kuna mambo manne ulinifanyia mwaka huu yalinikera sana japo sikusema ningependa kuona hayajirudii mwakani kama tutabahatika kuuona!
1. kumbuka mwezi wa tatu kunasiku ulitokea Riverside kwenye kikao ukanipitia Mwenge tukaenda Don bosco baadae posta na kurudi tena Don bosco, nilikulipia nauli muda wote huo nikabakiwa na mia tano tu, nikakuomba tutembee kwa muguu mpaka magomeni ili nipande gari za Mabibo nikidhani utauliza kwa nini tutembee kwa muguu ni kujibu sina nauli badala yake ukakubali tukatembea hadi magomeni sema kweli niliumia sana na niliumwa miguu wiki nzima bila nafuu! naomba isijirudie jaribu kunijali kama nami nifanyavyo kwako!
2. Kuna siku nilipata taarifa za kweli ulitaka kupeleka barua ya uchumba kwa mtu tofauti na mimi huku uko kwenye mahusiano ya kimapenzi nami niliumia sana japo sikusema.
3.Nilipo ugua mwezi wa tisa nikakutumia sms kuwa naumwa sikua na senti hata kidogo, ukaishia kusema pole bila kujua naponaje ilinilazimu kukopa kinyume na jadi yangu napo niliumia sana!
4.Nilipo kuwa na birthday pamoja na wewe kunipatia fedha ila hukufika niliumia sana japo nilikubaliana na taarifa yako kuwa hutofika uliyoitoa dakika za mwisho naomba lisijirudie mwakani!
Ndugu zangu wana jamvi sikupata kujua alikuwa anakereka moyoni hata kidogo kwa lolote maana alionekana mwenye furaha muda wote, na siku tunatembea kwa muguu nilijua namsaidia kufanya zoezi maana fedha sio siri ilikuwepo si tu kupanda dala dala bali hata kukodi tax! lakini hakupata kusema mpaka jana alipo nitumia hiyo sms niliumia sana kila muda nawaza juu ya sms hii na hakuna aliloongopa yote ni kweli! hata jibu hapa sina najibuje sasa?
fanya haya.....
1.peleka posa kwao kabla ya nusu mwaka yaani kabla mwezi wa 6 2014
2.ikipokelewa lipa mahali kabla ya robo ya yayu ya mwaka 2014 haijaisha
3.katika siku alizo kutumia huo ujumbe wa kukukumbusha uliyoyafanya Muoe huyo ni mke mwema.....
 
Soma vizuri ushauri wangu na utilie maanani. Mapenzi sio utumwa kwamba ukose uhuru wa kufanya mambo yako. Yeye atakuwepo na anatakiwa kujua kuwa una uhuru wa kufanya chochote - free will -- na hata yeye ana free will yake. Hiyo hakuna binadamu anatakiwa kuingilia - si mama wala baba wala mke na hata Mungu anaiheshimu hiyo. Ukipoteza hii mara moja unakuwa katika hali uliyonayo sasa - tayari umeshajisahau na hujifahamu tena kwani unatumia muda wako wa kufanya free will kufikiria mambo yake na yeye ama kwa hakika hafikirii chochote kukuhusu wewe ndio maana hakukuambia wakati mambo yanatokea kwa kuwa alikuwa anatumia muda wake kufanya mambo yake. Sasa kwa dakika kama 10 tu ametumia kukufikiria na kukuharibia mwaka. Ona free will inavyofanya kazi. Wa kupoteza ni wewe na yeye hana cha kupoteza, muda wake kautumia vizuri kwa mambo yake na sasa dakika chache tu kakumaliza -- FUNGUKA acha uzembe. Vijana wa karne hii hawawazi tena hivyo kama wewe kuwa HURU! Tafuta marafiki kadri free will yako inakutuma na atakayekufanya na furaha muda wote - huyo ndio bana naye.

Nitakupa mfano: sms hizo kama angekuwa hana passive aggressive disorder angeandika hivi:
1. kumbuka mwezi wa tatu kunasiku ulitokea Riverside kwenye kikao ukanipitia Mwenge tukaenda Don bosco baadae posta na kurudi tena Don bosco, nilikulipia nauli muda wote huo nikabakiwa na mia tano tu, nikakuomba tutembee kwa muguu mpaka magomeni ili nipande gari za Mabibo nikidhani utauliza kwa nini tutembee kwa muguu ni kujibu sina nauli badala yake ukakubali tukatembea hadi magomeni sema kweli niliumia sana na niliumwa miguu wiki nzima bila nafuu! naomba isijirudie jaribu kunijali kama nami nifanyavyo kwako!
SAHIHI: Nakupenda sana, na nakumbuka siku ile tulivyotembea kwa miguu ilikuwa zoezi zuri natamani siku nyingine tufanye tena mwakani.

2. Kuna siku nilipata taarifa za kweli ulitaka kupeleka barua ya uchumba kwa mtu tofauti na mimi huku uko kwenye mahusiano ya kimapenzi nami niliumia sana japo sikusema.
SAHIHI: Ingawa wewe ni mtu huru kifikra nakupenda sana na natamani siku moja tutakuwa pamoja. Nijibu kama wanipenda zaidi yangu.

3.Nilipo ugua mwezi wa tisa nikakutumia sms kuwa naumwa sikua na senti hata kidogo, ukaishia kusema pole bila kujua naponaje ilinilazimu kukopa kinyume na jadi yangu napo niliumia sana!
SAHIHI: Nakutakia mwaka huu ujao mpenzi tupate fedha za kutosha - sitaki kukumbuka kipindi kile nilipoumwa na wote hatuna fedha. Mwaka huu ujao uwe na mafanikio.

4.Nilipo kuwa na birthday pamoja na wewe kunipatia fedha ila hukufika niliumia sana japo nilikubaliana na taarifa yako kuwa hutofika uliyoitoa dakika za mwisho naomba lisijirudie mwakani!
SAHIHI: Mwaka ujao tuwe na muda pamoja zaidi na tupange mipango na kufurahia pamoja

Sasa ukiangalia mifano niliyoweka utaweza kuona jinsi alivyo na personality disorder. Nimekusaidia tu bure bila faranga.

Mapenzi si malalamiko. Usikubali. MAapenzi ni kila mtu kufanya responsibilities zake na kisha mnakutana kwa maongezi na kubadilisha mawazo na of course the thing. Hii ndio love. Kama love ni kuchukua mizigo basi ni aheri wanaume wote wangekuwa na orphanage centres kwani hawa wanahitaji msaada wa fedha zaidi.

Asante

Nashukuru kwa ushauri wako ntatumia baadhi tu katika mazungumzo yangu naye lakini pia umewafanya wengine wajifunze big up!
 
fanya haya.....
1.peleka posa kwao kabla ya nusu mwaka yaani kabla mwezi wa 6 2014
2.ikipokelewa lipa mahali kabla ya robo ya yayu ya mwaka 2014 haijaisha
3.katika siku alizo kutumia huo ujumbe wa kukukumbusha uliyoyafanya Muoe huyo ni mke mwema.....

nimekuelewa bro nadhani huko mbali na ushauri wa dada yangu naye mfuata mara ya pili kashauri hivi hivi japo yeye hajaweka muda sawa na wako! ahsante!
 
hata kama anafanya kazi lazima uwe unampa mpa hela mara kwa mara

Huu ni uozo wa kifikra kwa sisi wanawake. Tuelimike! Tunda tuwape sisi na tulete taabu duniani kisha fedha watupe sisi kutatua laana tulizozileta kuleee Eden? How come. Kila mtu afe lake na responsibilities zake. Criteria ya wanawake kudai fedha ni nini ikiwa wote wanakaa darasani na kupata kazi na mishahara sawa. Kama mtu akaa kigoigoi hajishughulishi aende magoti huko kuna fedha kibwena. Tusiwasumbue wanaume kila mara na kufanya hii dunia chungu kwao, hata life expectancy ya wanaume duniani ni chini kwa sababu ya wanawake - too stressful to be loved!
 
Yaani unalipiwa tu nauli hata humuungishi kumlipia hapa na pale, ukaona

Mpenzio anaumwa unaishia kumpa pole? Hata kumuona, kumuuliza kama kaenda hospitali? Kama ana pesa ya hospitali?
Ukaona heri umpe hela ya birthday badala ya hospitali???

Halafu ukarnda kujitambulisha kwingine??

Khaaaaaaaa

Alipaswa kukwambia mwaka 2014 uache ubinafsi na kutojali wengine
U
 
nimekuelewa bro nadhani huko mbali na ushauri wa dada yangu naye mfuata mara ya pili kashauri hivi hivi japo yeye hajaweka muda sawa na wako! ahsante!
huwezi kujua muda wa kumaliza kama huujui muda wa kuanza..........muda ni option tu niliiweka katika kufanya unielewe vizuri thanx comrade for your concern waweza panga vile waona yafaa....be blessed
 
Yaani unalipiwa tu nauli hata humuungishi kumlipia hapa na pale, ukaona

Mpenzio anaumwa unaishia kumpa pole? Hata kumuona, kumuuliza kama kaenda hospitali? Kama ana pesa ya hospitali?
Ukaona heri umpe hela ya birthday badala ya hospitali???

Halafu ukarnda kujitambulisha kwingine??

Khaaaaaaaa

Alipaswa kukwambia mwaka 2014 uache ubinafsi na kutojali wengine
U
sure nimeona kuna makosa ninayo japo si yote kama anavyo dhani yeye!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom