SMS iliyoniamsha.. kuna kusalimika?

Mtu mwenye busara hapuuzi lolote analoambiwa au kusikia hata kama ni la kipumbavu,analitafakari na kulichukulia kama changamoto kwa maisha ya kila siku.
Hayo nayaona ni maono ya kionambali.


Hapo umenena mkuu.. Big up! U'r a great thinker..
 
Hili suala lisipuuzwe tafadhali wahusika kwakuwa mpo humu lifuatilieni maana wakiwamaliza hao itafuata zamu yangu mimi na wewe.
 
Wataua wangapi? Kilio cha ufisadi ni cha watanzania wote; wanapoteza muda labda kama hajui historia ya Afrika Mobutu, Nguema, Bokasa na madikteta wengine waliua wangapi? na waliishia wapi?

Chama
Gongo la Mboto DSM
 
Nimejaribu kutumia mbinu ya kumtumia pesa kupitia M-PESA mwenye namba hiyo inayosambaza ujumbe huyo ni FAUSTINE KABUTA. Nimejaribu kuipiga hiyo namba ila haipatikani hewani! Viongozi wangu wameniambia haiwezi kupatikana kwa sababu huenda akakamatwa!

 
kwa heshima ninayo kupa Mzee MwanaKijiji, hapa nimesoma between the lines, nimekuelewa vyema, kweli kazi ipo !!
 
Jamani kumbukeni mada hii kaileta Mwanakijiji September 5 mwaka 2008. Hiyo namba leo hii inaweza kuwa na mtu mwingine maana hta anamba yangu ya mwaka 2007 sasa hivi ina mtu mwingine kabisa na hatujuani.
 
mwenye namba ni Faustine Kabuta. Igonge kwenye m pesa itakuleta hilo jina. Haya kazi kwenu watu wa usalama wa ccm
 
Jamani hiyo namba yawezekana haikuwa ya huyu bwana keo hii msimsumbue bure na kumletea matatizo.
 
ingawa uli2miwa ujumbe huu mwaka 2008,kilichoandikwa ndicho kilichomtokea mwakyembe....2naweza kusema haikuwa blah blah.
 
Mzee Mwanakijiji,
Kwa kuwa yale yaliyomhusu Mwakyembe yaelekea kutimia, si vibaya ukatujuza ile ilyomhusu Mtatiro.
 
ndugu wana JF kwanza nampongeza Mzee M/Kijiji kwa kuamua ku-disclose sms hiyo, mimi naona amefanya uamuzi sahihi kwa sababu amesaidia kufungua macho ya watu wengi zaidi kupanua hisisa zao. Ufisadi upo na mafisadi wapo.

Kosa moja ambalo sisi wananchi wa TZ tunafanya ni kutokuwa sensitive na hivyo kudharau mambo kirahisi kama tulivyobesa taarifa ya Dr Mwakyembe alipolalamika kuwa anataka kuuawa. Watu walikuja hapa na kumshutumu kuwa wanamfahamu Dr ni mwongo, ni mtu wa ku-pretend kuandamwa ili aonewe huruma, nk.. Sasa Dr Mwakyembe yuko hapo.

Nchi yetu ni tajiri sana, na watu wake wengi ni insensitive, uninformed na ileterate.. mataifa mengine yapo kwenye agenda mpya na zina changamoto mpya na kubwa kama overpopulation, inadequate resources, economical challenges na kadhalika. Lazima nchi yetu itakuwa target nzuri na hivyo ndivyo ilivyo ...tupende ama tusipende..

Kama huyo Ro ni agent wa mataifa ya nje, then kuna wazalendo ambao nao ni agent wa mfumo huo. watu wako tayari kuuza nchi yao kwa mataifa ya nje ili yawaunge mkono katika makusudi yao kutwaa uongozi...

SMS ya M/Kijiji, naomba ituamushe, tuamke na kuwa tayari kukabiliana na hujuma hizo kwa baadhi ya wazalendo wengi kabla hawajateketezwa na kubaki na mafisadi na masikini wasiojuwa nini wanahitaji na nini hawahitaji.
 
Wataua wangapi? Kilio cha ufisadi ni cha watanzania wote; wanapoteza muda labda kama hajui historia ya Afrika Mobutu, Nguema, Bokasa na madikteta wengine waliua wangapi? na waliishia wapi?

Chama
Gongo la Mboto DSM

unataka kumuweka kwenye kundi la kina mabutu hata walomuua nyerere?
 
Zamani ulikuwa unanunua lain kisha unatumia kwa maovu kisha unatupa.Naimani faustine kabuta siye mtumiaji wa namba hiyo kwa 08.Lakini yaliyoandikwa ni muhimu yote....MWAKYMEMBE SIKU YOYOTE ATAPOTEZWA..TUJIULIZE KWA NINI AUMWE SASA?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…