Sleep walking: Tatizo la kuamka ukiwa usingizini na kuanza kutembea ama kufanya vitendo bila kujitambua

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,408
19,033
Ni hali ambayo mtu hufanya vitendo akiwa usingizini bila kujitambua. Vitendo hivyo vinaweza kuwa kuzungumza, kuketi wima kitandani, kwenda msalani, kufanya usafi, kula au kuonyesha vitendo visivyo vya kawaida kama vile kunyakua vitu visivyoonekana hewani n.k. Wakati mwingine mtu anaweza kuonekana akifanya vitu kana kwamba hajalala lakini kiuhalisia bado anakuwa yuko usingizini.

Mtu anapokuwa kwenye hali hiyo hawi na ufahamu wa kawaida. Anaweza kufumbua macho yake na kupepesa lakini uoni wake juu ya mazingira yanayomzunguka huwa tofauti. Anaweza kuwa chumbani kwake lakini akajiona yuko nyumba nyingine tofauti asiyoijua ama yuko eneo geni ambalo hajawahi kufika.

Si vibaya kumwamsha mtu anapokuwa kwenye hali hiyo lakini inaweza kuwa hatari sana endapo ataitikia vibaya kitendo hicho. Hii ni kwa sababu vitu anavyoviona hutafsiriwa tofauti kwenye akili yake, anaweza kuona wewe si binadamu na unataka kumdhuru, kitakachotokea hapo itakuwa habari nyingine!

USALAMA
Si lazima mtu mwenye tatizo hilo kufanya mambo mabaya, lakini kuna visa vingi sana vya matukio ya ajabu ambayo watu wa namna hiyo huwa wanafanya bila kujitambua. Baadhi walikutwa wakifanya vitendo vya aibu wakiwa uchi, wengine walikuwa wakijidhuru wenyewe nyakati za usiku, wapo pia waliowafanyia vitendo vya kinyama watu wengine...

Wengine walikuwa wakitoka nje ya makazi yao usiku wa manane na kutembea umbali mrefu kwenda kusikojulikana.

Wengine walikuwa wakishangaa kuona kazi walizotarajia kufanya asubuhi zikiwa tayari zimefanyika.
Wengine kila kulipokucha walikuwa wakikutana na lawama baada ya kufanya matunyanga yasiyo eleweka usiku wa manane.

VISABABISHI VYA HALI HIYO
  • hurithishwa ikiwa mzazi mojawapo / wote wana hilo tatizo ama lipo kwenye familia zao.
  • tatizo sugu la kukosa usingizi wa kutosha
  • mawazo mengi yanaweza kumfanya mtu kunaongea njiani mwenyewe, wengine hali hii inaendelea usingizini
  • Ndoto, wapo wanaoota huku wanatenda
  • Wengine wamelihusisha tatizo hilo na nguvu za giza lakini sababu hiyo imekosa mashiko mbele ya wataalamu.
 
1701626670921.png
 
Nlikuwa na rafiki yangu yy mshabiki wa Chelsea mm Man U, siku hyo man u wakashinda nkaenda bwenini nikamwamsha tukapiga story kama nusu saa nzima yaan anajadili kbs wachezaji sijui flan huwa hakabi asubuh hajui lolote ananiuliza matokeo
 
Nlikuwa na rafiki yangu yy mshabiki wa Chelsea mm Man U, siku hyo man u wakashinda nkaenda bwenini nikamwamsha tukapiga story kama nusu saa nzima yaan anajadili kbs wachezaji sijui flan huwa hakabi asubuh hajui lolote ananiuliza matokeo
mlikuwa mnapiga story baada ya kuzima taa ama
 
Kuna Dogo alikua na tatizo Hili tukiwa shuleni bweni i yeye anaamka anashuka ngazi mpaka ground floor kutoka ghorofa ya 3
 
Nilikuwa na hilo tatizo kipindi mdogo, ila sijui lilipotelea wapi.... Sjui ndo katika harakati tu za Maisha matatizo mengne nahis huwa yanaamua yakupishe tu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom