Toka jana baada ya mkutano wa CCM pale jangwani na hasa baada ya magufuli kumaliza speech' Kila kona ninayo pita mjadala umekuwa magufuri wananchi wanamuona kama mkombozi wa taifa' Hawataki kusikia kabisa jina Lowassa kutokana na kashifa alizonazo na kifisadi pamoja na kukumbatiwa na matajiri pamoja na afya yake imekuwa tatizo kwani sio siri kwa sasa kila mtanzania ajua lowassa ni mgonjwa na hata weza kupambana na magufuri ambaye anaonekana yuko fiti kila idara.
Zaidi hapo bado wanaendelea kumkumbuka dk slaa kama mtu ambaye angeweza kupambana na magufuri kwani wote wanao uwezo wa kuongea na kujenga hoja tofauti ya sasa ya Lowassa ambae anatakiwa kubebwa katika speech kila sehemu anayokwenda na hawezi kuongea zaidi ya dk 15.
Mkuu nadhani hayo ni maoni yako, kama vile yeyote anaweza kuwa na maoni yake.
Kwa mtazamo wangu niliona Dr Magufuli alikuwa anawapigia debe wapinzani.
Unaposema utajenga au kuchukua viwanda vilivyobinafsishwa vikawa haviendelezwi, Ni nani aliuza au kubinafsisha kama sio CCM.
Mahospital Hayana dawa halafu daktari anaandika ukanunue dukani, hayo yapo ndani ya mfumo wa serikali gani kama sio CCM?
Vitu kadhaa alikuwa anailaumu serikali live na kusema yeye atarekebisha, Anayosema atayafanya kwa umakini inamaana hayafanywi sasa na CCM.
Mambo mengine mazuri kama barabara namuunga mkono ila kazi ipo.
Ukweli apunguze kulaumu maana CCM yake ndio iko madarakani, la sivyo wapinzani watakuja na hoja kwamba wameshindwa for 50 years sasa hawataweza tena.
Hayo mengine ni ya kishabiki tu hayana msingi, ugonjwa ni issue ya personal na daktari aliyemruhasu kufanya kazi anazofanya, ufisadi no comment, mana tunajikuta tunafuata mkumbo tu, wasiompenda wanamuita fisadi na wanaompenda wanasema SIO fisadi.