Slaa: Kikwete akipuuza nchi haitatawalika

Slaa: Kikwete akipuuza nchi haitatawalika

Poor tofyo, unayoongea yote ni hallucinations, sijui unapigaga vigoba vingapi! Mbaya zaidi wewe ni gamba tena la kobe, hata ukijaribu kulivua unamuua kobe mwenyewe. Mwenyekiti wenu anatumia bei gani kwa kila safari? Mengine sioni cha kujibu kwa kweli kwa kuwa ulichoandika ni upumbavu tu!

kama mnashindwa kujibu maswali mepesi mnang'ang'ania siasa ya nini?.na sio wewe tu hakuna punda yoyote anaeweza kujibu.
 
Uliwahi kusikia MOSHI wakipata huduma mbovu?
Halmashauri a Moshi iko chini ya CHADEMA!

mtoto wa hivi bora ubadilishane na chupa tupu la maji.we umeona ktk miji duniani moshi ni kitu gani.we unaona kuna huduma gani tembeeni au waulize walio tembea.
 
Hizi ni dalili za kufilisika mawazo
"Pasitawalike nyumban kwako na sio tanzania" kama mnataka mabadiliko na kutuletea maendeleo tupen sera zenu tunaweza kuwafikiria 2015 sio kauli mbofu mbofu
 
mtoto wa hivi bora ubadilishane na chupa tupu la maji.we umeona ktk miji duniani moshi ni kitu gani.we unaona kuna huduma gani tembeeni au waulize walio tembea.

Hayo ni mawazo ya kurithishana kwa magamba!
Mwenzio alisema ni bora wananchi wale majani ila ndege MBOVU inunuliwe!
Mtu wa namna yako hushangazi kuandika hivyo kwa sababu kutafakari hakujawahi kuwa jambo la lazima wakati wa kujifunza....
Ulivyojua kusoma na kuandika, BASI!
 
ni TANZANIA TU WAZIRI ANAFORGE CHETI CHA FORM FOUR NA BADO ANAENDELEA KUWA MADARAKANI (MULUGO) ni Tanzania tu, Rais anakuwa na safari za nje nyingi zisizo natija, RIDHIWANI AKIENDESHA NCHI ANAVYOTAKA, UZA UNGA, MAFUTA, DHULUMATI NA UPUUZI MWINGI, NCHI HAPO ITATAWALIKA????//
 
Huyu muwasilishaji wa mada nahisi anatatizo la kutojitambua. Mbona ameshindwa kuorodhesha matusi na lugha za kejeri zilizotolewa bungeni na akina lukuvi?
 
Well said. Bila shaka wapotoshaji wa kauli ile wanaweza kuwa na upeo wa kulielewa hili. Isije ikawa we are watching the same movie but seeing diffrent actors/ activities. Ha ha haaa!

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Slaa amuonya Kikwete

• ASEMA AKIPUUZA NCHI HAITATAWALIKA

na Charles Misango




KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, amemtaka Rais Jakaya Kikwete kuwa makini na kuchukua hatua za haraka kurejesha amani kabla Watanzania hawajaishiwa uvumilivu na utawala wa serikali yake.

Dk. Slaa amesema kuongezeka kwa matukio ya matumizi ya nguvu ya dola katika kulinda uhalali wa serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kiasi cha kufikia hatua ya kuua watu wasiokuwa na hatia, yanadhihirisha kuwa muda si mrefu ujao nchi itakuwa haitawaliki tena ikiwa Kikwete ataendelea kufumbia macho mauaji hayo.

Akifungua Ofisi ya Baraza la Vijana wa chama hicho (Bavicha) Mtaa wa Togo, Dar es Salaam jana, Dk. Slaa alisema kuwa mauaji yanayofanywa na vyombo vya dola chini ya serikali ya CCM kupitia kwa viongozi wake hususan Jeshi la Polisi, hayawezi kuvumilika tena na yanawasukuma wananchi kufikia mwisho wa uvumilivu.

Alisema sasa kuna dalili zote za wazi zinazotishia amani na mustakabali wa nchi na watu wake, zikiifanya nchi isitawalike, na wala serikali haiwezi tena kukwepa lawama za kuhusika na mauaji ya wananchi, na kutolea mfano wa tukio la kutwangwa risasi kwa watu wanne wasiokuwa na hatia waliokuwa wakiandamana kudai haki ya kulindwa na serikali yao mkoani Ruvuma mapema wiki hii.

Dk. Slaa akizungumza kwa uchungu alisema mauaji ya Songea yalitokana na uzembe wa hali ya juu wa viongozi wa serikali na vyombo vya dola ngazi ya wilaya na Mkoa wa Ruvuma.

“Napenda kutoa kauli juu ya mauaji dhidi ya raia yaliyofanywa na Jeshi la Polisi huko Songea. Kwa taarifa nilizonazo, mauaji yale yametokea kwa sababu ya uzembe wa hali ya juu na ufinyu tu wa akili ya viongozi, akiwamo mkuu wa Mkoa na polisi wale. Hivi unawaambiaje raia wenye uchungu na vifo vya wananchi wenzao, waliojikusanya na kuamua kuandamana kudai haki, eti wachague kiongozi wa kuonana na mkuu wa mkoa,” alisema.

Aliitaka serikali kuunda tume huru ya kuchunguza mauaji hayo ya Songea na kudai kuwa hakuna uhalali wowote wa viongozi wa serikali wa mkoa ambao ni watuhumiwa wa mauaji hayo kuunda chombo cha kuchunguza.

“Tunawapongeza wananchi na hasa vijana wa Songea kwa kuandamana kudai haki. Tunataka ufanyike uchunguzi huru juu ya mauaji hayo, yatakayoihusisha mahakama (Korona) na mkuu wa mkoa na polisi hawana uhalali wa kuunda tume za kuchunguza kwani wao pia ni watuhumiwa katika tukio hilo,” alisema.

Katibu mkuu huyo wa CHADEMA alilaani tukio la juzi usiku, ambapo polisi katika mji wa Tunduma wanadaiwa kushusha bendera za chama hicho katika maeneo mbalimbali ya mji huo.

Alisema kitendo hicho ni uchokozi tosha kwa CHADEMA na kimelenga kuleta fujo nyingine zinazoweza kuleta uvunjifu wa amani.

“Niliwasiliana na Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, pia mkuu wa mkoa, niliwaambia mimi sipendi kugombana nao kwa masuala ya hovyo kama hayo, tupo kwa mujibu wa sheria, bendera zetu zinatokana na kodi za Watanzania, wakasema eti zingine ziko sokoni, nikawauliza za CCM huwa zinawekwa wapi?

“Watu hawana maji, hawana zahanati, elimu inashuka, mkuu wa wilaya hajawahi kuamuka usiku, lakini kwenye kushusha bendera za CHADEMA wanaamka usiku wa manane,” alisema.

Alitumia wasaa huo kuwataka vijana wa CHADEMA wasimamie haki na kupinga dhuluma na uonevu popote pale wanapofanyiwa Watanzania na wahakikishe wanajua kinachoendelea katika maeneo ya Songea na Tunduma ili chama hicho kijue hatua za kuchukua.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bavicha, John Heche, mbali ya kumshukuru Dk. Slaa na makao makuu ya chama hicho kwa kuwawezesha kuwa na ofisi yao, alisema kuwa watakuwa mstari wa mbele kusimamia malengo ya chama hicho hasa katika kutetea haki za Watanzania, kudai uwajibikaji wa viongozi na serikali kwa wananchi, pia kulinda rasilimali za taifa.

Alisema kuwa vijana watakuwa mstari wa mbele katika vuguvugu la mageuzi yanayoendelea nchini, akisema kuwa ofisi hiyo itakuwa sehemu sahihi ya kuendeshea mipango ya ukombozi wa taifa ambalo pamoja na utajiri wa rasilimali za kila aina, bado wananchi wake wanaishi katika umaskini wa kupindukia.

Chanzo; Tanzania Daima
 
KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa amefafanua kauli yake, kwa kutaja sababu kadhaa ambazo zitasababisha nchi isitawalike kama alivyowahi kuonya.

Mwaka juzi, Dk. Slaa alimtaka Rais Jakaya Kikwete kuwa makini na kuchukua hatua za haraka kurejesha amani kabla Watanzania hawajaishiwa uvumilivu na utawala wa serikali yake.

Hata hivyo, kauli hiyo ya kwamba nchi haitatawalika, kwa siku za karibuni imekuwa ikipotoshwa na viongozi wa serikali na CCM wakidai kuwa CHADEMA ilikuwa ikimaanisha kufanya vitendo vya fujo ili kuidhoofisha Serikali ya Rais Kikwete.

Akihutubia mkutano wa hadhara jana mjini Njombe katika Jimbo la Njombe Kusini linaloongozwa na Spika wa Bunge, Anne Makinda uliofanyika kwenye viwanja vya National Housing, Dk. Slaa alisema alichomaanisha ni mtiririko wa matukio ya watu kunyanyaswa.

“Narudia tena hapa kuwa itafika mahali nchi hii haitatawalika na itamshinda Kikwete. Yaliyojiri Rwanda na Burundi kuhusu ukabila wananchi waliyapigia kelele mapema, lakini watawala wakapuuza, kilichofuata nchi zikavurugika,” alisema.

Dk. Slaa ambaye aliambatana na baadhi ya wabunge wa chama hicho waliokuwa wamesimamishwa kuhudhuria vikao vya Bunge kwa siku tano, alifafanua kuwa hatari hiyo ya amani kutoweka nchini aliiona mapema kama kiongozi wa siasa, ndiyo maana akaonya.

“Tangu mapema manyanyaso ya wananchi hayasikilizwi, sakata la korosho Lindi tuliliona kwenye ziara yetu mwaka jana, wabunge wetu wakalifikisha bungeni lakini serikali ikapuuza, sasa wananchi wa Lindi na Mtwara wameishiwa na uvumilivu, CCM wanadai ni CHADEMA,” alisema.

Katibu huyo alitumia fursa hiyo kuwapa pole wananchi wa Liwale kwa vurugu zilizotokea juzi na kuharibu mali mbalimbali akisema kuwa walipigwa mabomu wakidai haki zao.

“Adui wa Kikwete si CHADEMA, Slaa wala Mbowe kama CCM na serikali yao wanavyopotosha, bali wajue kuwa adui ni manyanyaso wanayofanyiwa wananchi, wamechoka na hilo ndilo nililoonya kuwa itafika mahali nchi haitatawalika,” alisema.

Dk. Slaa mbele ya wabunge wake, Mchungaji Peter Msigwa (Iringa Mjini), Joseph Mbilinyi (Mbeya Mjini) na Ezekiel Wenje (Nyamagana) alisema kuwa hata vurugu bungeni zinatokana na Bunge hilo kuongozwa kwa misingi ya vyama badala ya kujali maslahi ya kitaifa.

Alisema kuwa wananchi wa kila kada wamechoka na maisha duni, hivyo wanaishinikiza serikali yao iliyokuwa imekataa kuwasikiliza ichukue hatua sasa.

“Walimu kutopewa mishahara yao, wanafunzi wanaendelea kufeli kwa sababu walimu hawajaboreshewa mazingira ya kutoa elimu bora, watu wachache kuendelea kunufaika na jasho la wengi, hayo yote yamesababisha Watanzania kuishiwa uvumilivu.

“Na utawala wa serikali umedhihirisha kwa mara nyingine kuwa Kikwete ameendelea kufumbia macho mambo hayo, nchi inazidi kukosa mwelekeo,” alisema.

Dk. Slaa aliongeza kuwa aliposema nchi haitatawalika, alimaanisha serikali itatue kero za wananchi, itekeleze wajibu wake badala ya kufanya siasa kwenye matatizo.

“Serikali ingekuwa makini wangenisikiliza, mambo yanayotokea sasa yasingetokea. Serikali imekuwa ikiishi kwa matukio, likitoka hili linakuja jingine, likimalizika hili linaibuka jipya,” alisema.

LEMA AMUONYA MKUU WA MKOA.
Habari kutoka Arusha zinasema kuwa Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema ambae ametangazwa kusakwa na Jeshi la Polisi mkoani humo, jana alijitokeza na kutangaza mgogoro na Mkuu wa Mkoa Magesa Mulongo.

Lema alisema kuwa Mulongo amemtumia vitisho kupitia ujumbe wa maandishi kwenye simu (sms).

Akizungumza na waandishi wa habari katika mgahawa wa Ethiopia jijini Arusha, Lema alisema amepokea ujumbe wa maandishi kutoka kwa Mulongo ukisomeka; “umeruka kihunzi cha kwanza, nitakuonyesha kuwa mimi ni serikali, ulikojificha nitakupata na nitakupa kesi ninayotaka mimi.”

Lema alionesha sms hiyo kwa waandishi wa habari, ikiwa imetumwa kutoka katika namba 0752 960276 ambayo alidai ni ya Mulungo.

“Nilimjibu kuwa nimekupata, nimekuelewa na nipo tayari. Na ujumbe huo ulionesha kuwa ulipokelewa katika simu ya mkuu wa mkoa. Huo ni mwendelezo wa vitisho vyake kwangu,” alisema.

Alisema kuwa hatambui chanzo halisi cha Mulongo kumtumia vitisho hivyo, lakini akasema tayari ameishamjua vyema mkuu huyo wa mkoa na kamwe hatamuogopa bali atatoa ushirikiano wowote kwake.

“Nimeshangaa kusikia kwenye vyombo vya habari jana kuwa mkuu wa mkoa ameagiza nikamatwe kwa kuchochea vurugu katika Chuo cha Uhasibu wakati mimi nilifika hapo kuzungumza na wanafunzi na kuwazuia wasiandamane.

“Mimi namshangaa sana huyu Mulongo, nilimpigia simu mimi kumuarifu na kumuita kuzungumza na wanafunzi ili kutoa tamko la serikali na akaahidi kufika baada ya dakika 10, lakini akafika baada ya saa moja,” alisema.

Mulongo alipoulizwa na mwandishi wetu kuhusu madai ya kumtumia Lema ujumbe wa vitisho, alionesha kushangazwa na maelezo hayo lakini hakukiri wala kukataa.

“Unaandikia chombo gani? Sasa huo ujumbe anaosema nimemtumia umeuona unatoka kwangu?” Alihoji.

Akizungumzia vitisho hivyo, Dk. Slaa alisema kuwa CHADEMA wamekubaliana kumchukulia hatua za kisheria Mulongo kwa kumfungulia kesi mahakamani.

Alisema vitisho hivyo ni hatari na pia ni kielelezo cha matumizi mabaya ya madaraka.
 
Serikali ya CCM inapasa iache ujinga. hata siku moja kwa viongozi makini wa Nchi kauli ya mtu mmoja haiwezi kufanya nchi isitawalike. Kwa nini saa nyingine tunaruhusu ujinga utawale katka akili zetu na kutumia kichaka cha kauli toka midomo ya watu wengine kujificha wakati hatuwajibiki.
Mie nahuzunika sana serikali inapojificha kwenye kauli hizi na kushindwa kuwajibika.
 
Mnahangaika sana akina tumaini makene kutetea udhaifu wa dr slaa
 
KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa amefafanua kauli yake, kwa kutaja sababu kadhaa ambazo zitasababisha nchi isitawalike kama alivyowahi kuonya.
Kwa kawaida magaidi wote duniani wanatumia mbinu ya aina moja. Nayo ni kutahadhalisha jambo kabla hawajalitekeleza. Lengo ni kutaka waonekane kwenye jamii kuwa ni watu wema sana
 
Well said. Bila shaka wapotoshaji wa kauli ile wanaweza kuwa na upeo wa kulielewa hili. Isije ikawa we are watching the same movie but seeing diffrent actors/ activities. Ha ha haaa!

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
Mkuu hakuna cha upotoshaji. Dr Slaa alitamka alichokimaanisha. Usijaribu kupuliza pafyum kwenye kinyesi
 
Tupo pamoja katika harakati ya ukomboz wa nchi dhidi ya mafisadi wa ccm.
 
Slaa makanisa aliyaahidi kuongeza ruzuku andepo angechaguliwa mambo yakaenda kombo.
 
Serikali ya CCM inapasa iache ujinga. hata siku moja kwa viongozi makini wa Nchi kauli ya mtu mmoja haiwezi kufanya nchi isitawalike. Kwa nini saa nyingine tunaruhusu ujinga utawale katka akili zetu na kutumia kichaka cha kauli toka midomo ya watu wengine kujificha wakati hatuwajibiki.
Mie nahuzunika sana serikali inapojificha kwenye kauli hizi na kushindwa kuwajibika.
Yeye alikuwa mwakilishi wa kundi kubwa la wajinga waliojaa udini na ukabila hata baada ya uchaguzi walitumia nguvu nyingi kuchochea migogoro mpaka ya kuchinja lakini watanzania ni wamoja.
 
KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa amefafanua kauli yake, kwa kutaja sababu kadhaa ambazo zitasababisha nchi isitawalike kama alivyowahi kuonya.
Watumwa bado watu tanzania hata huyu ni miongoni mwa watumwa hao.
 
Suala la msingi ni kumuelewa Dk Slaa, ya kwamba ni mtu wa dhamira safi. Sasa wanafiki hawa wa CCM hawana jipya zaidi ya kujidhihirisha. Kumbuka usemi; njia ya mwongo ni fupi. Watajikanganya watachoka. Dhamira chafu haiwezi kutoa matunda bora hata siku moja.
 
Back
Top Bottom