Slaa: Kikwete akipuuza nchi haitatawalika | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Slaa: Kikwete akipuuza nchi haitatawalika

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by EasyFit, Jan 22, 2012.

 1. EasyFit

  EasyFit JF-Expert Member

  #1
  Jan 22, 2012
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 1,244
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, amemtaka Rais Jakaya Kikwete kuwa makini na kuchukua hatua za haraka kurejesha amani kabla Watanzania hawajaishiwa uvumilivu na utawala wa serikali yake.

  Dk. Slaa amesema kuongezeka kwa matukio ya matumizi ya nguvu ya dola katika kulinda uhalali wa serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kiasi cha kufikia hatua ya kuua watu wasiokuwa na hatia, yanadhihirisha kuwa muda si mrefu ujao nchi itakuwa haitawaliki tena ikiwa Kikwete ataendelea kufumbia macho mauaji hayo.

  Akifungua Ofisi ya Baraza la Vijana wa chama hicho (Bavicha) Mtaa wa Togo, Dar es Salaam jana, Dk. Slaa alisema kuwa mauaji yanayofanywa na vyombo vya dola chini ya serikali ya CCM kupitia kwa viongozi wake hususan Jeshi la Polisi, hayawezi kuvumilika tena na yanawasukuma wananchi kufikia mwisho wa uvumilivu.

  Alisema sasa kuna dalili zote za wazi zinazotishia amani na mustakabali wa nchi na watu wake, zikiifanya nchi isitawalike, na wala serikali haiwezi tena kukwepa lawama za kuhusika na mauaji ya wananchi, na kutolea mfano wa tukio la kutwangwa risasi kwa watu wanne wasiokuwa na hatia waliokuwa wakiandamana kudai haki ya kulindwa na serikali yao mkoani Ruvuma mapema wiki hii.

  Dk. Slaa akizungumza kwa uchungu alisema mauaji ya Songea yalitokana na uzembe wa hali ya juu wa viongozi wa serikali na vyombo vya dola ngazi ya wilaya na Mkoa wa Ruvuma.

  "Napenda kutoa kauli juu ya mauaji dhidi ya raia yaliyofanywa na Jeshi la Polisi huko Songea. Kwa taarifa nilizonazo, mauaji yale yametokea kwa sababu ya uzembe wa hali ya juu na ufinyu tu wa akili ya viongozi, akiwamo mkuu wa Mkoa na polisi wale. Hivi unawaambiaje raia wenye uchungu na vifo vya wananchi wenzao, waliojikusanya na kuamua kuandamana kudai haki, eti wachague kiongozi wa kuonana na mkuu wa mkoa," alisema.

  Aliitaka serikali kuunda tume huru ya kuchunguza mauaji hayo ya Songea na kudai kuwa hakuna uhalali wowote wa viongozi wa serikali wa mkoa ambao ni watuhumiwa wa mauaji hayo kuunda chombo cha kuchunguza.

  "Tunawapongeza wananchi na hasa vijana wa Songea kwa kuandamana kudai haki. Tunataka ufanyike uchunguzi huru juu ya mauaji hayo, yatakayoihusisha mahakama (Korona) na mkuu wa mkoa na polisi hawana uhalali wa kuunda tume za kuchunguza kwani wao pia ni watuhumiwa katika tukio hilo," alisema.

  Katibu mkuu huyo wa CHADEMA alilaani tukio la juzi usiku, ambapo polisi katika mji wa Tunduma wanadaiwa kushusha bendera za chama hicho katika maeneo mbalimbali ya mji huo.

  Alisema kitendo hicho ni uchokozi tosha kwa CHADEMA na kimelenga kuleta fujo nyingine zinazoweza kuleta uvunjifu wa amani.

  "Niliwasiliana na Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, pia mkuu wa mkoa, niliwaambia mimi sipendi kugombana nao kwa masuala ya hovyo kama hayo, tupo kwa mujibu wa sheria, bendera zetu zinatokana na kodi za Watanzania, wakasema eti zingine ziko sokoni, nikawauliza za CCM huwa zinawekwa wapi?

  "Watu hawana maji, hawana zahanati, elimu inashuka, mkuu wa wilaya hajawahi kuamuka usiku, lakini kwenye kushusha bendera za CHADEMA wanaamka usiku wa manane," alisema.

  Alitumia wasaa huo kuwataka vijana wa CHADEMA wasimamie haki na kupinga dhuluma na uonevu popote pale wanapofanyiwa Watanzania na wahakikishe wanajua kinachoendelea katika maeneo ya Songea na Tunduma ili chama hicho kijue hatua za kuchukua.

  Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bavicha, John Heche, mbali ya kumshukuru Dk. Slaa na makao makuu ya chama hicho kwa kuwawezesha kuwa na ofisi yao, alisema kuwa watakuwa mstari wa mbele kusimamia malengo ya chama hicho hasa katika kutetea haki za Watanzania, kudai uwajibikaji wa viongozi na serikali kwa wananchi, pia kulinda rasilimali za taifa.

  Alisema kuwa vijana watakuwa mstari wa mbele katika vuguvugu la mageuzi yanayoendelea nchini, akisema kuwa ofisi hiyo itakuwa sehemu sahihi ya kuendeshea mipango ya ukombozi wa taifa ambalo pamoja na utajiri wa rasilimali za kila aina, bado wananchi wake wanaishi katika umaskini wa kupindukia.
   
 2. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #2
  Jan 22, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,323
  Likes Received: 19,482
  Trophy Points: 280
  benki ya dunia nayo si wameshazipa developing countries alert kuwa lazima wapigike sasa hivvi.
   
 3. nitonye

  nitonye JF-Expert Member

  #3
  Jan 22, 2012
  Joined: Dec 18, 2011
  Messages: 7,167
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  dalili za kushindwa kutawalika maana yake nguvu ya umma itabide ishike madaraka
   
 4. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #4
  Jan 22, 2012
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Hadi Jumatano ya wiki iliyopita, mfumuko wa bei ulikuwa 19.9%.
  Nawezaje kuipenda Tanzania?
   
 5. Entrepreneur

  Entrepreneur JF-Expert Member

  #5
  Jan 22, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 1,092
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Wakati kama huu huwa napenda kupitia ile hotuba ya mwalimu ya September mosi. 1979 inayoitwa "mapambano yanaendelea". Kwa kweli hali ni ngumu kuliko inavyoelezeka na sidhani kama ni busara kuwasubiri hawa wanasiasa waje watutoe hapa walipotufikisha.

  Awali dalili zote za kufika hapa zilikuwa ni dhahiri na wadau wengi walito tahadhari lakini hawakusikilizwa, na sasa ni dhahiri tena tunaelekea kubaya zaidi kwani bado sijaamini kama kweli SERIKALI imeshatoa pamba masikioni mwake. Hivi kama hii issue ya umeme, ni kweli hawajui madhara ya kuongeza Bei? Na bado

  Wananchi tuchukue hatua sasa
   
 6. K

  Kubingwa JF-Expert Member

  #6
  Jan 22, 2012
  Joined: Apr 23, 2010
  Messages: 502
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Ikulu ni mahali patakatifu! Sijui sasa papoje,yangu macho na uzima.
  Mambo yanapoenda mrama kila ufanyalo haliendi.Maofisi hata hao wataalam hawafanyi tena kazi,kazi kutegea ama kufanya kazi zao na wengine hata kama hawana nia ya kwenda shule ndo muda wao wa kwenda kuchukua masomo yao zaidi.

  Mungu tunusuru na haya mambo kama andiko linavyosema Kumb.28:33
   
 7. Entrepreneur

  Entrepreneur JF-Expert Member

  #7
  Jan 22, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 1,092
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Swali la kizushi tu Mchaga!
  Hivi tunastahili kutawaliwa au kuongozwa? Haa haa haa
   
 8. 1800

  1800 JF-Expert Member

  #8
  Jan 22, 2012
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 2,217
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Mkuu umemsahau na ndugu yetu hojatete
   
 9. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #9
  Jan 22, 2012
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,559
  Likes Received: 1,917
  Trophy Points: 280
  Unajuwa walioko responsible kwa ujumla na hali ya uchumi ya dunia ni mabepari, lakini mabepari wa kwetu, wengi wao ndo hao mafisadi, kwasababu wengi wao chanzo cha utajiri ni pesa za umma na rasilimali za Taifa.

  Ndo maana unaona Obama anataka kuwapandishia kodi mabepari wa marekani ili kusaidia kuinua uchumi, kwasababu they were responsible since wakakati uchumi ukididimia na hali ya wananchi walio wengi kutokuwa njema, wao bado walikuwa ndo wanadouble mishahara, mabonus na maprofit kwa ujumla.

  Since mabepari wetu sisi ndo hao mafisadi, basi mali zao halali ya wananchi, na kama ni kweli hawataki kurudisha pesa na mali walizokwapua, basi hali kwa Tanzania itakuwa mbaya zaidi kwasababu hakuna wa kuwahold responsible.

  Kwenye mjadala wa kuhusu mustakabali wa Taifa, hili la mafisadi kurejesha walivyokwapua haliwezi kuwa out of the question, pia katiba tutakayoipata ni lazima i reflect azma yetu ya kuufutilia ufisadi na mafisadi mbali.
   
 10. M

  Mgaya D.W JF-Expert Member

  #10
  Jan 22, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 966
  Likes Received: 192
  Trophy Points: 60
  Tunapokosa uzalendo mara nyng viongoz hufikiria mambo yote mabaya huanzishwa na upinzani,napata taabu kuona maisha yasivyotuhurumia.nchi yangu naipenda lakin viongoz hawana huruma,hawana uzalendo hata kidogo ni kama kikundi cha wagen wamekuja kukwiba na kuondoka.mfumuko wa bei unapofika asilimia 19.9 tunaenda wap?kwanin viongoz hawatak kuchukua hatua?dah,lakini tutawapa zawad mwaka 2015 ili wajue upole wetu ktk sanduku la kura.
   
 11. B

  Bangoo JF-Expert Member

  #11
  Jan 22, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 5,594
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Natamani mfumuko uendelee nione serikali ikianguka pwaaaa. Ee Mungu saidia wanao.
   
 12. O

  Otorong'ong'o JF-Expert Member

  #12
  Jan 22, 2012
  Joined: Aug 17, 2011
  Messages: 31,105
  Likes Received: 10,457
  Trophy Points: 280
  Slaa ofcourse kwani hujui yule ni nanbii.
   
 13. kichomiz

  kichomiz JF-Expert Member

  #13
  Jan 22, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 11,996
  Likes Received: 2,650
  Trophy Points: 280
  Ndio maana mkulu ameanza kujipendekeza CDM,hana ujanja kwa sasa.
   
 14. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #14
  Jan 22, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  akili ni mali endapo wewe ungekabidhiwa nchi na chadema yako mambo yangekwenda vibaya zaidi
   
 15. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #15
  Jan 22, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  njozi kwamba chadema ikishika dola nchi hii itakuwa peponi ni fikra mgando. maendeleo ni zaidi ya chama cha siasa na itikadi zake
   
 16. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #16
  Jan 22, 2012
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  "haya matatizo yanayotokea hapa petu yanatokea pia nchi za ullaya kama Italy" .....anasahau kuwa wenzake wanajiuzuru wanapo ona nchi haiendi ina kuwa na madeni makubwa , mfumuko wa bei juu
   
 17. Gwallo

  Gwallo JF-Expert Member

  #17
  Jan 22, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 2,320
  Likes Received: 840
  Trophy Points: 280
  Shule gani unayo wewe, unamsaidiaje aliyeibiwa wife wake na Dr Slaa?
   
 18. Mumwi

  Mumwi JF-Expert Member

  #18
  Jan 22, 2012
  Joined: Jan 9, 2011
  Messages: 592
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kama ile ya ff inayosema mahindi au mabua.
   
 19. Mumwi

  Mumwi JF-Expert Member

  #19
  Jan 22, 2012
  Joined: Jan 9, 2011
  Messages: 592
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hojatele hana point mwizi hukamatwa kama kweli aliiba mbona mnaongea tu pembeni hata ujasiri Wa kumkamata huna usiongee kama unayeleta ushabiki tu hauna maana.
   
 20. Gwallo

  Gwallo JF-Expert Member

  #20
  Jan 22, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 2,320
  Likes Received: 840
  Trophy Points: 280
  Nilimwuliza tu kuona kama anamsaidia aliyeibiwa mke iwe kwa kufungua kesi au vinginevyo.
   
Loading...