Slaa: Kikwete akipuuza nchi haitatawalika

Slaa: Kikwete akipuuza nchi haitatawalika

nakumbuka huu usemi aliutoa raisi wa mioyo ya watu,doctor wa ukweli w.slaa,nakumbuka baada ya usemi huu viongozi wa ccm kwa wingi wao walisimama na kutamba kuwa lazima nchi itatawalika,hawakujua raisi anamaanisha nini.slaa alitambua wazi kuwa serekali ya ccm haina iwezo wa kutatua matatizo ya wananchi wake..kwa sasa wanalalamika tu ile ,kauli ya lazima nchi itawalike imepotelea wapi?wanachojaribu ni kuwashawishi watu kuwaonea huruma.
 
Liwalo na liwe,kauli ya mtendaji mkuu serikari.
 
chadema ndiyo isababisha hata mwinyi kuzabwa makofi..
 
itatawalikaje kama kiongozi wake ni dhaifu, na watendaji wake wote wapo influenced na upinzani zaidi ya raisi wake.Itatawalikaje ikiwa cdm wakigeuka serikali inatetemeka?Sasa CDm wawasaidie nini. CCM wamekuwa km ulimwengu wa uamsho kila kitu kiwashindacho huona mikono y amarekani na israel ikiwaharibia.CCM nao huwa wanaowaona CDM kwa kushindwa kwao.
 
Its a high time we tanzanians to know that this nation is more important than hao chai chapati maharage we should not take this things 4 granted this guy is an idiot am missing words to explain him Dr.Slaa hakuna siku ameropoka he alwayz talks whats he belives in wewe hapo unadai anawashwa pumbavu kabisa nyie baba zenu ndio wanaowashwa na hizo hela wanazopewa mpate mkate wa kila siku stupid kabisa shame on uuuuuuu!!!!
 
Ninyi wanaJF...mnashabikia CDM na huyo Slaa? Alisema punde tu baada ya uchakuzi 2010 kuwa nchi hii haitatawalika na hayo yalikuwa maazimio ya kanisa na Dr Slaa. hivyo wanajitahidi kila kukicha kuwahadaa wanchi kuleta vurugu ili kuthibitisha na kufikia malengo yao ya kuichafua nchi. Hawa wote wanaoleta vurugu wako backed na CDM na Kanisa...including migomo hii ya madaktari. wako pia wanaharakati na wa haki za binadamu ambao wamesema sana katika migomo mingi ukiangalia ile ya Mbeya, Ruvuma na mingine mingi. Ila ukitafakari sana na ukiangalia sana mafisadi wengi hutokea huko makanisani. nasema kanisani kwa kuwa sasa hivi hao waliotajwa mafisadi (Lowasa and the likes) wanapita makanisani mwetu kuomba support zetu ili tuwape ridhaa ya kuongoza nchi katika chaguzi zijazo... mimi sijui tunakwenda wapi
Kama nchi haitawaliki,kumlaumu Dr. Slaa ndo udhaifu wenyewe huo.
 
Malizia na conclusion kuwa CHADEMA ndio wanapuuza mapendekezo ya madaktari na waalimu lengo likiwa ni kufanya nchi isitawalike, mbona unazunguka zunguka na kujikanyaga kanyaga? Hushindwi kusema hivyo kwani unaonekana ni mvivu saana wa kufikiri!!

jibu swali uulize maswali. usipokuwa na sikio mdomo hAuna maana
 
Hii Kauli naona imefanya kazi yake ! Imetumika kila hila
HONGERA Dr SILAHA
 
Humu JF mnamo tarehe 22/1/2012 kuliwekwa thread inayo mnukuu Dk Slaa akisema nchi haitatwalika. Nakupa linki https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/227572-slaa-kikwete-akipuuza-nchi-haitatawalika-9.html
Je hii kauli inauhusiano na haya matukio ya vurugu yanayotokea sasa? Je ni kweli Dk Slaa alitamka hii kauli. Jamani ulimi ni kiungo kidogo sana mwilini lakini madhara yatokanayo na matumizi mabaya ya ulimi ni hatari sana.
Ukombozi au Mageuzi ni muhimu nchi hii lakini tusifanye Ukombozi kama wa Libya mpaka sas nchi haijatulia. Misri mambo ni yale yale mtu aliyeonekana anafaa Mohamed Morsi leo wa misri wamemjua undani wake baada ya kuingia Madarakani.
Ombi langu vyama vyote vya SIASA vishirikiane kutuliza hali hii ya utata inayoikumba TZ kwa sasa. Kamwe hakuna Chama kitakachokuja tawala kwa amani kama hakuna Heshima ya kisiasa.
Na sisi wananchi tusitumike kisiasa.
 
Kauli kama hii ya nchi haitatawalika waasisi wake ndio waliopo nyuma ya yanayoendelea mtwara sasa
 
Kauli kama hii ya nchi haitatawalika waasisi wake ndio waliopo nyuma ya yanayoendelea mtwara sasa

Watu wenye uelewa wa kutosha na wanaotumia busara katika kauli na kufikiri huwa hawaangalii pale waliposimama tu bali hufanya tathmini juu ya mambo yanayotokea kwa wakati uliopo na kuangalia matokeo yake kwa siku za baadaye.

Imekuwa bahati mbaya sana watawala wa sasa kwa jeuri na kulewa madaraka wameamua kupuuza mawazo ya wengi, kukataa kutumikia jamii na hata kushindwa kusoma alama za nyakati hali inayopelekea hayo tunayoshuhudia sasa. Kilio cha watu wa kusini hakijaibuka kama kimbunga ama tufani. Ni kilio cha muda mrefu ambacho watawala walitakiwa kukisikia na kukitafutia ufumbuzi lakini kwa jeuri yao waliamua kuwapuuza kwa kuamini kuwa wana dola hivyo watatumia nguvu kuwanyamazisha.

Haiingii akilini hata kidogo rais wa nchi anaamua kupuuza mambo ya msingi kama madai ya wanaMtwara na mbaya zaidi waziri wake ambaye hajapigiwa hata kura moja na Watanzania anadiriki kuwalinganisha na chura watu wa Mtwara halafu wanajigamba kuwa serikali ni sikivu. Yuko wapi mtu kama Ghadaffi aliyediriki kuwafananisha wananchi wananchi wake na mende.

Vifo vilivyotokea Mtwara leo pamoja na uharibifu wote vimesababishwa na Serikali na Kikwete kama rais katika hali yoyote ndiye mtu wa kwanza wa kubebeshwa hizo lawama na hakuna jinsi yoyote ataweza kujinasua katika hili.
 
KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, amemtaka Rais Jakaya Kikwete kuwa makini na kuchukua hatua za haraka kurejesha amani kabla Watanzania hawajaishiwa uvumilivu na utawala wa serikali yake.

Dk. Slaa amesema kuongezeka kwa matukio ya matumizi ya nguvu ya dola katika kulinda uhalali wa serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kiasi cha kufikia hatua ya kuua watu wasiokuwa na hatia, yanadhihirisha kuwa muda si mrefu ujao nchi itakuwa haitawaliki tena ikiwa Kikwete ataendelea kufumbia macho mauaji hayo.

Akifungua Ofisi ya Baraza la Vijana wa chama hicho (Bavicha) Mtaa wa Togo, Dar es Salaam jana, Dk. Slaa alisema kuwa mauaji yanayofanywa na vyombo vya dola chini ya serikali ya CCM kupitia kwa viongozi wake hususan Jeshi la Polisi, hayawezi kuvumilika tena na yanawasukuma wananchi kufikia mwisho wa uvumilivu.

Alisema sasa kuna dalili zote za wazi zinazotishia amani na mustakabali wa nchi na watu wake, zikiifanya nchi isitawalike, na wala serikali haiwezi tena kukwepa lawama za kuhusika na mauaji ya wananchi, na kutolea mfano wa tukio la kutwangwa risasi kwa watu wanne wasiokuwa na hatia waliokuwa wakiandamana kudai haki ya kulindwa na serikali yao mkoani Ruvuma mapema wiki hii.

Dk. Slaa akizungumza kwa uchungu alisema mauaji ya Songea yalitokana na uzembe wa hali ya juu wa viongozi wa serikali na vyombo vya dola ngazi ya wilaya na Mkoa wa Ruvuma.

“Napenda kutoa kauli juu ya mauaji dhidi ya raia yaliyofanywa na Jeshi la Polisi huko Songea. Kwa taarifa nilizonazo, mauaji yale yametokea kwa sababu ya uzembe wa hali ya juu na ufinyu tu wa akili ya viongozi, akiwamo mkuu wa Mkoa na polisi wale. Hivi unawaambiaje raia wenye uchungu na vifo vya wananchi wenzao, waliojikusanya na kuamua kuandamana kudai haki, eti wachague kiongozi wa kuonana na mkuu wa mkoa,” alisema.

Aliitaka serikali kuunda tume huru ya kuchunguza mauaji hayo ya Songea na kudai kuwa hakuna uhalali wowote wa viongozi wa serikali wa mkoa ambao ni watuhumiwa wa mauaji hayo kuunda chombo cha kuchunguza.

“Tunawapongeza wananchi na hasa vijana wa Songea kwa kuandamana kudai haki. Tunataka ufanyike uchunguzi huru juu ya mauaji hayo, yatakayoihusisha mahakama (Korona) na mkuu wa mkoa na polisi hawana uhalali wa kuunda tume za kuchunguza kwani wao pia ni watuhumiwa katika tukio hilo,” alisema.

Katibu mkuu huyo wa CHADEMA alilaani tukio la juzi usiku, ambapo polisi katika mji wa Tunduma wanadaiwa kushusha bendera za chama hicho katika maeneo mbalimbali ya mji huo.

Alisema kitendo hicho ni uchokozi tosha kwa CHADEMA na kimelenga kuleta fujo nyingine zinazoweza kuleta uvunjifu wa amani.

“Niliwasiliana na Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, pia mkuu wa mkoa, niliwaambia mimi sipendi kugombana nao kwa masuala ya hovyo kama hayo, tupo kwa mujibu wa sheria, bendera zetu zinatokana na kodi za Watanzania, wakasema eti zingine ziko sokoni, nikawauliza za CCM huwa zinawekwa wapi?

“Watu hawana maji, hawana zahanati, elimu inashuka, mkuu wa wilaya hajawahi kuamuka usiku, lakini kwenye kushusha bendera za CHADEMA wanaamka usiku wa manane,” alisema.

Alitumia wasaa huo kuwataka vijana wa CHADEMA wasimamie haki na kupinga dhuluma na uonevu popote pale wanapofanyiwa Watanzania na wahakikishe wanajua kinachoendelea katika maeneo ya Songea na Tunduma ili chama hicho kijue hatua za kuchukua.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bavicha, John Heche, mbali ya kumshukuru Dk. Slaa na makao makuu ya chama hicho kwa kuwawezesha kuwa na ofisi yao, alisema kuwa watakuwa mstari wa mbele kusimamia malengo ya chama hicho hasa katika kutetea haki za Watanzania, kudai uwajibikaji wa viongozi na serikali kwa wananchi, pia kulinda rasilimali za taifa.

Alisema kuwa vijana watakuwa mstari wa mbele katika vuguvugu la mageuzi yanayoendelea nchini, akisema kuwa ofisi hiyo itakuwa sehemu sahihi ya kuendeshea mipango ya ukombozi wa taifa ambalo pamoja na utajiri wa rasilimali za kila aina, bado wananchi wake wanaishi katika umaskini wa kupindukia.

Plz JK achilia madaraka nchi imekushinda hii. Marafiki zako wote wanakuona you are a joke na ndiyo maana wanajifanyia vitu bil kufikiri huku wakijuwa hutowafanya chochote. Plz achia madaraka.
 
Hivi watz hasa chadema wanatakaje?
-eti gold yote pale geita, ibaki geita, umeme wote wa kidatu ubaki moro, zanzibar umeme usiende,mto ruvu maji wauziwe dsm hela zirudi ruvu!:
hela yote ya utalii iwe Mali ya arusha na mara,
"Mind u ni upumbavu"
Mtwara kama gesi tu mnataka kujitenga na Tz.
(I wlb back)
 
Huyu Dr Slaa...anaupeo wa juu sana!!
YAMETIMIA!!
 
Yaani najisikia faraja sana watanganyika mnapotoana ngeu,angalau wazenj tunapumua.
 
Dr. Slaa ni Mtanganyika wa kweli kabisa kutoka katika moyo wake. Aliyayesema yalikuwa na yanaendelea kuwa ya msingi kwa JK kutekeleza na kuifanya serikali ya CCM ionekane iko makini japo kidogo. Mtampata wapi mpinzani anayeelekeza cha kufanya kwa ajili ya ustawi wa nchi inayoongozwa na chama asimu wake? Laiti JK angeyatekeleza, hakuna atakayekumbuka kwamba yalisemwa na mpinzani bali sifa njema zitakwenda kwa serikali pamoja na chama kinachoiunda serikali hiyo.

Tena mtu anakupa ushauri mzuri na wa thamani bila kukutoza na mchana kweupe bado unambwela-mbwelaaaa
 
>Nabii anapotabiri na yanapothibitika kutokea aliyoyatabiri, haimaanishi kwamba nabii ndio chanzo.
 
Hivi watz hasa chadema wanatakaje?
-eti gold yote pale geita, ibaki geita, umeme wote wa kidatu ubaki moro, zanzibar umeme usiende,mto ruvu maji wauziwe dsm hela zirudi ruvu!:
hela yote ya utalii iwe Mali ya arusha na mara,
"Mind u ni upumbavu"
Mtwara kama gesi tu mnataka kujitenga na Tz.
(I wlb back)

Aisee! Una akili fupi mpaka nakuonea huruma, pole sana.
 
Back
Top Bottom