Hivi watz hasa chadema wanatakaje?
-eti gold yote pale geita, ibaki geita, umeme wote wa kidatu ubaki moro, zanzibar umeme usiende,mto ruvu maji wauziwe dsm hela zirudi ruvu!:
hela yote ya utalii iwe Mali ya arusha na mara,
"Mind u ni upumbavu"
Mtwara kama gesi tu mnataka kujitenga na Tz.
(I wlb back)
haa kwani kauli hii tatizo lake ni nin? Kama serikali inaongoza nchi kiujanjaujanja je inaweza kutawalika hiyo nchi? Je kama serikali inang'oa kucha hao raia wake, je itatawalika hiyo nchi? Tatizo la mitanzania mingi ni kuwa na uzembe wa kufikiri!Nakemea kwa nguvu zangu zote kauli za hatari km hii
ni kweli mkuu, dr slaa alitahadharisha serikali, maana wamezoea kutumia mapolis kuua raia, na hata kung'oa kucha!Huyu Dr Slaa...anaupeo wa juu sana!!
YAMETIMIA!!
>Nabii anapotabiri na yanapothibitika kutokea aliyoyatabiri, haimaanishi kwamba nabii ndio chanzo.
Sideeq,
Kwa bahati mbaya hata hujui mazingira yaliyomfanya Dr Slaa kusema, Kikwete kama hutarekebisha na na kuendelea kwa Hali hii nchi haitatawalika. Naomba niwaambie Watanzania, kuwa sijutii kutoa onyo Hilo, na Leo naomba kulirudia, tena kwa mdisitiso zaidi.
Ningependa Watanzania tufike mahali na kuacha ushabiki na itikadi kwenye mambo yasiyohitaji ushabiki na itikadi. Kwa Mara ya Kwanza kauli hiyo niliitoa kwenye Mkutano tarehe 5 January 2011 siku ambayo kwa Mara ya kwanza Polisi wametumia mabomu mengi ya Machozi na Risasi za Moto na kuua watu 3 ( kwa taarifa ya Serikali).
Leo miaka 3 baadaye, ninairudia kauli hiyo kwa ujasiri zaidi, baada ya kuisoma Taarifa ya Kamissioner wa Haki za Binadamu Mhe. De Mello ( ambaye sasa ni Jaji wa Mahakama Kuu). Taarifa hiyo, haikuwekwa hadharani, kwa kuwa Serikali iliona inaidhalilisha.
Nilichokisema, kinathibitishwa na Taarifa hiyo,
(1) Wahalifu wa Siku hiyo wa kwanza ni Polisi kwa kufuta maandamano ya Chadema yaliyokuwa halali mpaka usiku yalipofutwa na polisi bila kufuata utaratibu wa Sheria. Taarifa inataja kabisa kuwa Sheria ya vyama vya siasa ilivunjwa na polisi.
2) haki za binadamu zilivunjwa na Polisi kwa kutumia nguvu kubwa kinyume na Sheria, na Taarifa iliwataka wahusika wote kuchukuliwa hatua.
3) IGP ndiye kinara wa kuvunja Sheria kwa kuingilia kuzuia maandamano kinyume na Sheria.
Baadhi ya Watanzania wakaendeleza ushabiki wa "Dr Slaa kachochea kwa kueleza nchi haitatawalika"..... Taarifa hiyo ya Arusha, inathibitishwa kwa mara ya pili na Taarifa ya Tume ya Haki za Binadamu ( ambayo ni chombo cha Serikali) ambayo nayo katika tukio la Mabomu lililosababisha kifo cha Mwandishi wa Habari Daudi Mwangosi, Polisi wakiongozwa na Kamanda Kamuhanda ndio wanaotuhumiwa kuvunja Sheria ya vyama vya siasa kwa kuingilia mikutano ya Chadema ten a ya ndani. Katika Tukio la Mwangosi, naye msajili wa vyama vya siasa anatuhumiwa kuvunja Sheria ya nchi kwa kuzuia mikutano ya Chadema wakati sheria ya Sensus haizuii shughuli.
Watanzania wenye kutafiti na kusoma Taarifa hizi badala ya kuandika kwa ushabiki. Kwa Taarifa yako ndio maana Dr. Slaa anaconda nje, kwa kuwa Serikali inajua onyo lilikuwa sahihi, kwa mujibu wa sheria, na lingetekelezwa maisha ya watanzania yasingeliangamia. Aidha, yote niliyoonya, mishahara, maisha magumu, ufisadi, ulinzi wa rasilimali za Taifa, tusingelifika tulipofika Leo. Serikali ijilaumu yenyewe, na mashabiki nanny mnasehemu yenu ya lawama.
Inaripotiwa na kukaririwa mara kwa mara kuwa baada ya kushindwa uchaguzi wa 2010 Dr.Slaa alisema waziwazi kuwa nchi haitatawalika na kweli tunashuhudia kwa macho yetu, tokea sababu za kukamatwa kwa Lwakatare mpaka bomu lililolipuliwa Kanisani huko Arusha!
Hali ni mbaya kiasi Watanzania wamekaa na kujiuliza baada ya matukio haya ni kipi kinachofuatia? kulipua Bunge na kuambiwa aliyerusha bomu ameonekana na mtoto mdogo akiwa kavalia kanzu? Ikulu? Airport...wapi? maana yake tumeambiwa kuwa nchi haitatawalika.
Kimtazamo wangu na nadhani kuna wengi tu watakaokubaliana na mimi ni kuwa Dr.Slaa hastahili kuwa uraiani na kuishi kwa kodi ya haohao anaotaka kuwaharibia nchi.

mkuu mtazamo wako ni hasi, dr slaa kusema nchi haitatawalika hakufanyi nchi isitawalike, kinachotakiwa hapa ni kuchunguza kwa nini aseme hivyo? Mimi binafsi naungana na dr. Ni kweli kwa hali ilivyo tanzania kutawalika ni ngumu, tanzania sheria inaendeshwa kiubaguzi, kwa mfano wabunge wa chama tawala ni bora mbele ya sheria kuliko wa upinzani hata wavunje sheria waziwazi, lakini wabunge wa upinzani hukamatwa kama majambazi na vyombo vya dola kana kwamba hawajachaguliwa na wananchi. Pili wananchi wengi wanabambikiziwa kesi hovyohovyo na mapolis, pia kunyanyaswa na hata kudhulumiwa mali zao na hao mapolis, tumeshuhudia wabunge kama mwigulu nchemba kutukana wapinzani kwake ni kawaida, ametuhumiwa kufadhili magaidi kwa kuwalipa pesa kupitia mpesa, lakini hajahojiwa na polis, vyombo vya habari ambavyo vinakosoa serikali vinafungiwa bila utaratibu. Je kweli nchi inaweza ikatawalika hivo? Kiujumla serikali ndo tatizo!Inaripotiwa na kukaririwa mara kwa mara kuwa baada ya kushindwa uchaguzi wa 2010 Dr.Slaa alisema waziwazi kuwa nchi haitatawalika na kweli tunashuhudia kwa macho yetu, tokea sababu za kukamatwa kwa Lwakatare mpaka bomu lililolipuliwa Kanisani huko Arusha!
Hali ni mbaya kiasi Watanzania wamekaa na kujiuliza baada ya matukio haya ni kipi kinachofuatia? kulipua Bunge na kuambiwa aliyerusha bomu ameonekana na mtoto mdogo akiwa kavalia kanzu? Ikulu? Airport...wapi? maana yake tumeambiwa kuwa nchi haitatawalika.
Kimtazamo wangu na nadhani kuna wengi tu watakaokubaliana na mimi ni kuwa Dr.Slaa hastahili kuwa uraiani na kuishi kwa kodi ya haohao anaotaka kuwaharibia nchi.
Slaa hakukosea, nchi haiwezi kutawalika kama hakuna haki kwa raia wote bila ubaguzi, tumeshuhudia mtwara na maeneo mengine katika taifa letu!