Elungata
JF-Expert Member
- Jan 28, 2011
- 40,206
- 33,223
Dr Slaa siwezi kupinga unachokiongea maana wewe ni miongoni mwa viongozi wa kisiasa hapa Tanzania, je? vipi wananchi tunaweza kuthibitisha kauli zako unazosema tunaomba utuletee na ushahidi na sio maneno maana tunawaelewa wana siasa mulivyo na maneno mengi vinywani mwenu, kama unazo hizo documents za ushahidi wa mapato ya Muheshimiwa RA na RIZ kwa nini musiwatumie wanasheria wenu wa CHADEMA kuwapeleka mahakamani kama muna wasiwasi na source za mapato yao.
Mengi unayoyaongea ni kwa ajili ya maslahi ya nchi lakini je Rizwan Kumiliki mabilioni ni kitu cha hatari? Naelewa kwa ufahamu wangu Rizwan ni mtoto wa RAIS na baba yake alikuwa waziri katika wizara nyingi sana hapa Tanzania kabla ya kuwa Rais; ninavoelewa mimi Rizwan kumiliki Bilioni moja si kitu cha ajabu, eti kamaliza shule juzi ndio asiweze kumiliki hiyo ela haiingii akilini hata kidogo kwa mtoto wa kimasikini sawa ila Riz sio mtoto wa kimasikini akashindwa kujiingiza kwenye masuala ya kutafuta pesa.
Kama mna ushahidi wa wizi wa fedha muende mahakamani au kama ni siasa tu basi endeleeni (sikupingi Dr Slaa huwa napenda ila ushahidi wako uko wapi?) tuwekee ushahidi ila tunapomwita mtu fisadi kama Riz kweli tujue ili tusipate dhambi kumjadili mtu bila ya ushahidi.
Huyo Slaa, hebu mwambieni aende unyantuzu (Bariad) akawaone vijana wadogo under 25 wakimiliki mali za mabilioni, hawajaenda hata zaidi ya std seven. Sio watoto wa katibu tarafa wala rais.
Ajue kuwa ukiwa na mtaji ku-make ni suala la mwaka. Aende Kahama aone vijana wa kinyantuzu wanavyoporomosha maghorofa, hawakusoma wamefanya biashara ya maduka, mifugo leo wana pesa.
Aache kulalama afanye kazi