Ninamhurumia sana Kikwete. Laiti kama bidii na nguvu anazotumia kupambana na Mungu angeitumia kuboresha maisha , leo hii Tanzania ingelikuwa ni hadithi nyingine duniani.
Maskini Jakaya anaponzwa na kutokumjua Mungu wala Uweza wa Nguvu zake. Mwisho wa yote atawaponza na anoawatumia kama vile farao wa Misri alivyowaponza wamisri na wanajeshi wake katika bahari ya shamu wakati kawatuma kuwafukuzia wana wa Israel.
Hivi Ccm kwa nini hammpi ushauri huyu mtu? Ni nani alimdanganya kwamba Tanzania ni mali ya ccm? Atasemaje kwamba Tanzania inautawala wa kidemokrasia ikiwa yuko tayari kumtumikia shetani hata kuangamiza taifa ili mradi maslahi yake yalindwe?
Kikwete amefanya nini kibaya hicho ambacho anatumia kila njia kuhakikisha anaweka mamluki wake serikalini la sivyo huu utakuwa mwisho wake?
Kwa nini asikumbuke namna Watanzania walivyomkabidhi nchi ikiwa na ahueni tena kwa amani na kumwacha kwa miaka kumi hata alipokuwa ameiharibu nchi namna hii?
Ni binadamu wa namna gani aliyejaa viburi, visasi na uharibifu mkuu namna hii?
MWAMBIENI HAWEZI KUWA NA UWEZO KULIKO MUNGU. MWISHO WA SIKU LAZIMA MUNGU AJITUKUZE.