Mengi ameingilia bunge na kuhongo baadhi ya wabunge na kuwafanya waimbe nyimbo za mafisadi kama mengi na mkono wametia aibu sana.Pesa ya mfanyabiashara dalali na mwenye uchu,ndg Reginard Mengi.Huyu anatamani awe Aliko Dangote ndani ya mda mfupi,anataka rasilimali yote iwe chini yake na pia aiendeshe serikali kwa jinsi anavyotaka.
Kwani wewe ni miongoni mwa wabunge waliohongwa na mafisadi ili kufanikisha malengo ya mafisadi?
Karibu JF. Piga kazi uliyopewa, usije ukakosa kwenda choo
Tunasubiri kesho kama mapemdekezo yenu yatatekelezwa na mshirika wa mwajiri.
umeme tunalipa, hatuishii hapo bali tunalipa mpaka madeni ya tanesco; ndiyo maana nasema hakuna mwananchi yeyote anayeunga mkono upuuzi huu. kutumia jina "wananchi" kuhadaa watu haitawasaidiaSi uoneshe walioiba, ripoti ya CAG hujaiona? ni nani kaiba? mlitaka umeme wa bure?
Ni wazi kwamba kama watu watakuwa wakifungwa kwa kuwa kuna kundi la watu linahisi kwamba ni wahalifu basi tumekwisha. Uongo uliosambazwa na watu waliokuwa na lengo maalum umekuwa ni sumu kali lakini hatimaye ukweli unajitokeza na utajipembua.
Busara ni kukubali kwamba tuliingizwa mkenge na akina Zitto et al na kwamba tuna bahati hatukuchinjana kwa uongo huo. tamwimu zinaongea na ukweli ni kwamba hiyo jinai inatafutwa kwa ajili ya kuwasiadia nbaadhi ya watu kuupata urais kwa urahisi, wengine kupata faida ya kuondokana na ushindani katika biashara ya umeme na wengine ni roho mbaya tu ya kutotaka ye yote yule apate fedha. Kwa mtindo huu ni wazi tutaendelea kudumaa na kutawaliwa milele kwani wanaochezesha mchezo huu wako London na New York wanatucheka tu.
Umme hulipi hela yote,kuna subsidy kutoka serkalini.umeme tunalipa, hatuishii hapo bali tunalipa mpaka madeni ya tanesco; ndiyo maana nasema hakuna mwananchi yeyote anayeunga mkono upuuzi huu. kutumia jina "wananchi" kuhadaa watu haitawasaidia
Wamemuibia nani?
Mmekazana wameiba, wameiba, mkulizwa nani kaibiwa? hamna majibu. Ulifikiri Hebinder Singh anagawa umeme wa bure?
Jiulize, ulitaka umeme wa bure?
Ukitaka kujua kwa uhakika PAP ilichepuka kwa manufaa ya nani, wallah utaandika kitabu! Kwa kifupi Tegeta Escrow Account ilitumiwa kama wimbo mzuri wa kuwahamasisha watanzania waone wameibiwa, wawachukie viongozi wao, wachukie IPTL, wachukie PAP, wachukie VIP kwa maslahi binafsi yanayotokana na (1) Chuki Binafsi (2) Siasa - Daraja kuelekea 2015 (3) Maslahi binafsi na (4) Hila za Standard Chartered Bank!Mleta mada must be on payroll ya mafisadi
Amerudia-rudia maneno
ameshindwa kuthibitisha chochote zaidi ya too many words in the post
bado anakubali kwamba escrow ni tatizo na anashindwa kusema ni uthibitisho upi unaweza kutumia kusema yupi amedanganya, lakini tayari ameamua yupi mwongo
Ukitaka kujua kwa uhakika PAP ilichepuka kwa manufaa ya nani, wallah utaandika kitabu! Kwa kifupi Tegeta Escrow Account ilitumiwa kama wimbo mzuri wa kuwahamasisha watanzania waone wameibiwa, wawachukie viongozi wao, wachukie IPTL, wachukie PAP, wachukie VIP kwa maslahi binafsi yanayotokana na (1) Chuki Binafsi (2) Siasa - Daraja kuelekea 2015 (3) Maslahi binafsi na (4) Hila za Standard Chartered Bank!
Tuanze na Msingi wa tatizo la Tegeta Escrow Account – Kwamba IPTL iliinyonya TANESCO na kuilipisha capacity charge kubwa (overcharging), kiasi kwamba fedha zilizowekwa kwenye Tegeta Escrow Account zilikuwa za TANESCO na hivyo mali ya Umma.
Ni budi watanzania wafahamu kwamba hela iliyowekwa kwenye Tegeta Escrow Account ilitokana na Invoice zilitolewa na IPTL kuhusu huduma iliyotolewa na IPTL kwa TANESCO- Invoice hizo zilihusu tozo ya uwekezaji (capacity charges) na zilidai capacity charges kwa mujibu wa ukokotoaji uliotokana na Maamuzi ya ICSID ya mwaka 2001 –Maamuzi haya mpaka leo tarehe 18/12/2014 hayajawahi kupingwa na TANESCO na yanasimama kama maamuzi halali juu ya tozo ambayo TANESCO wanatakiwa kuilipa IPTL.
Tegeta Escrow Account ilifunguliwa kwa jitihada za Mkono Advocates waliosema eti uwekezaji wa IPTL ni TZS 50,000/=, yaani kwa kiswahili rahisi kuwa gharama za uwekezaji wote wa IPTL, yaani ardhi, mitambo n.k ni Shilingi za Kitanzania Milioni Hamsini! Labda utakuwa unashangaa! Si wewe peke yako, nami nashangaa!
Wakili mwenza wa Mkono katika kuitetea TANESCO ananukuriwa katika ripoti ya CAG ukurasa wa 20 hivi: "katika uchunguzi wao Hunton and Williams waliainisha kuwa ujenzi wa mitambo ya IPTL kwa kutumia mtaji (owners equity) wa TShs 50,000 hauleti mantiki katika uhalisia wake kinyume na ilivyoanishwa na Mkono & Co. Advocates" Baada ya kufunguliwa Tegeta Escrow Account, hakuna shauri lolote lilofunguliwa (na lisingefunguliwa sababu ICSID ilishaamua tangu mwaka 2001) – Lakini angalau Mkono & Co. Advocates, waliweza kuhakikisha kuwa kuna mgogoro hewa na kuendelea kujipatia fedha isiyo haramu kutoka TANESCO – TZS Bilioni 62 ambazo Mkono alilipwa si mada ya watanzania kujadili.
Ripoti ya CAG inatambua kuwa kwa kuzingatia invoice za IPTL ambazo zinaendana na uamuzi wa ICSID wa mwaka 2001, TANESCO ilikuwa inadaiwa na IPTL sababu TANESCO haikuweka kiasi chote ilichokuwa inadaiwa kwenye Escrow Account
Ripoti ya CAG kwa ukamilifu wake, kwa wale walioisoma haikutamka popote kuwa kuna fedha ya Serikali kwenye Tegeta Escrow Account, PAC ndio walioona hilo kwa kuipindisha ripoti, na wenye akili tunajua wale mashabiki pia wamejitahidi kupinga ripoti ya CAG kuwekwa hadharani kwa sababu inawaumbua!!! Ni kweli PAC walichepuka!!
Sasa tumeshajua kuwa kinachoweza kufanya kilichomo kwenye Tegeta Escrow Account ni KAMA FEDHA WALIYOWEKA TANESCO walipokuwa wanalipa kwa mujibu wa Invoice za IPTL kilikuwa ni kiasi cha juu – yaani kama "TANESCO was overcharged" kwa lugha ya kizungu.
WAS TANESCO OVERCHARGED BY IPTL? Jibu ni hapana, Kwanza, malipo yote yalizingatia invoice zilizofuata maamuzi ya ICSID ya mwaka 2001 [Ningependa Zitto and Team waseme hapa kama ninachosema siyo sahihi kwa hoja]
Pili, IPTL ni kampuni pekee inayotoza tozo ya chini kabisa ya uwekezaji kati ya makampuni yote yanayouzia umeme TANESCO [Ningependa Zitto and Team kama wanabisha basi wataje kampuni moja yoyote ambayo tozo yake ya capacity charges ipo chini ya ile ya IPTL]
NI DHAHIRI HAKUNA kitu kinachoitwa pesa za Umma katika Akaunti ya Escrow...
Jana, niliandika kwenye thread: Re: Vip engineering yashinda kesi hapa Jamii Forum kwenye jukwaa la Biashara na Uchumi, kwa nia ya kueleweshana nikaibua hoja kadhaa ili zijibiwe! Naomba nisamehewe, nirudishe maoni au maono yangu hapa, ili wenye hoja tuchangie, kwani kusema ukweli, sikupata hoja za wale wanaopinga ukweli kwa ushabiki:
Nimesoma nyaraka hizi za ushindi wa VIP Engineering! Nilipita tu ili nisome nielewe ndo nirudi. Nimesoma, nimeelewa, ni wakati wa kuwaambia Watanzania ukweli.
Bila kupepesa macho, naona dhahiri kuwa Zitto na PAC wametumiwa katika wimbo huu wa ESCROW! Nakubali kusahihishwa kwa hoja!! Ndiyo Hoja zije!
1. Zitto na PAC katika ripoti yao wanasema "kamati imebaini kuwa madai ya Standard Chartered ya Hong Kong kwa IPTL ni halali" – Najiuliza vipi Zitto na kamati yake waliweza kuthibitisha uhalali wa Madai ya Standard Chartered wakati suala la kwamba Standard Chartered ni mdai halali liko bado mahakamani?
2. Nimesoma nyaraka zote zinazohusu ushindi wa VIP Engineering taarifa mbalimbali zinazotolewa kuhusu mashauri haya, nalazimika kusema kuwa kama haya niliyogundua ni ya kweli, basi kazi bado ipo kubwa kufikia ukomavu wa kisiasa wa wanasiasa tunaodhani wanatetea Umma. Hebu twende pamoja:
(a) Standard Chartered Bank ambao wanalalamikia Mahakama za Tanzania baada ya kushindwa kuthibitisha kuwa wanalo deni halali (wanalosema eti walilinunua mwaka 2005 huku IPTL ikiwa tayari katika shauri la ufilisi) wanashitakiwa na VIP Engineering ya Ruge nchini Marekani ili kule zijulikane mbichi na mbivu hasa kuhusu uhalali wa linaloitwa deni na madhara ambayo Standard Chartered Bank imesababisha kwa VIP Engineering kwa kujiita mdai wa IPTL.
(b) Standard Chartered Bank baada ya kushitakiwa Marekani kwa woga wa kuumbiliwa tena huko dunia ya kwanza, wanaiambia Mahakama, IPTL imesajiliwa Tanzania, mtambo upo Tanzania, mashahidi wengi wapo Tanzania, tena kesi nyingine kuhusu IPTL zipo Tanzania!!! na wanaendelea kuiambia Mahakama ya Marekani kuwa shauri la Marekani lifutwe ili kesi ikasikilizwe kwenye Mahakama za Tanzania ambako wanakubali kutii amri yoyote ya Mahakama itakayotolewa. Jaji wa Marekani anakubalina na Standard Chartered Bank na kuamua kuwa mgogogo ulioanzishwa na VIP Engineering upelekwe Tanzania.
(c) VIP Engineering kwa kuzingatia maelekezo yaliyotolewa na Standard Chartered inafungua shauri la madai nchini Tanzania dhidi ya Standard Chartered Bank-Shauri ambalo kimantiki ni lilelile lililokuwa Marekani.
(d) Baada ya kuona kweli kuwa VIP Engineering haiweki mzaha katika madai yake, sasa Standard Chartered Bank wanajaribu kukana walichokisema Mahakamani Marekani [WANAKANA KWAMBA WALIKUBALI KUSHITAKIWA TANZANIA, WANAKANA KWAMBA WALIJIFUNGA KUHESHIMU HUKUMU ITAKAYOTOLEWA NA MAHAKAMA YA TANZANIA –AIBU! Wanakata rufaa ambayo ndo sasa wameshindwa. Mahakam ya Rufaa inakubalina na Maamuzi ya Jaji Victor Marrero yaliyosema:
The Court reaffirms its September 10 Order, which relied on Standard Chartered's representations that it considered Tanzania an adequate alternative forum, and which the Court deems an expression of Standard Chartered's consent to the adjudication of this action in Tanzania, and to comply with any final judgment rendered by any court of competent jurisdiction there in connection with the parties' underlying dispute.
(e) Kama vile haitoshi, WAKIWA TAYARI WAMESHITAKIWA NCHINI TANZANIA, baada ya wao wenyewe kuwa wameomba hivyo kwenye kesi waliyoshitakiwa nchini Marekani, wanafungua kesi dhidi ya VIP Engineering nchini Uingereza ambapo wanapinga kushitakiwa Tanzania [HAWA NDIO ZITTO NA PAC wanasema wana deni halali.
(f) Hawa ndio Standard Chartered Bank ambao Zitto na PAC wanasema kwamba mgogoro wao hauwezi kusikilizwa na Mahakama za Tanzania. Hivi haya majumuisho Zitto aliyapata wapi??? Hivi Zitto ni mweredi sana kuliko Mahakama ya Rufaa ya Nchini Marekani??? KWANINI tusiamini Zitto anatumiwa kuendesha kesi ya Standard Chartered kisiasa kwa sababu anauwezo wa kuongelea Bungeni ambako labda waathirika hawawezi kupata nafasi ya kuongelea.
(g) Wakati kukiwa na kesi nchini Tanzania, na kesi iliyofunguliwa baadaye nchini Uingereza, wakati Standard Chartered Bank ikiwa imefungua rufaa ya kukana iliyoyatamka nchini Marekani (Rufaa ambayo dhahili wameshindwa), ni kitu gani kilichofanya Mheshimiwa Barozi wa Uingereza .... atamke kuhusu yaliyo mahakamani, kama kweli haki ndo inayotafutwa. Zitto mwenyewe alitamka Bungeni kuwa alifuatwa – Aibu tupu?
(h) Hivi tukijaribu kuuvaa umakini, kwa wale waliosoma ripoti ya CAG, hivi ni kweli ripoti ya PAC imezingatia mapendekezo ya CAG, au hata kuyatilia maanani, na kama haikufanya hivyo, kwanini sasa CAG alipewa kazi ya kutayarisha ripoti (wakati PAC ilikuwa na uwezo wa kugundua, kuamua na kutoa hukumu.
(i) Zitto! Huyu huyu na PAC eti "kamati ilishangazwa kuona kwamba katika hali isiyokuwa ya kawaida, mahakama .... ilikwenda mbali zaidi na kupanga kiwango cha bei ya umeme kuwa USD 0.6 hadi 0.8 kwa uniti moja ya umeme. Sasa kama VIP Engineering iliweka sharti kuwa anayenunua hisa zake lazima ashushe bei ya umeme, na mnunuzi akakubali, wewe Zitto ni nani hata upinge hiyo bei ya chini! Na hutaki gharama ya umeme ishuke ili iwe nini! Hapo unamtetea Mtanzania kama unavyotaka uaminike?
(j) SASA SWALI LA MWISHO KWA WENYE AKILI: mgogoro wote unaohusu Tegeta Escrow Account unaanzia kwenye suala kuwa – IPTL ime-i-overcharge TANESCO kwenye CAPACITY CHARGES –SASA, ZITTO TWAMBIE, ni kampuni gani inayouza umeme TANESCO ambayo inatoza capacity charges ambazo ni za chini kuliko IPTL? Mimi nafahamu kuwa IPTL ndiyo inatoza tozo ya chini kabisa kwa maana ya capacity charges.
(k) Mpaka ZITTO na wenzako mkiweza kujibu kwa kutaja kampuni yoyote inayotoza tozo ndogo kuliko IPTL (Ili umma ujue kuwa IPTL inainyonya TANESCO) nitaendelea kusema kuwa MNATUMIWA KWA MASLAHI BINAFSI
(l) Ni wakati wa kuacha ushabiki na kujadili hoja...
HALAFU NAENDELEA KUJIULIZA TENA KWA SAUTI: 1. Hivi baada ya ule uamuzi wa ICSID wa mwaka 2001 katika kesi ambayo TANESCO walifungua dhidi ya IPTL, kesi ambayo ndiyo iliyoweka kiasi cha tozo ambacho TANESCO walitakiwa kulipa kwa IPTL, Je kuna uamuzi wowote ambao ulishabatilisha huo uamuzi wa mwaka 2001? Zitto twambie ripoti ya CAG inasemaje kuhusu hili? 2. Je TANESCO kwa mujibu wa uamuzi wa ICSID wa mwaka 2001 wanadaiwa fedha kiasi gani na IPTL kwa maana ya fedha waliyotakiwa kuweka kwenye Tegeta Escrow Account lakini hawakuweka? 3. Mtu mwenye busara atusomee ukurasa wa 24 wa ripoti ya CAG, na baada ya hapo atusomee mapendekezo yanayofuata. 4. Ni dhambi kubwa kufanyia siasa za chuki, siasa za maslahi, siasa za visasi kwenye chombo tukufu kama Bunge! Bunge ni chombo kitakatifu (au kinatakiwa kuwa chombo kitakatifu)
ZILETWE HOJA HAPA TUZIJADILI, Watanzania wajue pumba zipi au upi mchele... tumechoshwa na propaganda zisizokuwa na mantiki
SASA, maadamu hoja zipo mtajua sasa majibu kwanini PAC walichepuka
BUNGE ni Taasisi yenye heshima kubwa ndani na nje ya Nchi. Heshima ya Bunge inatokana na umuhimu wa kazi yake kwa maslahi ya nchi na wananchi.
Kazi za Bunge kupitia kamati zake mbalimbali zina manufaa makubwa kwa Taifa. Mathalani, Kamati ya Hesabu za Serikali ya Bunge ina kazi muhimu ya kuhakikisha kuwa hesabu za serikali zinakuwa bayana na sahihi.
Kwa kufanya kazi zake kwa uadilifu na uzalendo, Kamati za Bunge zina nafasi muhimu ya kuisukuma na kuiwajibisha serikali kwa manufaa ya Umma. Kwa kiasi fulani, hatusiti kusema kuwa Kamati hizo zinajitahidi kutimiza wajibu wao.
Hata hivyo, tunalazimika kuikosoa hadharani Kamati ya Hesabu za Serikali ya Bunge kwa namna ilivyoandaa na kuwasilisha ripoti yake ya Fedha za Akaunti ya Escrow.
Taifa lilishitushwa na taarifa ya Kamati hiyo kuwa fedha nyingi za nchi zimechotwa kinyume na taratibu. Kamati imetaja majina ya watu na hata mazingira ya wizi ikiwa ni pamoja na maboksi, viroba na masandarusi yaliyotumika kubebea fedha hizo!
Mjadala ukawa mzito ambapo ndani ya Bunge na nje yake, moto wa hasira uliwaka kwelikweli. Ni ujasiri wa hali ya juu uliohitajika kutuliza hasira hizo kwa
maneno tofauti na yale ya Kamati.
Ilikuwa kana kwamba kila mtu alitakiwa kuamini bila kuhoji. Aliyehoji au kutoa maoni tofauti akaonekana kama mchawi na labda ni sehemu ya watu waliopata mgao.
Ndani ya Bunge, ujasiri wa mawaziri kama Hawa Ghasia, Celina Kombani na Angellah Karuki pamoja na Wabunge kama Asumta Mshama na Job Lusinde na waziri mahiri Simbachawene wa kukataa uongo ulionekana kama kero tu ambayo Taifa halikutakiwa kuisikia. Mawaziri hawa wanwake na Wabunge hawa wanabaki kama wapiganaji waliojitoa muhanga kuhakikisha kuwa ukweli unachukua nafasi masikioni na machoni mwa wananchi.
Pale mwanzo, ujasiri huo ulionekana kwa wachache ambao ilionekana kama vile wangeshindwa na wengi walioamini kila kilichoandikwa na kusemwa na Kamati hiyo ya Bunge!
Ni kweli, PAC ilivuna imani ya wananchi wengi. Lakini, kadiri muda ulivyokwenda hasa baada ya ripoti kukabidhiwa kwa Rais,na serikali kufanya uamuzi wa kuichunguza upya kadhia nzima ya Escrow,kiwango cha imani ya watu juu ya Ripoti ya Kamati kimeonekana kupungua.
Hatua ya Rais kuteua CAG mpya yaweza kuhesabika kama msingi wa kujenga mazingira ya kupata ukweli juu ya hesabu zilizoleta utatanishi. Kila mtu sasa akatulia kusubiri CAG mpya angesema nini.
Yumkini wengi waliamini kuwa majibu ya CAG yangewaweka pagumu wale waliotuhumiwa. Lakini Ripoti ya CAG,baada ya uhakiki, imewalowesha wale
ambao awali waliamini Ripoti ya PAC!
Kusawajika huko kunatokana na masahihisho ya hesabu zilizowasilishwa na Kamati. Mgongano wa kimahesabu kati ya dola milioni 306.6 zilizodaiwa na PAC kuwemo katika Akaunti ya Escrow na dola milioni 182.7 ambazo CAG anasema ndizo zilizokuwemo kwenye Akaunti hiyo umewashangaza wengi!
Taifa linamwamini CAG kwa asilimia 100 kwamba ndiye chombo cha kuweza kutoa taarifa sahihi. Na hata PAC inategemea taarifa za CAG. Swali linaweza kuulizwa, ni nani aliyesababisha mgongano wa mahesabu kwa kughushi na kukikuza kiasi cha fedha kinyume na taarifa ya CAG?
Na aliyefanya hivyo alikusudia nini? Na alifanya kwa maslahi ya nani? Je, huu sio mchezo mchafu wa kuchezea hesabu za serikali kwa malengo yaliyojificha yakiwemo ya kimasilahi, kisiasa na kibiashara?
Kwa kuwasilisha hesabu ambazo CAG anasema si sahihi, maana yake PAC imelidanganya Bunge na Taifa kwa ujumla! Kwa kuwa uongo huu umeleta usumbufu na umegharimu heshima za watu, pamoja na kulishulishushia heshima Tiafa mbele ya jumuiya ya kimataifa kuwa la wala rushwa na wafuja pesa, sisi tunapendekeza kuwa Bunge likutane kwa dharura ili PAC iliombe radhi Taifa kwa uongo huo.
Zaidi ya hivyo, kwa kuwa imepoteza imani ya watu juu ya umakini na uadilifu wake, PAC haina sababu ya kubaki na uongozi uliopo hivi sasa. Bunge linahitaji kujisafisha kwa kuivunja PAC na kuiunda upya.
Ni muhimu kuivunja PAC na kuipatia uongozi mpya kwani, kwa sura ya sasa haitaaminika tena masikioni na machoni mwa wananchi. Sio tu viongozi wake wa sasa hawapaswi kuwepo madarakani bali wana kila sababu ya kukabiliwa na jinai ya kuwapotosha Wananchi na kuhatarisha usalama wa Taifa.
BUNGE ni Taasisi yenye heshima kubwa ndani na nje ya Nchi. Heshima ya Bunge inatokana na umuhimu wa kazi yake kwa maslahi ya nchi na wananchi.
Kazi za Bunge kupitia kamati zake mbalimbali zina manufaa makubwa kwa Taifa. Mathalani, Kamati ya Hesabu za Serikali ya Bunge ina kazi muhimu ya kuhakikisha kuwa hesabu za serikali zinakuwa bayana na sahihi.
Kwa kufanya kazi zake kwa uadilifu na uzalendo, Kamati za Bunge zina nafasi muhimu ya kuisukuma na kuiwajibisha serikali kwa manufaa ya Umma. Kwa kiasi fulani, hatusiti kusema kuwa Kamati hizo zinajitahidi kutimiza wajibu wao.
Hata hivyo, tunalazimika kuikosoa hadharani Kamati ya Hesabu za Serikali ya Bunge kwa namna ilivyoandaa na kuwasilisha ripoti yake ya Fedha za Akaunti ya Escrow.
Taifa lilishitushwa na taarifa ya Kamati hiyo kuwa fedha nyingi za nchi zimechotwa kinyume na taratibu. Kamati imetaja majina ya watu na hata mazingira ya wizi ikiwa ni pamoja na maboksi, viroba na masandarusi yaliyotumika kubebea fedha hizo!
Mjadala ukawa mzito ambapo ndani ya Bunge na nje yake, moto wa hasira uliwaka kwelikweli. Ni ujasiri wa hali ya juu uliohitajika kutuliza hasira hizo kwa maneno tofauti na yale ya Kamati.
Ilikuwa kana kwamba kila mtu alitakiwa kuamini bila kuhoji. Aliyehoji au kutoa maoni tofauti akaonekana kama mchawi na labda ni sehemu ya watu waliopata mgao.
Ndani ya Bunge, ujasiri wa mawaziri kama Hawa Ghasia, Celina Kombani na Angellah Karuki pamoja na Wabunge kama Asumta Mshama na Job Lusinde wa kukataa uongo ulionekana kama kero tu ambayo Taifa halikutakiwa kuisikia.
Mawaziri hawa wanwake na Wabunge hawa wanabaki kama wapiganaji waliojitoa muhanga kuhakikisha kuwa ukweli unachukua nafasi masikioni na machoni mwa wananchi.
Pale mwanzo, ujasiri huo ulionekana kwa wachache ambao ilionekana kama vile wangeshindwa na wengi walioamini kila kilichoandikwa na kusemwa na Kamati hiyo ya Bunge!
Ni kweli, PAC ilivuna imani ya wananchi wengi. Lakini, kadiri muda ulivyokwenda hasa baada ya ripoti kukabidhiwa kwa Rais, na serikali kufanya uamuzi wa kuichunguza upya kadhia nzima ya Escrow, kiwango cha imani ya watu juu ya Ripoti ya Kamati kimeonekana kupungua.
Hatua ya Rais kuteua CAG mpya yaweza kuhesabika kama msingi wa kujenga mazingira ya kupata ukweli juu ya hesabu zilizoleta utatanishi. Kila mtu sasa akatulia kusubiri CAG mpya angesema nini.
Yumkini wengi waliamini kuwa majibu ya CAG yangewaweka pagumu wale waliotuhumiwa. Lakini Ripoti ya CAG, baada ya uhakiki, imewalowesha wale ambao awali waliamini Ripoti ya PAC! Kusawajika huko kunatokana na masahihisho ya hesabu zilizowasilishwa na Kamati.
Mgongano wa kimahesabu kati ya dola bilioni 306.6 zilizodaiwa na PAC kuwemo katika Akaunti ya Escrow na dola bilioni 182.7 ambazo CAG anasema ndizo zilizokuwemo kwenye Akaunti hiyo umewashangaza wengi!
Taifa linamwamini CAG kwa asilimia 100 kwamba ndiye chombo cha kuweza kutoa taarifa sahihi. Na hata PAC inategemea taarifa za CAG. Swali linaweza kuulizwa, ni nani aliyesababisha mgongano wa mahesabu kwa kughushi na kukikuza kiasi cha fedha kinyume na taarifa ya CAG?
Na aliyefanya hivyo alikusudia nini? Na alifanya kwa maslahi ya nani? Je, huu sio mchezo mchafu wa kuchezea hesabu za serikali kwa malengo yaliyojificha yakiwemo ya kimasilahi, kisiasa na kibiashara?
Kwa kuwasilisha hesabu ambazo CAG anasema si sahihi, maana yake PAC imelidanganya Bunge na Taifa kwa ujumla!
Kwa kuwa uongo huu umeleta usumbufu na umegharimu heshima za watu, pamoja na kulishulishushia heshima Tiafa mbele ya jumuiya ya kimataifa kuwa la wala rushwa na wafuja pesa, sisi tunapendekeza kuwa Bunge likutane kwa dharura ili PAC iliombe radhi Taifa kwa uongo huo.
Zaidi ya hivyo, kwa kuwa imepoteza imani ya watu juu ya umakini na uadilifu wake, PAC haina sababu ya kubaki na uongozi uliopo hivi sasa. Bunge linahitaji kujisafisha kwa kuivunja PAC na kuiunda upya.
Ni muhimu kuivunja PAC na kuipatia uongozi mpya kwani, kwa sura ya sasa haitaaminika tena masikioni na machoni mwa wananchi. Sio tu viongozi wake wa sasa hawapaswi kuwepo madarakani bali wana kila sababu ya kukabiliwa na jinai ya kuwapotosha Wananchi na kuhatarisha usalama wa Taifa.
Kwani zile pesa za ESCRO zilikuwa malipo ya umeme? Ndio maana nimeomba CV ya huyu bibi maana anasoma taarifa Laki sina uhakika kama anaielewa...anataka mpaka akute sentensi inayosema mhongo ameiba....vitu vingine vinatakiwa viwe digested kuvielewa kama elimu yako ya kuunga unga omba msaada ueleweshwe
Just how much are they paying you?? do you know how many people die (daily) kwasababu ya haya mabao mnayopiga
Just how much humanity imebaki kwako aisee?? do you fear God??
kuna thread zaidi ya tano humu, chambuzi mbalimbali na post zaidi ya 1000 zenye hoja, chambuzi nk. pia kuna forums nyingine, email groups etc. wamejadilikati ya anayetoa hoja ambazo hazipingiki kwa hoja zozote za mwenye akili..na anayeshabikia bila hoja yoyote ni nani anayepaswa kuulizwa kama analipwa, sasa tupe majibu ya maswali ambayo ni ya msingi na kama huna utwambie umelipwa Shilingi ngapi kuimba chorus ya Escrow bila data.
Just how much are they paying you?? do you know how many people die (daily) kwasababu ya haya mabao mnayopiga
Just how much humanity imebaki kwako aisee?? do you fear God??
jamaa ametoa hoja za kueleweka kama wewe unazo tofauti na zile zitoe nazo tuzipime acha siasa na ushabiki