Kujenga hoja ni kazi ngumu sana. Ninachoona Mimi ni kejeli tupu badala ya mjadala wa kina na mashiko. Kukimbilia hukumu bila ya kuainisha mlolongo mzima wenye uthibitisho wa jinai ni kukurupuka. Prof AT kaombea taasisi yake fedha kazipata na kuwakabidhi. Waliokabidhiwa wakiongozwa na Balozi Paul Rupia wamekiri kuzipokea zote. Sasa kama ni kuwachinja tuanze na waliomtuma yaani Bodi ya Balozi Rupia na wengineo. Tumekimbia hoja tunapiga mayowe. Ni hatari sana kufanya maamuzi mazito kwa hisia.