Sizonje usichanganyikiwe, Mambo bado!!

Sizonje usichanganyikiwe, Mambo bado!!

Sizonje anacheza nje ya ni bit ,najiuliza mpaka sasa nakosa majibu nani alimsajili huyu kwenye timu yetu? Kutoka kua mchezaji wa kawaida mpaka kocha??? Ona sasa timu inashuka daraja kocha hajali ,ameshindwa kupanga first eleven,capten hasikilizwi kwa ushauri,anasikilizwa under 21 wa timu B,sizonje hii timu yetu mbona hatushindiiii?
 
ifike point mkue hii forum ni kwa ajili ya kutoa la moyon sasa we kama yanakuuma ukisikia mabaya kaa kimya kuliko kuita wenzio wapuuz kwao limewafika kama bado kwako ni suala la mda ingekua ni mwanafunz uliekosa mkpo usinge sema haya sa iz,ungekosa chanjo hospital usinge uona upuuz wa watu.tuachen unafki na ubinafsi kisa wewe yamekunyookea kusema watu waliish kwa dil lakin chanjo zilikuepo na leo dil hamna na chanjo kwisha nani mjanja hapo? kizur chajiuza kibaya ndo kinapenda kelele.Mungu anawaona.

Hii forum nitasema chochote naji feel, utakaa kimya mwenyewe, ungenielezea ni chanjo gani hazipatikani mahospital, na ni mwaka gani wanafunzi wote walipata mkopo. Me sio kwamba nimenyokewa na wala hakuna mtu anaenyokewa mambo yake yote, siku zote duniani kuna changamoto, tusiwe watu wa kulaumu laumu.
 
Hii forum nitasema chochote naji feel, utakaa kimya mwenyewe, ungenielezea ni chanjo gani hazipatikani mahospital, na ni mwaka gani wanafunzi wote walipata mkopo. Me sio kwamba nimenyokewa na wala hakuna mtu anaenyokewa mambo yake yote, siku zote duniani kuna changamoto, tusiwe watu wa kulaumu laumu.
Acha panik hayajakukuta ndo mana unasema tunalaumu na usijishaue et hujui hivo vitu hamna.punguza mahaba niue.
 
Hii forum nitasema chochote naji feel, utakaa kimya mwenyewe, ungenielezea ni chanjo gani hazipatikani mahospital, na ni mwaka gani wanafunzi wote walipata mkopo. Me sio kwamba nimenyokewa na wala hakuna mtu anaenyokewa mambo yake yote, siku zote duniani kuna changamoto, tusiwe watu wa kulaumu laumu.
Ndugu yangu bora ungenyamaza humu tunajuana wengi wao wanapenda mafanikio bila kuyahangaiki elewa hizi ni tabia za kibongo tabia za kiswahili.hata wote wangepata bado wangedai mengine umesahau tabia za waswahili?
 
Lakini mbona Sizonje anatamani kuwa beki wa kati? nana atakua kocha?
 
~~~~~>>>>Uchumi wa Tanzania ulijengwa ktk Misingi ya Ufisadi na Ujanja Ujanja....

~~~~>>>>Awamu ya Tano wameziba mianya ya Wizi ghafla..... Lazima mtikisiko utokee kidogo....

~~~~~>>>> Le Châtelier's principle...... If the system is in Equilbrium and the changes occurs, the sytem will do what it can to oppose the Changes...

Kwahiyo haya matusi na vijembe ni ktk kukabiliana na mabadiliko.......
bei ya sembe na yenyewe ilikua ya ujanja ujanja? kushuka kwa Tsh vs $ je? bei ya mafuta leo 2060 je?
 
Acha panik hayajakukuta ndo mana unasema tunalaumu na usijishaue et hujui hivo vitu hamna.punguza mahaba niue.

Me sijapanick bhana, najishaua aje sasa, hujanijibu chanjo gani haipatikani hospitals, hujanijibu mwaka gani wanafunzi wote walipata mkopo, sasa nani mwenye mahaba niue kati yangu nawe.
 
Uzuri wake makamisaa wanamwambia time IPO kwenye kiwango bora haijawah tokea tangu kuumbwa kwa duara hili
 
Mpendwa Sizonje habari za siku.... natumaini u buheri wa afya kibaiolojia japokuwa kiroho u tofauti...

Rafiki yangu Sizonje nakumbuka enzi zile tukijadili mpira ulivyokua hodari kumlaumu kocha!! Kwamba kocha wa timu yetu hawezi... kocha mzembe na anafuga uvundo....

Kadiri tulipokutana kila baada ya sentensi tatu lazima umseme kocha kila siku ikawa hamkani si shwari!!

Sizonje utakumbuka kocha alikuvumilia sana japokuwa ulikua huwezi!! Mdomo na maneno mengi yalikubeba kwa mashabiki lakini wachezaji wenzio walikujua!! Ulikua bingwa wa kukariri tarakimu za mchezo bila ujuzi na weledi wa mchezo!! Hata kocha alipoonywa sana juu ya kiwango chako kibovu bado alikubeba ingawa ulimsogoa!!

Hayawi hayawi yakawa Sizonje!! Kauli zako zikalipa!! Kocha akastaafu na ukocha ukapewa wewe!! Kila mtu ndani ya timu akiduwaa mashabiki waliolewa kauli zako tamu ziso kifani walikubeba hatimaye ukawa kocha!!

Awali ulionesha uwezo wa kukonga mashabiki kwa sifa na vitimbi kemkem!! Siku zikasonga mashabiki wakaona timu inarejea nyuma kuliko ilikokuwa kwa kocha mzembe!!

Nakujua Sizonje!! Hupendi kukosolewa na wala hupendi kimya cha sifa!! Vigelegele vya mashabiki na vifijo vimekoma!! Mbinu zote za michezo ulizotumia zimebuma!! Timu inarudi nyuma kwa kasi na wachezaji wameshapoteza mori!! Kila ugusapo sasa hapagusiki!! Wachezaji wanaonesha ari machoni pako tu lakini uwanjani wamedorora!!

Sizonje usichanganyikiwe... mambo bado ndio kwanza safari inaanza!! Ishike ngao na kigao kuyahimili majira!!!

Kwa leo naishia hapa Sizonje nikija mjini ntakutembelea tule maboga ya enzi zetu.

-----------------------------------------------------------------
UPDATES:
----------------------------------------------- ---------------
Wakuu napenda kuwaarifu kuwa nimepata taarifa nyeti na rasmi kuwa kocha wetu mpendwa Sizonje ameusoma uzi huu na comments zenu zote. Shukrani kwa wote mliotoa ushauri kwa kocha wetu.
Sikh hizi anabutua butua mpira
 
Back
Top Bottom