Sizonje usichanganyikiwe, Mambo bado!!

Sizonje usichanganyikiwe, Mambo bado!!

Kaka mbona umekazania kwenye tafsiri? Unataka kuuaminisha umma kuwa Rais ndio Sizonje?
U.ji.nga ni mtu kujiwezea kuufanya usinilishe maneno vijana wa siku hizi viroba na shisha za kuiga zimewavuruga akili mtaita majina yoote mnayojisikia kuyaita lakini ukweli unasimama asiyefanya kazi na asile na ole wenu na hayo majina ya kebahi msije jutia baadae.
 
~~~~~>>>>Uchumi wa Tanzania ulijengwa ktk Misingi ya Ufisadi na Ujanja Ujanja....

~~~~>>>>Awamu ya Tano wameziba mianya ya Wizi ghafla..... Lazima mtikisiko utokee kidogo....

~~~~~>>>> Le Châtelier's principle...... If the system is in Equilbrium and the changes occurs, the sytem will do what it can to oppose the Changes...

Kwahiyo haya matusi na vijembe ni ktk kukabiliana na mabadiliko.......
 
Mpendwa Sizonje habari za siku.... natumaini u buheri wa afya kibaiolojia japokuwa kiroho u tofauti...

Rafiki yangu Sizonje nakumbuka enzi zile tukijadili mpira ulivyokua hodari kumlaumu kocha!! Kwamba kocha wa timu yetu hawezi... kocha mzembe na anafuga uvundo....

Kadiri tulipokutana kila baada ya sentensi tatu lazima umseme kocha kila siku ikawa hamkani si shwari!!

Sizonje utakumbuka kocha alikuvumilia sana japokuwa ulikua huwezi!! Mdomo na maneno mengi yalikubeba kwa mashabiki lakini wachezaji wenzio walikujua!! Ulikua bingwa wa kukariri tarakimu za mchezo bila ujuzi na weledi wa mchezo!! Hata kocha alipoonywa sana juu ya kiwango chako kibovu bado alikubeba ingawa ulimsogoa!!

Hayawi hayawi yakawa Sizonje!! Kauli zako zikalipa!! Kocha akastaafu na ukocha ukapewa wewe!! Kila mtu ndani ya timu akiduwaa mashabiki waliolewa kauli zako tamu ziso kifani walikubeba hatimaye ukawa kocha!!

Awali ulionesha uwezo wa kukonga mashabiki kwa sifa na vitimbi kemkem!! Siku zikasonga mashabiki wakaona timu inarejea nyuma kuliko ilikokuwa kwa kocha mzembe!!

Nakujua Sizonje!! Hupendi kukosolewa na wala hupendi kimya cha sifa!! Vigelegele vya mashabiki na vifijo vimekoma!! Mbinu zote za michezo ulizotumia zimebuma!! Timu inarudi nyuma kwa kasi na wachezaji wameshapoteza mori!! Kila ugusapo sasa hapagusiki!! Wachezaji wanaonesha ari machoni pako tu lakini uwanjani wamedorora!!

Sizonje usichanganyikiwe... mambo bado ndio kwanza safari inaanza!! Ishike ngao na kigao kuyahimili majira!!!

Kwa leo naishia hapa Sizonje nikija mjini ntakutembelea tule maboga ya enzi zetu.

-----------------------------------------------------------------
UPDATES:
----------------------------------------------- ---------------
Wakuu napenda kuwaarifu kuwa nimepata taarifa nyeti na rasmi kuwa kocha wetu mpendwa Sizonje ameusoma uzi huu na comments zenu zote. Shukrani kwa wote mliotoa ushauri kwa kocha wetu.

Hongera sana kwa mashairi yaliyojaa ukweli, ingawa muanzilishi wa hili jina "sizonje" nae ametekwa na Sizonje na kuamua kumpaka mafuta kwa mgongo wa chupa. Muasisi wa "Sizonje" amesahau kwamba ni yeye aliyejijengea heshma kwa kutaka kwenda kumuona "mjomba" ili amueleze matatizo ya wachezaji na washangiliaji wa timu, lakini leo anaogopa kumueleza "Sizonje" kwani sizonje hataki "kujaribiwa." Tafadhali, naomba mashairi yako ili niingie nayo studio...
 
Haha shukrani mkuu.
 
U.ji.nga ni mtu kujiwezea kuufanya usinilishe maneno vijana wa siku hizi viroba na shisha za kuiga zimewavuruga akili mtaita majina yoote mnayojisikia kuyaita lakini ukweli unasimama asiyefanya kazi na asile na ole wenu na hayo majina ya kebahi msije jutia baadae.
Unamtishia nani wewe? We ungekuwa unafanya kazi, usingekuwa maskini kama ulivyo sasa!!
moja ya dalili ya umaskini kwa mtanzania wa sasa ni kuufurahia mfumo anaoutumia Sizonje kuichezesha timu.
 
hshhaaaaaaaaaa hlf ndani kuna giza mlango hauonekani.duuuu
Wote mnaomchukia "Sizonje" ni majipu na wapiga "dili". Kama mnaendesha maisha yenu ya halali kabisa hamwezi kumchukia Sizonje.
Sizonje kaka usiogope kelele za hawa wezi na majambazi, sisi tupo pamoja na wewe, endelea hivyo, hivyo kuwabana mpaka wakome ubishi. Tuko pamoja Sizonje.
 
Sizonje hali inazidi kuwa tete. Timu imeelemewa bado unakomalia kazi liyokushinda? Hebu achia ngazi ili timu isishuke daraja!!
 
Back
Top Bottom