Sizonje usichanganyikiwe, Mambo bado!!

Sizonje usichanganyikiwe, Mambo bado!!

Mpendwa Sizonje habari za siku.... natumaini u buheri wa afya kibaiolojia japokuwa kiroho u tofauti...

Rafiki yangu Sizonje nakumbuka enzi zile tukijadili mpira ulivyokua hodari kumlaumu kocha!! Kwamba kocha wa timu yetu hawezi... kocha mzembe na anafuga uvundo....

Kadiri tulipokutana kila baada ya sentensi tatu lazima umseme kocha kila siku ikawa hamkani si shwari!!

Sizonje utakumbuka kocha alikuvumilia sana japokuwa ulikua huwezi!! Mdomo na maneno mengi yalikubeba kwa mashabiki lakini wachezaji wenzio walikujua!! Ulikua bingwa wa kukariri tarakimu za mchezo bila ujuzi na weledi wa mchezo!! Hata kocha alipoonywa sana juu ya kiwango chako kibovu bado alikubeba ingawa ulimsogoa!!

Hayawi hayawi yakawa Sizonje!! Kauli zako zikalipa!! Kocha akastaafu na ukocha ukapewa wewe!! Kila mtu ndani ya timu akiduwaa mashabiki waliolewa kauli zako tamu ziso kifani walikubeba hatimaye ukawa kocha!!

Awali ulionesha uwezo wa kukonga mashabiki kwa sifa na vitimbi kemkem!! Siku zikasonga mashabiki wakaona timu inarejea nyuma kuliko ilikokuwa kwa kocha mzembe!!

Nakujua Sizonje!! Hupendi kukosolewa na wala hupendi kimya cha sifa!! Vigelegele vya mashabiki na vifijo vimekoma!! Mbinu zote za michezo ulizotumia zimebuma!! Timu inarudi nyuma kwa kasi na wachezaji wameshapoteza mori!! Kila ugusapo sasa hapagusiki!! Wachezaji wanaonesha ari machoni pako tu lakini uwanjani wamedorora!!

Sizonje usichanganyikiwe... mambo bado ndio kwanza safari inaanza!! Ishike ngao na kigao kuyahimili majira!!!

Kwa leo naishia hapa Sizonje nikija mjini ntakutembelea tule maboga ya enzi zetu.

-----------------------------------------------------------------
UPDATES:
----------------------------------------------- ---------------
Wakuu napenda kuwaarifu kuwa nimepata taarifa nyeti na rasmi kuwa kocha wetu mpendwa Sizonje ameusoma uzi huu na comments zenu zote. Shukrani kwa wote mliotoa ushauri kwa kocha wetu.
Sizonje ndiye nani?
 
SIZONJE sijui anapeleka wapi timu.....

Alafu mbona Sizonje amepewa majina mengi this time?.......

Mala Juma Ponda Mali ,Mala Nyampala,Tembo, Sasa nasikia anaitwa Trump ......

Kuna ukweli juu ya majina ya Shizonje?.......
Pogba naye ni nani?
 
Mpira ni rahisi sana kuuchezea nje,unaona makosa yote,
 
is creator chaos, not chaos solver

The majority of Tanzanian people say the agenda of....... is to create chaos and worsen issues day by day
 
kama imesemwa na TRA hawaikanushi na mbaya zaidi wananchi hawasomewi tena mapato ya kila mwezi kwanini tusiamini ni kweli?
Kweli hii kitu ya kusomewa mapato yetu sijui imeota mbawa...nakumbuka mtu mmoja alinimbia hii kusomewa mapato ni kiki ya kuvuta sapoti ya raia baada ya hapo itapotea.....
 
Kweli hii kitu ya kusomewa mapato yetu sijui imeota mbawa...nakumbuka mtu mmoja alinimbia hii kusomewa mapato ni kiki ya kuvuta sapoti ya raia baada ya hapo itapotea.....
mapato yameshuka wanaona serikali itaonekana imeshindwa kukusanya mapato hivyo haitangazwi tena.
 
sisi huku kwetu tunamuita mami (mjomba)7m sina lakini natamani kusema kitu bora niishie kuguna tu mhuuuuuuuuuuuuuuu.
 
Ukinunua dai risiti ...teh teh teh!! Sizonje atapata laana ya waathirika wa tetemeko
Sizonje alisema kuna wapiga dili walikuwa wanalipisha kiingilio mlangoni ila hela haionekani..mashabiki wanajaa uwanjani lakini hela hazionekani.....sa sijui kama ni kweli make kocha huyu ana tabia ya uwongo.
 
Back
Top Bottom