Sizonje usichanganyikiwe, Mambo bado!!

Sizonje usichanganyikiwe, Mambo bado!!

Mpendwa Sizonje habari za siku.... natumaini u buheri wa afya kibaiolojia japokuwa kiroho u tofauti...

Rafiki yangu Sizonje nakumbuka enzi zile tukijadili mpira ulivyokua hodari kumlaumu kocha!! Kwamba kocha wa timu yetu hawezi... kocha mzembe na anafuga uvundo....

Kadiri tulipokutana kila baada ya sentensi tatu lazima umseme kocha kila siku ikawa hamkani si shwari!!

Sizonje utakumbuka kocha alikuvumilia sana japokuwa ulikua huwezi!! Mdomo na maneno mengi yalikubeba kwa mashabiki lakini wachezaji wenzio walikujua!! Ulikua bingwa wa kukariri tarakimu za mchezo bila ujuzi na weledi wa mchezo!! Hata kocha alipoonywa sana juu ya kiwango chako kibovu bado alikubeba ingawa ulimsogoa!!

Hayawi hayawi yakawa Sizonje!! Kauli zako zikalipa!! Kocha akastaafu na ukocha ukapewa wewe!! Kila mtu ndani ya timu akiduwaa mashabiki waliolewa kauli zako tamu ziso kifani walikubeba hatimaye ukawa kocha!!

Awali ulionesha uwezo wa kukonga mashabiki kwa sifa na vitimbi kemkem!! Siku zikasonga mashabiki wakaona timu inarejea nyuma kuliko ilikokuwa kwa kocha mzembe!!

Nakujua Sizonje!! Hupendi kukosolewa na wala hupendi kimya cha sifa!! Vigelegele vya mashabiki na vifijo vimekoma!! Mbinu zote za michezo ulizotumia zimebuma!! Timu inarudi nyuma kwa kasi na wachezaji wameshapoteza mori!! Kila ugusapo sasa hapagusiki!! Wachezaji wanaonesha ari machoni pako tu lakini uwanjani wamedorora!!

Sizonje usichanganyikiwe... mambo bado ndio kwanza safari inaanza!! Ishike ngao na kigao kuyahimili majira!!!

Kwa leo naishia hapa Sizonje nikija mjini ntakutembelea tule maboga ya enzi zetu.

-----------------------------------------------------------------
UPDATES:
----------------------------------------------- ---------------
Wakuu napenda kuwaarifu kuwa nimepata taarifa nyeti na rasmi kuwa kocha wetu mpendwa Sizonje ameusoma uzi huu na comments zenu zote. Shukrani kwa wote mliotoa ushauri kwa kocha wetu.
Unajua mwanzo nilipousoma uzi huu sikuuelewa vizuri , ila sasa nimetambua .

Mungu ibariki JF .
 
Sizonje amefanya makubwa ambayo ni mazuri kama mwanadamu hakosi kasoro. Inshaalah Mwenyezi Mungu amjalie afanikiwe katika utendaji wake wa kazi
 
Dhalimu aliyejaa dhuluma za kutisha itapendeza na mengineyo pia.

SIZONJE sijui anapeleka wapi timu.....

Alafu mbona Sizonje amepewa majina mengi this time?.......

Mala Juma Ponda Mali ,Mala Nyampala,Tembo, Sasa nasikia anaitwa Trump ......

Kuna ukweli juu ya majina ya Shizonje?.......
 
Kamati ya usajili yeye, kamati ya mipango na fedha yeys, Benchi la ufundi yeye, Kocha mkuu na. Msaidizi yeye,kamati ya maadili yeye, dah kwa mgawanyo huu wa vyeo nadhani timu itashika nafasi ya kwanza kutoka chini muda si mrefu.
 
Hilo la trump duuu
Juzi sema kukabiliana n.a. matatizo ya watoto kupiga wenzao bunduki ni walimu wapewe silaha
Yako nafikiri kafika mwisho you ni copy na huyu?
 
Kwa nini Rais wetu anatabirika kirahisi hivi.
Yani Uzi huu wa tangu Novemba 2016, hadi leo unaleta maana sana.

Yani ni mtu ambae in and out, watu wanajua hatafanikiwa ...!!

Mpaka siku Airtel yetu ikirudishwa TTCL ndo ntamwamini Sizonje..

Nje ya hapo, Sizonje anatakiwa akaigize huko Hollywood.. Viwango vyake ni zaidi ya Nollywood na Bollywood..
 
Sizonje kama sio yy hajali wala kutafakari likitokea yy kama hayupo
 
Back
Top Bottom