Sizonje usichanganyikiwe, Mambo bado!!

Sizonje usichanganyikiwe, Mambo bado!!

Maana ya sizonje ni ile uliobaki nayo kichwani lakini huwezi ,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,, kweli chungu hakimlaumu mfinyanzi,
 
sizonje.......kweli mambo bado,usichanganyikiwe,kama mwaka jana ulisema sherehe ni matumizi mabaya ya fedha,mwaka huu umetumia fedha kufanya sherehe hizohizo
 
Tatizo lenu mpo kama watoto walioachishwa ziwa kunyonya huwa wanalia usiku kucha wakiona wanaonewa na ni haki yao kunyonya siku zote kumbe hawajui kuna hatua zinazofuatia mbeleni pengine zitakuwa nzuri au mbaya huo ni mfano tatizo sio Magufuli tatizo ni mfumo na maisha tuliozoeya kuishi ya wizi, ulaghai ,rushwa, dhuluma na mengine yafananayo nayo, sasa Rais anajitahidi kurudisha katika misingi na mfumo uliobora wa kuyafikia malengo watu mnaona taabu ,

Hii nchi jama hata angelishuka malaika kwa hali iliyokuwa imefikia hangeweza kuiongoza humu kila mtu msemaji kila mtu mjuaji cheusi kita takatishwa kuwa cheupe inabidi kujitoa ufahamu tu kuiongoza hii nchi watanzania hatubebeki ,

Mmesahau kuna mikataba ya miaka mia moja humu hembu tuwe na utu jama tumsaidie Rais kuendesha hili gurudumu la maendeleo tuache kulia lia Mungu hapendi namalizia kusema asiyefanya kazi na asile na mikono milegevu hujenga paa bovu.
We unatafuta ukapteni Mwenye timu ya sizonje huna lolote!
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Mpendwa Sizonje habari za siku.... natumaini u buheri wa afya kibaiolojia japokuwa kiroho u tofauti...

Rafiki yangu Sizonje nakumbuka enzi zile tukijadili mpira ulivyokua hodari kumlaumu kocha!! Kwamba kocha wa timu yetu hawezi... kocha mzembe na anafuga uvundo....

Kadiri tulipokutana kila baada ya sentensi tatu lazima umseme kocha kila siku ikawa hamkani si shwari!!

Sizonje utakumbuka kocha alikuvumilia sana japokuwa ulikua huwezi!! Mdomo na maneno mengi yalikubeba kwa mashabiki lakini wachezaji wenzio walikujua!! Ulikua bingwa wa kukariri tarakimu za mchezo bila ujuzi na weledi wa mchezo!! Hata kocha alipoonywa sana juu ya kiwango chako kibovu bado alikubeba ingawa ulimsogoa!!

Hayawi hayawi yakawa Sizonje!! Kauli zako zikalipa!! Kocha akastaafu na ukocha ukapewa wewe!! Kila mtu ndani ya timu akiduwaa mashabiki waliolewa kauli zako tamu ziso kifani walikubeba hatimaye ukawa kocha!!

Awali ulionesha uwezo wa kukonga mashabiki kwa sifa na vitimbi kemkem!! Siku zikasonga mashabiki wakaona timu inarejea nyuma kuliko ilikokuwa kwa kocha mzembe!!

Nakujua Sizonje!! Hupendi kukosolewa na wala hupendi kimya cha sifa!! Vigelegele vya mashabiki na vifijo vimekoma!! Mbinu zote za michezo ulizotumia zimebuma!! Timu inarudi nyuma kwa kasi na wachezaji wameshapoteza mori!! Kila ugusapo sasa hapagusiki!! Wachezaji wanaonesha ari machoni pako tu lakini uwanjani wamedorora!!

Sizonje usichanganyikiwe... mambo bado ndio kwanza safari inaanza!! Ishike ngao na kigao kuyahimili majira!!!

Kwa leo naishia hapa Sizonje nikija mjini ntakutembelea tule maboga ya enzi zetu.

-----------------------------------------------------------------
UPDATES:
----------------------------------------------- ---------------
Wakuu napenda kuwaarifu kuwa nimepata taarifa nyeti na rasmi kuwa kocha wetu mpendwa Sizonje ameusoma uzi huu na comments zenu zote. Shukrani kwa wote mliotoa ushauri kwa kocha wetu.
Sizonje, jukwaa kuu tu ndio linalipia kuangalia mechi, mashabiki wengine wote unawaingiza bure kuangalia mechi. Sasa pato la kuendeshea timu litapatikana vipi?
 
Kabisa Mkuu halafu hata vyeti vyake vilivyomuwezesha kupewa ukocha wengi wameanza kuvitilia mashaka na kudai hana sifa ya kuwa kocha hata kwenye timu za mchangani achilia mbali hii timu yetu pendwa.

Sizonje anaweza kuwa na akili ya kuku, yeye kusahau alichokisema ni ndani ya muda mfupi tu.
 
Mpendwa Sizonje habari za siku.... natumaini u buheri wa afya kibaiolojia japokuwa kiroho u tofauti...

Rafiki yangu Sizonje nakumbuka enzi zile tukijadili mpira ulivyokua hodari kumlaumu kocha!! Kwamba kocha wa timu yetu hawezi... kocha mzembe na anafuga uvundo....

Kadiri tulipokutana kila baada ya sentensi tatu lazima umseme kocha kila siku ikawa hamkani si shwari!!

Sizonje utakumbuka kocha alikuvumilia sana japokuwa ulikua huwezi!! Mdomo na maneno mengi yalikubeba kwa mashabiki lakini wachezaji wenzio walikujua!! Ulikua bingwa wa kukariri tarakimu za mchezo bila ujuzi na weledi wa mchezo!! Hata kocha alipoonywa sana juu ya kiwango chako kibovu bado alikubeba ingawa ulimsogoa!!

Hayawi hayawi yakawa Sizonje!! Kauli zako zikalipa!! Kocha akastaafu na ukocha ukapewa wewe!! Kila mtu ndani ya timu akiduwaa mashabiki waliolewa kauli zako tamu ziso kifani walikubeba hatimaye ukawa kocha!!

Awali ulionesha uwezo wa kukonga mashabiki kwa sifa na vitimbi kemkem!! Siku zikasonga mashabiki wakaona timu inarejea nyuma kuliko ilikokuwa kwa kocha mzembe!!

Nakujua Sizonje!! Hupendi kukosolewa na wala hupendi kimya cha sifa!! Vigelegele vya mashabiki na vifijo vimekoma!! Mbinu zote za michezo ulizotumia zimebuma!! Timu inarudi nyuma kwa kasi na wachezaji wameshapoteza mori!! Kila ugusapo sasa hapagusiki!! Wachezaji wanaonesha ari machoni pako tu lakini uwanjani wamedorora!!

Sizonje usichanganyikiwe... mambo bado ndio kwanza safari inaanza!! Ishike ngao na kigao kuyahimili majira!!!

Kwa leo naishia hapa Sizonje nikija mjini ntakutembelea tule maboga ya enzi zetu.

-----------------------------------------------------------------
UPDATES:
----------------------------------------------- ---------------
Wakuu napenda kuwaarifu kuwa nimepata taarifa nyeti na rasmi kuwa kocha wetu mpendwa Sizonje ameusoma uzi huu na comments zenu zote. Shukrani kwa wote mliotoa ushauri kwa kocha wetu.

Ninaomba msaada. Nini maana ya neno Sizonje?
 
Back
Top Bottom