Sizonje usichanganyikiwe, Mambo bado!!

Sizonje usichanganyikiwe, Mambo bado!!

Sizonjeeee...think tank wake eti ni Abdallah Bulembo!
 
Sizonje kampanga captain wa timu acheze dimba la katikati lakini cha kushangaza captain muda wote anacheza wing ya kushoto anajifanya 'winga teleza' muda wote anapiga chenga nyingi mashariki mwa uwanja na kusahau nafasi yake katikati ya uwanja ambako ndio ngome kuu ya mipango ya timu kushambulia.
 
Tatizo lake ni ubishi na kujifanya anajua kila kitu,yeye ni kuteua,kutengua,kuteua,kutengua kashachanganyikiwa na bado mpk atabaki mwenyewe apambane na hali yake,kashavuruga kila mtu.hakuna anaemjali wala kumsifia sasa
 
Naona nchi kurud nyuma kwa miaka 25,milo mitatu kwa cku hiz ni ndoto hapa tz.
 
Sizonje kubali wakwambie ukweli..!!!

Huku uwanjani wachezaji wanafanya mazoezi ya nguvu, ILA HAWAJALA!

Tia maji tia maji, huchelewi kuwakuta ni mizoga wanaliwa na ndege! NIKIJA DAR NTAKUNONG'ONEZA!!!
Sizonje kasema waambieni wachezaji watakula pindi wakifanya mazoezi yakamridhisha na mechi wakashinda
 
sizonje,naona wachezaji hawakabi wala kushambulia,mmoja yule kule kalala chali,mwingine yule kipa,hapigi mpira mbele,kakalia kupiga danadana tu,mwingine yule beki anaenda kubadili bukta,aliyonayo imechanika kwa nyuma,bora ulimwambia IGP asimamishe mpira kwanza,hawa ukawa wanashambulia sana,na nina hisi wana njumu za chuma,wachezaji wetu kila wakiwakaba wanaumia
 
Umea
Mpendwa Sizonje habari za siku.... natumaini u buheri wa afya kibaiolojia japokuwa kiroho u tofauti...

Rafiki yangu Sizonje nakumbuka enzi zile tukijadili mpira ulivyokua hodari kumlaumu kocha!! Kwamba kocha wa timu yetu hawezi... kocha mzembe na anafuga uvundo....

Kadiri tulipokutana kila baada ya sentensi tatu lazima umseme kocha kila siku ikawa hamkani si shwari!!

Sizonje utakumbuka kocha alikuvumilia sana japokuwa ulikua huwezi!! Mdomo na maneno mengi yalikubeba kwa mashabiki lakini wachezaji wenzio walikujua!! Ulikua bingwa wa kukariri tarakimu za mchezo bila ujuzi na weledi wa mchezo!! Hata kocha alipoonywa sana juu ya kiwango chako kibovu bado alikubeba ingawa ulimsogoa!!

Hayawi hayawi yakawa Sizonje!! Kauli zako zikalipa!! Kocha akastaafu na ukocha ukapewa wewe!! Kila mtu ndani ya timu akiduwaa mashabiki waliolewa kauli zako tamu ziso kifani walikubeba hatimaye ukawa kocha!!

Awali ulionesha uwezo wa kukonga mashabiki kwa sifa na vitimbi kemkem!! Siku zikasonga mashabiki wakaona timu inarejea nyuma kuliko ilikokuwa kwa kocha mzembe!!

Nakujua Sizonje!! Hupendi kukosolewa na wala hupendi kimya cha sifa!! Vigelegele vya mashabiki na vifijo vimekoma!! Mbinu zote za michezo ulizotumia zimebuma!! Timu inarudi nyuma kwa kasi na wachezaji wameshapoteza mori!! Kila ugusapo sasa hapagusiki!! Wachezaji wanaonesha ari machoni pako tu lakini uwanjani wamedorora!!

Sizonje usichanganyikiwe... mambo bado ndio kwanza safari inaanza!! Ishike ngao na kigao kuyahimili majira!!!

Kwa leo naishia hapa Sizonje nikija mjini ntakutembelea tule maboga ya enzi zetu.
umeandika vizuri sana...hongera
 
SIZONJE sijui anapeleka wapi timu.....

Alafu mbona Sizonje amepewa majina mengi this time?.......

Mala Juma Ponda Mali ,Mala Nyampala,Tembo, Sasa nasikia anaitwa Trump ......

Kuna ukweli juu ya majina ya Shizonje?.......

Na Pia Sizonje wanamwita MUngu wao
 
Sizonje natamani nikutane nawe mchana kweupeeeee kisha kwa sauti iliyojaa ujasiri bila hata lepe la hofu nikuambie ''UMEFULIA BABA IN JOTIZ VOICE'' 😉😛😛😛
 
Sema we mpigaji ndo huna hamu nae. Sisi huku ni mkombozi wetu wanyonge. 2020 lazima spate kula nyingi sana asilimia mia

Hii ni sababu ya kijinga kabisa ambayo hutolewa na mjinga na kushabikiwa na wajinga ,Uchumi ni kanuni sio mambo ya amri amri tu na kutumia nguvu nyingi ku-force yasio wezekana ktk nyanja hizo..

Hapa tuna jadili mpira ,tafadhali usitutoe ktk reli na Sizonje wetu..
 
Kocha mpya kaja na mifumo yake kocha wa timu yetu ambae mkataba wake uliisha kuna mapungufu tulikuwa tunayaona na kupiga kelele beki yule mbovu mara nyingine alisikia kilio chetu wapenzi na kufanya masahihisho mara nyingine tulilaumu timu inacheza vibaya kocha hasimami na kuwaelekeza wachezaji wake yeye kakaa tu benchi kama haoni tunashambuliwa vile.
Mpaka anaondoka kuna sehemu tuliona amefanikiwa kuleta vipaji vipya na kuzimudu nafasi japo si kwa asilimia 100 sasa kocha sizonje kaingia nae ana mfumo wake kafanya reshuffle kubwa tu na wale wachezaji wengine wametolewa penye timu na kusajiri wapya kwa kipindi alichokaa na timu na hasa timu yetu wenyewe tunaijua ilivyokuwa tumpe muda kocha mabadiliko yana changamoto zake ni kipindi cha mpito sio kama mashabiki tusiongee kabisa ila miluzi mingi humpoteza mbwa mara oooh kaharibu kabisa kumuingiza yule mara aaah yaani fulani kamuacha kama anaona wanamfaa penye mfumo wake awatumie sisi tunapenda kuona timu yetu inatandaza kandanda Safi na hata tuweze kushiriki mashindano ya kimataifa na kushinda.
 
siznjo ukada ni mbaya sana na mgonjwa wa kansa ya mkono usiokate vidole kata mkono mzima.
 
sizonje sifa zinaponza pia sizonje jaribu kubadili baadhi ya wapiga bendi wako wakuu lakin c hawa wengine.
 
Mmesahau kuna mikataba ya miaka mia moja humu hembu tuwe na utu jama tumsaidie Rais kuendesha hili gurudumu la maendeleo tuache kulia lia Mungu hapendi namalizia kusema asiyefanya kazi na asile na mikono milegevu hujenga paa bovu

Magufuli ana nia njema sana na chi hii na jitihada zake zinaonekana lakini tatizo alilonalo linalomrudisha nyuma ni kutotaka kusikiliza ushauri na kujifanya kuwa yeye ana majibu ya kila tatizo la nchi hii!! Mheshimiwa ni vyema ukasikiliza ushauri mzuri kutoka popote pale na ufanyie kazi; kazi uliyonayo ni ngumu na nzito lakini KUKUOMBEA TU hakutoshi sikiliza ushauri; A ONE MAN"S ARMY CAN NEVER WIN A WAR!!!
 
Magufuli ana nia njema sana na chi hii na jitihada zake zinaonekana lakini tatizo alilonalo linalomrudisha nyuma ni kutotaka kusikiliza ushauri na kujifanya kuwa yeye ana majibu ya kila tatizo la nchi hii!! Mheshimiwa ni vyema ukasikiliza ushauri mzuri kutoka popote pale na ufanyie kazi; kazi uliyonayo ni ngumu na nzito lakini KUKUOMBEA TU hakutoshi sikiliza ushauri; A ONE MAN"S ARMY CAN NEVER WIN A WAR!!!
Sizonje kashachanganyikiwa,yeye ni kuteua kutengua.kila aliemzunguka hamuamini,anaona yy ni mtakatifu sanaa.
 
Back
Top Bottom