DSN
JF-Expert Member
- Feb 2, 2011
- 2,837
- 1,686
Uzi uko pale pale hakuna cha matangazo ya NSSF au NIHF wala nini sasa macho kodo..kilichopo ngoja tujaribu kumnanga..hivi kweli na uwezo wote ule Kitaifa Nchi nzima walijua kuwa jamaa anajiweza na kipimo ni jinsi aliyoweza kusimamia mazoezi pale kocha alipo mkabidhi idala ya uwanja na miundo mbinu kuhakikisha mashabiki na wachezaji wanapata kila kinachostahiki kama running truck za uwanja na ambullance zikivuka madaraja na kufika kwenye kiwanja bila shida...na hata mashabiki wanasafiri kwa mabasi nchi nzima kwa sababu kocha alimwamini msaidizi kuwa anaweza..na kweli aliweza kujenga miundo mbinu ya viwanja.Mpendwa Sizonje habari za siku.... natumaini u buheri wa afya kibaiolojia japokuwa kiroho u tofauti...
Rafiki yangu Sizonje nakumbuka enzi zile tukijadili mpira ulivyokua hodari kumlaumu kocha!! Kwamba kocha wa timu yetu hawezi... kocha mzembe na anafuga uvundo....
Kadiri tulipokutana kila baada ya sentensi tatu lazima umseme kocha kila siku ikawa hamkani si shwari!!
Sizonje utakumbuka kocha alikuvumilia sana japokuwa ulikua huwezi!! Mdomo na maneno mengi yalikubeba kwa mashabiki lakini wachezaji wenzio walikujua!! Ulikua bingwa wa kukariri tarakimu za mchezo bila ujuzi na weledi wa mchezo!! Hata kocha alipoonywa sana juu ya kiwango chako kibovu bado alikubeba ingawa ulimsogoa!!
Hayawi hayawi yakawa Sizonje!! Kauli zako zikalipa!! Kocha akastaafu na ukocha ukapewa wewe!! Kila mtu ndani ya timu akiduwaa mashabiki waliolewa kauli zako tamu ziso kifani walikubeba hatimaye ukawa kocha!!
Awali ulionesha uwezo wa kukonga mashabiki kwa sifa na vitimbi kemkem!! Siku zikasonga mashabiki wakaona timu inarejea nyuma kuliko ilikokuwa kwa kocha mzembe!!
Nakujua Sizonje!! Hupendi kukosolewa na wala hupendi kimya cha sifa!! Vigelegele vya mashabiki na vifijo vimekoma!! Mbinu zote za michezo ulizotumia zimebuma!! Timu inarudi nyuma kwa kasi na wachezaji wameshapoteza mori!! Kila ugusapo sasa hapagusiki!! Wachezaji wanaonesha ari machoni pako tu lakini uwanjani wamedorora!!
Sizonje usichanganyikiwe... mambo bado ndio kwanza safari inaanza!! Ishike ngao na kigao kuyahimili majira!!!
Kwa leo naishia hapa Sizonje nikija mjini ntakutembelea tule maboga ya enzi zetu.
Sasa hili la mnangaji eti Sizonje akuweza toka awali, kwanini mnangaji nae alijua Szonje hawezi akaenda kuvaa vibwebwe mbele ya hadhara na matambala mwili mzima na kushabikia Kocha ampe ukocha Sizonje wakati yeye binafsi alijua kuwa kocha kasema alimbeba Sizonje yeye pia anashiriki vipi usichokiamini.
Na kweli mlikutana na Sizonje wakati kocha anampitisha na uongozi wa timu kwa mashabiki ...wewe ulijua Sizonje akija atakufaidisha kama Kocha mstaafu ulivyomfanyia akaamua kukuzawadia fursa. Sasa fursa ya cheki toka kweye mifuko ya vyanzo vya Team Kocha kasema hapana viende kuboroshea Timu ili Wachezaji na Wanachama na Wapenzi wa Timu wapate matokeo sahihi na si kuwa kichwaa cha mwendawazimu kila mmoja anajifunzia kunyolea kama alivyosema Mzee Mwinyi.
Ili la kusema alikua anakwambia inakuwaje Mazungumzo binafsi mlioyayafanya na kocha wa zamani na huyu kocha wa sasa ukadiriki kuyaweka hadharani kwanini hukuyaweka hadharani kipindi hicho..na si baada ya matarajio uliyoyatarajia MNANGAJI kushindwa sasa ukaamua kumnanga huku ukitumia fursa hiyo kujifurahisha kwa kukosa weredi wa kuhalalisha malalamiko yako.
Sizonje ana maalifa na anajua anachofanya na hata ilipomlazimu kocha kumkabidhi timu Sizonje utendaji wa Szionje ndio ulikuwa turufu namba moja...kwani pamoja na kuwa kocha mstaafu aliwahi kumpereka jikoni akawandaliwe na kupima chakula cha wachezaji na wapenzi wa timu wanaofika kula kwenye club bado Sizonje alionyesha umahiri kiasi kuwa wachezaji waliweza kujua vitu mbalimbali vilivyoko jikoni kiasi ikawapa hamasa kuanza kufuatilia ni aina gani ya chakula kinafika kwenye jiko lao na kuandaliwa kwa ajili yao ..ili wajue ni aina gani ya vyakula walivyo navyo na vina thamani gani kwa afya yao na maendeleo ya Team yao. Ni Sizonje aliyekua mstari wa mbele kusimama na kusema kile alichokiamii kwenye vikao vya clabu toka enzi hizo za kocha Mkubwa Mstaafu kabla ya alieondoka kumpisha Sizonje.
Muache Sizonje apige kazi ushapata mtaji fanya FURSA nyingine ...ikibidi hata Mataifa ya Nje waweza tembea nao kwenye fursa milango itafunguka ...lakini hii kulazimisha milango ya Club..itumike ovyo kutunisha mifuko ya wachache nooooo Mnangaji tafuta jingine la kumnanga Sizonje ...ametutoa kimaso maso sie wengine wenye mapenzi ya kuona keki ya TEAM YA TAIFa inaliwa na wengi na si viongozi wachache wa Klub