CCM imekuwa na tabia ya kuwatumia baadhi ya wanasiasa nyakati za mawimbi makali ya kisiasa na kisha kuwatupa.
Malecela miaka ya nyuma alikuwa na nguvu sana ya kisiasa. Kwa taarifa yenu tu ni kwamba mzee Mwinyi hakuwa chaguo la Nyerere la kurithi kiti cha urais baada ya yeye kung'atuka. Lkn ni nguvu ya Malecela iliyomfanya Mwinyi akawa rais na hatimaye Malecela kulamba uwaziri mkuu (nitawapa kisa kizima siku nyingine).
Malecela na Mwinyi hawakupendwa sana na Nyerere, hotuba zake (Nyerere) zilijaa vijembe kwa rais Mwinyi na Malecela. Ilienda hivyo mpk Malecela akaundiwa zengwe la OIC na kung'atuliwa uwaziri mkuu.
Malecela alitupwa pembezoni mwa ulingo wa siasa na huku akilalama kuwa amekuwa akitumika kama Tingatinga kuwachongea wengine barabara za kisiasa.
Mwingine ni mzee Mangula. Huyu alitupwa nje ya siasa mara tu baada ya Kikwete kuukwaa urais (kwann ? Nitawapa kisa kizima siku nyingine). Mzee wa watu akarudi kwao Iringa kulima nyanya. Mpk pale walipoona (muhula wa pili wa awamu ya 4) chama kinataka kuwafia mkononi ndipo mzee Mangula akaenda kubembelezwa na kurudishiwa nafasi yake chamani.
Kwahiyo Makonda anatumika tu ili kukivusha chama lkn baadaye yeye na sukuma gang wengine watatupwa kama toilet paper.