Siungi mkono Vipengele vya Mkataba wa DP lakini Rais Samia pekee ndiye mwenye Uwezo wa kutuvusha 2025-30

Huihui2

JF-Expert Member
Jan 5, 2012
5,277
8,004
Hata mimi nina threads kadhaa za kuuponda mkataba wa DP World na Tanzania kutokana na vipengere visivyo na manufaa kwa nchi yetu. Kimsingi kila mwananchi kwa sasa amekuwa bingwa wa mikataba na uwekezaji kutokana na maamuzi ya Rais Samia kufungua uhuru wa maoni ambao ulidhibitiwa na mtangulizi wake.

Aidha watu wanaongea kwa vile teknolojia ya mawasiliano imepanuka sana ukilinganisha na miaka ambayo akina Mkapa au Kikwette walipokuwa wanafanya maamuzi mbalimbali.

Maamuzi ya Rais Samia pamoja na mapungufu yake ni maamuzi ya kawaida tu kwa Marais waliopita au kwa Marais wengine wa Afrika. Ila yeye ameshambuliwa left, right, front and back kutokana na wakati, vilevile na haiba yake kama Rais Mwanamke, Muislamu na Mzanzibari.

Bado kwa mtazamo wangu huyu ndiye Rais aliyeituliza nchi iliiyokuwa imekumbwa na sintofahamu za kibabe na kidikteta zilizofanywa na mtangulizi wake. Nitampa kura yangu kwa uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 kwa kuwa yeye ndiye mwenye uwezo kuliko Watanzania wengine wenye visasi, jazba na taharuki.
 
Tusikae kimya sasa kusubiri miaka 10 ijayo Rais wetu aandike Kitabu cha kujutia kuingia mkataba huu mbovu wa Bandari, tumkosoe mapema ili akija kuandika kitabu hicho aseme nilishauriwa ila nilikataa Ushauri"-Baba Paroko wetu leo 27/08/2023
 
Unavuka Kwenda Wapi Wewe
Umesikia Ya Mbeya
Mapato Yanaibwa Tu Na Watendaji
 
Hujielewi, unakiri Samia ndie mwenye matatizo mpaka akatuletea vifungu vya hovyo kwenye ule mkataba wa bandari, kisha akaweka na saini yake, ajabu tena unasema ndie pekee mwenye uwezo wa kutuvusha mpaka 2030!

Hizi thread sioni kama huwa mnajiuliza vyema kabla hamjaandika na ku post hapa jukwaani, chenga tupu!.
 
Hujielewi, unakiri Samia ndie mwenye matatizo mpaka akatuletea vifungu vya hovyo kwenye ule mkataba wa bandari, kisha akaweka na saini yake, ajabu tena unasema ndie pekee mwenye uwezo wa kutuvusha mpaka 2030!

Hizi thread sioni kama huwa mnajiuliza vyema kabla hamjaandika na ku post hapa jukwaani, chenga tupu!.
Ukweli ndiyo huo, hakuna aliye mkamilifu ila mazuri ya Samia ni mengi kuliko hivyo vipengele. Lakini kwa vile wewe denooJ huwa unachefukwa likitajwanjina la Samia, hakuna namna tutakusaidia
 
Back
Top Bottom