TUJITEGEMEE
Platinum Member
- Nov 6, 2010
- 27,297
- 28,006
Maadili katika muktadha wa mazingira na tamaduni za kitanzania.Obama hana maadili!!? Ni lazima utetee kwa kulazimisha?
Maadili katika muktadha wa mazingira na tamaduni za kitanzania.Obama hana maadili!!? Ni lazima utetee kwa kulazimisha?
Kwa hiyo unataka kujilinganisha na Rais wa nchi?
Gharama za kukutunza unataka kuzilinganisha na gharama za kumtunza Rais?
Ok so ukiona mwana wa jiran anatukana mama yake na wewe utaenda kumtukana wako??
Inawezekana mwenzako ni utamaduni wao na wewe je?????
Ni wazi kwa post hii ya Lema hajapendezwa na kile kitendo tena kuchanga hadharani ndio kumeonesha kejeli zaidi na kuyaunga mkono matusi dhidi ya Rais...!
Hakika Lema kanitoa machozi kwa uzalendo alio onesha!
Lema amepingana nao wazi wazi wala hajajificha!
Ni Kweli, Lakini Busara Ya Kumkanya Na Kumsaidia Ni Bora Zaidi Kuliko Kumwacha Akaozee Jela Wakati Inawezekana Kumrekebisha Mtaani.
Je, Huyo Hakuwa Mmoja Kati Ya Vijana Walioitwa Wapumbavu Kisa Wanataka Mabadiliko?
Ahsante Lema. Kwa mara ya kwanza nakuunga mkono
kwa hiyo na hapa ni MarekaniRais wa Marekani anaitwa majina mengi mabaya kuliko hilo la bwege...
Sheria hizi lengo ni kuleta hofu kwa ujumla kwa watu
wasiwe free kumkosoa....
Great thinking Godbless"Ninafikiri ni vyema na muhimu tukaendelea kukosoana kwa njia mbali mbali, lakini kwa hakika kabisa siungi mkono rais kutukanwa kwa kejeli ambazo zina sura ya mizaha na sio mabadiliko, Rais kuitwa BWEGE ni kosa na utovu wa nidhamu.
Kosa hili halipaswi kutiwa moyo wala kuungwa mkono, lakini kumwambia Kijana huyu kuwa alikosea ni jambo muhimu zaidi na la busara"
Godbless Lema (Mp)
️Sasa nikikuita wewe bwege unaonaje? Halafu ndio mtu kwa chuki tu anamuita rais wa jamhuri bwege. Yaani Watanzania wengi waliyomchagua na wao ni mabwege. Kumchangia huyo kijana ni sawa na kuunga mkono alichokifanya.Mkuu Godbless J Lema Mbona wewe ulimuita waziri Mkuu Pinda MWONGO kama SHETANI? Bwege na shetani lipi kubwa?
Hata mimi siungi mkono, ila adhabu aliyopewa huyu kijana ni kubwa kuliko! Hatukuwa na namna zaidi ya kumuwezesha ili amalizane na tatizo hilo.
Hata hivyo hii sheria ya mtandao ni kandamizi mno halafu inakata upande mmoja.
Godbless Lema kwa hili kajitofautisha na wale wanaokwenda kwa mihemko na hasira ya kushindwa uchaguzi mkuu wa mwaka jana.Godbless J Lema kwa bandiko hili hujatutendea haki kabisa sisi wanamabadiliko!
"Ninafikiri ni vyema na muhimu tukaendelea kukosoana kwa njia mbali mbali, lakini kwa hakika kabisa siungi mkono rais kutukanwa kwa kejeli ambazo zina sura ya mizaha na sio mabadiliko, Rais kuitwa BWEGE ni kosa na utovu wa nidhamu.
Kosa hili halipaswi kutiwa moyo wala kuungwa mkono, lakini kumwambia Kijana huyu kuwa alikosea ni jambo muhimu zaidi na la busara"
Godbless Lema (Mp)
Mkuu, kama umemsoma vema Lema amewakemea na hao wanaomchangia. Soma vizuri utaelewa
Kama unaonavema, kutukana kwa madai raisi wa marekani anatukanwa hamia huko Tanzania Hatuna utamaduni huo
Haiyumkini utadai nawe uongozwe na ving'ora kama ilivyo kwa rais. Tuifunze kuheshimu mamlaka hata kama waliokabidhiwa hatuwapendi.Sawa, lakini hata mimi sidhani kabisa kama hilo kosa linaendana na adhabu aliyopewa huyo kijana.
Angeniita mimi 'bwege' unadhani hata angekamatwa?
Au hata ningeenda kumfungulia mashitaka unadhani angepewa hiyo adhabu aliyopewa?
Haiyumkini utadai nawe uongozwe na ving'ora kama ilivyo kwa rais. Tuifunze kuheshimu mamlaka hata kama waliokabidhiwa hatuwapendi.
Hivi kwa mfano kumuita Kingwendu kichaa na kumuita mh. rais kichaa, ipi ni habari ya magazeti ya udaku na ipi itaingia main stream?