Siungi mkono Rais kutukanwa!

Siungi mkono Rais kutukanwa!

Ni Kweli, Lakini Busara Ya Kumkanya Na Kumsaidia Ni Bora Zaidi Kuliko Kumwacha Akaozee Jela Wakati Inawezekana Kumrekebisha Mtaani.
Je, Huyo Hakuwa Mmoja Kati Ya Vijana Walioitwa Wapumbavu Kisa Wanataka Mabadiliko?
Asante asante kwa maneno yenye ukweli unaouma.
 
"Ninafikiri ni vyema na muhimu tukaendelea kukosoana kwa njia mbali mbali, lakini kwa hakika kabisa siungi mkono rais kutukanwa kwa kejeli ambazo zina sura ya mizaha na sio mabadiliko, Rais kuitwa BWEGE ni kosa na utovu wa nidhamu.

Kosa hili halipaswi kutiwa moyo wala kuungwa mkono, lakini kumwambia Kijana huyu kuwa alikosea ni jambo muhimu zaidi na la busara"

Godbless Lema (Mp)

Na je N/Spika kumuita Mbunge wenu wa upinzani BWEGE, ni sahihi?

Mbona hilo hulisemei boldly Kamanda?
 
Wakiitwa wao wanachukua hatua za kuwafunga walio warudishia. Ila wao wakitukana wananchi ni sawa!? Oooh malofa, wapuuzi, mabwege, vihiyo, nk.
Baba ukikosa heshima watoto watakuiga na usishangae.
Ushawahi kuona mtuhumiwa anakwenda kujishitaki? Mkuu josam kama uanona umetukanwa si unakwenda kushitaki. Au hata kushitaki ulizuiliwa? Hebu tuache katabia ka kulalamika bila kuchukua hatua stahiki kisheria. Mtu unahisi amekutukana unataka yeye aende akajishtaki?
 
Nadhani mawazo yako yanania njema. Tatizo ni pale ambapo vyombo vya kutoa usuluhishi/ maamuzi havina Uhuru usiotiliwa shaka na jambo hilo lipo dhahili. Hakuna kimbilio.
 
Sasa mwenye haki ya kutukana ni nani mkuu?kwahiyo kuna watu maalumu wa kutukanwa na wengine si ruhusa kutukanwa?
tatizo hauelewi we ndo kilaza .....yaaaan unatAKA RAIS ATUKANWE WE PUNGA KWELI
 
Kuitwa bwege faini milioni 7 kuiba hela za walalahoi na kukwepa kodi faini ni kurudisha ulichoiba! nchi ngumu kweli hii.
 
Hii post ya lema ilijificha wapi? Ndio naiona leo...
 
Kwani bwege maana yake ni nini wakuu, hata mimi siungi mkono matusi, na kwa humu JF ukitukana huchelewi kupata ban

Elimu haina mwisho-kupitia tukio hili naamini neno hilo na yafana nayo yatapata tafsiri sahihi kwenye Kamusi ya kiswahili/kisheria.


Maana ya neno"bwege"kwa mujibu wa kamusi ya kiswahili sanifu ...
www.jamiiforums.com › ... › Jukwaa la Lugha
Translate this page
Apr 16, 2016 - Ingia kwny kamusi ya kiswahili angalia maana ya neno bwege utaona tafsiri yake ni. . . . "mtu asiye na akili sawa sawa, hafundishiki, ********"

Kote mia kuwa na mdomo hakuhalalishi kutumia maneno yasiyo na staha dhidi ya mtu yoyote! Lakini adhabu iliyotolewa nayo imekaa kiupendeleo/kikandamizi! Ndiyo maana mfumo wetu wa Mahakama hautapata hadhi stahili ya lengo halisi ya haki na kurekenbisha jamii,kijana yule angeweza pata adhabu mbadala kama ya akina Mramba na Yona na jamii safi ikapata nafasi ya kumhukumu kinafsi.
 
"Ninafikiri ni vyema na muhimu tukaendelea kukosoana kwa njia mbali mbali, lakini kwa hakika kabisa siungi mkono rais kutukanwa kwa kejeli ambazo zina sura ya mizaha na sio mabadiliko, Rais kuitwa BWEGE ni kosa na utovu wa nidhamu.

Kosa hili halipaswi kutiwa moyo wala kuungwa mkono, lakini kumwambia Kijana huyu kuwa alikosea ni jambo muhimu zaidi na la busara"

Godbless Lema (Mp)

Unajua mie mara nyingine napata wakati mgumu kutofautisha kati ya sifa au tusi. Hivyo naomba kuuliza; tukianza na hili lililopo; bwege maana yake nini? Je ni sifa anayepewa mtu kutokana na jambo fulani au tusi?

Maana ya neno"bwege"kwa mujibu wa kamusi ya kiswahili sanifu ...
www.jamiiforums.com › ... › Jukwaa la Lugha
Translate this page
Apr 16, 2016 - Ingia kwny kamusi ya kiswahili angalia maana ya neno bwege utaona tafsiri yake ni. . . . "mtu asiye na akili sawa sawa, hafundishiki, ********"


Okay, hapo nimeelewa. Hivyo bwege inafanywa kuwa tusi kwa mintarafu ya mtu asiye na akili sawasawa, na hivyo unapaswa kumwita mtu bwege ikiwa tu utathibitisha kuwa hana akili sawasawa. Hivyo kumbwambia mtu acha ubwege wako ni kumtusi kimsingi.

Sasa je, katika visa vitakavyofanana na hilo;

Kwa mfano, mtu akiwa mvivu, nikamwita mvivu, nimemtukana au nimeelezea sifa yake?

Na akiwa mchapa kazi, nikamwita mvivu, inakuwa tusi?

Na je, ikiwa mtu ana sura nzuri sana, nikamwambia una sura mbaya sana - anapaswa kukasirika?

Na vipi akiwa na sura mbaya nikamwambia ana sura nzuri sana?

Na pia vipi akiwa na sura mbaya sana, nikamwambia una sura mbaya sana - anaweza kunishitaki mahakamani?
 
Sio rais tu kutukanwa,mtu yeyote kutukanwa,tunatakiwa tukosoane kwa kuheshimiana kama watanzania,adhabu aliopata jamaa ni sahihi kabisa.
 
Nahonyo, uko sahihi kabisa kabisa ! 100%. Argument yangu ni kuwa ushoga ni personal issue. Ni uhuru wa mtu - hakuna haki ya jamii iliyovunjwa. Mila ni mambo yanayobadilika as long as huvunji haki ya mtu au jamii! Ni kama tendo la ndoa, haliruhusiwi hadharani lakini watu wanafanya vyumbani. Sitetei ushoga, ila natetea haki ya mtu kuwa huru bila kuvunja haki binafsi ya wengine au jamii! Mwanangu akifanya ushoga nitamfukuza kwangu na kumtolea radhi, lakini uhuru wake afanyie huko sio kwangu na sitamuingilia kwake!
Kama una uumini uhuru wa mtu, iweje mwanao ameamua kuwa shoga, umtolee radhi,wakati hajakukosea wewe, huku ukijua kumtolea radhi ni kumuadhibu.
 
Bwege si tusi. Ni neno lenye maana katika lugha ya Kiswahili.

Angeukizwa kwa nininkasema rais bwege ajitetee.

Kwangu mimi Magufuli ni bwege.

Kwa sababu hajui kachagukiwa kufanya nini.

Kachagukiwa kutetea utawala wa sheria halafu anawaambia polisi waibe matairi ya magari na kudanganya kwamba hawajaiba kama vike magari yanaweza kuja kituoni bula matairi.

Rais anayetoa kauli hii ni bwege.
Kama bwege si tusi ,basi wewe ni bwege
 
Kama una uumini uhuru wa mtu, iweje mwanao ameamua kuwa shoga, umtolee radhi,wakati hajakukosea wewe, huku ukijua kumtolea radhi ni kumuadhibu.
Radhi ni mli yangu lakini uhuru wake sio wangu! Sijaingilia uhuru wake katu!
 
Ni Mara ngapi JK alitukanwa mpaka kwa njia ya picha? Mbona hukutia neno?
Au akina Lowassa,mgombea wa chama chako ametukanwa Mara ngapi? Au yeye anastahili matusi ya kuji.NY.ea KWA kuwa sio rais? Sasa bwana mkubwa,kila enzi na kitabu chake.
Acha akina Pepsin tuendelee kutukanwa KWA kuwa sisi sio marais!
Nimekusoma kwa uzuri mkuu, kwanza Nchi hii kwa sasa haina system yeyote. Kwanza nchi ikombolewe kwanza, ndipo heshima iwepo!
 
Marekani ya leo siyo ya kujifananisha nayo hasa linapokuja suala la maadili! Hatuwezi kukubali Rais wetu atukanwe kisa Obama amatukanwa. Rais wetu anatofauti kubwa na rais Obama kimsimamo na kimaadili lazima tukubaliane na hili. Lazima TUJITEGEMEE katika maamuzi yetu ya kujiongoza.

Obama hana maadili!!? Ni lazima utetee kwa kulazimisha?
 
Kama unaonavema, kutukana kwa madai raisi wa marekani anatukanwa hamia huko Tanzania Hatuna utamaduni huo

Hata huko Marekani hakuna utamaduni wa mkuu wa nchi kuita watu lile neno la UDOM.

Mimi nachoona, jamii yetu imepotoka. Tunaishi kwa kutafuta sifa, kuanzia juu mpaka chini. Siku moja kwenye taarifa ya habari nilimsikia mkuu wa mkoa wa Mwanza akitoa maagizo kwa lugha isiyo na staha 'sasa mimi leo naagiza...sasa kama kuna kidume zaidi yangu...' Mimi sikuona haja ya kujitanabahisha kwa kauli za 'ukidume' ikiwa si mihemko.

Katika haya yote, tumuombe Mungu. Hata hawa wakubwa wanatutukana. Mwingine aliita watu wapumbavu tena kwenye kadamnasi
 
Siyo rais wa Marekani tu.

Hata wa Kenya tu hapo.

Achilia mbali akina David Cameron, Jacob Zuma, Francois Hollande na wengineo huko kwenye demokrasia kutushinda sisi.

Ok so ukiona mwana wa jiran anatukana mama yake na wewe utaenda kumtukana wako??

Inawezekana mwenzako ni utamaduni wao na wewe je?????
 
Back
Top Bottom