Siungi mkono Rais kutukanwa!

Siungi mkono Rais kutukanwa!

Hoja yako ni nini sasa hapo?
Kuna matukio ambayo moja kwa moja yanadhalilisha mamlaka, si mtu. Ukinisukuma nyenyere mie si habari kwani tutazozana yakaisha. Lakini ukamsukumu waziri mkuu, umeisukuma mamlaka iliyo ndani yake. Sidhani kama mwisho wake utakuwa mwema. Fact of life!
 
Ninakubaliana na wewe kwamba haipendezi kumtukana siyo rais Bali mtu yeyote yule. Cha kushangaza ni kwamba wapo watu wazima na waliowahi kushika Maharaja mkubwa sana hapa njini waliwahi kusikika live wakiporomosha matusi mazito hadharani; lakini hamkukemea. Nafikiri ni vyema kutokuwa na ubaguzi kwenye kukemea maovu bcz we r all God's creatures regardless of our political and civic status or positions
 
Kwani aliyesemwa " bwege" ndiye huyohuyo aliyeitwa" dictator uchwara"?
Msaada tafadhali
 
Heshima iwe kwa wote sio kwa viongozi wa serikali tu. Viongozi wetu waache kutumia madaraka yao vibaya. Hizo hela za kushuhulika na vikesi hivi vya kipuuzi wafanyie mambo ya kuleta faida kwa wananchi. Kiongozi bora anatakiwa kuwa jasiri na mwenye busara kiakili sio kimwili tu.
 
Huyo kijana na mzee Mkapa wote sawa, maana mzee naye alimwaga matusi pale Jangwani
 
"Ninafikiri ni vyema na muhimu tukaendelea kukosoana kwa njia mbali mbali, lakini kwa hakika kabisa siungi mkono rais kutukanwa kwa kejeli ambazo zina sura ya mizaha na sio mabadiliko, Rais kuitwa BWEGE ni kosa na utovu wa nidhamu.

Kosa hili halipaswi kutiwa moyo wala kuungwa mkono, lakini kumwambia Kijana huyu kuwa alikosea ni jambo muhimu zaidi na la busara"

Godbless Lema (Mp)
Kamanda lema ni wewe, fake ID au hackers wamedukua account yako???
 
Kwani bwege maana yake ni nini wakuu, hata mimi siungi mkono matusi, na kwa humu JF ukitukana huchelewi kupata ban
Bwege maana yake ni MTU mzembe/mwenye malinji linji anayeambiwa kila neno na kulikubali yaani kama kisonoko vile
 
Sawa, lakini hata mimi sidhani kabisa kama hilo kosa linaendana na adhabu aliyopewa huyo kijana.

Angeniita mimi 'bwege' unadhani hata angekamatwa?

Au hata ningeenda kumfungulia mashitaka unadhani angepewa hiyo adhabu aliyopewa?
Ila Rais ni mkubwa aisee sio sawa na normal person.
 
Aliyewaita wapinzani wapumbavu na malofa kachukuliwa hatua gani?
 
Ndio maana Mnyika alidiriki kumuita dhaif. Sasa huyu ni strong, mnalialia nini?
Tehetehe! Even I am strongman. Maneno huwa hayaishi, hata huyu akiondoka utasikia aheri JPM
 
Nawaza kwa sauti enzi za Gadafi mlibya angemuita gadafi bwege sijui nini kingetokea, au Iddi Amin
 
Back
Top Bottom