Siungi mkono mgomo wa madaktari...

Siungi mkono mgomo wa madaktari...

kama KCM C siyo ya serikali kwanini inatengewa fedha za ruzuku? tumia akili wewe usikurupuke
 
MAZINGIRA MAZURI ILI WAPELEKE DAWA KUUZA PRIVATE HOSPITAL NA KUFUNGUA HOSPTAL MPYA NA MADUKA YAO YA DAWA; KUMUONA SHILING 10000, DAWA UNANUNUA KWENYE DUKA LAKE. ANAPEWA COMMISSION REGENCY/HINDU MANDARI AKUPELEKE INDIA WKT ANAJUA UTAKUFA ILI APATE 10% NA KUKUONGEZEA GHARAMA BURE AKIJUA MAKUSUDI UTAPONA ; HII WAANZISHE FANI YA MEDICAL BUSSINESS ADMN au MSYRGICAL WITH ACCOUNTANCY; WAPO KIBIASHARA ZAIDI

mkuu kama hospitali za serikali au za umma zingelikuwa zinatoa huduma bora kungelikuwa hakuna hospitali za private kama zilivyo sasa hivyo ndo madaktari wanadai huduma ziboreshwe ili waweze kutoa huduma bora na zenye kiwango ili kutibu watanzania wengi ambao hawana uwezo wa kwenda kwenye hospitali za binafsi
 
ni kweli wengi wanachuki na serikali na kugoma kwa madaktari wanaona ni kuishikisha adabu hiyo serikali,lakini si kweli wanaoshikishwa adabu ni sisi walalahoi.si vema kushabikia ujinga huu watu wanakufa na kupata maumivu wewe unaona sawa.

hivi unajua kuwa akinamama 100 wanakufa kila siku pale ocean road kwasababu ya kuugua kansa ya tumbo la uzazi eti machine ya mionzi imeharibika kwa miezi 7 na serikali yako dhaifu, na chama chako cha kipuuzi wewe mnasema serikali haina fedha tuvumiliane? Huku vasco da gama akivoyage kwenda kuuchapa usingizi!!!!! Shame on you all ccm.
 
Sacrifice! generation ipi ya ku-sacrifice! Hii inayofikiria kuandamana, kwenda China na kucheza pool!
Sacrifice! wapi bwn. kila kijana anayemaliza chuo anafikiria "wage employment" hakuna mjsiriamali mwenye guts za kujiajiri na ku-own business. Generation hii ni siasa tu. Kama makinda ya ndege-wanaamka asubuhi wanauliza, wewe nchi yangu utatufanyia nini na sio wajiulize wataifanyia nini.
 
Ndugu yangu mpendwa Zemarcopolo, pole sana kwa hali hii inayokusibu. Mimi siungi na wala sipingi mgomo huu. Siungi kwa sababu majeruhi ni wagonjwa ambao ni ndugu,jamaa zangu na hata mimi mwenyenyewe kwa maana ugonjwa haupi hodi. Sipingi kwa sababu majeruhi wa kwanza kaitka sakata la mgomo huu wa madaktari ni UKWELI. Serikali haisemi ukweli, watanzania hawasemi ukweli na hakika tumekuwa wabinafsi mno kutojua kilio cha madaktari na watumishi wengine wa Tanzania.

Madaktari na walimu huwa wanasikilizwa labda kuliko watumishi wengine wote wa nchi hii. Sababu kubwa ni wingi wao na umuhimu wa dhahiri wa kazi zao. Watumishi wengine wengi na hata wanasiasa( sijasema wote) wamekuwa wa kihongwa/kupokea rushwa kwa kisingizio cha ugumu wa maisha. Kwa kisingizio hicho wamejilimbikizia utajiri wa kutisha kiasi kwamba hoja ya ugumu wa maisha inakosa mashiko.

Watu ambao ukwasi wao ni mkubwa hawakutani na madaktari wetu katika hospitali za serikali, hii inatoa picha kuwa madaktari wapokea rushwa wamekuwa wakipokea rushwa ya kukidhi ugumu wa maisha kwa maana halisi. Ninaongelea madaktari wanaowaona na kuwatibu wagonjwa na sio madaktari watawala wa Wizara ya afya, mashirika ya kimataifa( WHO,WB,Global Fund, TACAIDS, Benjamini Mkapa foundation, Bill Clinton foundation nk.). Rushwa ya kujikumu inayotolewa na walala hoi wa nchi hii ni kero kubwa kwa maana inawagusa watu masikini sana na walio wengi. Ndio maana inapigiwa kelele sana.

Anayesema madaktari hawafanyi kazi aende kwenye hospital za umma asubuhi aone umma unaokuwa pale ndipo atakapojua mgogoro unao wasibu madaktari wa hospitali za serikali. Asipo jipa ruhusa ya kunywa chai atashinda njaa. Na hakuna mfumo wa kumtetea. Chai hiyo anayokwenda kunywa sio chai itokanyo na mfumo ni chai inayochangiwa na mke/mme na watoto kwa maana atapunguza stahili ya familia kwa ajili ya chai, ambayo ni muhimu sana kwake ili aendelee kutoa huduma!

Ukienda BoT, Wizara ya Fedha, NHIF, LAPF, TRA, Tume ya mawasiliano,PSPF,PPF,NSSF na mashirika mengine ambayo nayo ni ya Kitanzania ukaona chai, vitafunio, soda, maziwa vivyoshushwa kutoka kwenye magari kwa ajili ya watenda kazi wa ofisi hizo, ukienda majumbani kwao ukaona nyumba bora za kifahari wanazoishi watumishi hawa, ukaona usafiri wanao utumia na ambao unamilikiwa na wao, ndipo utakapo ona kuwa utume/wito wa kazi za madaktari na walimu wetu ni dhihaka isio kuwa na mfano.

Katika mazingira kama haya kwa nini wasigome na kugomea sifa hizi bandi wanazopewa leo? Haki iko wapi?
 
Mimi siyo daktari. I am a mere simple teacher who makes doctors and other professionals. Mimi ni mwalimu wa kawaida sana. Ninafundisha watu wote. Nafundisha watoto wa madaktari kwa upendo bila kinyongo japokuwa nimefanya kazi miaka 20 na mshahara wangu haujafikia laki 500,000/-. Sasa naelekea , kwenye uzee. Serikali yetu hii inasema sisi ni maasikini, haina uwezo wa kuwalipa walimu wote, eti ni wengi kiasi cha fedha wanazotaka kulipwa. Walimu ni watumwa wa serikali.

Leo tunajadili mgomo wa madakatari na athari za mgomo huu kwamba ni vifo vya watanzania wengi. Ni kweli, wapo wanaosema kuwa ni sacrifice, sawa. Ni vyema kuwatetea madaktari wapewe hicho wanachokitaka toka serikalini. Je, sisi wengine ambao bila sisi, hao madaktari watatoka wapi?

Mimi mkulima, mkulima masikini ninayetumia jembe la mkono, leo nimeugua nakutatana a mgomo wa daktari, ila daktari huyu anataka nimuuzie mchicha na maharage niliyolima shambani kwangu. Daktari anataka milioni 4 kama mashahara, akija sokoni kwangu, analazimisha kunipa sh.600/= kwa kilo, sawa na maskini mkulima mwenzangu. NI NANI WA KUNITETEA MIYE?

Ni mara ngapi madaktari huwakuti kwenye vyumba vya kutibia (ofisi zao?). Wakipewa hicho wanachokidai, tabia yao itabadilika na watachapa kazi kwa kuwajibika? Ninachelea kusema kuwa HAPANA, wataenda kwenye starehe zaidi badala ya kuchapa kazi.

HITIMISHO. Kama mwalimu ambaye anafanya kazi katika mazingira magumu, na mkulima anayepinda mgngo ili kuwalisha watu wote bila ubaguzi wataendeleal kunyanyaswa na system hii,halafu tu madkatari wapewe wanachotaka, nachelea kuwa nchi hii hapo mbele haitatawalika!

sipingi madaktari kudai haki yao, waidai with a highest degree of abstraction. Hawa ni wasomi, na sisi tunavivunia kuwwa nao, kwa nini watutese watu wa professions zingine? Mwalimu akiamua kugoma kweli kweli will create a mental genocide, na watakaokufa kialkili na pamoja na watoto wao madaktari. nk.
Mkulima akigoma, wote tutakufa njaa. We must think as much for solutions of our problems kuliko ku create matatizo makubwa kama haya.
 
taifa hli linawajinga wengi sana. Wewe ni mjinga namba moja.
Ni kweli wewe mwelevu jenga nchi!!!!, Niache mjinga nife kifo cha mende!. ila mwisho wa siku na akili yakoitakuja kuelewa ila najua hutokuja kukili.
 
kama ilivyo kawaida humu jamvini idadi kubwa ya wachangiaji siku zote hawapendi mada yoyote ambayo wanadhani inasaidia kuitetea serikali lakini masauala ya ukweli lazima yaanikwe hadharani,katika madai kumi na mawili ya madaktari ni dai la kumi na moja pekee ndilo linaloeleza uboreshaji wa huduma za afya lakini mengine yote ni ubinafsi wa madaktari.


katika utekelezaji wa uboreshaji huo mimi katika hospitali ya wilayani kwangu serikali imejenga chumba cha upasuaji cha kisasa chenye vifaa vingi hivyo nakubaliana na kwamba kumekuwepo na jitihada za kuboresha huduma-roma haikujengwa siku moja.


dk ulimboka kasafirishwa kwenda afrika ya kusini kwa ndege ya kukodi achilia mbali gharama za matibabu hapo siyo michango tu kupitia katika sms lazima kuna nguvu iliyojificha nyuma ya pazia-serikali haziondolewi kwa mtindo huo.


Hivi madaktari na kitabu chote walichopiga wanakubali kurubuniwa n dk ulimboka ambaye si mfanyakazi mwenzao bali ni mtu wa ngo's wanaokula deal la kuhakikisha nchi inaingia machafukoni nao wakiona mambo mabaya wakodi ndege na kukimbia nchi


nimesoma makala haya na yamenikuna ingawa dada yangu happy kwa makala haya nategemea utashambuliwa sana lakini hawa watu kama mheshimiwa Godbless Lema ni wa kuwaambia tukiendelea kuwaita makamanda tutakuwa tunawatia ujinga:

· TUMECHOSHWA NA UKATILI WA MADAKTARI

Na Happiness Katabazi


JANUARI 30 mwaka huu, gazeti hili lilichapisha makala niliyokuwa nimeiandika mimi iliyokuwa na kichwa cha habari kisemacho ‘Ni mgomo wa madaktari kweli au?

Walivyogoma mara ya pili ulioanza Machi 7 mwaka huu, niliandika makala ndefu iliyokuwa na kichwa cha habari kisemacho ‘Madaktari waungwana hawasifiwi ushenzi'.Haikuchapishwa na gazeti hili kwasababu ambazo sitazitaja adharani ila niliisambaza kwenye mitandao ya kijamii.

Na ndani ya makala hizo mengi niliyokuwa nimeyabashiri ndiyo sasa yameanza kujitokeza na tunayashudia.Lakini leo tena naandika makala ya tatu kuhusu mgomo huu wa tatu ulioanza wiki iliyopita naninasisitiza tena mgomo huo ni batili na umedharau amri ya Mahakama Kuu Disheni ya Kazi, ambayo wiki iliyopita ilitoa amri ya kutangaza mgomo huo kuwa ni haramu lakini cha kushangaza madaktari wetu ambao ni wasomi ndiyo wamekuwa mstari wa mbele kukaidi amri hiyo halali ya mahakama na mhimili wa serikali kisheria ndiyo unatakiwa uhakikishe amri hiyo na nyingine za mahakama zinatekelezwa kwa vitendo na sivinginevyo umeshindwa kusaidia utekelezaji wa amri hiyo kwa kuwakamata madaktari hao waliokaidi amri ya mahakama na kuwafikisha mahakamani ili wajibu mashitaka ya ni kwanini wamekaidi amri ya mahakama.

Matokeo ya kushindwa kutekeleza amri hiyo ya mahakama ndiyo sasa kunasababisha maskini wenzetu ambao ni wagonjwa wanashindwa kutibiwa na wengine kudaiwa kupoteza maisha kwasababu ya madaktari hao ambao kwa makusudi wameamua kukaidi amri ya mahakama na serikali inaendelea kuwachekea.

Ibara ya 13 (1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania ya mwaka 1977 inasema " Watu wote ni sawa mbele ya sheria,na wanayo haki ,bila ya ubaguzi wowote,kulindwa na kupata haki sawa mbele ya sheria' .

Sasa kwa Ibara hiyo ya Katiba inaanza kuonekana sasa baadhi ya madaktari waliogoma wapo juu ya sheria kwani wanakataa kutekeleza amri ya mahakama na serikali inawaacha watu hao waendelee kudharau amri hiyo wakati siku zote inafahamika kuwa nchi yetu inaongozwa na misingi ya sheria.

Lakini ni serikali hii kupitia jeshi la polisi ndiyo imekuwa ikiakikisha amri mbalimbali zinazotolewa na mahakama zinatekelezwa kikamilifu lakini cha kushangaza serikali hii inashindwa kuwafikisha mahakamani madaktari hao wanaoikaidi amri hiyo jambo ambalo hivi sasa limeanza kutafsiriwa kuwa kada ya madaktari wapo juu ya sheria.

Nikiachana na hilo nivigeukie vyombo vyetu vya habari kuhusu ushiriki wao katika mgomo huu wa madaktari,kwa namna moja au nyingine vyombo vingi vya habari vimekuwa vikitoa nafasi kubwa kwa madaktari wanaogoma na kuinyima serikali na jamii inayopinga mgomo huo kusikika kupitia vyombo vya habari na baadhi ya wanahabari wakiwa ndani na nje ya vyombo vya habari wamekuwa wakisikika wakikerwa na tabia hiyo ya madaktari ila wanaogopa kuandika makala na habari za kuwakosoa madaktari kwasababu ya kuhofia eti siku wakiugua na kwenda hospitalini huko wanaweza kujikuta wakichomwa sindano za sumu na madaktari hao.

Hali iliyosababisha wananchi wengi katika mgomo wa kwanza na wa pili kuona madaktari wapo sahii na mgomo huu wa tatu kadri siku zinavyozidi kusonga mbele wananchi na baadhi waandishi wa chache wameanza kutowaunga mkono hadi kufikia kuwapachika majina mabaya madaktari hao kuwa wana roho za kikatili zaidi ya wa kikundi cha ‘Boko Haram' .

Hii ni changamoto kwa sisi vyombo vya habari tujitazame upya na tuifanyie kazi.
Hakuna ubishi kwamba madaktari wanadai maslahi yao na serikali katika mgomo wa pili uliyatimiza baadhi ya madai na ukaidi kuendelea kuyafanyia kazi madai yaliyosalia na hakuna ubishi kwamba wanafanyakazi katika mazingira magumu na pia nao wagonjwa nao wakati mwingine hawapatiwi tiba za uhakika kutoka kwa madaktari.

Lakini cha kushangaza madaktari hawa wameonekana ni watu walafi na wabinafsi wanaotaka masulufi manono wapewe wao tu na kada nyingine zisipate,wameonekana kukosa subira,hawana imani na serikali yao ambayo ndiyo mwajiri wao na ndiyo anayewalipa mishahara na wengine walisomeshwa na serikali hiyo.

Kwa mtindo huu ni wazi kabisa hawa wanaonekana hawana dhamila ya dhati ya kuitumikia serikali kwa moyo wa uzalendo kwani wamedhiirisha wazi kuwa muhimu kwao ni fedha kuliko kuokoa maisha na kutibia wagonjwa ambao ndiyo hasa wanasababisha wao wapate mshahara,wasome.Hivi bila wagonjwa nyie madaktari mngekuwa na hiyo ajira ya udaktari?

Ni madaktari hawa hawa akiwemo huyo Dk.Steven Ulimboka wamekuwa wakiutangazia umma kuwa pale hospitali ya Muhimbili hakuna dawa wala vifaa, sasa mbona tumeshuhudia yeye Ulimboka ambaye amepigwa na watu wasiyojulikana akifikishwa hospitalini hapo na kulakiwa madaktari wenzake wakaanza kumtibia na jinsi gani walivyomakatili wakagoma kuwatibia wananchi wenzetu siku hiyo wakamkimbilia kumtibu Ulimboka kwa dawa na vifaa ambavyo vimenunuliwa kwa kodi zetu.

Ni madaktari hawa hawa wanaojigamba kuwa wao ni madaktari bingwa sasa mbona wameshindwa kumtibia mwenzao hadi wamempeleka nje ya nchi akatibiwe?
Tumesikia madaktari hawa ambao kila kukicha wanadai mishahara wanayolipwa ni midogo na mazingira ya kazi ni mabovu, tuwaulize hayo mamilioni waliyochanga ghafla ya kumsafirisha mwenzao wameyapata wapi? Kama wanauzalendo kweli wa hili ni kwanini hizo fedha walizozichangisha wangezitumia kununulia vifaa na kuviweka pale Muhimbili ili vije kumtibia mwenzao na watanzania wengine?

Imeelezwa kuwa safari ya Ulimboka kwenda nje imegubikwa na usiri mkubwa,hivi kama siyo upuuzi ni kitu gani?Mnaficha nini na mnamficha nani kwamba Ulimboka ameendakutibiwa nchi gani?

Hivi leo hii mtu anaweza kwenda nje ya nchi bila kukata tiketi ya ndege,visa ambazo zitaonyesha anakwenda nchi gani? Kama mnaisi serikali ndiyo imemfanyia unyama ule na mkaamua kumuondoa kwa siri pale Muhimbili, hivi kwa akili zenu mnafikiri huko mlikopo mpeleka kutibiwa ndiyon serikali ya Tanzania haipo?
Na kama mnafahamu serikali ndiyo imemtendea unyama huo pelekeni ushahidi mahakamani au pelekeni ombi mahakamani na kutaka muendeshe kesi binafsi(Private Prosecution).

Hivi kama sio uhuni na ukatili tunafanyiwa na hawa baadhi ya madaktari wa serikali ambao mishahara yao inatokana na kodi zetu nini na wakati huu wanagoma bado wanaendelea kupewa mishahara?

Na mbaya zaidi wananchi wanashindwa kuwachachamalia hawa madaktari lakini ingetokea vyama vya siasa vimeitisha maandano ya kupinga mfumuko wa bei,malipo ya Dowans ni sisi wananchi tungejitokeza kuundamana tena hata kama hayo maandamano ni haramu lakini hili la madaktari kuendesha mgomo haramu ambao wananchi wenzetu wanaumia na kupoteza maisha wala hatuonekani kabisa kulichukulia uzito wa aina yake.Sisi ni watu wa ajabu sana.Tumekuwa na kasumba ya kushabia mambo yasiyo na msingi ila mambo ya msingi ambayo yanatuhusu moja kwa moja hatuyatilii maanani.

Rai yangu kwa madaktari wanaogoma, kama wanaona serikali haiwalipi vizuri siwaache hiyo kazi wakatafute kazi sehemu nyingine ambapo watalipwa mishahara minono?Kwanini muundelee kumng'ang'ania bwana(serikali) ambayo kwa akili zenu mnaona haiwajali na haiwapendi?

Tanzania bado ina ardhi kubwa ambayo imegunduliwa kuwa ina madini, simuende basi kwenye ardhi hizo mkachimbe madini ili muwe na mahela mengi kama mnavyotaka kuliko kung'ang'ania kazi serikali ambayo nyie mnadai hamlipwi vizuri?Kwani mmekatazwa.

Maana ninachokiona mimi hivi sasa hawa wanaogoma ni watu ambao kwa akili zao timamu wameamua kukiuka viapo vyao, wameichoka kazi ya kuwatibu wa gonjwa kwa kisingizio cha kudai maslahi manono,daktari mwenzao Ulimboka kafanyiwa ukatili.Sasa kama kafanyiwa ukatili na watu wasiyojulikana ni kwanini sasa mgomee amri ya mahakama,agizo la serikali la kuwataka mrejee kazini na mgome kuwatibu wagonjwa?Kwani ndiyo waliomfanyia ukatili huo?

Mkae mkijua hizo roho za wananchi wenzetu zinazopotea kwaajili ya mgomo wenu ipo siku mtadaiwa na mungu na mathara yake mtayapata hapa hapa duniani kwani mungu amewapa vipawa mje mvitumie duniani kwaajili ya kuwahudumia watu wake,sasa nyie mnapingana na agizo la mungu na maadili ya taaluma yenu, minaamini ipo siku mungu atawaadhibu na msije kulia na mtu.

Mwisho ni malizie kwa kuwataka wanaharakati na wale vyama vya siasa akiwemo Kada ya Chadema, Godbles Lema ambao wametoa matamko ya kulaani kitendo alichofanyiwa Ulimboka na Lema akasema akifa Ulimboka atalala barabarani, nawataka wageuze upande wa pili wa shilingi na waone kuwa kuna mamia ya wagonjwa wanakosa huduma na kupoteza maisha yao kwaajili ya mgomo huo haramu,mbona makundi hayo hatusikii yakitoa tamko ya kuwasema wananchi hao na kulaani mgomo huo haramu wa kisheria ambao mahakama ilisema mgomo huo ni batili?.

Wewe Lema unayesema utalala barabarani Ulimboka akifa, tumuulize huyu Lema ni kwanini alishindwa kulala barabarani siku ile Jaji Gabriel Rwakibalila wa Mahakama Kuu Kanda ua Arusha alipotoa hukumu dhidi yake ambapo alimvua ubunge na kumfungia kugombea ubunge baada ya kumtia hatiani kwa makosa ya kutoa lugha chafu?

Maana hukumu hiyo ndiyo imemfanya Lema hivi sasa awe kaka sisi tusiowabunge kwani analifuatilia bunge kupitia redio na televisheni, hapati tena posho na mshahara na hapewi heshima na stahili za kibunge tena,sasa tumuulize sasa alishindwa kulala barabarani kwa hukumu hiyo iliyokuwa ikumuhusu na imemwathiri yeye binafsi ndiyo leo hii atakuwa na ujasiri wa kufanya hivyo kwa Ulimboka ambaye hawana hata undugu?

Nimalizie kwa kuwataadhalisha madaktari wetu kuwa huo mgomo haramu wanaoufanya ipo siku watakuja kutokea baadhi ya ndugu wa wagonjwa watakaofika mahospitalini hapo halafu mkatae kuwapa huduma watajiuliza maswali yafuatayo;

Hivi hospitali hizo ni za serikali?Dawa na vifaa vya mahospitalini humo sizimenunuliwa kwa kodi za wananchi?Madaktari siwamesomeshwa kwa kodi za wananchi?

Wakimaliza kujiuliza maswali hayo watamalizia kwa kuwadhuru na wala msije kulia na mtu kwani sikila mtu anaweza kuvumilia huo uhuni na ukatili mnaotufanyia.

Mungu ibariki Tanzania,Mungu Ibariki Afrika


0716 774494
www.katabazihappy.blogspot.com


Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumanne, Julai 3 mwaka 2012.
 
Katabazi ameandika kwa hisia sana. Ufisadi unaua watu wengi sana kuliko migomo ya ma dr. Kwakuwa vifo vya vyenye kusababishwa na ufisadi viko indirect wengi hawalioni hilo.
 
We dada yangu mdogo Katabazi

Hivi kuna mgomo Halali mahali popote duniani???? Tihi! Tihi! Tihi!


Halafu hili la lema kufungiwa kugombea ubunge ni jipya kwangu. Inaoneka wewe mwenzetu uliisoma hukumu original toka Ikulu.
Ile hukumu ya jaji pale Arusha sikusikia ikitamka kumfungia Lema kugombea Ubunge.
 
Nadhani umempenda lema ila hutaki kusema direct.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
ukitaka kuona kwamba alichoandika huyu m2 hakina mantik na ni hisia kutokana na kuathirika na mgomo SOMA PARAGRAPH ZAKE KUTOKA CHINI KWENDA JUU
 
Yaani wewe dada unashabikia watu kutekwa, kuteswa, na kutishiwa maisha yao! halafu unatishia eti vurugu zikitokea watapanda ndege na kukimbia! Hii inanikumbusha bastola ya ismail aden rage jukwaani igunga.

Nimeamini CCM ndiyo itaanzisha vurugu nchi hii baada ya kukataliwa na wananchi kwani kama wasemavyo akina nape "ccm itatawala nchi hii milele"

We dada sisi ndio tumekiajiri CCM kuiendesha serikali kwa manufaa yetu, kama wameshindwa kuwalipa madaktari mishahara ili wafanye kazi kwa tija, lakini wanazo hela za kuongeza mishahara ya wabunge, kununua magari mapya ya kifahari kwa bei MBAYA, kutenga fedha nyingi kwenye matumizi ya kawaida kwa ajili ya posho, vitafunio maofisini, ukarabati wa ikulu n.k

Ni dhahiri kuwa hamjui waajiri wenu wanataka nini. No point of return, CCM haijui, na haijijui kwamba kwa sasa haijitambui. Achilia mbali kutekwa ingekuwa mwanaasha ameibiwa mdoli (toy) tu ungeona utendaji wa jeshi la polisi uliotukuka.
 
hongera happy kwa makala yenye mantiki

endelea kuandika mambo kwa kuangalia upande wa pili siyo kufuata mkumbo! umeeleza ukweli. tatizo ni kwamba watu wengi hawataki kusikia ukweli huu
 
Happiness Happiness... hivi aliekwambia Lema alienda bungeni ili kuchukua posho na marupurupu nani?

Yani unataka kutuaminisha kwamba wabunge wote wanaenda bungeni kwa sababu ya posho na marupurupu? acheni hizo bana, halafu sio kwamba ndugu wa madakatari hawafi.. wanakufa sana! hata bila mgomo wanakufa sana tu kutokana na miundombinu na vitendeakazi hafifu katika sekta ya afya. Tusiandike upuuzi ili kupotosha uma kwa sababu ya shibe ya muda mfupi

Tumia taaluma yako kwa mabadiliko endelevu sekta ya afya na sio propaganda za muda mfupi ambazo hazitusaidii
 
Jitahidi dada Katabazi....utaukwaa uDC soon! Ongeza ongeza mbwe mbwe tu kuipamba serikali, JK keshapata CV yako hivi ninapoandika hivi!
 
Nadhani umempenda lema ila hutaki kusema direct.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums

DSC01138.JPG
Katabazi.jpg
_DSC0102.JPG
 
Monday, January 30, 2012

Happiness Katabazi:Ni Mgomo Wa Madaktari Au?



kkk.JPG
Mwandishi Wa Makala Happiness Katabazi
---
KWA takribani wiki moja sasa vyombo vya habari vimekuwa vikipambwa na habari za mvutano baina ya serikali na madaktari kuwa wamegoma kufanyakazi kwa kile wanachodai kupandishiwa mishahara, kujengewa nyumba za kuishi na kuongezewa masurufi yao.

Taarifa za mvutano huo binafsi zimekuwa zikinikosesha raha na kunikera mno na kuanza kutamani kuwa na viongozi madikteta.

Nao baadhi ya madaktari walinukuliwa wakisema wameishapita kiwango cha kuongea na waziri wa afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Juma Mponda kwani ameshindwa utatua mwenye uwezo wa kuongea nae hivi sasa ni Waziri Mkuu Mizengo Pinda na kushinikiza Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Brandina Nyoni, hii ni dharau ya aina yake.

Wakati madaktari hao wakitoa maneno hayo, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk.Mponda, Alhamisi ya wiki iliyopita aliifanya mkutano na waandishi wa habari na kutoa tamko la serikali na ufafanuzi kuhusu madai ya madaktari hao na bila kumung'unya maneno alisema serikali haiwezi kuwaongezea mishahara na kufikia shilingi milioni 3.5 kwa kuwa kada hiyo inalipwa vizuri.

Dk.Mponda alisema mishara ya watumishi wa serikali hufuata miundombinu ya watumishi iliyopo ambayo iliboreshwa kwa sekta ya afya na hivi sasa watumishi wa afya wanapata mishahara mikubwa kuliko watumishi wengine serikalini.

Ieleweke kwamba baadhi ya madai ya madaktari ni ya msingi na tayari serikali imesema inayafanyia kazi.

Ila sikubaliani na hatua ya madaktari hao kukiuka viapo vyao walivyoapa kuwa wataakikisha wanahudumia wagonjwa katika mazingira yoyote yale lakikini hivi sasa wameamua kuwatoroka wagonjwa nakwenda kufanya migomo na kufanya deiwaka katika mahospitali binafsi ili waweze kujiongezea kipato.

Na kitendo hicho hakina tofauti na jambazi ambaye anamwelekezea bunduki kichwani mwananchi akimtaka ampatie fedha ama sivyo anamuua au akina tofauti na daktari ambaye anamtibu mgonjwa halafu anamwambia hawezi kukupatia dawa hadi unipatie hongo..

Kwanza nakubaliana na maelezo ya Waziri Mponda kuwa suala la kupandishiwa mishahara na masurufi mingine kwa watumishi wa umma kuna utaratibu wake.Wafanyakazi wa serikali wanaodai kuongezewa mishahara na masurufi mengine wanapaswa kufuata utaratibu mahususi ulianishwa ndani ya Civil Service Negotiation Machinery Act, na kama serikali itashindwa kutekeleza madai yao yaliyofuata utaratibu wa sheria sheria hiyo wanaruhusiwa kugoma.

Sasa tuwaulize hawa madaktari walifuata utaratibu ulioanishwa katika sheria hiyo hadi wafikie uamuzi wa kugoma ?

Na kama hawakufuata utaratibu sheria za nchi zipo wazi ambazo zinawabana wale wote wanaofanyakazi au kutoa ushahidi chini ya kiapo na pindi wanapokiuka viapo vyao wanatakiwa waadhibiwe mara moja.

Maana ni wenyewe walieleza kuwa madai yao waliyafikisha wizarani na waziri Mponda akasema aliupokea ujumbe wa chama cha madaktari na wakajadiliana na serikali ikaueleza ujumbue huo kuwa baadhi ya madai yao serikali inayafanyia kazi.

Na baada ya Dk. Mponda kutoa ufafanuzi huo,hatujakisikia chama hicho cha madaktari kikipinga maelezo ya waziri huyo kwa kutoa ushahidi mbadala matokeo yake tunakisikia chama hicho kikisema kuwa hadhi hayo kwa sasa si ya kuongea na waziri huyo ,hadhi yao hivi sasa ni yakuzungumza na waziri mkuu.

Haya Pinda waliokuwa wakimtaka alikwenda Karimjee kuzungumza na madaktari hao lakini madaktari hao walishindwa kutokea kwa sababu za kijinga ambazo sasa zimetulazimu tuanze kuwamini huu siyo mgomo wa madaktari bali unaajenda mbaya nyuma yake.

Hivi nani kairoga nchi hii?Madaktari ndiyo wenye shida na waziri Mponda ndiyo waziri wao lakini cha kushangaza madaktari hao ambao ndiyo wenye shida wamegeuka kuwa manyapara wa kutoa amri ya wanataka nini na nani wazungemze na nani na cha ajabu hadi sasa serikali inaendelea kuwakumbatia?

Nyie madaktari kwa akili zenu waziri alichokizungumza mnafikiri kabla ya kukizungumza huyo waziri mkuu Pinda alikuwa akijui? Waziri wenu kasema serikali inayafanyiakazi madai yenu hamsikii sasa mnataka nini?

Tuulize ule ujumbe wa madaktari uliokiwenda kuzungumza na Dk.Mponda kuhusu madai yao na akawasikiliza, walikuwa hawajui waziri huyo siyo saizi yao na kwamba hana huwezo wa kuwatatulia kero zao?Mlimfuatia nini ?

Ni lini wamegundua waziri Mponda siyo saizi yao? Je ni baada ya waziri huyo kuwaambia ukweli kuwa haitaweza kuwapandishia mshahara?

Na wewe Pinda aibu uliyoipata jana ulijitakia kwani haiwezekani wewe ndiyo Waziri Mkuu Mawaziri wote wapo chini yako na wanakusaidia katika utendaji kazi wako wa kila siku, madaktari hao wanamtolea maneno ya shombo waziri wa Afya Dk.Mponda na maofisa wake ambao ndiyo wenye dhamana ya sekta hiyo, halafu na wewe unakubaliana na upuuzi na dharau hiyo ya madaktari kwa waziri wako , unakwenda kuwaona , na matokeo yake na wewe wamekudhalilisha umejikuta ukumbini peke yako.

Nchi hii hivi sasa si ngazi ya familia wala nje ya familia, hatuheshimiani tunadharauliana bila sababu za msingi. Hajulikani baba ni nani, mama ni nani, mkubwa ni nani,mtoto ni nani na kiongozi ni nani kila mtu anaongea na kufanya analotaka.Na hali hii isipotokomezwa ipo siku taifa hili litajikuta limetumbukia mtoni.

Kwa akili yenu nyie madaktari mliogoma, hivi hayo madai mnayodai ya kupandishwa mshahara ndiyo mtapandi leo leo? Je hizo nyumba mnazodai mjengewe ndiyo ujenzi wake utakuwa umekamilika ndani ya siku mbili?

Lakini wafanyakazi wengine kwa uhalisia wa fani zao walioajiriwa serikali hawawezi kufanyakazi kazi serikali na sekta binafsi kwa wakati mmoja lakini wafanyakazi wa aina hiyo hatujawasikia wakigoma.

Sasa kama hivyo ndivyo ni kwanini madaktari mnaofanyakazi sehemu mbili na mwisho wa mwezi mnapata mishahara miwili.Mbona kule kwenye hospitali za sekta binafsi mnapofanyiakazi hamuwagomeagi mnakuja kuigomea serikali?

Na kama mnaona serikali iliyowaajiri haiwalipi vizuri si mtafute sehemu nyingine ambako mtalipwa vizuri kuliko kung'ang'ania kufanyakazi sehemu ambayo hulipwi vizuri ambapo mwishoe mtakuja kuwaua makusudi wagonjwa kwa kuwachoma sindano za mikojo ili wafe?

Na kama siyo ubinafsi na unafki ni nini, kipindi hicho mmeongezewa mishara na masulufi hatukuwasikia mkijitokeza adharani kutangaza mmeongezewa mishahara?
Watanzania wanaheshimu haki za binadamu sote tuamke tuupinge mgomo huo kwani mgomo huo ni haramu na umeanza kuleta madhara makubwa kwa wananchi wetu ambao hawana uwezo wa kwenda kutibiwa hospitali binafsi na nje ya nchi.

Ieleweke wazi kuwa ni kweli gharama za maisha zimepanda na ukali huo wa maisha unatuhumiza wote lakini hicho kisiwe kigezo cha madaktari wetu kutoroka wagonjwa mahospitali na kwenda kufanya migomo huku wananchi wasiyo na hatia wakipoteza maisha kwa kukosa huduma.

Minaamini kuwa kila mtu awe na elimu na asiye na elimu ana umuhimu hapa duniani na wote tunategemeana hivyo ni vyema na haki madaktari wakaacha na kingizio kuwa taaluma yao ni muhimu kuliko taaluma zingine.

Mwisho nimalizie kwa kuishauri serikali ijenge utaratibu wa kuyashughulikia mapema malalamiko ya kada yoyote inayoyalalamikia kabla ya kada hizo kuanza kujichukulia sheria mkononi na kugoma kwani mwisho wa siku wanaothirika ni wananchi na taifa linajikuta likipata sifa mbaya kuwa taifa la Tanzania hivi sasa limekuwa ni taifa la migomo.


0716 774494

 
Back
Top Bottom