Wakuu JF.
Waweza kuwa mwepesi kushabikia mgomo wa madaktari kwa sababu kuu zifuatazo:
- Unaichukia serikali iliyoko madarakani, hivyo unashabikia mgomo wa madaktari kwa kuwa unahisi wanaishikisha adabu serikali hiyo.
- U mzima wa afya, wewe pamoja na familia yako yote hivyo kwa muda huu, huhitaji huduma yoyote kutoka kwa madaktari hawa wanaogoma.
- Una pesa za kutosha kwamba hata ukiumwa leo hii, unao uwezo wa kwenda kutibiwa Aga Khan, AAR, Regency etc bila bughudha wala shida yoyote.
Napenda niwakumbushe watanzania wenzangu kwamba maisha magumu kwa nchi hii hayapo kwa madaktari tu, nina uhakika yapo makundi ambayo yanamaisha magumu zaidi ya madaktari, wapo walimu, wapo polisi, wapo wakulima ambao ndio wengi zaidi ya wengine, na kubwa zaidi
watanzania ambao hawana ajira/kazi maalum ni kundi kubwa zaidi ya makundi yote niliyotaja, na ndio wenye maisha magumu zaidi kuliko wengineo licha ya kwamba katika kundi hili pia wamo wasomi ambao wamemaliza kwenye vyuo vikuu lakini hawana hata uhakika wa mlo mmoja au pesa ya ku print CV.
Tuachane na ushabiki,
roho ya mtu akishakufa hairudi hata kama hayo madai ya Madaktari yatatekelezwa, wananchi tusikubali wanasiasa watuingize kwenye siasa zao kwa kutumia mgomo wa madaktari, by the way I hate CCM kwa sababu ndio iliyotufikisha hapa tulipo kwa kushindwa ku plan vyema jinsi ya kulilea taifa la Tanzania na Watanzania, but kwa hili la Madaktari kugoma siungi mkono hata asilimia 1, hao akina
Mzee Mwanakijiji et al wanaounga mkono madaktari kugoma yatupasa tutambue kwamba hawaishi Tanzania na hawajui shida wanazokutana watanzania wa kawaida kwa mgomo huu wa madaktari.
Nahitimisha kwa kulaani wote waliohusika kujaribu kumuua Dr. Ulimboka.
Na pia kama viongozi wetu wangekuwa na hekima za kutosha, wasingeruhusu kauli kama
LIWALO NA LIWE kutoka vinywani mwaol.
God Bless Tanzania, God bless Tanzanians.