Siungi mkono mgomo wa madaktari... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Siungi mkono mgomo wa madaktari...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by ZeMarcopolo, Jan 28, 2012.

 1. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #1
  Jan 28, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,589
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Nimejaribu kukaa kimya lakini nafsi yangu inanisuta. Siwezi kuendelea kukaa kimya. My opinion is unpopular, lakini nitasema.

  Nitagusa hoja moja baada ya nyingine kama zilivyotolewa na "jumuiya ya madaktari".

  Kuongezwa mshahara: Jumuiya imetoa tarakimu zisizo sahihi kuwa mshahara wa daktari ni sh. laki 7. Hii imeandikwa katika ripoti waliyoipeleka kwa waziri mkuu. Hii inadhihirisha kuwa jumuiya hii haiko serious katika hili swala. Lakini tuangalie uhalisia - jumuiya inataka mshahara uongezwe toka hiyo laki 7 (ambayo si sahihi) mpaka miil. 3.5 with immediate effect. Hivi kweli is it reasonable kudai ongezeko la asilimia 500 la mshahara na uongezwe mara moja la sivyo unagoma? Katika historia, swala hili madaktari hawajafanya jitihada za kujadiliana na serikali kidiplomasia. Ulipotokea mgogoro wa interns wa muhimbili kuhamishwa vituo, basi madaktari wakaibuka na kutaka mshahara wa 3.5 mil na kugoma. Mambo hayafanyiki hivi! Tukiwaambia madaktari waonyeshe barua waliyokwishawahi kuiandikia serikalli kuomba mshahara huo, hakuna atakayetoa barua au ushahidi wowote kwa sababu madaktari wameanza na mgomo moja kwa moja. Siungi mkono mgomo wa namna hii.

  Madaktari kupewa nyumba: Mara nyingi adui wa daktari huwa daktari mwenzake. Hili swala la nyumba lilishajadiliwa huko nyuma. Nini kilitokea? Baada ya madaktari wa muhimbili kuthibitishiwwa kuwa wao watalipwa sh laki 4 kila mwezi basi chama cha madaktari ambacho viongozi wake wengi ni madaktari wa muhimbili wakapoteza interest ya kubargain na serikali ili posho hiyo wapate madaktari wa nchi nzima. Chama hicho kilikataa kabisa mara kadhaa kuitisha vikao vya kujadili posho za nyumba huku wakitoa sababu za kuepusha migomo. Sasa hivi inakuja "jumuiya ya madaktari" na kuilazimisha serikali kutoa posho hizo with immediate effect. Siku zote madaktari walikuwa wapi? Je walikuwa wanangoja interns wafukuzwe muhimbili ndio wakumbuke kuwa wanahitaji nyumba? Standing orders za mwaka 1994 zinaeleza kinaga ubaga kuwa daktari anastahili kupewa nyumba, standing orders za mwaka 2009 hazimtaji daktari katika watumishi wanaostahili kupewa nyumba. Maafisa utumishi wote wanatafsiri kuwa standing orders za mwaka 2009 zimemtoa daktari kwenye kundi la watakaopewa nyumba. Ni lini madaktari walienda kujadili hili na wizara ya utumishi? je ni sahihi kuanza na mgomo? Ili madaktari warudishiwe stahili hiyo ni LAZIMA kifungu kwenye standing orders za mwaka 2009 kifanyiwe marekebisho. Je, hilo linaweza kufanyika with immediate effect? Madaktari wamekuwa wavivu kufuatilia mambo yanayowahusu na siwezi kuunga mkono mgomo wa kundi la wavivu wa kubargain na kulobby.

  Call allowance: "Jumuiya ya madaktari" inataka call allowance ilipwe kwa half per diem. This is very simple! Kwa nini mnagoma kwenda kazini during working hours? Ni kweli kuwa daktari anastahili kulipwa angalau sh. elfu 40 kwa call lakini solution yake ni rahisi kuliko zote. Madaktari waingie kazini, muda wa kazi ukiisha madaktari warudi nyumbani kama watumishi wengine. Wasikae call mpaka watakapokubaliwa kulipwa kiasi hicho. Kugoma kwenda kazini asubuhi kwa sababu ya malipo madogo ya zamu ya usiku doesn't make sense. lakini again, jitihada gani zimefanyika awali kuhakikisha call inaongezwa? Can doctors provide evidence of their effeorts? HAKUNA.

  Mazingira duni ya kazi: Swala la mazingira duni ya kazi ikiwemo wagonjwa kulala chini sio la kulalamikiwa na madaktari. Hili swala waachieni wananchi wenyewe. Daktari unachotakiwa kujua ni capacity ya hospitali yako, beyond that usipokee mgonjwa. Ukishampokea basi unalea ubovu. MV Bukoba, MV spice zilizama kwa sababu ya kubebeshwa mzigo mkubwa kuliko uwezo wake. MV Muhimbili nayo inaingia kwenye hili kundi. Nani alaumiwe? Nahodha lazima awe miongoni mwa watu wa kulaumiwa. Kama madaktarri wataendelea kupekea wagonjwa wengi kuliko idadi ya vitanda it is obvious kuwa wengine watalala chini. hata Ulaya wangekubali kupokea wagonjwa wengi kulikoi uwezo kungekuwa na wagonjwa wanaolala chini. Ila Ulaya swala hilo halipo. Nafasi zikijaa zimejaa, mgonjwa apelekwe wapi, sio swala la daktari. Hata hiyo hospitali unayofanya kazi hujaijenga wewe daktari, ilijengwa kwa sababu mahitaji yalikuwepo. Ukiendelea kupokea wagonjwa wengi kuliko uwezo unaonyesha kuwa mahitaji sio urgent. Wagonjwa wakikosa pa kulazwa ndipo wananchi watashinikiza viongozi wao wawahakikshie facilities za kutosha.

  Interns kuhamishiwa hospitali nyingine: Sababu iliyotolewa kuwa hospitali nyingine hazina vifaa inakosa uzito kwa sababu kuna madaktari ambao wapo huko kwenye hizo hospitali nyingine wanafanya intern. Hata hivyo hili swala ni so benign, haliwezi kusababisha mgomo nchi nzima.

  Huduma huuzwa na kununuliwa. Bei ya huduma uamuliwa na nguvu za mahitaji na upatikanaji wa huduma. Hakuna daktari aliyelazimishwa kufanya kazi serikali. Kwanini madaktari wanakimbilia kufanya kazi serikalini? Madaktari wawe wakweli na watuambie faida zilizopo serikalini. kwanini madaktari wasitoe notice ya kuacha kazi serikali na kwenda kufanya kazi sehemu bora zaidi. Tanzania kuna soko huria. Kama watu walitumia mamilioni kwenda Loliondo basi hata daktari wanayeamini huduma zake watamfuata popote alipo. Madaktari mnangoja nini kutambua hili?

  Mwisho: Mgomo ni risasi ya mwisho. Si sahihi kwa wasomi kutatua changamoto wanazokutana nazo kwa kuanzia na mgomo. Tanzania ni nchi masikini, ili umasikini huo uondoke ni LAZIMA tushirikiane WOTE kuutoa. Ewe daktari, jiulize ni mara ngapi umeingia kazini kwa muda unaostahili na ukafanya kazi mpaka muda wa kazi kuisha? Je, tabia yako ya kila siku kazini inachangia kuondoa umasikini wa nchi yetu? Kila mtu aweke jibu lake moyoni na kujiuliza tena, je mgomo unaoendelea hivi sasa unapaswa kuungwa mkono? Je, kwa siku hizi mlizogoma mshahara mnauchukua wote bila aibu?

  Also: Am just curious, nani analipia gharama za kukodi ukumbi wa mikutano wa Starlight Hotel ambao madaktari wamekuwa wakikutania kwa siku kadhaa?!

  Mungu Ibariki Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
   
 2. arabianfalcon

  arabianfalcon JF-Expert Member

  #2
  Jan 28, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 2,292
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Kitanda usicho kilalia hujui kunguni wake wanaumaje.
   
 3. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #3
  Jan 28, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,011
  Likes Received: 1,816
  Trophy Points: 280
  Mgomo ni risasi ya mwisho mkuu. Hasa mgomo wenyewe ukiwa unahusu maisha ya binadamu na wala si mgomo wa kutengeneza soda. Risasi hiyo inaonekana kutumika vibaya dhidi ya wanyonge wasiokuwa hata na bakora. Naunga mkono kichwa cha habari
   
 4. k

  kuzou JF-Expert Member

  #4
  Jan 28, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 200
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  hawa jamaa hawajui wanachotaka hawaeleweki,wengine wanagoma wengine wanafanya kazi,hivi fabi yao kama ingekua kutibu ngombe wangegoma au kwa kua wanajua wameshika roho za watu,ni dhambi kwa mungu na si utu,walaaaniwe
   
 5. measkron

  measkron JF-Expert Member

  #5
  Jan 28, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 3,713
  Likes Received: 365
  Trophy Points: 180
  Asante mkuu, hata swala la kumeandikia mgonjwa dawa na hazipo inabidi anunue na Hana pesa hivyo hawezi kupona pia sio la madaktari? Huyu jamaa haelewi namwalika aje kazini kwangu ashinde siku nzima aone tunayokumbana nayo ndo arudi hapa kuandika
   
 6. measkron

  measkron JF-Expert Member

  #6
  Jan 28, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 3,713
  Likes Received: 365
  Trophy Points: 180
  Ilaaniwe serikali yako isiyotupatia vitendea kazi, nimepita Kilimanjaro hospitali ya mkoa haina chumba cha upasuaji tangu wafunge kilichokuwepo 27/12/2010 ni zaidi ya mwaka sasa wananchi wanateseka. KCMC is congested inabidi kuwalaza chini. Hapo nani alaaniwe? Mbona husemi rais wako apumguze miziruro tujenge theatre na kununua vifaa na kuwalipa wanaokesha 24 hours call posho
  Iongezeke toka 10,000?
   
 7. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #7
  Jan 28, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,589
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Swala la kumuandikia mgonjwa dawa akakosa pesa ya kununua liko dunia nzima, sio kwenye kituo chako cha kazi tu. Na kama umeelewa mafunzo yako shuleni hupaswi kuwa na sympathy, unapaswa kuwa na empathy. Ukigoma humsaidii huyo mgonjwa aliyekosa dawa, kwa sababu the fact is hakuna serikali duniani yenye uwezo wa kuwanunulia dawa wananchi wake wote. Hata hivyo, swala hilo ni la wananchi na viongozi wao.
   
 8. Dark City

  Dark City JF-Expert Member

  #8
  Jan 28, 2012
  Joined: Oct 18, 2008
  Messages: 16,277
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Hadi leo na umri wangu huu nashindwa kabisa kuwaelewa watanzania wenzangu...

  Ni jambo la kawaida kabisa kukuta mtu ambaye hajawahi kugusa shule analaani wanafunzi wa vyuo vikuuu kwa kugoma. Wakati wakigoma masaa 2, maji ambayo yalikatika kwa week nzima yanaanza kuflow kwenye mabomba.....Very pathetic in deed!

  Hivi kwa nini madaktari na watumishi wengine kama walimu ndio wafuate utaratibu mrefu kurekebishiwa maslahi yao wakati wanasiasa wanarekebishiwa ndani ya masaa?

  Marekebisho yawe kwa asilimia ngapi nalo ni issue...hivi kutoka 70K kwenda 200K ni asilimia ngani na ilichukua miaka mingapi kubadili sera?

  Mara ngapi order ya kupandisha mishahara ya madaktari wakati mgomo imetolewa na kutekelezwa ndani ya 24hrs???

  Bado nasikitika sana!!
   
 9. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #9
  Jan 28, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Unaunga mkono hali ya sasa ilivyo ambayo imefikisha mahali hapa; kuanzia 2006 kumekuwa na changamoto zile zile. Hoja ya umaskini haina mshiko kwa sababu kama ingekuwa kweli unaweza vipi kuelezea ongezeko la posho za wabunge katika nchi maskini?
   
 10. H

  Honolulu JF-Expert Member

  #10
  Jan 28, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 5,654
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Bado tunawasubiri na maaskari waunge azimio!!! Matatizo si kwa madaktari tu!! nanyi askari amkeni!! Tokeni usingizini!! Someni kwa haraka waraka huu KISHA muwaunge mkono madaktari!!!

  Waraka maalum kwa Askari wote


  MAKALA hii ilikuwa itoke Jumatano ya wiki iliyopita lakini kwa sababu za kiufundi ikashindikana. Imekuwa ni bahati nzuri kwamba inapotoka leo, ijibu swali la askari polisi dereva wa gari la maji ya kuwasha.

  Askari huyo alimweleza Mwalimu Mkuu wa watu jinsi roho inavyomuuma pale anapowamwagia Watanzania wenzake maji hayo ya kuwasha wakati wakidai haki yao. Askari uliyeuliza na wenzako wote someni makala hii kwa utulivu. Huu ni waraka maalumu kwa askari wote wa majeshi yote vikosi vyote Tanzania Bara na Visiwani.

  Kwa lugha ya wazi zaidi nazungumza na askari wa Jeshi la Polisi Tanzania, Askari wa Jeshi la Kujenga Taifa, askari wa Kikosi Maalumu cha Kuzuia Magendo (KMKM), askari wa Jeshi la Magereza na wale wa Jeshi la Wananchi (JWTZ).
  Kuwa mwanajeshi lolote kati ya hayo niliyoyataja si dhambi na si kweli kwamba kuwa mwanajeshi kunakuondolea uwezo wa kufikiri na badala yake ukawa unafikiriwa na watu wengine.

  Wala haimaanishi kuwa askari kuwa kama robot ndio nidhamu bora kuliko zote duniani. La hasha! Mimi nilikataa utumwa huo!

  Mwaka 1999 nilihitimu elimu ya cheti cha ufundi mchundo, yaani Full Technician Certificate (FTC) katika uhandisi wa Elektroniki na Mawasiliano ya Anga, yaani Electronics & Telecommunications Engineering kutoka Taasisi ya Teknolojia ya Dar es Salaam (DIT).

  Nikiwa bado sijapata kazi ya maana, mwezi Aprili mwaka 2000 niliona tangazo la kazi ya Radio Technician katika Jeshi la Magereza. Nikatuma maombi na kuitwa kwenye usaili uliofanyika Chuo cha Maofisa wa Jeshi la Magereza Ukonga, Dar es Salaam mwezi Juni 2000.

  Wote tuliofaulu usaili tulipangiwa siku ya kuripoti Chuo cha Magereza Kiwira kule Tukuyu, Mbeya.

  Kufika kule nilishuhudia mambo ya ajabu. Ingawa wao hufurahia na kusema eti wanakutoa uraiani na kuwa mwanajeshi lakini baadhi ya matendo yanayofanyika wakati wa mafunzo ya jeshi ni ya kuwapumbaza askari wetu ili baadaye wakiwa kazini, watawala wawatumie watakavyo.

  Nilishindwa kuvumilia kaulimbiu ya wakufunzi wa jeshi pale walipoelekeza kwamba chochote kruta (askari mpya mafunzoni) unachoambiwa lazima uitikie "ndiyo afande". Nilishindwa kuitikia kwa mfano pale mkufunzi mmoja mwenye cheo cha koplo alipotutamkia mfululizo wa sentensi zifuatazo:
  Mkufunzi: Nyinyi makruta mbona wote hamkuja na majembe?
  Makruta: Ndiyo afande!
  Mkufunzi: Hamkuambiwa makao makuu ya jeshi kwamba lazima mje na majembe?
  Makruta: Ndiyo afande!
  Mkufunzi: Kwa hiyo kwa kuwa hamkuambiwa na nyinyi hamkuyabeba?
  Makruta: Ndiyo afande!
  Mkufunzi: Wote ni wapumbavu pamoja na mama zenu waliowazaa.
  Makruta: Ndiyo afande!

  Ni hayo pamoja na mambo mengine ya kulazimishwa kwenda kwenye kile kinachoitwa disko, ambapo pamoja na uchovu wa kutwa nzima wa kazi ngumu na nyingi bado ni lazima ukae hapo mpaka saa 4 usiku tena ukinyooshewa kidole tu na mwenzako lazima usimame na kuimbisha wimbo tena kwa tabasamu, wimbo mmoja wapo ukisema "Magereza ninavyokupenda nitakunywa sumu juu yako", ndiyo yaliyonifanya nikakataa kazi ya jeshi baada ya wiki moja tu ya mafunzo.

  Siku niliyokataa jeshi ilikuwa ni Jumatano asubuhi ambapo sikwenda mchakamchaka na wakati wenzako wanatawanyika kufanya usafi wa nje maeneo mbalimbali, mimi nilibeba begi langu na kuanza kuondoka chuoni majira ya saa moja na nusu hivi asubuhi.

  Nilikamatwa na mkufunzi mmoja wa jeshi na kupelekwa pamoja na begi langu kwa Ofisa Mafunzo wa chuo. Aliponiuliza sababu nilimtajia mbili, kwanza kwamba sifurahii mambo ya jeshi na kubwa zaidi kwamba mimi ni Msabato na nimeambiwa na wenzangu kwamba hapa hakuna kwenda kusali, siku zote za juma ni kazi.

  Kitu ambacho sitaweza maana Sabato takatifu lazima nipumzike! Bila kuuliza zaidi aliconclude kwa kuniambia kwamba, "Sijawahi kuona mtu anaacha kazi kwa ajili ya mambo ya dini.

  "Ni dhahiri wewe ulikuja kutupeleleza na hivyo kazi yako imeisha sasa unataka kurudi. Tutakuweka rumande, tena ile ya polisi kwa wiki mbili wakati tunafanya upelelezi juu yako."

  Askari aliyenileta alianza kunivuta ili kunipeleka rumande lakini nilikataa huku nikiendelea kujieleza kwa ofisa mafunzo ili ajue kwamba sikuwa na mpango huo aliousema.

  Baada ya kuelemewa na hoja zangu alinipeleka kwa makamu mkuu wa chuo ambaye yeye alitumia zaidi Biblia kunihubiri kwamba nakaidi amri ya mamlaka wakati hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu.

  Jibu langu lilikuwa fupi na lenye msimamo mzito kwamba ikiwa mamlaka ya wanadamu inafika mahali inanena tofauti na Mungu, Mtume Petro ametuandikia kwamba katika hali ya namna hiyo, "Imetupasa kumtii Mungu kuliko mwanadamu".

  Na yeye alinishindwa akanipeleka kwa mkuu wa chuo na wao wote wakiwapo. Ushauri waliokuwa wakimpa mkuu wa chuo ni kwamba mimi niwekwe rumande kwanza ili wafanye upelelezi. Lakini sikuyumba katika msimamo wangu.

  Nilimweleza mkuu wa chuo kwamba mimi ni raia na si mpelelezi. Nilizirudia rudia sababu zangu za kuacha jeshi tena kwa ujasiri mkubwa na kumhakikishia mkuu wa chuo kwamba akinipa hayo ninayoyataka niko tayari kubaki jeshini.
  Hatimaye kauli ya mwisho ya mkuu wa chuo ilikuwa ni hii: "Jeshi ni wito. Tunaweza kumlazimisha huyu kijana kuwa mwanajeshi lakini baadaye ikatuletea madhara makubwa sana." Akamalizia kwa kusema, "chukueni maelezo yake kwa maandishi kisha arudishe vifaa vya jeshi."

  Wakati naondoka nilimsikia ofisa mafunzo akitoa maelekezo kwa walio chini yake kwamba mwanafunzi mwingine wa jeshi akija kuripoti na kwenye daftari akajaza kwamba ni Msabato, msimsajili kwanza mpaka aje kwangu! Sijui kama Wasabato wameendelea kupokewa kwenye hicho chuo cha magereza lakini ninachotaka askari wote wa majeshi yetu yote na vikosi vyote, ni kwamba askari unaweza kusimama kwa miguu yako na kufikiri kwa akili yako mwenyewe!
  Ndugu zangu askari, nchi imefika mahali ambapo Waingereza hupenda kupaita ‘critical point'. Ni mahali ambapo wananchi wako tayari kwa mabadiliko na watawala wako tayari kwa mapambano ili kubaki madarakani.

  Katika point hii askari wetu wanakuwa na nafasi kubwa ya aidha kuwezesha mabadiliko hayo kutokea kwa wakati wanaoutaka wananchi, tena kwa amani ama kuyachelewesha (si kuyazuia) na kusababisha yatokee baadaye kidogo kuliko wananchi walivyotaka, tena baada ya kumwaga damu nyingi ya Watanzania wasio na hatia!

  Napenda kurudia kwamba hakuna jeshi lolote duniani hata kama tungekusanya majeshi yote ya dunia hii na kuyaleta Tanzania hawataweza kuizuia nguvu ya umma pale inapokuwa imeamua kufanya mabadiliko.

  Napenda tena kurudia kwamba si lazima askari mfanye kile ambacho wakubwa wenu wanataka na kuwaamuru kufanya. Tunaweza kusimama imara na kutetea haki za Watanzania tukiwamo na sisi askari. Niliwahi kugoma kutii amri ya kukamatwa na kuwekwa rumande.
  Lakini pia mifano ni mingi na nisingependa kuchukua mifano kutoka nchi za Ulaya kama Uingereza ambako tulishuhudia wananchi wakiandamana mitaani na askari wao hawakuwahi hata kumpiga kofi tu mwandamanaji hata mmoja.
  Walipohojiwa na vyombo vya habari walisema dhahiri kwamba waandamanaji ni raia halali wenye haki ya kufanya kile wanachokifanya kwa mujibu wa katiba na sheria za nchi yao. Katiba ya Tanzania na sheria za nchi hii zinatoa haki kama zile za Uingereza. Tofauti ni utekelezaji wa matakwa hayo ya kikatiba na kisheria. Watawala wa Uingereza wako tayari hata kung'oka madarakani ili kutekeleza matakwa ya nguvu ya umma.

  Lakini wale wa Tanzania wako tayari kung'oa uhai wa raia wengi ili mradi kuzuia nguvu ya umma inayodai haki na wananya hivyo kwa sababu ya hofu ya kung'oka madarakani, jambo ambalo hawataki kabisa kulisikia. Na ndugu zangu askari napenda kuwaambia kwamba yote yanafanywa na watawala wetu kwa kuwategemea nyinyi.

  Wanaminya haki zenu nyinyi wenyewe, haki za wazazi wenu, dada na ndugu zenu, marafiki zenu, jamaa zenu na majirani zenu. Chukulia mfano rafiki zangu Mtaki na Edwin. Tumesoma wote shule ya msingi pale Magu.

  Nilichaguliwa kujiunga na Mazengo Sekondari, shule kubwa na ya muda mrefu ambayo sasa imegeuzwa kuwa chuo kikuu bila mabadiliko ya majengo.

  Shule iliyokuwa na maabara nne kwa maana ya maabara ya baiolojia, kemia, fizikia na jiografia. Ilikuwa ni sekondari ya ufundi na hakuna karakana ambayo haikuwapo.

  Shule iliyokuwa na walimu wa kutosha, vyumba vya kutosha vya madarasa na vya kulala mabwenini.
  Katika bweni la Ujamaa kwa mfano, nilikokuwa naishi mimi, kuna vyumba kadhaa havikuwa na watu. Darasa la Form IVA ambalo nilikuwamo lilikuwa na wanafunzi 21 tu darasani.

  Na mazingira mengine mengi ambayo sitaweza kuyataja hapa ambayo yanafanya wanafunzi wa leo wa Chuo Kikuu cha Mt. John wajiulize kama kweli ile ilikuwa ni shule ambayo haina maktaba wala vitabu vya kutosha, na mengineyo mengi mnayoyafahmu.

  Nikafaulu kwa kiwango cha daraja la juu lililoniwezesha kuendelea mpaka chuo kikuu na kupata kazi nzuri kwenye Umoja wa Mataiifa.

  Rafiki zangu nakumbuka mlivyoamua kujiunga na Jeshi la Polisi si kwa sababu mlipenda kazi hiyo ama kwamba mlikuwa na wito wa kuwa polisi kama mnavyodanganywa kwamba jeshi ni wito.

  Nakumbuka mlijiunga huku mkilalamika kwamba mnalazimika kujiunga huko kwa sababu kiwango chenu cha ufaulu hakiwapi fursa ya kazi bora zaidi ya hiyo. Lakini mimi nawafahamu vizuri. Najua uwezo wenu wa darasani. Mliathiriwa na mazingira ya hovyo ya shule mlizosoma.

  Rafiki zangu nyinyi wote leo ni wakuu wa vituo vikuu vya polisi vya wilaya katika wilaya za Mbozi na Igunga.
  Leo hii mimi nimeacha kazi ya Umoja wa Mataifa kwa ajili ya kushiriki vema katika mapambano ya kutafuta ukombozi wa taifa hili.

  Wadogo zenu na wadogo zangu mnawajua wako katika juhudi za kutafuta maisha lakini ni magumu. Wengine walikosa kabisa nafasi ya kujiunga hata na hiyo Magu Day.

  Wakaishia Bulima na Kinango, ambako hali ilikuwa mbaya zaidi. Wakafeli kabisa na leo wanahangaika hapa na pale lakini watawala wanawawekea mazingira magumu mno ya kuendesha maisha.

  Na sasa chukulia nao wametambua hali yao duni inasababishwa na watawala walafi na walaghai. Wamejaribu kutumia njia za kidiplomasia kudai haki zao wanakutana na watu wanaitwa wakuu wa wilaya na mikoa.

  Wanaamua kuandamana, mnashiriki kuamrisha askari walio chini yenu kuwapiga na kuwaweka rumande na hatimaye kuwafungulia kesi za kubumba!

  Askari wetu igeni mfano wa askari wa Misri! Pale wananchi walipoamua kuandamana kukomesha utawala wa kidhalimu wa miaka 30 chini ya Hosni Mubarak, askari waliwalinda badala ya kuwapiga.

  Walikataa kwa sababu hata wao walikuwa wakiumizwa na Mubarak lakini zaidi ya hayo, waliokuwa wakiandamana walikuwa ni dada zao na ndugu zao na marafiki zao.

  Hivi sasa nchi iko njia panda. Ugumu wa maisha umeongezeka mara nne na zaidi. Watawala hawalioni hilo wala hawajishughulishi kurekebisha hali ya mambo hususan hali ya uchumi.

  Wako busy na kujiandaa kwa uchaguzi wa 2015. Mawaziri wako busy na kampeni za kuteuliwa kuwa wagombea wa urais kupitia chama tawala hapo 2015 na rais naye yuko busy kuandaa mtu wake ambaye anadhani akimrithisha jumba jeupe la pale Magogoni atasema mwacheni Ndugu Kikwete apumzike kwa amani.

  Taifa limeamua kuandika katiba mpya, rais na serikali yake na chama chake wameamua kuuteka mchakato ingawa haikuwemo kwenye ilani yao ya uchaguzi ili tu waturudishie katiba ya mwaka 1977 na kuipa jina juu ya jalada KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA MWAKA 2014.

  Natambua juhudi zinazoendelea hasa zikiongozwa na CHADEMA kujaribu kumkumbusha rais kwamba katiba iko juu yake na katiba ni mali ya wananchi na yeye anaajiriwa kwa katiba hiyo na si yeye kujiandalia katiba ili atawale kwa ulaini.

  Lakini juhudi za kidiplomasia zikishindikana hapo ndipo itabidi haki ya watu idaiwe kwa maandamano na hapo askari wote tuungane na kuwa kama Misri, kwa kuwa Katiba mpya ni kwa masilahi yenu pia! Jaribuni kutafakari!
   
 11. k

  kuzou JF-Expert Member

  #11
  Jan 28, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 200
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  play ur part kaka usigome kisa hospitali vitanda havitoshi, ingekua unafanya kazi zimamoto gari ipo moja ungegoma.unaweza kuokoa maisha ya mtu hata kama kalala chini hospitali,kina mama wajawazito wanavitanda nyumbani wanalala chini kuwafuata nyie halafu mmegoma nafsi inawasuta,kazi yenu ni wito,ni sawa na kuona mtu kagogwa na gari humjui ukaitwa na kitu kumsaidia bila kutegemea malipo.lkn hospitali za serikali mnazuga tu mpate majina mwende aga khan badae jioni.mna bahati ipo siku mtkua wengi we utakua ushakufa hamtaringa.
   
 12. F

  FJM JF-Expert Member

  #12
  Jan 28, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Huungi mkono mgomo wa madaktari lakini unaunga mkono hatua ya kugeuza Muhimbili kuwa kituo cha wakubwa kupumzikia kabla ya kwenda India? Huungi mkono mgomo wa madaktari lakini unaunga mkono kwa sababu wanadai nyongeza ya mshahara lakini unaunga mkono hatua ya serikali ya ccm ya kuongeza posho za wabunge? Pengine nikuulize, utamlipa kiasi gani mtu anamtibu ndugu/mtoto ugonjwa ambao potentially unaweza kumuua?
   
 13. Mwakalinga Y. R

  Mwakalinga Y. R Tanzanite Member

  #13
  Jan 28, 2012
  Joined: Oct 22, 2008
  Messages: 2,718
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  Hata Blandina Nyoni ,Pinda ,baazi ya wafuasi wa Magamba na Mganga JK hawaungi mkono huu mgomo .Kwa hiyo usijione mpekwe ukafikiri upo peke yako.
   
 14. T

  Tata JF-Expert Member

  #14
  Jan 28, 2012
  Joined: Dec 3, 2009
  Messages: 4,730
  Likes Received: 646
  Trophy Points: 280
  Naunga mkono juhudi za mtu yoyote yule kudai haki zake. Madaktari wamenyimwa haki zao kwa muda mrefu na wamekuwa wakionewa, wakinyanyaswa na kudhalilishwa na serikali kila mara wanapojaribu kudai haki hizo. Suala la wagonjwa kufa halipendezi wala halikubaliki. Lakini je ni kweli kwamba ni madaktari pekee ndio wenye wajibu wa kuhakikisha kuwa wagonjwa hawafi wanapofika hospitalini? Kila mtu akitimiza wajibu wake hakuna mgonjwa atakayekufa kwa magonjwa yanayotibika nchi hii.
   
 15. T

  Topical JF-Expert Member

  #15
  Jan 29, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  KCMC ni ya Serikali??? kwanini mnachanganya madawa?
   
 16. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #16
  Jan 29, 2012
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Zemarcopolo... unakumbuka Nyerere alivyotuaminisha mapinduzi ya russia , cuban revolution, mahatma gandhi, nk??

  Na je unafahamu madaktari wanasaidia watanzania wote kwa serikali kukumbuka wajibu??

  je unajua kwamba no pain no gain??

  pia si unafahamu katika kila generation kuna sacrifices??

  I expected you to be against drs. lakini kwasababu sijui nafasi yako kwa jamii, naishia hapo

  MIE NAUNGA MKONO DRS STAND
   
 17. Dunda kwetu

  Dunda kwetu JF-Expert Member

  #17
  Jan 29, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 265
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kiasi usiuunge mkono mgomo kwa sababu ukiumwa pesa za ufisadi zitakutibi nje ya nchi
   
 18. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #18
  Jan 29, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Wapo watu wanataka mema lakini hawataki kulipia gharama ya mema hayo. Wapo wanataka waone kuwa huduma ya afya nchini inaboreshwa lakini hawako tayrai kuona kuwa serikali inalazimishwa kuboresha huduma hiyo baada ya njia nyingine zote kushindwa. Ni sawasawa na mtu ambaye anataka kubakia na keki yake lakini wakati huo huo anataka kuila.
   
 19. T

  Topical JF-Expert Member

  #19
  Jan 29, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Mengi ya madai ya madaktari ni illusion hayawezi kutekelezeka kwa uchumi uliopo...

  So kwa madai hayo na kutaka yafanyiwe kazi immediately...inabidi watafute kazi sehemu nyingine..this is free market

  Kama unaona muajir wako hawezi kukutimizia maslahi yako kama upendavyo unaweza kwenda kufanya kazi kwa wahindi...au private sector au waanzishe hospitali zao walipane wenyewe kama watakavyoona inafaa..

  Mapato ya madaktari ni sawa na ya mwalimu, ni sawa na ya Askari, ni sawa na ya Mkulima????

  Natoa hoja.
   
 20. T

  Topical JF-Expert Member

  #20
  Jan 29, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Kwani lazima daktari afanye kazi serikalini?????

  Wafungue hospitali zao walipane wapendavyo..
   
Loading...