Siungi mkono mgomo wa madaktari...

Siungi mkono mgomo wa madaktari...

MAKALA hii ilikuwa itoke Jumatano ya wiki iliyopita lakini kwa sababu za kiufundi ikashindikana. Imekuwa ni bahati nzuri kwamba inapotoka leo, ijibu swali la askari polisi dereva wa gari la maji ya kuwasha.

Askari huyo alimweleza Mwalimu Mkuu wa watu jinsi roho inavyomuuma pale anapowamwagia Watanzania wenzake maji hayo ya kuwasha wakati wakidai haki yao. Askari uliyeuliza na wenzako wote someni makala hii kwa utulivu. Huu ni waraka maalumu kwa askari wote wa majeshi yote vikosi vyote Tanzania Bara na Visiwani.
Kwa lugha ya wazi zaidi nazungumza na askari wa Jeshi la Polisi Tanzania, Askari wa Jeshi la Kujenga Taifa, askari wa Kikosi Maalumu cha Kuzuia Magendo (KMKM), askari wa Jeshi la Magereza na wale wa Jeshi la Wananchi (JWTZ).
Kuwa mwanajeshi lolote kati ya hayo niliyoyataja si dhambi na si kweli kwamba kuwa mwanajeshi kunakuondolea uwezo wa kufikiri na badala yake ukawa unafikiriwa na watu wengine.
Wala haimaanishi kuwa askari kuwa kama robot ndio nidhamu bora kuliko zote duniani. La hasha! Mimi nilikataa utumwa huo!
Mwaka 1999 nilihitimu elimu ya cheti cha ufundi mchundo, yaani Full Technician Certificate (FTC) katika uhandisi wa Elektroniki na Mawasiliano ya Anga, yaani Electronics & Telecommunications Engineering kutoka Taasisi ya Teknolojia ya Dar es Salaam (DIT).
Nikiwa bado sijapata kazi ya maana, mwezi Aprili mwaka 2000 niliona tangazo la kazi ya Radio Technician katika Jeshi la Magereza. Nikatuma maombi na kuitwa kwenye usaili uliofanyika Chuo cha Maofisa wa Jeshi la Magereza Ukonga, Dar es Salaam mwezi Juni 2000.
Wote tuliofaulu usaili tulipangiwa siku ya kuripoti Chuo cha Magereza Kiwira kule Tukuyu, Mbeya.
Kufika kule nilishuhudia mambo ya ajabu. Ingawa wao hufurahia na kusema eti wanakutoa uraiani na kuwa mwanajeshi lakini baadhi ya matendo yanayofanyika wakati wa mafunzo ya jeshi ni ya kuwapumbaza askari wetu ili baadaye wakiwa kazini, watawala wawatumie watakavyo.
Nilishindwa kuvumilia kaulimbiu ya wakufunzi wa jeshi pale walipoelekeza kwamba chochote kruta (askari mpya mafunzoni) unachoambiwa lazima uitikie “ndiyo afande”. Nilishindwa kuitikia kwa mfano pale mkufunzi mmoja mwenye cheo cha koplo alipotutamkia mfululizo wa sentensi zifuatazo:
Mkufunzi: Nyinyi makruta mbona wote hamkuja na majembe?

Makruta: Ndiyo afande!
Mkufunzi: Hamkuambiwa makao makuu ya jeshi kwamba lazima mje na majembe?
Makruta: Ndiyo afande!
Mkufunzi: Kwa hiyo kwa kuwa hamkuambiwa na nyinyi hamkuyabeba?
Makruta: Ndiyo afande!
Mkufunzi: Wote ni wapumbavu pamoja na mama zenu waliowazaa.
Makruta: Ndiyo afande!
Ni hayo pamoja na mambo mengine ya kulazimishwa kwenda kwenye kile kinachoitwa disko, ambapo pamoja na uchovu wa kutwa nzima wa kazi ngumu na nyingi bado ni lazima ukae hapo mpaka saa 4 usiku tena ukinyooshewa kidole tu na mwenzako lazima usimame na kuimbisha wimbo tena kwa tabasamu, wimbo mmoja wapo ukisema “Magereza ninavyokupenda nitakunywa sumu juu yako”, ndiyo yaliyonifanya nikakataa kazi ya jeshi baada ya wiki moja tu ya mafunzo.
Siku niliyokataa jeshi ilikuwa ni Jumatano asubuhi ambapo sikwenda mchakamchaka na wakati wenzako wanatawanyika kufanya usafi wa nje maeneo mbalimbali, mimi nilibeba begi langu na kuanza kuondoka chuoni majira ya saa moja na nusu hivi asubuhi.
Nilikamatwa na mkufunzi mmoja wa jeshi na kupelekwa pamoja na begi langu kwa Ofisa Mafunzo wa chuo. Aliponiuliza sababu nilimtajia mbili, kwanza kwamba sifurahii mambo ya jeshi na kubwa zaidi kwamba mimi ni Msabato na nimeambiwa na wenzangu kwamba hapa hakuna kwenda kusali, siku zote za juma ni kazi.
Kitu ambacho sitaweza maana Sabato takatifu lazima nipumzike! Bila kuuliza zaidi aliconclude kwa kuniambia kwamba, “Sijawahi kuona mtu anaacha kazi kwa ajili ya mambo ya dini.
”Ni dhahiri wewe ulikuja kutupeleleza na hivyo kazi yako imeisha sasa unataka kurudi. Tutakuweka rumande, tena ile ya polisi kwa wiki mbili wakati tunafanya upelelezi juu yako.”
Askari aliyenileta alianza kunivuta ili kunipeleka rumande lakini nilikataa huku nikiendelea kujieleza kwa ofisa mafunzo ili ajue kwamba sikuwa na mpango huo aliousema.
Baada ya kuelemewa na hoja zangu alinipeleka kwa makamu mkuu wa chuo ambaye yeye alitumia zaidi Biblia kunihubiri kwamba nakaidi amri ya mamlaka wakati hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu.
Jibu langu lilikuwa fupi na lenye msimamo mzito kwamba ikiwa mamlaka ya wanadamu inafika mahali inanena tofauti na Mungu, Mtume Petro ametuandikia kwamba katika hali ya namna hiyo, “Imetupasa kumtii Mungu kuliko mwanadamu”.
Na yeye alinishindwa akanipeleka kwa mkuu wa chuo na wao wote wakiwapo. Ushauri waliokuwa wakimpa mkuu wa chuo ni kwamba mimi niwekwe rumande kwanza ili wafanye upelelezi. Lakini sikuyumba katika msimamo wangu.
Nilimweleza mkuu wa chuo kwamba mimi ni raia na si mpelelezi. Nilizirudia rudia sababu zangu za kuacha jeshi tena kwa ujasiri mkubwa na kumhakikishia mkuu wa chuo kwamba akinipa hayo ninayoyataka niko tayari kubaki jeshini.
Hatimaye kauli ya mwisho ya mkuu wa chuo ilikuwa ni hii: “Jeshi ni wito. Tunaweza kumlazimisha huyu kijana kuwa mwanajeshi lakini baadaye ikatuletea madhara makubwa sana.” Akamalizia kwa kusema, “chukueni maelezo yake kwa maandishi kisha arudishe vifaa vya jeshi.”
Wakati naondoka nilimsikia ofisa mafunzo akitoa maelekezo kwa walio chini yake kwamba mwanafunzi mwingine wa jeshi akija kuripoti na kwenye daftari akajaza kwamba ni Msabato, msimsajili kwanza mpaka aje kwangu! Sijui kama Wasabato wameendelea kupokewa kwenye hicho chuo cha magereza lakini ninachotaka askari wote wa majeshi yetu yote na vikosi vyote, ni kwamba askari unaweza kusimama kwa miguu yako na kufikiri kwa akili yako mwenyewe!
Ndugu zangu askari, nchi imefika mahali ambapo Waingereza hupenda kupaita ‘critical point’. Ni mahali ambapo wananchi wako tayari kwa mabadiliko na watawala wako tayari kwa mapambano ili kubaki madarakani.
Katika point hii askari wetu wanakuwa na nafasi kubwa ya aidha kuwezesha mabadiliko hayo kutokea kwa wakati wanaoutaka wananchi, tena kwa amani ama kuyachelewesha (si kuyazuia) na kusababisha yatokee baadaye kidogo kuliko wananchi walivyotaka, tena baada ya kumwaga damu nyingi ya Watanzania wasio na hatia!
Napenda kurudia kwamba hakuna jeshi lolote duniani hata kama tungekusanya majeshi yote ya dunia hii na kuyaleta Tanzania hawataweza kuizuia nguvu ya umma pale inapokuwa imeamua kufanya mabadiliko.
Napenda tena kurudia kwamba si lazima askari mfanye kile ambacho wakubwa wenu wanataka na kuwaamuru kufanya. Tunaweza kusimama imara na kutetea haki za Watanzania tukiwamo na sisi askari. Niliwahi kugoma kutii amri ya kukamatwa na kuwekwa rumande.
Lakini pia mifano ni mingi na nisingependa kuchukua mifano kutoka nchi za Ulaya kama Uingereza ambako tulishuhudia wananchi wakiandamana mitaani na askari wao hawakuwahi hata kumpiga kofi tu mwandamanaji hata mmoja.
Walipohojiwa na vyombo vya habari walisema dhahiri kwamba waandamanaji ni raia halali wenye haki ya kufanya kile wanachokifanya kwa mujibu wa katiba na sheria za nchi yao. Katiba ya Tanzania na sheria za nchi hii zinatoa haki kama zile za Uingereza. Tofauti ni utekelezaji wa matakwa hayo ya kikatiba na kisheria. Watawala wa Uingereza wako tayari hata kung’oka madarakani ili kutekeleza matakwa ya nguvu ya umma.
Lakini wale wa Tanzania wako tayari kung’oa uhai wa raia wengi ili mradi kuzuia nguvu ya umma inayodai haki na wananya hivyo kwa sababu ya hofu ya kung’oka madarakani, jambo ambalo hawataki kabisa kulisikia. Na ndugu zangu askari napenda kuwaambia kwamba yote yanafanywa na watawala wetu kwa kuwategemea nyinyi.
Wanaminya haki zenu nyinyi wenyewe, haki za wazazi wenu, dada na ndugu zenu, marafiki zenu, jamaa zenu na majirani zenu. Chukulia mfano rafiki zangu Mtaki na Edwin. Tumesoma wote shule ya msingi pale Magu.
Nilichaguliwa kujiunga na Mazengo Sekondari, shule kubwa na ya muda mrefu ambayo sasa imegeuzwa kuwa chuo kikuu bila mabadiliko ya majengo.
Shule iliyokuwa na maabara nne kwa maana ya maabara ya baiolojia, kemia, fizikia na jiografia. Ilikuwa ni sekondari ya ufundi na hakuna karakana ambayo haikuwapo.
Shule iliyokuwa na walimu wa kutosha, vyumba vya kutosha vya madarasa na vya kulala mabwenini.
Katika bweni la Ujamaa kwa mfano, nilikokuwa naishi mimi, kuna vyumba kadhaa havikuwa na watu. Darasa la Form IVA ambalo nilikuwamo lilikuwa na wanafunzi 21 tu darasani.
Na mazingira mengine mengi ambayo sitaweza kuyataja hapa ambayo yanafanya wanafunzi wa leo wa Chuo Kikuu cha Mt. John wajiulize kama kweli ile ilikuwa ni shule ambayo haina maktaba wala vitabu vya kutosha, na mengineyo mengi mnayoyafahmu.
Nikafaulu kwa kiwango cha daraja la juu lililoniwezesha kuendelea mpaka chuo kikuu na kupata kazi nzuri kwenye Umoja wa Mataiifa.
Rafiki zangu nakumbuka mlivyoamua kujiunga na Jeshi la Polisi si kwa sababu mlipenda kazi hiyo ama kwamba mlikuwa na wito wa kuwa polisi kama mnavyodanganywa kwamba jeshi ni wito.
Nakumbuka mlijiunga huku mkilalamika kwamba mnalazimika kujiunga huko kwa sababu kiwango chenu cha ufaulu hakiwapi fursa ya kazi bora zaidi ya hiyo. Lakini mimi nawafahamu vizuri. Najua uwezo wenu wa darasani. Mliathiriwa na mazingira ya hovyo ya shule mlizosoma.
Rafiki zangu nyinyi wote leo ni wakuu wa vituo vikuu vya polisi vya wilaya katika wilaya za Mbozi na Igunga.
Leo hii mimi nimeacha kazi ya Umoja wa Mataifa kwa ajili ya kushiriki vema katika mapambano ya kutafuta ukombozi wa taifa hili.
Wadogo zenu na wadogo zangu mnawajua wako katika juhudi za kutafuta maisha lakini ni magumu. Wengine walikosa kabisa nafasi ya kujiunga hata na hiyo Magu Day.
Wakaishia Bulima na Kinango, ambako hali ilikuwa mbaya zaidi. Wakafeli kabisa na leo wanahangaika hapa na pale lakini watawala wanawawekea mazingira magumu mno ya kuendesha maisha.
Na sasa chukulia nao wametambua hali yao duni inasababishwa na watawala walafi na walaghai. Wamejaribu kutumia njia za kidiplomasia kudai haki zao wanakutana na watu wanaitwa wakuu wa wilaya na mikoa.
Wanaamua kuandamana, mnashiriki kuamrisha askari walio chini yenu kuwapiga na kuwaweka rumande na hatimaye kuwafungulia kesi za kubumba!
Askari wetu igeni mfano wa askari wa Misri! Pale wananchi walipoamua kuandamana kukomesha utawala wa kidhalimu wa miaka 30 chini ya Hosni Mubarak, askari waliwalinda badala ya kuwapiga.
Walikataa kwa sababu hata wao walikuwa wakiumizwa na Mubarak lakini zaidi ya hayo, waliokuwa wakiandamana walikuwa ni dada zao na ndugu zao na marafiki zao.
Hivi sasa nchi iko njia panda. Ugumu wa maisha umeongezeka mara nne na zaidi. Watawala hawalioni hilo wala hawajishughulishi kurekebisha hali ya mambo hususan hali ya uchumi.
Wako busy na kujiandaa kwa uchaguzi wa 2015. Mawaziri wako busy na kampeni za kuteuliwa kuwa wagombea wa urais kupitia chama tawala hapo 2015 na rais naye yuko busy kuandaa mtu wake ambaye anadhani akimrithisha jumba jeupe la pale Magogoni atasema mwacheni Ndugu Kikwete apumzike kwa amani.
Taifa limeamua kuandika katiba mpya, rais na serikali yake na chama chake wameamua kuuteka mchakato ingawa haikuwemo kwenye ilani yao ya uchaguzi ili tu waturudishie katiba ya mwaka 1977 na kuipa jina juu ya jalada KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA MWAKA 2014.
Natambua juhudi zinazoendelea hasa zikiongozwa na CHADEMA kujaribu kumkumbusha rais kwamba katiba iko juu yake na katiba ni mali ya wananchi na yeye anaajiriwa kwa katiba hiyo na si yeye kujiandalia katiba ili atawale kwa ulaini.

Lakini juhudi za kidiplomasia zikishindikana hapo ndipo itabidi haki ya watu idaiwe kwa maandamano na hapo askari wote tuungane na kuwa kama Misri, kwa kuwa Katiba mpya ni kwa masilahi yenu pia! Jaribuni kutafakari!

Kiukweli umenikumbusha mbali sana. Nimekumbuka nilipokuwa jeshi la kujenga Taifa pale Itende JKT Mjini Mbeya. Kruta neno lake moja tu "Ndio Afande" nimekumbuka mchakamchaka, kuimba disco nk. Ni kweli kwamba hakuna nguvu yeyote duniani iwe ya majeshi au kutoka kuzimu inayoweza kuishinda nguvunya umma. Tanzania tunaelekea huko maana dhuluma imezidi kwa Watanzania, wanasiasa wametugeuza miradi yao. Ipo siku tutaimba nyimbo za ushindi na kuwaonyesha watoto wetu kuwa "Tazama magofu yale yalikuwa makasri ya Mawaziri wa Madini, tazama kijiji kile kilikuwa mali ya Waziri furani, tazama shamba lile kubwa kama Wilaya walinyang'anywa Wazee wetu, lakini sasa tumeyarudisha, tazama kaburi lile ni la Waziri wa Uchuzi alipewa sumu na Serikali, tazama mashimo haya wageni walichimba madini yetu yote lakini sasa imejaa sumu nk". Si mbali sana hayo mambo yatatimia. "Freedom is Coming Tomorrow"
 
Du this is so tough thread. Lakini wakati tunatafakari swala hili zito tuangalie makundi matatu
1. Serikali ambayo ni baba wa watanzania
2. Madaktari ambao wanatoa huduma ya utabibu kwa watanzania
3. Watanzania ambao wanastahili huduma stahiki ili walete maendeleo.
Swali ni kwamba Kati ya haya makundi 3 ni nani aliyesababisha tufikie Hali hii?
 
una blame DR'S kwa uthaifu wa sirikali yako c'mon brother put your self together...there is no turning back this time lets face the consequences...ndio wataacha kusinzia mjengoni wakat mambo muhimu yakiwasilishwa.
 
Ni wakati wa Ulimboka kutafakari u nyeti wahuduma mahospitalini,
si furahishwi na alicho tendewa ulimboka ila pia sifurahishwi na maamuzi ya madkari akiwemo na Ulimboka kama kinara wa mgomo,
naamini dr ulimboka akipata nafuu anaweza hisi watanzania wanateseka kwa kiwango gani na migomo yenu,je kama wewe ungeachwa bila huduma nini ingekua hatma ya maisha yako?
lazma tuache ushabiki kwani watu wanaangamia kwa mgomo huu,
ni ajabu watu kuonesha huruma kwa ulimboka pekee ambae kimsingi hakuwahurumia wagonjwa wenye hali kama yake au mbaya zaidi ya hali alionayo sasa.
Madkatari tafuteni njia mbadala kuwabana serikali kwani mnatuua watanzania wenzenu bila hatia


Serikali inajaribu kuwahadaa wananchi kwa kudai kuwa mgomo wa Madaktari unahusiana na swala la kuongezewa mishahara tu kitu ambacho si cha kweli.

Mgomo wa madaktari umebeba vitu vingi sana na miongoni mwao ni mazingira mabovu ya kazi na uduni wa vitendea kazi...
Haya wanayogomea madaktari ni pia kitendo cha kumzalisha Mwanamke bila kuvaa Glovsi, je huoni kuwa ni hatari?
Au ungekuwa ni wewe Dokta ungekubali au unajishaua tu?
 
ulimboka akipata nafuu apelekwe mahakamani kwa kukaidi amri ya mahakama kuu
 
naomba usikurupuke kwani mimi siitetei serikali hapa,
nipe kosa la hawa wagonjwa wanaotaabika sasa kwa kukosa matibabu,kama kosa ni la serikali kwanini wahanga wawe watanzania.
watanzania wameanza kuteseka leeo siku ya ngapi?huyu ulimboka yeye ni nani hata awe na thamani zaidi yetu sisi wananchi tunao teswa kwa kosa lisilo letu?
What do u think, u think ur smart? Listen very carefully at urself
 
Hao the so-called 'wanaharakati' same as wanasiasa watafute real jobs. kuwa na lundo la 'wakaa bure' ni mzigo mkubwa kwa taifa. watu kaa hawa ambao wanaruhusiwa kukaa idle tu na ku-hatch mawazo hasi dhidi ya serikali yao badala ya kuijenga wakipewa platform ndo matokeo yake. nchi imejaa politiki kila kona watu hawataki kufanya kazi, kila mmoja akidai anadhulumiwa ! nnchi ya kijinga sana hii, watu hawawajibiki ni kulalama tu usiku kucha.
 
Baada ya kutafakari nasema, Ulimboka ni turufu iliyotumiwa na wasiyoitakia mema Serikali iliyopo madarakani:

Haiingii akilini kwa binaadam yeyote mwenye fikra japo kidogo, eti Serikali wakuchukuwe, wakupige, wakutupe Mabwepande halafu waje haki za binaadam kukuota.


Mlio tumia hii turufu mmelamba jike.

Nakubaliana na mleta mada kwa kilichomkuta Ulimboka.

Hajaokotwa na hao watu wa haki za binadamu,ni wanachi tu wa kawaida ambao hata hawamfaham,na yy ndo aliwaambia kuwa yy ni nani na kafikaje pale!...then wakataka kupiga cm polic bt kuna mtu akawazuia,na ndo kilichosaidia laa sivyo wangemmalizia,wakapiga kwanza kwa watu wa haki za binadam,ndo wakajipanga wakaja,wakamtoa pale polic na kuchukua pf3 coz huwez kutibiwa bila hyo!...

Imagine, mtu wa kitengo cha ambulance muhimbili alikataa kutoa gari kwenda kumchukua,jiulize y?...mtu wa usalama aliyekuwa hapo na kupigwa na kuokolewa na walinzi, coz alionekana akiwasiliana na watu kuwa akiwaambia 'bado mzima'...kwahiyo ndo alihusika!...tena ni ss unataka kutuambia nani kahucka?!....fikiri,chukua hatua
 
Hajaokotwa na hao watu wa haki za binadamu,ni wanachi tu wa kawaida ambao hata hawamfaham,na yy ndo aliwaambia kuwa yy ni nani na kafikaje pale!...then wakataka kupiga cm polic bt kuna mtu akawazuia,na ndo kilichosaidia laa sivyo wangemmalizia,wakapiga kwanza kwa watu wa haki za binadam,ndo wakajipanga wakaja,wakamtoa pale polic na kuchukua pf3 coz huwez kutibiwa bila hyo!...

Imagine, mtu wa kitengo cha ambulance muhimbili alikataa kutoa gari kwenda kumchukua,jiulize y?...mtu wa usalama aliyekuwa hapo na kupigwa na kuokolewa na walinzi, coz alionekana akiwasiliana na watu kuwa akiwaambia 'bado mzima'...kwahiyo ndo alihusika!...tena ni ss unataka kutuambia nani kahucka?!....fikiri,chukua hatua

Hiyo version yako sasa inakuwa ya tano.

Nakwambia hakuna ukweli mpaka tupate official version ya uchunguzi wa wazi na huru.
 
Nimekuwa nikifuatilia madai ya Madaktari baadthi ya mambo wanayohitaji yametekelezwa na serikali ila wanalotaka kwa sasa ni Mshahara wa Milioni 3.5 kwa Mwezi, Katika hali ya kwaida Mshahara huo katika Nchi za Africa Mashariki hakuna nchi iliyofikia hapo na Nchi Maskini kama Tanzania Haiwezekani kulipwa pesa hizo katika Watumishi waSerikali wanaomaliza chuo na kuanza kulipwa Mshahara mkubwa ni Madaktari wanaanza na Laki Tisa na Sehemu nadhani imefika wakati tufanye Analysis Kuna Watumishi wangapi wa Serikali nao ni muhimu kuongezewa Mishahara kwa sababu nao ni Wasomi wazuri Si kwamba nchi hii wasomi ni Mdaktari Tu, Kila mmoja ni MSOMI NA anahitaji Mshahara mzuri kama ambavyo wanataka Madaktari hata Wabunge hawalipwi Mshahara huo ni 2.5Milioni mnayoyasikia ni Posho za Vikao tu inayopandisha,

Madaktari wanapewa Mkopo 100% na Board ya Mkopo.

Nawashauri kama mnaona Mshahara Mdogo mkasome Course nyingine zenye Maslai kuliko kuhangaika na Course isiyolopa au Acheni kazi Serikalini mkafanye Private sector Serikali ifahamu ina upungufu wa Madaktari haiwezekani Ulipwe laki Tisa bado uone Unalipwa kidogo wakati wapo watumishi wana degree wanalipwa laki Mbili kwa Mwezi Serikalini.

SERIKALI IMEKUBALI KUWAKOPESHA MAGARI , KUWAONGEZEA POSHO ZA NYUMBA NA POSHO NYINGINE,

Pia napenda kuwafahamisha wana JF idara ya ya Tatu kwa kupokea Rushwa ni Watumishi wa Afya ..

Badilikeni na Toeni data mnagoma mnataka nini na kwa nini mnataka Toeni data kama wasomi msije mkawa mnatumika kisiasa.
 
jimy nakubaliana na wewe 101%...wamekuwa wakidai..ila ukweli hakuna mtanzania anajua wanaadai kitu gani...
Hawajawahi kuweka hizo data hadharani
hawasemi wanataka mshahara wa kiasi gani
kwa nini wasitumie mfano gazeti la kiswahili na la ki english wakatoa press release page nzima ni ni wanataka wafanyiwe
hii itaweka wazi madai yao na watanzania watapata picha halisi
kina chofanywa sasa ni siasa ...mbinu ya kujaribu kuipaka matope serikali
sote tunajua walitaka katibu mkuu aondoke kwenye mgomo wa mwanzo
ameondoka katibu na waziri
na baadhi ya madai yao yame tekelezwa
tunawaomba wache siasa
warudi kazini
kama hawataki fukuza wote
na hakuna ruhusa ya kufanya kazi private
kwani uongo hakuna private hospital inayolipa zaid ya serikali
 
Last edited by a moderator:
Asante sana ndugu yangu, wewe huenda ukawa wa kwanza kuanzisha huu uzi, na watu wanaweza kukuona mkatili but message uliyobeba ni kubwa sana hapa #Nimeisoma Hii pia!!!

taifa hli linawajinga wengi sana. Wewe ni mjinga namba moja.
 
Nilikuwa naangalia tv nikamuona mama mmoja dr anang'aka kwa uchungu kweli anasema
" hawa polisi wanyama sana wanaona mtu yupo hoi badala ya kumkimbiza hospitali kwanza wao wamemuweka tu kituoni, akifa je?"

Nikajisemea mkuki kwa nguruwe tu.......

Sijawahi kuunga mkono mgomo wa drs
Na sijawahi kuunga mkono namna gvt inavyoshughulikia matatizo ya drs
Lakini pia siungi mkono namna walivyo mtendea Ulimboka

2015 sio mbali sana drs warudi kazini baada ya Cdm kuchukua nchi then kila kitu kitakuwa ok

msijitambua kama wewe ndo Cameroon anawataka.
 
Madaktari walishaweka ukweli wa madai yao kwenye series ya threads 'Ukweli wa madai ya madaktari na tumewaelewa
Msichotaka kukubali ni kuwa wanasiasa wameivuruga nchi hii
Nape anatembelea Shangingi
Beno anatembelea shangingi
Mukama hali kadhalika
Utasema ni mamboo ya chama na si serikali
Si kweli maana hayo yanatokana na ruzuku tunatolipa sisi tusio na vyama
Ruzuku iliyopangwa na wanasiasa
Mipango inayomtukuza na kumneemesha mwanasiasa na si mtu wa fani
Nina maana Serikali ina hela za mambo yasiyo na umuhimu kwa jamii pana kama ruzuku za vyama lakini haina za kuboresha huduma za afya!

Kuhusu madaktari kugoma wakilipwa laki tisa na watu wanaolipwa laki mbili hawagomi nadhani wa kulaumiwa ni hao wasiogoma wakati wanakandamizwa
Tunaweza hata kuwatuhumu kwa wizi maana haiwezekani kuishi maisha wanayoishi kwa mshahara huo
Tunawashauri waungane na wenzao kudai haki halali wanazonyimwa na wanasiasa
 
Hiyo version yako sasa inakuwa ya tano.

Nakwambia hakuna ukweli mpaka tupate official version ya uchunguzi wa wazi na huru.

Uchunguzi utakaofanywa na nani?
Polisi?
Hakuna atakayeamini taarifa yao kama ana akili timamu
 
Kama usalama wa taifa mgekuwa na akili jk na pindi wangekuwa Mortually na tayari kwa mazishi. Jk msasi sana fikiria bob seya na juz hapa G. Lema.
 
Hawa viongozi wa madaktari wanadhani wanaongoza serikali za wanafunzi vyuoni.

Suala la kujustify kupewa pesa nyingi eti kwa sababu wabunge wanalipwa nyingi ni uelewa mdogo.
Nenda popote duniani wanasiasa wako hivo hata kiingie chama kipi wataendelea kujilipa tu na kura watu wataendelea kuwapa maana wao ndo wenye kufanya maamuzi yote ya nchi.

Prof wangu wakati nasoma europe tena nchi tajiri alitwambia mshahara wake ukilinganisha na mtu aliyefanya kazi ya ujenzi (a mere technician) ni kama anazidiwa na huyo mjenzi.
So the world will never be fair as we dream.
 
Back
Top Bottom