Siungi mkono mgomo wa madaktari...

Siungi mkono mgomo wa madaktari...

Nasikitishwa na kuwa na waatu wasioelewa na kuongea.Moja bila utafiti huruhusiwi kuongea ni kauli mbiu iliyopo ssijaiweka mimi.Sasa kaka nenda pale muhimbili agiza I/V Metronidazole jibu ni o/s.Nimetolea mfano mdogo tu wa hiyo dawa ndogo sana ila yenye matumizi makubwa surgical wards.Unataka madaktari wafanye nini?Kuondoka kwa hao waliokuwa wizarani ni moja ya hatua kuelekea wanapopatamani haimaanishi kazi imeisha. Naionea huruma nchi hii.
 
Ni ajabu kuna watu wenye ubongo dhaifu kama wewe na wapo upande wa jamii wenye nafuu
Kutumiwa huku, usaliti huu dhidi ya jamii mnaoufanya utakuja watokea puani
Hata wa-Misri wakati wanadai mabadiliko kuna wapuuzi walikuja na farasi kupambana na waandamanaji na wakshindwa
Wewe na wenzako mlionunuliwa, mnaotumika kuzuia wa_Tz kudai haki zao mtashindwa tu.
Haiingii akilini Katibu wa chama itikadi na porojo anatembelea Shangingi, kwa ruzuku ambayo ni kodi zetu, halafu daktari hana hata baiskeli
Wacha madaktari wagome ili wananchi tudai mabadiliko
 
Ni lazima utukanwe,kwasababu hoja zako ni za kijinga!
Pole ndugu yangu.Nilianzisha uzi mwingine kama huu na kuna ambao mpaka wametukana katika kuuetea mgomo.
Ningekuwa na uwezo wa kukuwasiliana na Mkuu wa Kaya ningempa mbinu moja tu ambayo ingewanyoosha na wakashika adabu.
 
Medical doctors wa bongo wanapenda kunyenyekewa sana wanataka sijui wananchi wawaabudu kabisa.
 
kaeni nao muwasikilize kabla ya kuwalaumu! Wale ni wasomi na wana madai yao ya msingi kabisa! Ubabe au kuchafua image yao katika jamii badala ya kukaa na kufikia makubaliano italeta migongano zaidi. This time, wakikaa nao waweke mfumo ambao utafanya wapate wanachotakiwa kupata kwa wakati ili kuhakikisha hali kama hii haijirudiirudii mara kwa mara.
 
mtawaonea na kuwatishia hao hao walimu, ila mkae mkijua madaktari ni kitu kingine kabisaaaaaaaaaaaaa hatutishiwe nyau kamwe, hata mkituacha peke yetu bila sapoti yenu tutapigania haki yetu kufa na kupona
 
Hivi nyie ma-dr kwanini mnagoma? ACHENI kazi nendeni huko kwenye 3.5M salary na vifaa vzr. Mnagoma huku mnachukua mshahara! Acha kazi kama unaona mshahara mdogo na mazingira magumu.
 
Ni wakati wa Ulimboka kutafakari u nyeti wahuduma mahospitalini,
si furahishwi na alicho tendewa ulimboka ila pia sifurahishwi na maamuzi ya madkari akiwemo na Ulimboka kama kinara wa mgomo,
naamini dr ulimboka akipata nafuu anaweza hisi watanzania wanateseka kwa kiwango gani na migomo yenu,je kama wewe ungeachwa bila huduma nini ingekua hatma ya maisha yako?
lazma tuache ushabiki kwani watu wanaangamia kwa mgomo huu,
ni ajabu watu kuonesha huruma kwa ulimboka pekee ambae kimsingi hakuwahurumia wagonjwa wenye hali kama yake au mbaya zaidi ya hali alionayo sasa.
Madkatari tafuteni njia mbadala kuwabana serikali kwani mnatuua watanzania wenzenu bila hatia
 
hakuna lolote!
serikali yetu inatumia silaha ya kuwa kama huwezi kugoma then hawana haja ya kukusikiliza! madaktari hawana option nyingine kwa sababu wanakabiliana na serikali hii ambayo inaweza kuexist kwa sababu ya watu wenye akili kama zako gimmy's! waache wagome, kwani watanznia wataofaidika na huduma za afya endapo madaktari watafanikiwa watakua ni wengi kuliko wanaopatwa na maafa sasa hivi na kwa vizai vingi vya mbele! msifikirie leo tu, fikiia na wajukuu zako! fight a bigger fight!
 
Ni wakati wa Ulimboka kutafakari u nyeti wahuduma mahospitalini,
si furahishwi na alicho tendewa ulimboka ila pia sifurahishwi na maamuzi ya madkari akiwemo na Ulimboka kama kinara wa mgomo,
naamini dr ulimboka akipata nafuu anaweza hisi watanzania wanateseka kwa kiwango gani na migomo yenu,je kama wewe ungeachwa bila huduma nini ingekua hatma ya maisha yako?
lazma tuache ushabiki kwani watu wanaangamia kwa mgomo huu,
ni ajabu watu kuonesha huruma kwa ulimboka pekee ambae kimsingi hakuwahurumia wagonjwa wenye hali kama yake au mbaya zaidi ya hali alionayo sasa.
Madkatari tafuteni njia mbadala kuwabana serikali kwani mnatuua watanzania wenzenu bila hatia

Asante sana ndugu yangu, wewe huenda ukawa wa kwanza kuanzisha huu uzi, na watu wanaweza kukuona mkatili but message uliyobeba ni kubwa sana hapa #Nimeisoma Hii pia!!!
 
Mawazo yako yakiwa yanaishia mwisho wa pua yako you will definitely think kwamba drs wanaumiza nenda mbele kidogo 50yrs
 
watu wengi wanasashau 'mkuki kwa nguruwe kwa binadamu mchungu' kupata kwake matatizo ni njia moja wapo ya kumwonyesha maumivu wanayoyapata wagonjwa wengine wanapokosa huduma ya daktari, naomba kuuliza mgomo huu wa madaktari anayathirika ni nani kama siyo mwananchi wa hali ya chini jamani? Wakuu wote katka serikali wanatibiwa nje ie India South afrika, Ujerumani nk, hivyo madaktari tunayakubali madai yen lkn kumbukeni na afya zetu
 
afu serikali imenichekesha eti wameenda mahakamani kuzuia migomo, hivi kweli unaweza mlazimisha mtu kufanya kazi? kweli hii ni bongo
 
nina dalili ya maralia Eee Mungu niepushe na ugonjwa huu madaktari wamegoma siwezi kutibiwa katika hospital za private sina uwezo najua nikimwa ntafia ndani, oooppps nasikia na wahudumu wa mochwali wamegoma so sio kuogopa kifo tu but may be naweza hata wanikia ndugu zangu nikiwa ndani....

Real siungi mkono maamuzi inayochukua serikali kushughulikia tatizo hili na magaktari pia.


Jamani tunakufa sisi maskin kunawanaopata ajari wanafia reception, mama na dada zetu wanauchungu wa kuzaa wanakufa pia..

Eee Mungu epusha taifa na wananchi sisi hasa masikini katika adha hiii... Naumia sanaaa kwa hali hiiiii.
 
Kama uliyeanzisha huu uzi si mzee basi nina Imani kama ukali wa maisha hautakuua na maginjwa kama ukimwi hayatakugusa , baada ya miaka ishirini ijayo utakuja mshukuru Ulimboka na utamuomba msamaha kama atakuwa hai.
 
Ama kweli kila kitu kina positive na negative sides......
sasa ni jukumu letu kupima lipi liko juu.
 
wewe ni chichidodo,kwani asingegoma ulimboka pekee ndo huduma zingekuwa nzuri? Je,hao wagonjwa wengine wanapigwa pia kama Ulimboka? Kama ni mgomo wa wote then,kwa nini adhurike Ulimboka peke yake? We ni mtu dhaifu kabisa-kabisa,kwani kati ya serikali na madaktari ni upande upi uliochanzo cha mgomo? Nasema wewe ni DHAIFU barabara,kwani madaktari wamezungumza na serikali mara ngapi? Wameipa muda kadiri gani lakini hakuna lolote zaidi ya kelele za wabunge wa ccm -SERIKALI YETU NI SIKIVU,inamsikiliza nani? Achana na nidhamu ya uoga na udhaifu la sivyo hata ndoa yako haitodumu.Unasema madaktari wangetafuta njia nyingine ya kuibana serikali,sema njia ipi? Usiwe dhaifu kiasi hicho:serikali inazo hela za kumpa Lowassa na kamati yake kwenda kutalii kwenye balozi za Tanzania lakini haina hela za kuboresha mazingira ya kazi kwa waalimu na madaktari. Mimi pia ni mlalahoi na hata kama nitakufa leo nitailaumu serikali dhaifu siyo madaktari.
 
Back
Top Bottom