Situmii tena Facebook na Instagram kwa ubaguzi huu

Situmii tena Facebook na Instagram kwa ubaguzi huu

iko sahihi ni kweli tena ukiandika mambo ya maana kufundisha upati kabisa like ila ukiandika upumbavu utazipata kidogo ila watu ndio walivyo.

Pia watu wana wivu balah ukiweka ata picha za kula bata unyamwezin wanaumia sana.Na ukiweka una matatizo hawakusaidii zaidi ya kukutangaza.

bora mitandao kama ya JF utaelimika,kupata habari na kuburudika.Mi kule uwa naweka picha za kuwalusha roho tu bata batan unyamwezin na kupotea walike wasilike watajiju hainiumizi.

Muda mwingi nakuwa kwenye mitandao kama JF au Youtube nasoma mambo mbalimbali
 
Mkuu Kibo10,

Kama issue ni "Like" na unaona ubora wa JF kwa ajili ya hizo Like basi niseme tu kwamba Jamii Forums ni zaidi ya uijuavyo!!! Si kila "Like" unayoipata humu inaonesha mtu ame-appreciate... wengine watakupa "Like" kama njia ya kuku-ignore!!!

Katika siku zangu za mwanzo kabisa hapa JF, kuna post niliandika mtu aka-comment "cra'p!" Na hiki kizungu changu cha Division 5 ya Mulugo nikadhani jamaa kanipigia makofi; mwenyewe wacha ninenepe bichwa kujiona nimedondosha full masi nondo... maskini ya mungu nikidhani cra'p ndio clap! Kwahiyo, hata hizo Like za JF inabidi uzisome mara mbili mbili...
 
Last edited by a moderator:
Whatsapp ni mtandao wa kibeya unafanana na text sms za mitandao ya simu kama voda n.k lakn haiwezi ikakubadili na kukuongezea wazo yoyote kama hapa jf au yahoo answer

inategemea na watu unaowasilina nao.
Kuna watu wana-make money kupitia social network hadi utajilaumu kuwa wewe unapoteza muda tu.
Kupitia Facebook nilishapata vitu vingi ila vya kununua so nimewapa watu faida( nami nimepata faida maana sikupoteza muda wa kuzunguka madukani, nimeona kitu nikasema niwekewe nakifata saa fulani)
hata hapa jf wapo time westers na hawafaidiki na chochote yaaani yeye ni kivuruge tu, na wapo wanaopata mafunzo na kupata solution za shida zao na hata kufanya biashara pia.
Kila kitu kinafaida inategemea unakitimiaje
 
We sail in the same boat mkuu. mimi naisikia tu hiyo mitandao, mimi JF YATOSHA sana, na wala sijawahi kujuta kuwepo hapa JF mwaka wa tano huu!

Acha zako huo ni uongo ukikubal uliwah kuwa fb ndio ukajiunga jf nan atakusema? Fb ni kama kwa walevi wengi wanajifunzia safari!
 
Wengi humu mnajifanya cijui fb nn cjui vile,ila wengi mnatoa vitu humu mnapeleka fb na vi id vyenu fake! Hata mpumbavu unapaswa umsikilize ndio ujue upumbavu wake,kama wengi mnajifanya hampo fb,mmejuaje kama utoto na kuuza sura ni kwingi kule? Mi nipo kote fb nipo,IG nimo,na humu nimoooo
 
Wasalaam waungwana!
Bila shaka Januari ipo shwari kwenu wote,Kwa wale wenzangu waliobanwa na Karo za Shule poleni ndio ukubwa wenyewe.
Na raha kero ya Januari ndio hiyo,nisiwachoshe acha niwatemee hii sumu nione kama ni mimi tu inanitafuna au tupo wengi.
Kuna hii mitandao inaitwa Facebook na Insagram kuna vitu nimevifanyia utafiti nikagundu ni mitandao ya kipuuzi sana bora mara bilion hii JF yetu maana inatupa elimu na burudani pia.

"Mfano"Istargram ninao marafiki walionifuata (Followers) wengi tu kama 1500 na mimi nimewafuata pia(Following) ila kinachonishangaza ni jambo moja tu,Unakuta mtu mnafahamiana ni ndugu au rafiki yako wa karibu lakini ukipost kitu anakupa mikausho ya Like post yako lakini wakati huo huo kwa kiherehere chake na kujipendekeza post za Diamond,Jayz,Wema na wasanii wengine wajinga wajinga tena hata hawafaamiani ana Like kila post na vipicha vya ovyo wanavyoweka.

Ukirudi Facebook nako mambo ni hayo hayo ila post hiyo hiyo iliyo pata mikausho kwa marafiki zako ukiitupia JF Aaaah vicomment kadhaa na vilaiki unapata kama kawaida tena kutoka kwa watu walewale waliokupa mikausho kule FB na IG
Nimejiuliza lipi tatizo kwenye jambo hili kichwa kikauma nikaona isiwe kesi ngoja nilete swala hili hapa JF kuna vichwa vingi vikifikiri najuwa majibu yatapatikana tu,Ila kwa sasa hiyo Mifacebook na Miinstargram nimeacha kuitumia mpaka nijuwe haswa hizo Like na Comments kule zimegeuka dili?
Na kama ni dili si unatakiwa ummpe mtu unayemfahamu?
Ni hayo tu waungwana!

Mi huwa napost sana IG na like sipat za kutosha,nahis we unapenda kuuza sura so ukikosa like unajisikia vibaya,kwan like ndio nn had zikunyime raha? Pole
 
Facebook ni mtandao wa kujifunzia kuingia jf. Hata mi nilikuwa huko lakini kwa mwez naingia mara2. Ila jf kila siku
 
Wasalaam waungwana!
Bila shaka Januari ipo shwari kwenu wote,Kwa wale wenzangu waliobanwa na Karo za Shule poleni ndio ukubwa wenyewe.
Na raha kero ya Januari ndio hiyo,nisiwachoshe acha niwatemee hii sumu nione kama ni mimi tu inanitafuna au tupo wengi.
Kuna hii mitandao inaitwa Facebook na Insagram kuna vitu nimevifanyia utafiti nikagundu ni mitandao ya kipuuzi sana bora mara bilion hii JF yetu maana inatupa elimu na burudani pia.

"Mfano"Istargram ninao marafiki walionifuata (Followers) wengi tu kama 1500 na mimi nimewafuata pia(Following) ila kinachonishangaza ni jambo moja tu,Unakuta mtu mnafahamiana ni ndugu au rafiki yako wa karibu lakini ukipost kitu anakupa mikausho ya Like post yako lakini wakati huo huo kwa kiherehere chake na kujipendekeza post za Diamond,Jayz,Wema na wasanii wengine wajinga wajinga tena hata hawafaamiani ana Like kila post na vipicha vya ovyo wanavyoweka.

Ukirudi Facebook nako mambo ni hayo hayo ila post hiyo hiyo iliyo pata mikausho kwa marafiki zako ukiitupia JF Aaaah vicomment kadhaa na vilaiki unapata kama kawaida tena kutoka kwa watu walewale waliokupa mikausho kule FB na IG
Nimejiuliza lipi tatizo kwenye jambo hili kichwa kikauma nikaona isiwe kesi ngoja nilete swala hili hapa JF kuna vichwa vingi vikifikiri najuwa majibu yatapatikana tu,Ila kwa sasa hiyo Mifacebook na Miinstargram nimeacha kuitumia mpaka nijuwe haswa hizo Like na Comments kule zimegeuka dili?
Na kama ni dili si unatakiwa ummpe mtu unayemfahamu?
Ni hayo tu waungwana!

Mkuu kama ni hivyo hata JF jitoe tuu,,hapa umetupia Thread hadi sasa hivi una Like 1 tu na page 3 sijui lakin kuna watu wakitoa Uzi humu Like za kumwaga na Page za kutosha tu.
Hah hah hah wabongo wana msemo mpya "Kama tatizo ni NYOTA basi bonyeza RELI"
 
hivi mtu anajitoaje jf nielekeze plz
 
jamani mpeni mdau like na comment za kutosha apunguze hasira za IG na fb
 
Back
Top Bottom