Situmii tena Facebook na Instagram kwa ubaguzi huu

Situmii tena Facebook na Instagram kwa ubaguzi huu

Kibo10

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2013
Posts
11,278
Reaction score
8,868
Wasalaam waungwana.

Bila shaka Januari ipo shwari kwenu wote,Kwa wale wenzangu waliobanwa na Karo za Shule poleni ndio ukubwa wenyewe. Na raha kero ya Januari ndio hiyo, nisiwachoshe acha niwatemee hii sumu nione kama ni mimi tu inanitafuna au tupo wengi.

Kuna hii mitandao inaitwa Facebook na Instagram kuna vitu nimevifanyia utafiti nikagundua ni mitandao ya kipuuzi sana, bora mara bilion hii JF yetu maana inatupa elimu na burudani pia.

Mfano, Instagram ninao marafiki walionifuata (Followers) wengi tu kama 1500 na mimi nimewafuata pia (Following) ila kinachonishangaza ni jambo moja tu, Unakuta mtu mnafahamiana ni ndugu au rafiki yako wa karibu lakini ukipost kitu anakupa mikausho ya Like post yako, lakini wakati huo huo kwa kiherehere chake na kujipendekeza post za Diamond, Jayz, Wema na wasanii wengine wajinga wajinga tena hata hawafahamiani ana Like kila post na vipicha vya ovyo wanavyoweka.

Ukirudi Facebook nako mambo ni hayo hayo, ila post hiyo hiyo iliyo pata mikausho kwa marafiki zako ukiitupia JF Aaaah vicomment kadhaa na vi-like unapata kama kawaida tena kutoka kwa watu walewale waliokupa mikausho kule FB na IG.

Nimejiuliza lipi tatizo kwenye jambo hili kichwa kikauma nikaona isiwe kesi ngoja nilete swala hili hapa JF kuna vichwa vingi vikifikiri najua majibu yatapatikana tu, Ila kwa sasa hiyo Mifacebook na Miinstargram nimeacha kuitumia mpaka nijue haswa hizo Likes na Comments kule zimegeuka dili? Na kama ni dili si unatakiwa umpe mtu unayemfahamu?

Ni hayo tu waungwana.
 
Tatizo swagzz mkuu na kingine umaarufu wako unakomea kishumundu!! sa nani akushobokee kule instagram!?
Mi sijawahi kujiunga huko coz sura yangu ngumu!
 
mbona wajaja tushaligundua mapema hilo, wengine hata whatsapp hatutumii tunajifajari jf vyakutosha nikitoka hapa naenda yahoo answer kutafuta thread za kuanzisha. yaani wewe uwezo wa kufikiri amekushida shy land alieishia la saba, kweli kazi unayo
 
Ni tatizo la "marienge" kule ya akili mkuu.JF hapa ids nyingi fake,hatuoneani wivu,tunatoa ukweli.

Tukilihusisha hili jambo na wivu naweza kukuelewa mkuu
Maana haiwezekani Shilole au Linex wapige picha za kijinga na caption ya ovyo mtu ana Like the akishuka chini nakuta picha yangu na caption ya akili "eti"ananiruka kisa tunafahamiana kama sio wivu ni nini?
 
Kuwa active katika kila social network nakwo ni ishara mbaya...!
Huku Insta, kule FB, hapa JF, pale Twitter...
Bado hizo chat rooms....aaah!
 
Kitu kimoja najivunia, sina instagram wala fb account. Yaani picha zangu hazijasambaa kwenye mtandao hata kidogo ilhali nina digital photo kibao. Naona kama huko ni kwa wauza sura!
 
Amemaanisha yeye shy land na yule mwenzie mwenye ID inayoishia na .... land
nimechoka ku type hapo kwenye dot unganisha mwenyewe

Sasa yeye Shy land ni mjanja wa fb na ig au jf 😬😬
 
Last edited by a moderator:
Mtoa mada Umenigusa hapo tu ulipotupa pole tuliobanwa na karo za shule yaani binafsi imeniacha mweupeeee
 
Amemaanisha yeye shy land na yule mwenzie mwenye ID inayoishia na .... land
nimechoka ku type hapo kwenye dot unganisha mwenyewe

huyo Bush land ni mjinga tu, sijui watu huwanga wanakosa id za kutumia ili wafahamike wanatumie inayofanana na id ya mtu, tena nimeshearch google nikaona jina la id yangu ishaaza kutumika kwenye fb, sijui ndie yeye.
 
Last edited by a moderator:
huyo Bush land ni mjinga tu, sijui watu huwanga wanakosa id za kutumia ili wafahamike wanatumie inayofanana na id ya mtu, tena nimeshearch google nikaona jina la id yangu ishaaza kutumika kwenye fb, sijui ndie yeye.
pole mkuu shy land
 
Back
Top Bottom