Situmii tena Facebook na Instagram kwa ubaguzi huu

Situmii tena Facebook na Instagram kwa ubaguzi huu

Shida yako ni kupata "like". kwa hiyo ukikosa like hapa JF unajitoa?
 
Kweli mkuu umenena, watu hawaelewi, unajua tatizo ni matumizi tu, ni kama vile kisu lengo lake ni kutumia kwa mambo ya maana kama vile kumenyea ndizi, kuchunia mbuzi n.k,lkn mpumbavu anatumia kwa kumchoma binadamu mwenzake.

absolutely mkuu.
Mfano nzuri kabisa ambao sikuwahi kuufikiria.
Keep it up
 
Kuwa active katika kila social network nakwo ni ishara mbaya...!
Huku Insta, kule FB, hapa JF, pale Twitter...
Bado hizo chat rooms....aaah!

Mkuu eli79 muda wenyewe uko wapi wewe full time uwe active hiyo mitandao yote!?mimi JF tu bado muda haunitoshi!!!
 
Nilichobaini huko kote kuna unafiki wa hali ya juu. Watu kujipendekeza kwa masupastar kwa 'likes' na 'comments' hata kwa vitu/picha za kijinga.
Wewe mwenzangu usiye anuani mjini hata 'like' moja ukipata shukuru Mungu hata kama umetoa taarifa ya tsunami...
 
FB na Insta ili upate likes nyingi piga picha ukionyesha makalio,manyonyo au onyesha ndinga ya maana au onyesha mjengo wa ghorofa,hapo utapata likes mpaka utazichoka.
 
Hata hapa JF,ukitoa mada za ushuzi,kufikishana,mada za uongo uongo mara mke/mme wangu kafanya hivi oh mara nimemzzimikia feis buku utapata likes na comment za kutosha,lakini Mwanakijiji akitupia nondo za maana anapata comments nne au tano.
 
Last edited by a moderator:
Nenda Chit-chat JF au MMU halafu weka uzi japo unaosomeka "nina hamu ya kufanya mapenzi" Uone "Like" na Comment za kutosha.
 
Kutumia hiyo mitandao inabidi kwanza ujitoe ufahamu.
Instagram Diva.jpg
 
Kuna watu facebook tangu 2011 walipojiunga hawajawahi ku update status ila daily wapo online wazee wa underground movement kama Luddism vile

Kamanda umeniona nini? Nina account toka 2010 sijawahi kupost chochote wala kumtumia mtu msg wala kujibu mtu msg, natumia fcbk kusoma habari kwenye pages nilizo like, pia situmii jina langu wala sijawahi kuweka picha yangu, ukifatilia hiyo fcbk kama una mke basi ndoa unaweka rehani, na kama una mwanamke ndoa anaweka rehani, pale ni full maigizo tu hakuna watu halisi insta au fcbk,
 
Wasalaam waungwana.

Bila shaka Januari ipo shwari kwenu wote,Kwa wale wenzangu waliobanwa na Karo za Shule poleni ndio ukubwa wenyewe. Na raha kero ya Januari ndio hiyo, nisiwachoshe acha niwatemee hii sumu nione kama ni mimi tu inanitafuna au tupo wengi.

Kuna hii mitandao inaitwa Facebook na Instagram kuna vitu nimevifanyia utafiti nikagundua ni mitandao ya kipuuzi sana, bora mara bilion hii JF yetu maana inatupa elimu na burudani pia.

Mfano, Instagram ninao marafiki walionifuata (Followers) wengi tu kama 1500 na mimi nimewafuata pia (Following) ila kinachonishangaza ni jambo moja tu, Unakuta mtu mnafahamiana ni ndugu au rafiki yako wa karibu lakini ukipost kitu anakupa mikausho ya Like post yako, lakini wakati huo huo kwa kiherehere chake na kujipendekeza post za Diamond, Jayz, Wema na wasanii wengine wajinga wajinga tena hata hawafahamiani ana Like kila post na vipicha vya ovyo wanavyoweka.

Ukirudi Facebook nako mambo ni hayo hayo, ila post hiyo hiyo iliyo pata mikausho kwa marafiki zako ukiitupia JF Aaaah vicomment kadhaa na vi-like unapata kama kawaida tena kutoka kwa watu walewale waliokupa mikausho kule FB na IG.

Nimejiuliza lipi tatizo kwenye jambo hili kichwa kikauma nikaona isiwe kesi ngoja nilete swala hili hapa JF kuna vichwa vingi vikifikiri najua majibu yatapatikana tu, Ila kwa sasa hiyo Mifacebook na Miinstargram nimeacha kuitumia mpaka nijue haswa hizo Likes na Comments kule zimegeuka dili? Na kama ni dili si unatakiwa umpe mtu unayemfahamu?

Ni hayo tu waungwana.

napenda kukuambia kuwa watu hupenda ya kijinga kuliko ya maana, mabaya kuliko mazuri, ya shetani kuliko ya mungu, mada za ajabu ajabu kuliko za maana na zenye kuleta maendeleo, n.k hivyo hupaswi kushangaa bali kuelewa kuwa ndio mambo ya binadamu yalivyo.we potezea
 
huyo Bush land ni mjinga tu, sijui watu huwanga wanakosa id za kutumia ili wafahamike wanatumie inayofanana na id ya mtu, tena nimeshearch google nikaona jina la id yangu ishaaza kutumika kwenye fb, sijui ndie yeye.

hapo kwenye red wewe Shy land ndo unamaanisha nini?
 
acha wivu komaa na wewe uwe SUPERSTAR upate hizo LIKE unazozililia...wenzio wasanii wanatumia FACEBOOK na INSTAGRAM kujitanua kibiashara na kupiga hela wewe umeng'ang'ana huko upate umaarufu uchwara na LIKE ambazo haziwezi kuongeza wala kupunguza chochote kwenye kipato chako
 
acha wivu komaa na wewe uwe SUPERSTAR upate hizo LIKE unazozililia...wenzio wasanii wanatumia FACEBOOK na INSTAGRAM kujitanua kibiashara na kupiga hela wewe umeng'ang'ana huko upate umaarufu uchwara na LIKE ambazo haziwezi kuongeza wala kupunguza chochote kwenye kipato chako

Utafiti umegeuka wivu?We ngifi kweli!
 
Back
Top Bottom